Simiyu: Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali katika msafara wa Mkuu wa Mkoa Mwanza

bagabe

JF-Expert Member
May 8, 2014
459
549
Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari ya waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.

--
Rais Samia atoa salamu za Rambirambi

''
1641891554448.png

====

Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari la waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu akiwa eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.

Amesema kati ya vifo hivyo kuna vifo vya waandishi wa habari wanne na dereva wa waandishi na watu wengine sita walifariki papo hapo

“Ni kweli ajali hiyo imetokea, watu 11 wamefariki kwenye eneo la tukio wakiwemo waandishi wa habari 4 na dereva na wengine sita waliokuwa kweneye gari lingine” amesema Zakaria na kuongeza

“Dakika chache majeruhi waliopelekwa kwenye kituo cha afya cha Nasa watatu walifariki, wakiwemo wale waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyo, Blasius Chatanda yupo katika hospitali ambako majeruhi walikopelekwa akiahidi kuwa atatoa taarifa baadaye.

Chanzo: Mwananchi

======

UPDATES;

=====

Waandishi waliofariki kwenye ajali ya gari ni

1. Husna Mlanzi wa ITV

2. Johari Shani wa Uhuru Digital pia ni askari Polisi WP11158DC

3. Antony Chuwa wa Habari leo Digital

4. Abel Ngapemba Afisa habari Mwanza

5.Steven Msengi Afisa Habari Ukerewe

6. Paul Silanga Dereva wao

Miili yao imehifadhiwa katika Kituo cha Afya Nassa wilayani Busega mkoani Simiyu.

Majeruhi ni:

1. Vanny Charles wa Icon. TV

2. Tunu Heman -Mwandishi wa habari wa kujitegemea

Wamelazwa Hospitali ya Bugando Mwanza

=====

RC KAFULILA ATOA SALAMU ZA RAIS SAMIA KUFUATIA AJALI MBAYA YA GARI MKOANI SIMIYU

MKUU wa Mkoa Simiyu, David Kafulila amewapa pole wakazi wa wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla kufuatia ajali mbaya ya gari iliyochukua maisha ya watu14.

" Huu ni msiba mkubwa kwenye historia ya wilaya na mkoa wetu. Kupoteza watu14 kwa ajali ni msiba mkubwa kitaifa. Nimewasiliana na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, amepokea taarifa ya ajali hii kwa masikitiko makubwa na amenituma kufikisha kwenu salamu za pole, na kwamba yupo nasi katika majonzi haya".

" Ni ajali mbaya lakini niwaombe utulivu. Miili 6 kati 14 imetambuliwa na walikuwa sehemu ya msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na hivyo ameondoka nayo tayari kuelekea mwanza kwa taratibu zingine, kwetu hapa zoezi la kutambua miili 8 linaendelea,hivyo niwaombe wananchi tuendelee kuwa watulivu,".amesema.

Ajali hii imetokea siku moja kabla ya siku iliyopangwa kwa ajili ya maombi maalumu mkoa huo itakayangozwa na viongozi wa dini zote mkoani hapa Januari 12 mwaka huu majira ya saa 3.00 asubuhi.

Akizungumzia Ajali hiyo amesema imetokea Leo saa 12.25 asubuhi katika Kijiji cha Kalemela katika Barabara ya Musoma- Mwanza ,Wilaya ya Busega.

Magari mawili STK 8140 TOYOTA LANDCRUISER iliyokuwa ikitokea Mwanza kwenda Wilaya ya Ukerewe kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza iliyogongana uso kwa uso na gari Na. T.281 DER aina ya TOYOTA HIACE iliyokuwa ikitoka Lamadi( Simiyu) kwenda Mwanza.

Mpaka saa 6.00 mchana watu 14 wamefariki na kati yao wanawake ni 5 na wanaume 9.

Aidha wanahabari 6 waliokuwa kwenye gari la Serikali na dereva wao ni sehemu ya waliofariki.

Majeruhi wa ajali ni sita, ambapo 2 wapo kituo cha afya NASA na 4 wamepekwa hospitali ya Rufaa Bugando.

Waliofariki waliokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza ni pamoja na-:
Husna Milanzi - ITV,Johari Shani - Uhuru Digital
,Antony Chuwa - Habari leo Digita,Abel Ngapenda - Afisa Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza na Steven Msengi - Afisa Habari Ukerewe.

Majeruhi ni pamoja na Tunu Heman -Mwandishi wa habari wa kujitegemea na Vany Charles - Icon TV

Chanzo cha ajali nI mwendokasi wa magari yote mawiliambapo dereva wa LANDCRUISER alianza kuligonga ubavuni gari Na T 816 DCY TATA BUS akiwa amehama na kwenda kulia na baadaye kwenda kuligonga gari aina ya Hiace iliyokuwa nyuma umbali wa kama M.38..

