Rais Samia awekwe kwenye fedha, tuache wivu na chuki

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
RAIS SAMIA AWEKWE KWENYE FEDHA, TUACHE WIVU NA CHUKI.

Na; Suphian Juma Nkuwi

Nilishalisema sana hili humu mtandaoni tangu Mhe. Rais Dkt Samia akiwa na miaka miwili ya Utumishi wake Ikulu. Na hata mwishoni mwa mwaka uliopita wa wa 2023 nilipohojiwa na Mtangazaji Chief Odemba katika kipindi cha Medani za Siasa Star TV nililisisitiza hili.

Binafsi nimefurahi mno leo kusikia Mbunge Ng'wasi Kamani kuipeleka hoja hii Bungeni na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa kuipokea na kuahidi Serikali kuifanyia kazi.

Aidha nimesikitishwa na baadhi ya Watanzania wenzetu hususani wa vyama vya Upinzani wanaopinga hoja hii. Hoja zao zote ukizitathmini unaona kabisa wanaendeshwa na WIVU, CHUKI na GUBU. Ndio kuna mapungufu ya kiuongozi, ila tutambue hata Marekani na nchi zilizoendelea kero zipo na maendeleo ni process, matatizo ya wananchi huwezi kuyamaliza yote siku moja, Kikubwa ni nia na vitendo vya Kiongozi ndivyo vya kutilia maanani.

Ifike pahala tumheshimishe Rais wetu Dkt Samia kwenye fedha ANGALI HAI tusisubiri siku akitoweka duniani ndio tuanze kujidai kumpamba na sifa nukuki.

Hoja zangu ni mbili; kwanza kwa hakika hadi sasa ametufanyia Mapinduzi makubwa mno ya kisekta ndani ya muda mfupi kama Rais, na pili ikumbukwe kwa unyeti Mama Samia ndiye mwanamke wa kwanza kuwa Rais Tanzania tangu 1961. Kwanini tusimuenzi kwenye fedha zetu?

Ndugu zangu Watanzania naomba kwa pamoja kwa sauti moja tukemee pepo la chuki na wivu tukubali kumheshimisha Rais wetu Dkt Samia kwa kukubali sura yake iwekwe kwenye fedha zetu. Hii itamtia moyo azidi kutuongoza vema zaidi na zaidi hadi 2030 kama Rais.

Tuachane na Mapinduzi makubwa ya miaka ya nyuma, hebu tujadili na kutafakari mafanikio ya baadhi ya Sekta ambayo Mheshimiwa Rais chini ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ameyafanya mwaka jana 2023 tukilinganisha na mwaka juzi 2022 kama nilivyorejea kwenye hotuba yake Rais mwenyewe ya kufunga mwaka 2023 kuelekea mwaka mpya tuliopo sasa wa 2024.

AMANI, ULINZI NA USALAMA.

Mheshimiwa Rais alituthibitishia kwamba vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama vipo imara, wanalinda vema mipaka yetu, mali na sisi wananchi, na pia kutusaidia pale tupatapo majanga hapa akirejea namna Jeshi nilivyowasaidia waathirika wa mafuriko na maporomoko ya ardhi (Landslide) ya Wilaya ya Hanang yaliyoharibu makazi na kupoteza uhai wa maelfu ya ndugu zetu. Allah awalaze pema peponi.

Ndugu zangu tumshukuru Rais wetu kama Amiri Jeshi Mkuu maana amani ndio nguzo ya kila kitu katika maisha, nchi zenye machafuko ya Amani kutwa tunashuhudia wananchi wake wanavyokufa na kuteseka.

MAPITO YA UCHUMI.

Hapa Mhe. Rais Dkt Samia ametaja maneno kadhaa.

a) PATO LA TAIFA
Pato la Taifa licha ya changamoto za kivita zilizoathiri chumi za nchi zote duniani, kwa Tanzania kutokana na uimara wa Serikali, pato la Taifa limeongezeka kufikia 5.2% kwa mwaka 2023 kutoka 4.7% ya mwaka 2022.

b) UWEKEZAJI
Kutokana na ziara tija za nje za Mhe. Rais Dkt Samia, na utekelezaji wa Sera ya uwekezaji, uwekaji mazingira rafiki kwa Wafanyabiashara vimepelekea miradi 504 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 5.6 imesajiliwa 2023 ukilinganisha na miradi 292 iliyosajiliwa 2022, hili ni ongezeko la 58%. What a wondrous news!!

