Killings in custody

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,914
A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

KILLINGS IN CUSTODY

Hit me!

Jab Me!

Make me say I did it.

When you pour Cold water on me,

I’ll Sign the Paper.

This is a two in one Thread

Yes!

Huu ni Uzi wenye mikasa miwili

Naanza kwa kunukuu Barua ya rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi (Kipindi akiwa ni waziri wa mambo ya ndani), aliyomwandikia Rais Julius Nyerere kumtaarifu nia yake ya kujiuzuru baada ya mauaji ya wananchi mikononi mwa polisi Mwanza na shinyanga Mwaka 1977

“Polisi ni chombo cha kulinda amani,mali na maisha ya watu wake. Si chombo cha kuwaua.”

“Pia polisi ni chombo cha kuhifadhi na kudumisha usalama na haki. Si chombo cha kudhulumu, kuonea na kuwatesa wananchi wale wale wanaogharamia kukiweka”

Barua inaendelea

“Kwa bahati mbaya,maovu kama haya ndiyo haswa yalitendwa na vyombo vya serikali huko mikoa ya Shinyanga na Mwanza”

Mwinyi akaendelea

“Kijinai, mimi binafsi nisingehusika kwani sikushiriki wala sikushauri, Sikuagiza wala kuelekeza mambo yale yafanywe kama hivyo yalivyofanywa”

Mwinyi akaonyesha uungwana

“Hata hivyo,kisiasa nakiri kuwa nahusika. Siwezi kukwepa kwa sababu dhamana yangu ya uwaziri inaambatana na wajibu unaonitaka nijue yanayotendeka wizarani na pia niweze kudhibiti na kuhakikisha mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi.”

Mwinyi akanukuu msaafu

“Msaafu unatuusia kwa kusema “WALA HATABEBA MZIGO WA MWINGINE”

“Kisiasa MZIGO HUU NI WANGU NA NAKUBALI KUUBEBA KWANI HAKUNA MWINGINE WA KUUBEBA”

Then Mwinyi threw the towel

“Kwa hiyo,Mwalimu nakuomba mambo matatu.Kwanza naomba radhi mimi nafsi yangu na pia naomba radhi kwa niaba ya askari wote wema walipo. Pili naomba vilevile uelewe sehemu yangu katika kosa hili.Tatu kwa fedheha hii,naomba unikubalie kujiuzuru”.

Mwinyi akawa amemaliza barua yake.

Naiita barua hii kama barua ya kiungwana na ya Kihistoria.

Ni barua pekee ya Kiongozi wa Taifa letu aliyejiuzuru huku akikubali makosa bila kumtupia mzigo mtu mwingine.

Barua hiyo ilifuatiwa na kustaafishwa kwa manufaa ya umma, Director wa Tiss, Mzena, IGP, Pundugu, na maofisa kibao.

Mtiti huu ukahamia Mwanza kulikotokea vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, Masanja Makhula Mazengenuka na Issack Mwanamkoboko.

RC wa Mwanza, Peter Kisumo,
RSO Andrew Mayalla, DSO Ihuya, RPC Mkwawa, na OCD, wakastaafishwa kwa manufaa ya umma, kisha wakapandishwa kizimbani kwa Kesi ya Mauaji Mwanza. Washitakiwa wote walikutwa na hatia, isipokuwa Andrew Mayalla aliyekuwa akitetewa na wakili Murtaza Lakha.

Je Tangu mwaka 1977 mpaka leo, ni matukio mangapi yametukia kwa watu kuuwawa wakiwa mikononi mwa polisi?

Je, alishawajibika kiongozi yeyote wa kisiasa?

Alishawajibishwa kiongozi yeyote kwa ngazi ya RPC, RSO, RCO nk?

Sasa nakukaribisha katika uzi huu kuyaangazia matukio mapya

Sheria inasema

“When a person in in trusted as a custodian of a suspect or convict. He or she will be liable of anything that might befall to that suspect /Convict”

Kwa tafsiri isiyo rasmi maneno hayo yanamaanisha”

“Mtu aliyeaminiwa kumshikilia mahabusu au mfungwa atawajibika kwa lolote litakalomtokea mahabusu au mfungwa wakati yuko chini ya uangalizi wake”

Tuendelee

Nianze na mkasa wa kwanza

Mkuu wa gereza la Liwale mkoani Lindi alikuwa amesafiri kikazi kwenda mkoani Dar Es salaam.

Huko nyuma katika gereza lake kukawa kuna kazi ya kuvuna mahindi katika shamba la gereza.

Wafungwa wakifanya kazi hiyo chini ya usimamizi wa askari Magereza

Baada ya kuvuna ikafata kazi ya kusomba mahindi hayo kupeleka kwenye ghala la gereza na mengine yalipaswa kupelekwa nyumbani kwa Bwana jela ACP Gilbert Sindani ambaye kwa wakati huo alikuwa safarini Dar es salaam.

