Cantalisia
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 5,222
- 2,929
Habari zenu wapendwa,
Kuna mkaka ni mkazi wa dar ila anafanya kazi mgodini huko mwanza huku anakuja kila baada ya miezi miwili,Alikutana na mdada huko mwanza Mdada anafanya kazi huku dar kule alienda kikazi,wakapeana kontakt, na mawasiliano yakaendelea na wakawa wapenzi.
Kwa kipindi cha miezi minne ya mahusiano yao hakuna aliyekua anajua kwa mwenzie,basi wakapanga jamaa atakapokuja dar wakaoneshane makwao,basi jamaa akarudi dar ijumaa iliyopita km kawa wakakutana na jmosi jamaa kampeleka mdada kwake tabata wakashinda huko wakapika na kupakua.
Jpili mdada naye akampeleka jamaa kwake maeneo ya Sinza hapo ndio balaa lilipoanzia kwan muda wote wakiwa pale yule mkaka alikuwa hana raha mwenzie akamuliza kulikon mbona ulikuja vizuri,yy akamuuliza pale anaishi na nani akamwambia mbona nilishakwambia naishi peke yangu.
Akamwomba amwonyeshe slip yake ya mshahara mdada akapigwa butwaa ila akamwonyesha kumbe kaharibu jamaa kanyanyuka na kuondoka akiwa amekasirika mdada hakumwelewa akambembeleza bila mafanikio,usiku wake jamaa akamtumia bint msg kuwa hamtaki tena,kwa sababu anahisi huyo mdada atamtawala maishani kwa vile kwanza ana kipato kikubwa,na ameshajijenga sana kimaisha,hivyo ni rahisi yeye kutokuwa na sauti ndani ya nyumba,au huyo dada anaweza kumwaga wakati wowote na kutoka na wenye uwezo km yy.
Mpaka ninavyoandika huu uzi jamaa hapokei simu na jana kaondoka kurudi mwanza,dada watu kachanganyikia alishampenda jamaa kupita kiasi hata hajui cha kufanya!
Asa mi nauliza hivi nyie wanaume hivi binti kuwa na kipato kikubwa kuliko mwanaume ni kweli ni tatizo kwenye mahusiano?
Na dada afanyaje ili jamaa aelewe na waendelee?