Wawe wanatumia helicopta wajinga hao week end Msonga!
wanaogopa kutunguliwa mkuu. si unajua hata 'bazoka' inashusha hiyo kitu kilaini.
Wawe wanatumia helicopta wajinga hao week end Msonga!
pole ya nini wakati anajitakia kwani angekaa nyumbani kwake akampikia mumewe angepata hiyo ajali? kiherehere tu bora angekufa yeye kuliko huyu dreva anaacha pengo kwenye familia yake bila sababu ya msingi eti msafara wa Salma Kikwete
Tuwe na huruma zaidi kuliko ushabiki, vp kama ajali hiyo ingemuhusu ndugu yako wa damu (mama, dada, shangazi, mpwa, baba au kaka) ungetoa comments gani?
Bazoka sijui nini hiyo achana nayo mkuu!! Jiwe tu linaishusha helkopta, kumbuka wale jamaa wa Tarime wiliidungua moja mwaka juzi au?!wanaogopa kutunguliwa mkuu. si unajua hata 'bazoka' inashusha hiyo kitu kilaini.
Kama dereva alikuwa anajari-kuserve maisha ya huyu mama ndio akafa yeye basi Marehemu alikuwa Mpumbavu, hayo siyo mafunzo ya kivita; askali anatakiwa kuokoa maisha yake yeye mwenyewe kwanza, maana yeye ndio nguzo ya Ushindi maana huyo mama akifa siyo hasara kwa taifa kama akifa yeye, inawezekana kupata askali shupavu na makini kama yeye itakuwa kazi ngumu sana kwa taifa ukinganisha na kifo cha Fisadi mmoja, Government can get First ladies at low costs kuliko ku-train Kachero, tumepata hasara kubwa sana, hawa makachero wetu nadhana hawajapata elimu ya kutosha huyo mama hayumo katika list ya watu wakulinda ikibidi ufe!! nadhani watu wakulinda ikibidi ufe hapa TZ ni Rais na Waziri Mkuu.
Mama Salma, gari yake yeye ipo salama na yeye yupo salama. Msafara ulikuwa na gari kama 10, gari ya Mama Salma ilikuwa ya tatu toka mbele, na ile Toyota LX ilikuwa ya 5 toka mbele ..
Katika masuala ya misiba ni vema tuweke ushabiki na chuki zetu dhidi ya viongozi na wake au waume zao pembeni. Mtu yeyote ambaye ana jukumu la kulinda kiongozi anaapa kutoa uhai wake kuhakikisha mlindwa wake hauawi au kudhurika. Ni kweli kabisa kuwa kuna matatizo makubwa katika masuala ya misafara ikiwa ni pamoja na watu kusimamishwa kupisha misafara ya watu ambao hata ambao si viongozi kama mke wa raisi, wake za makamu wa raisi na waziri mkuu, na misafara ya mabalozi na viongozi wa jeshi la polisi.
Hoja yangu ni kuwa kama huyo afisa usalama wa taifa alifanya hivyo ili kumnusuru Salma Kikwete huko ni kutimiza wajibu wake na anastahili heshima zote. Lakini kuna haja ya kupiga marufuku utitiri wa viongozi wenye haki ya kupishwa katika misafara. Viongozi hao wawe Raisi, Makamu wa Raisi na Waziri Mkuu na ni lazima muda wa kusimamisha magari husizidi dakika tano. Hivyo kitendo cha Jeshi la Polisi kusimamisha magari kwa nusu saa au zaidi wakati viongozi hao ndio kwanza wanaingia bafuni kiwe marufuku. Hhivyo basi wananchi wawe na haki ya kuendelea kutumia magari kama muda wa dakika tano utapita bila msafara wa kiongozi huyo kupita. Nasisitiza kuwa wake au waume wa viongozi hawana haki ya kusimamishiwa magari ili wapite wanatakiwa kutumia barabara kama wananchi wengine.
Punguza jazba na tumia maneno laini utaeleweka tuu
Magari kama kumi? Nimeamini kwanini alikuwa akimpigia mumewe kampeni!Mama Salma, gari yake yeye ipo salama na yeye yupo salama. Msafara ulikuwa na gari kama 10, gari ya Mama Salma ilikuwa ya tatu toka mbele, na ile Toyota LX ilikuwa ya 5 toka mbele ..
Mkuu umetuelekeza Fikrapevu kumbe nao wamezichota hapa manake naona wameelekeza tena hapa!