Madereva wote wamefariki kwenye ajali. .Aidha RC Kafulila amesisitiza kwamba taarifa ya mwisho kuhusu uchunguzi wa ajali itapatikana baada ya Kamati ya Usalama Mkoa kupokea taarifa ya uchunguzi wa ajali hiyo.

IMG-20220111-WA0003.jpg
IMG-20220111-WA0004.jpg

20220111_111146.jpg

20220111_140041.jpg

IMG_20220111_183425_171.jpg

20220111_184454.jpg

Husna Mlanzi wa ITV

IMG_20220111_184932_133.jpg

Antony Chuwa wa Habari leo Digital

IMG_20220111_185204_436.jpg

Steven Msengi Afisa Habari Ukerewe

IMG_20220111_210755_419.jpg

Abel Ngapemba Afisa habari Mwanza

IMG_20220111_211145_394.jpg

Johari Shani wa Uhuru Digital(Polisi WP11158DC)
20220112_142708.jpg

20220112_143743.jpg

IMG_20220113_001848_314.jpg
IMG_20220113_001947_433.jpg
 
Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari la waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu akiwa eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.

Amesema kati ya vifo hivyo kuna vifo vya waandishi wa habari wanne na dereva wa waandishi na watu wengine sita walifariki papo hapo

“Ni kweli ajali hiyo imetokea, watu 11 wamefariki kwenye eneo la tukio wakiwemo waandishi wa habari 4 na dereva na wengine sita waliokuwa kweneye gari lingine” amesema Zakaria na kuongeza

“Dakika chache majeruhi waliopelekwa kwenye kituo cha afya cha Nasa watatu walifariki, wakiwemo wale waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyo, Blasius Chatanda yupo katika hospitali ambako majeruhi walikopelekwa akiahidi kuwa atatoa taarifa baadaye.

ADVERTISEMENT

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel naye amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema yuko njiani kuelekea eneo la tukio.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi
 
Ajabu waandishi wa habari wanabebwa kama magunia na kupewa vibahasha vya posho ya mboga ilimradi tu wakaripoti habari kumpaisha mwanasiasa.. waandishi wa habari mjitathmini...kutwa kikimbilia kwenda kuripoti matukio ya wanasiasa na huku mtaani matukio ya wananchi, kero na maoni kuhusu serikali yao yamejaa ila hamuendi..
 
Huu utaratibu wa magari yaliyoko kwenye msafara wa viongozi kuendeshwa kama yanaendeshwa na vichaa ufikia mahali ufe.

Hakuna wanapowahi zaidi ya kaburini tu halafu utasikia "ni mpango wa Mungu".

Stupid fools.
Kwa kweli umeongea jambo la muhimu sana.

Nimewahi kuwa mikoani kwa shughuli kadhaa zinazohusiana na ofisi ya mkuu wa mkoa, wilaya ama mkurugenzi.

Kwa kweli kama ni kwenda kukagua miradi, misafara ya magari kwenye ziara huwa inakiuka kwa wazi kabisa sheria za usalama barabarani katika maeneo yafuatayo:
1. Mwendo kasi - ni kama vile kwa kuwa tu mpo kwenye msafara basi hakuna anayejali tena kuhusu mwendo kasi uliopitiliza.( Hata maaskari wa usalama wa barabarani huwa hawafanyi chochote kwa kuwa tu ni msafara wa mkuu wa mkoa, wilaya ama mkurugenzi.

2. Matumizi ya ''Hazard'' - yaani kwenye hii misafara kitu madereva wanajua ni kuwasha taa za hazard kisha wanakuwa huru kufanya chochote barabarani.

Ni muhimu sasa kwa madereva na wale wanaokuwa kwenye hii misafara kuzingatia sheria za barabarani.
 
Sure mkuu. Bila hivyo hizi ajali za kujitakia hazitakaa ziishe.
 
ajabu waandishi wa habari wanabebwa kama magunia na kupewa vibahasha vya posho ya mboga ilimradi tu wakaripoti habari kumpaisha mwanasiasa.. waandishi wa habari mjitathmini...kutwa kikimbilia kwenda kuripoti matukio ya wanasiasa na huku mtaani matukio ya wananchi, kero na maoni kuhusu serikali yao yamejaa ila hamuendi..
Hao ni waajiriwa, ni maafisa habari wa halmashauri.
 
Huu utaratibu wa magari yaliyoko kwenye msafara wa viongozi kuendeshwa kama yanaendeshwa na vichaa ufikia mahali ufe.

Hakuna wanapowahi zaidi ya kaburini tu halafu utasikia "ni mpango wa Mungu".

Stupid fools.
Nina rafiki zangu kibao kwenye tasnia hiyo waliopo Mwanza. Natamani nifahamu majina ya waathirika, lakini nimeshindwa kuwapigia simu mmoja mmoja! Natamani niwatambue kwa njia nyingine!
Aliyepata majina, naomba atupatie!
 
Back
Top Bottom