Mkuu wa gereza akiwa bado yuko Dar es salaam akapigiwa simu na “vichomi” wake kuwa katika mahindi yake yaliyovunwa kuna mengine yameibiwa.

Mkuu wa gereza akarudi Liwale.

Akamuita msaidizi wake na kumhoji juu ya taarifa mahindi yake kuibiwa.

Msaidizi akakubali ni kweli tuhuma hizi amezipata lakini bado hajazichunguza hivyo bado hakuna yeyote aliyetuhuniwa kuiba mahindi au kupokea mahindi ya wizi.

Taarifa hii haikumridhisha mkuu wa gereza.

Kesho yake tarehe 8 june 2022 Mkuu huyu akawaita Nyampala wa gereza pamoja na “Kiherehere” wake,

Usishangae ndugu msomaji,

Kiherehere ni cheo gerezani na huyu huwa ni mpambe wa Nyampala na muda wowote anaweza kupanda cheo kuwa Nyampala.

Nyampala alikuwa ni mfungwa namba 70/2020 ABDALAH NGATUMBALA

Kiherehere alikuwa ni mfungwa namba 76/2021 SIABA MBONJOLA

Hawa wote waliitwa na mkuu wa gereza na kuhojiwa akiwataka wampe taarifa kamili juu ya wizi wa mahindi yake.

Wawili hawa wakakana kujua lolote.

Baada ya majibu hayo Palepale Mkuu wa gereza akaanza kuwapiga akiwataka wamtaje aliyechukua mahindi na amechukua kiasi gani.

Alipochoka Mkuu wa gereza akawaita askari wawili;

1.SGT.YUSUPH SELEMANI

na

2.CORPORAL FADHILI MAFOWADI

wamsaidie kuwapiga hadi watakapotaja wezi

Kipigo hicho hakikuwafurahisha askari wengine ambao waliwazuia Sajenti Yusuph na Koplo Fadhili wasiendelee kuwapiga, wakihoji iwapo wana uhakika kweli kuna wizi umetokea?

Wengi waliamini kuwa uchache wa mavuno ya mwaka huu ndiyo sababu ya kudhani kwamba wizi umefanyika.

Mkuu wa gereza alipobaini kuwa wafungwa wale wameumizwa sana, akaondoka.

Muda mfupi baadaye akarudi na kuwapakia kwenye gari kuwapeleka hospitalini hospitali ya wilaya Liwale.

Pale hospitali kwa kuwa walipelekwa wakiwa na hali mbaya madaktari wakashauri kwanza wapatiwe Form ya polisi namba 3 PF3 ndio waendelee na matimabu.

Wakati haya yanaendelea mmoja ya Wagonjwa alimfahamu Nyampala Ngatumbara

Akampigia simu ndugu yake aitwaye SAID MOHAMED

Baadaye madaktari wakabaini kuwa tayari Nyampala Ngatumbala alikuwa amekwisha kufariki dunia.

Na kwa kuwa hali ya kiherehere ilizidi kuwa mbaya wakamwandikia rufaa akimbizwe hospitali ya Mifupa Moi

Ndugu wa Nyampala akiambatana na diwani wao Nassoro wakaenda hospitali ya liwale lakini wakazuiwa kumuona mgonjwa wao (marehemu) bila ya kibali cha mkuu wa gereza.

Wakampigia simu Mkuu wa wilaya aliyewataka waende ofisini kwake.

Walipofika Mkuu wa wilaya akawaeleza kuwa tayari ana taarifa hizo na kwamba ameshawasiliana na mkuu wa Mkoa ili atume timu kuchunguza sakata hilo.

Kesho yake Mkuu wa gereza akawapigia simu diwani na ndugu wa marehemu waende Kipute (liliko gereza la Liwale)

Walipoenda wakamkuta Mkuu wa gereza akiwa na Mkuu wa gereza wa mkoa wa Lindi (RPO)FELSCHEME MASSAWE

Mbele ya RPO mkuu wa gereza akawaeleza kuwa ndugu yao amefariki kutokana na maradhi ya shinikizo la damu.

Ndugu hawakuridhika na maelezo hayo ambapo wakaomba postmortem ifanyike

Ripoti ya daktari ikabainisha kuwa marehemu alikuwa kavunjika mguu mmoja, mshipa wa nyuma wa mguu mwingine umechanika huku damu ikiwa imeganda maeneo ya mikononi.

Ripoti ikahitimisha kuwa marehemu alifariki kwa kipigo na sio shinikizo la damu.

Mfungwa huyo aliyeuwawa alikuwa akitumikia kifungo cha miaka mitano tu jela baada ya kukutwa na hatia ya kukamatwa na nyama pori ya nguruwe.