C) MFUMUKO WA BEI
Serikali kupitia Mkuu wake Dkt Samia kwa mwaka 2023 Januari hadi Novemba imefanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei kupungua kwa wastani 3.9% ukilinganisha na wastani wa 4.3% kwa Januari hadi Novemba mwaka 2022.

d) UKUSANYAJI KODI
Ndugu zangu sote tunajua nchi haiwezi kuendeshwa bila kodi kwani hata wafanyakazi na hata bidhaa na huduma tunazozitumia kila siku ni matokeo ya kodi, hivyo kulipa kodi ni uzalendo. Kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 2023 kwa mujibu wa Rais wetu, Serikali ilikusanya kodi Shilingi trilioni 22.6 likiwa ni ongezeko la 8% ukilinganisha na mwaka 2022.

USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Sote tunafahamu kabla ya kuingia madarakani Rais Dkt Samia, mahusiano na Mashirikiano ya nchi yetu Kimataifa yalikuwa yanachechemea; kwa mwaka 2023 Rais amefanya ziara makumi kwa makumi ndani na nje ya Bara la Afrika na hivyo kuleta mafanikio yafuatayo katika nchi:-

Dola za Marekani 550 kwa ajili ya miradi ya Usalama wa Chakula

Dola la Marekani 297.64 kuwezesha mawasiliano vijijini

Chuo cha Teknolojia cha IIT Madras kutoka India kimefungua kampasi yake Zanzibar

Tumepata soko la uhakika la mabondo ya samaki, parachichi, kahawa soya na kadhalika katika nchi mbalimbali duniani

Nafasi za kazi 500 kwa wauguzi wetu Saud Arabia

Tumerejeshwa kwenye mfumo wa changamoto za milenia (MCC) wa Marekani baada ya kusitishwa kwa takribani miaka 6.

Tumepokea viongozi Wakuu mashuhuri kutoka Marekani, Ujerumani, Indonesia, Hungary, Romania, pamoja na viongozi wa Nchi za Afrika.


UTALII

Hii sekta imekua sana tangu Mhe. Rais Dkt Samia aingie madarakani ikichagizwa zaidi na filamu yake ya The Tanzania Royal Tour, na uimarishwaji wa mahusiano mema ya Kimataifa. Kwa Januari hadi Octoba mwaka 2023, idadi ya Watalii imeongezeka hadi kufikia 1, 471, 567 kutoka watalii 1, 175, 930 katika kipindi cha miezi hiyo mwaka 2022.

MADINI
Rais Dkt Samia hakuiacha nyuma Sekta hii adhimu nchini ambapo kwa mwaka 2023 pamekwepo kwa ongezeko la 6.43% la thamani ya madini yaliyozalishwa, na ongezeko la 5.8% ya madini yaliyouzwa nje ya nchi hadi kufikia dola za kimarekani bilioni 3.15

KILIMO
Kwa kutambua Kilimo ndio utu wa mgongo wa Taifa letu; Serikali ya Rais Dkt Samia kwa mwaka 2023 imeongeza bajeti ya kilimo hadi kufikia bilioni 970 kutoka bajeti ya bilioni 751 ya mwaka 2022 ambalo ni ongezeko la 29% kiwango ambacho hakijawahi mithilika katika historia ya nchi yetu.

Aidha hadi kufikia Novemba 2023 Serikali imesambaza mbolea mikoa yote Tanzania bara yenye jumla ya tani 204818.16 na kutoa ruzuku ya bilioni 67.82. Mama "ameupigaje hapo"? (kwa sauti ya Miso misondo)

Sio hivyo tu; mnada mpya wa zao la chai umeanzishwa. Serikali imetoa pia bilioni
116 kununua tani 200293 za mazao mbalimbali ya wakulima kama sehemu ya kuchochea soko.

Mafanikio kwenye kilimo ni mengi, bila kusahau pia, Rais Samia kwa kuwapenda vijana na Wanawake ametenga ekari 201241.6 za uzalishaji, na kuanzisha program ya kilimo cha kisasa iitwayo Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ili kuongeza uzalishaji na Ajira kwa vijana.

ELIMU
Moja ya mafanikio ya Sekta ya Elimu mwaka 2023 ni pamoja na kubadilishwa Sera ya Elimu na mitaala ili kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi wa kujiajiri na kukidhi mahitaji ya soko la ajira. Mikopo ya Elimu ya Juu imeongezwa kufikia bilioni 731 kutoka bilioni 654 ya mwaka 2022. Aidha Mheshimiwa Rais amewaahidi walimu kuwajengea makazi na kuwaimarishia mahitaji yao muhimu ili waweze kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi.

MAJI
Rais Dkt Samia kwa kutambua maji ni uhai, kwa mwaka 2023 amesimamia ukamilishwaji wa miradi 506 ya Maji; 436 vijijini na 70 mijini yenye kuhudumia wananchi 5754340 ambapo hadi sasa upatikanaji maji Safi na salama imefikia 88% Mjini na 77% vijijini.

