Msafara wa First Lady waua mmoja Ruvu

mgodi

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
2,780
1,845
Ajari mbaya imetokea maeneo ya Vigwaza, msafala ulikuwa unatoka Dsm unaelekea Chalinze (Msoga). Magari matatu yamegongana, gari 1 aina ya toyota Land Cruiser ambalo lilikuwa kwenye msafara limegongana uso kwa uso na Basi la Moro Best, pia basi hilo liligonga kwa nyuma Toyota Hiace.

Dereva wa Toyota LX amefariki hapo hapo, katika ajali hiyo watu kadha wamejeruhiwa.

Dereva wa Usalama afa kumuokoa Salma Kikwete http://bit.ly/gGG9P1"

MSAFARA wa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete umepata ajali na kusababisha kifo cha dereva wa Idara ya Usalama wa Taifa, Ramadhani Mkoma, Fikra Pevu, limethibitishiwa. Habari zilizoifikia Fikra Pevu na ambazo zilianza kumiminika katika mtandao wa Jamiiorums.com zimeeleza kwamba ajali hiyo imetokea eneo la Ruvu saa 6.30 Jumapili (Februari 13,210), wakati Mama Salma akielekea katika nyumba yao mpya kijijini Msoga.

Soma Zaidi (FIKRA PEVU)
 
Je bi Salma kanusurika maana umesema msafara wa Bi salma wapata ajali tujuvye zaidi.:embarrassed:
 
Leo nimesafiri bila Laptop, ningeweza kutuma picha. Nimepiga kadhaa lakini zipo kwny camera, nikifika Arusha nitaweka picha.
 
Mama Salma, gari yake yeye ipo salama na yeye yupo salama. Msafara ulikuwa na gari kama 10, gari ya Mama Salma ilikuwa ya tatu toka mbele, na ile Toyota LX ilikuwa ya 5 toka mbele ..
 
Ziara za jumapili nazo, poleni majeruhi na innalillah wainailaih rajiuun kwa waliopoteza maisha.
 
Msafara wa first lady umepata ajali eneo la ruvu baada ya gari iliyokuwa kwenye msafara kugongana na basi na gari la first kugonga nyuma ya gari hilo lililokuwa kwenye msafara.nikipata picha na habari zaidi nitawafahamisha.
 
Nimesikia kwenye Radio sidhani kama kuna majeruhi

By the way.... Hivi hii misafara huoni kwamba inapunguza maendeleo ? Mfano hawa jamaa wakija mikoani barabara zinafungwa mpaka Nusu Saa.. Je huko sio kupotezeana muda ? Watu tupo busy na kusimama barabarani eti fulani apite ni mambo yaliyopitwa na wakati na inabidi tuangalie upya hii issue..
 
heshima yako Mkuu,
kwani tz tunajali mda tangu lini?
tunaanza kazi saangapi?
tunkwenda kunywa chai sana ngapi?
then lunch saangapi na kurudi ofisini?
baada ya hpo saa 9 tunrudi nyumbani eti off duty..mmh
sijui hata masaa 5 kama yanfika kwa siku.
Nimesikia kwenye Radio sidhani kama kuna majeruhi

By the way.... Hivi hii misafara huoni kwamba inapunguza maendeleo ? Mfano hawa jamaa wakija mikoani barabara zinafungwa mpaka Nusu Saa.. Je huko sio kupotezeana muda ? Watu tupo busy na kusimama barabarani eti fulani apite ni mambo yaliyopitwa na wakati na inabidi tuangalie upya hii issue..
 
Msafara msafara...wana sifa za kipumbavu kweli!!
Hizo pesa za kusafiri na misafara isiyo na maana wangewekeza kwenye maendeleo ya Mtanzania tungesogea angalau:coffee: robo hatua!!
 
nimepita hapo ruvu, kweli gari ya Usalama wa Taifa aina Ya LandCruiser imeharibika vibaya sana upande wa dereva, inaonyesha dereva ameumia vibaya sana, basi la Moro Best pia limehusika ktk ajali, First Lady ameahirisha safari karudi Dar.....
 
Tuwe na huruma zaidi kuliko ushabiki, vp kama ajali hiyo ingemuhusu ndugu yako wa damu (mama, dada, shangazi, mpwa, baba au kaka) ungetoa comments gani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom