Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Hii imevuka mpaka. Chuki iko kwenye mioyo na roho za watu. Hata wakiombewa vipi, hawabadiliki. Cha shetani ni cha shetani...
Na Mungu hadhihakiwi......Si kila alitajae jina na bwana ataingia peponi wengine ni wauaji wakuu na wanyang'anyi wa haki ya kuishi ya watu wengine
 
Sasa wataendaje msibani huku wanashangilia vidole juu km waimba taarabu?

Hyo si kebehi kwa msiba wa Taifa.
Huo sio msiba wa taifa ni wa ccm.......sisi wenye taifa ambao ni malofa haituhusu
 
Viongozi wakuu wa Chadema wamefika uwanja wa Uhuru leo saa moja asubuhi ndipo wakazuiwa kuingia wakiambiwa wasubiri kwanza utaratibu.

Ilipofika saa tatu asubuhi viongozi kadhaa walianza kumiminika na kuruhusiwa kuingia uwanjani huku viongozi wa Chadema wakiwa bado getini.

Rais alipofika akaingia ndipo viongozi wa Chadema wakaambiwa hakuna tena kuingia uwanjani.

Ndipo nasema sasa kila mtu afanye shughuli yake ili mradi hatutavunja katiba.

Makamanda, msibani kwa wastarabu huwa hakuna mwenyewe. Mmefanya sehemu yenu vyema. Sehemu yenu ya nia njema imeonekana na kila mwenye macho na masikio.

Msichoke kuonyesha nia njema. Hiyo ndiyo maturity.

Wanasema, tenda wema wende zako.

Tusisahau wakuu zitakuwapo provocations nyingi na hata mbaya zaidi. Muhimu kujizatiti vilivyo.

Kama kuja nyumbani salama *kulivyoratibiwa vilivyo* tusiangukie kwenye vimitego vya kipuuzi.

Kumbukeni kama msingeenda kuhani, kwa wasiotutakia mema, hiyo mbona ingekuwa habari kubwa?

Ni wazi kuwa walioingilia hilo walikuwa na nia ovu kwa kujua au kutokujua kwao. Tusiwape nafasi za kufanikisha nia zao kwa kujipanga well above the horizon.

Pumzika kwa amani mzee Mkapa.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Mbona baada ya kuzuiwa viongozi wa chadema bado watu waliendelea kuingia......

Kwa nn ccm wanaleta siasa kwenye kila kitu?
 
Tangazo la jana hawakulisikia? Msemaji wa Serikali Dr. Hassan Abas aliweka wazinutaratibu wa uingiaji uwanjani leo.

TAFAKURI
Kama maelezo mafupi Kama yale yanashindwa kutafsiriwa na watu wanaotaka kuchukua dola, hivi Mambo complex ya kuendesha nchi watawezana nayo kweli?
We ng'ombe kwako kifo cha mkapa ndio jambo complex....... kuwaelezea watz ulipo uchumi wa kati ndio swala complex....
 
Viongozi wa CHADEMA mjitahidi sana kuwahi kweye matukio kama haya, mnapofika uwanjani mkuu wa nchi kashaingia tayari, mnakuwa mnawapa nafasi wapinzani wenu kujenga hoja.
 
Msafara wa Viongozi Wakuu wa CHADEMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Freeman Mbowe, wamezuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru walikokuwa wameenda kuhudhuria shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa.

Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Mbowe aliongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Bara), Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mhe. John Mnyika, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Mhe. Hashim Juma Issa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama, Mhe. Suzan Kiwanga na viongozi wengine waandamizi kutoka Makao Makuu ya CHADEMA, Viongozi wa Kanda 10 za chama, Viongozi CHADEMAwa Mikoa, Wilaya na Majimbo mbalimbali nchi nzima.


Kutoka Uwanja wa Uhuru hapa, Dar es Salaam.
Jamani mbona Maalim Seif yupo tena kakaa nyuma ya akina Magu?

Hao Chadema walifuata taratibu zilizowekwa au Walifuata taratibu zao binafsi?

Hivi Chadema Magu mpaka leo wameshindwa kucheza naye kweli? Mbona jamaa mwepesi sana???
 
Sawa hata wakenya mmewazuia wasitue kuungana nanyi kwenye msiba hawa nao hawakufata protokali.......

Ni ujingaujinga tu wa maccm
 
Kwa jinsi walivyojikusanya na kwenda Uwanja wa Taifa, ni wazi kabisa walitaka kick ya kisiasa, sasa hao walikuwa hawana nia ya kuhani msiba bali kujitangaza kisiasa na wangevuruga sana..
Msiba mkubwa wa Taifa na Kimataifa kama huu wa Mh. Mkapa, alafu unakuja na sura au mlengo wa kisiasa ili ujipatie kick au publicity ni mbaya sana, watu wako katika majonzi ww uje na magwanda yako ya CDM unatafuta nn? Alafu wanakuja Mh. Rais tayari yuko ndani ya Uwanja wa Taifa, hata hawajui itifaki, hii ni kosa.
Kila kitu mnawaza siasa tu, ndio maana we are one of the poorest countries in the world, now upgraded to lower middle income, with squatters all over the place.
 
Viongozi wa CHADEMA mjitahidi sana kuwahi kweye matukio kama haya, mnapofika uwanjani mkuu wa nchi kashaingia tayari, mnakuwa mnawapa nafasi wapinzani wenu kujenga hoja.

Ok, kaa wamefika Baada ya viongozi wa nchi, walifanya kusudi, wala hawakuwa na nia ya kuomboleza ila kiki. Maana protocol wanaijua.

Kwanini hawakufika kwa muda uliopangwa? Mbona Maalim alifika na kakaa jukwaa kuu, nyuma tu ya Magu?

Ningependa sana kumuona TL karibu na mbaya wake.
 
Mwanahabari Huru,

Nafikiri kwenye hili tuache ushabiki Viongozi wa Chadema wamechelewa kufika uwanjani na walipaswa kukaa presidential Area wangekaaje na je uwanjani wangeingia vp wakati Rais kaishaingia?

Wakubwa sehemu yeyote ambayo kama kuna event mtu wa mwisho kuingia ni Rais ukichelewa kaa mbali tu!
Na inawezekena hawakukubali mualiko na waandaaji hawakujua kuwa wataenda. Mbona Maalim kapokelewa vizuri, na kakaa nyuma tu ya Magu, tena Hussein Mwinyi yuko nyuma ya Maalim.

Chadema wasipoacha ujinga, ACT- itawazidi kete kwenye uchaguzi huu na kuchukuwa kambi rasmi bungeni. Sijui watasemaje pale Zitto atakapokuwa KUB na mgawaji wa wizara vivuli.
 
Back
Top Bottom