Kwa ushawishi wa Mhe. Rais Dkt Samia, zimepatikana dola za Marekani milioni 600 kukamilisha mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Dodoma.

NISHATI
Kwa kurejea kwenye Nishati ya umeme kama Nishati muhimu; Mhe. Rais Dkt amesema hadi kufikia Novemba 2023 Serikali imefanikiwa kupeleka umeme kwa vijiji 11447 Sawa na 96% ya vijiji vyote 12318 vya Tanzania bara. Kwa upande mwingine, kutambua adha ya kukatika Umeme, Serikali imeendelea kupambana kuharakisha mradi mkubwa Umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ulioanzishwa 2017 kukamilika ili kuongeza megawati 2115 kwenye gridi ya Taifa.

AFYA
Kwa mwaka 2023 Serikali imeajiri wataalam wa afya 17309 na kutenga bilioni 190.9 kununua dawa, sambamba na kununua mashine 140 za kutibu sarakatani ya mlango wa kizazi kwa akina Mama na kusambaza magari 369 ya kubeba wagonjwa kote nchini.

MAZINGIRA
Katika harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi, Mhe. Rais Dkt Samia 2023 alizindua program ya Matumizi ya Nishati Safi ambayo imelenga hadi ifikapo 2033 Watanzania 80% waachane na matumizi ya mkaa na kuni Kupikia. Aidha Jumuiya za Kimataifa Global Centre on Adaptation na Benki ya AFDB zimetoa Dola bilioni 9.9 na Global Environment Fund wametoa dola milioni 53 zote zenye lengo la kuisaidia Tanzania kudhibiti athari za mabadiliko ya tabia Nchi.

MICHEZO
Pamoja na mambo mengine, kwa mwaka 2023 Serikali imesaidia katika kupatikana mafanikio yafuatayo;

Ukarabati wa uwanja wa Mpira wa Benjamin Mkapa

Yanga mshindi wa pili Kombe la CAF Federations Cup, Simba mshindi wa kwanza African super League kutoka ukanda wa CECAFA, JKT Queen kuwa mabingwa CECAFA, Karume Boys mabingwa CECAFA umri chini ya miaka 15 na kubwa zaidi ni Tanzania kushinda fursa ya kuwa moja ya Waandaaji wa mashindano ya AFCON mwaka 2027

UCHUKUZI
Sekta imepiga hatua kubwa mwaka 2023; Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)kutoka Dar es Salaam, Morogoro hadi Makutupora umefikia 90%, ndege moja ya Mizigo na moja ya abiria zimenunuliwa, ujenzi wa gati ya bandari mpya ya Karema Ziwa Tanganyika itakayotuunganisha na nchi ya DRC.

Bado tu kuna mtu hataki tumuenzi kwenye fedha zetu? Actually hakuna Kiongozi anayependwa na watu wote, hebu sisi tunaompenda tukubali hili, wasiompenda leo, watampenda kesho.

Wahenga wanasema; asiyeshukuru kwa kidogo hatashukuru kwa Kikubwa; Tumpongeze, tumshukuru na kumtia imani Rais wetu mpendwa Dkt Samia na Serikali yake kwa kutuletea haya mageuzi makubwa ya kisekta, ili mwaka huu na miaka ijayo hadi kufikia 2030 kama Rais aendelee kutuongezea mageuzi na matokeo makubwa zaidi na zaidi Tanzania nasi tutoke kwenye "nchi inayoendelea kwenda kwenye nchi iliyo endelea".

KAZI IENDELEE,
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Suphian Juma Nkuwi,
Kada - CCM,
Februari 08, 2024
Singida.
Simu: +255717027973

IMG_20240209_081721.jpg
 
NCHI INA KAMPENI ZA AJABU HII........

KUCHAPISHA HELA NI GHARAMA...
HUKU:
UMEME HAUKIDHI...
MIKOPO KWA WANAFUNZI HAITOSHI..
BIMA YA AFYA HAIJAKAA SAWA...
MISHAHARA KADA MBALIMBALI IKO CHINI..
GHARAMA ZA MAISHA PIA....

Mnafanya kampeni za ajabu kwa manufaa ya wachache.
 
Mkapa licha ya mapungufu yake lakini hata issue ya kubali katiba ili aendelee aliwaambis wazi machawa, hawahawa ndorobo ndio waliopoteza Magufuli kiasi cha kuamini Bila yeye hakuna Tanzania.

Machawa hawa ni Enemy of statement, tisiwachekee.
Kabisa mkuu, hawa wapo kwa maslahi yao tu hawajali chochote kile.

Hawa wanafiki ndio maadui wa maendeleo ya hii nchi.
 
Back
Top Bottom