Lakini askari hao wakaamua kubadilisha adhabu yake kugeuka kuwa ya kifo.

Katika nusa nusa ndipo ikabainika kuwa Mfungwa huyu aliuwawa kwa bahati mbaya tu Wakati watu wakitaka kutekeleza visasi vyao.

Nanukuu

“Kuna watu ambao Mkuu wa Gereza hapatani nao. Kuna askari anawatafutia sababu awafukuzishe kazi. Ni bahati mbaya kuwa askari hao hawakutajwa na Marehemu Ngatumbara na mwenzake,”

Quoted from a source within, under anonymity conditions

Hili sio tukio la kwanza kwa mfungwa kufia mikononi mwa askari Magereza.

Mwaka 2010 Mfungwa namba 214 Khassim Kumchaya aliuwawa na askari wanne mwenye namba B 5147 WDR Swalehe, A 854 Sajenti Mohamed, 4264 Sajenti Jason aka Machozi na askari mwenye namba A 5294 Sajenti Shaibu.

Mfungwa huyu aliuwawa katika gereza la Lilungu mkoani Mtwara.

Mwaka 2019 askari wa gereza la Kilombero walimuua mfungwa Basiri Makungu.

Mnahisi nimemaliza?

Hapana ndio naanza!

Sasa Nageukia tukio la mauaji ya Kijana mfanyabiashara wa madini aliyeuwawa na Polisi mkoani Mtwara.

Ilikuwa hivi;

Mussa Hamisi alikuwa akijishughurisha na biashara ndogo ndogo ikiwemo kuuza mitumba katika kijiji cha Luponda wilayani Nachingwea mkoani Lindi.

Baadae Mussa akaondoka kijijini Luponda Kwenda kwenye machimbo ya dhahabu kijiji cha Mpiruka B hukohuko Nachingwea.

Mungu amtupi mja wake na penye nia pana njia.

Mwezi october 2021 Mussa akapata bahati ya kengewa baada ya shimo lao kutema.

Baada ya kusafisha dhahabu musa akapata dhahabu ya kutosha kubadili maisha yake.

Madalali wakamuunganisha Mussa na mnunuzi wa dhahabu yake raia wa kigeni

Kweli biashara ikafanyika!

Mussa akiibuka na kiasi kikubwa cha pesa ambayo hakupata kuiota.

Naam!

Alilipwa kiasi kikubwa cha dola za Kimarekani yapata 31,500 usd

Ukikileta kikwetu kwetu ni sawa na milioni 74 na ushee.

Musa akaondoka machimboni na kurudi kijijini kwao Luponda.

Kule akamnunulia mama yake Battery Solar na Inverter

Kichwani akipanga kupabadilisha kabisa pale nyumbani kwao.

Akaficha nusu ya pesa ile pale nyumbani.

Akaondoka na nusu ya pesa kwenda kuibadilisha Mtwara mjini.

Alipofika Mtwara akamjulisha mjomba wake aitwaye SALUM NG’OMBO kuwa yuko Mtwara.

Huyu mjomba wake alikuwa ni dalali wa kwenye mabasi akifanyia kazi yake kituo cha mabasi MKANALEDI pale pale Mtwara Mjini.

Mussa alamjuza sababu ya ujio wake na akamuomba amsindikize kwenda Bank

Wakaona benki ya BMN (code) ndiyo ingefaa kutumika kubadilisha Biden kuwa Samia.

Mussa akazama BMN bank Mtwara

Pale Bank akahudumiwa na mdada flani hivi

Biden wakageuka Samia kama milioni 30 hivi

Baada ya kubadili yule dada akamuuliza anaishi wapi?

Mussa akasema kuwa anaishi Nachingwea na anapanga kuondoka siku ile ile.

Mdada akamshauri kuwa sio salama kusafiri na pesa ile kuwa kuwa muda umeenda.

Akamshauri aende nyumba ya wageni aliyomtajia ili kesho mapema arudi Nachingwea

Mussa Akakubali kiroho safi

Jioni Mussa akatoka kujivinjari na akaenda kwenye Club maarufu pale Mtwara Kama Triple V

Sasa hapa ndipo ndugu msomaji inabidi nirudie kauli moja ambayo niliwahi kumnukuu Kachero mmoja wakati “tunabadilishana kahawa”

Nanukuu

“Makachero huwa tunavutiwa sana na mtu anayekunywa “bia msitu” awapo bar... Sio kwamba tunamuonea wivu.. Hapana! Bali huwa ni msingi mkubwa wa kuanza kuwa suspicious kutaka kujua anafanya kazi gani inayompa kipato cha kunywa “bia msitu””.

Hapa bia msitu anamaanisha ile tabia ya kuagiza vinywaji vingi kwa wakati mmoja na kutapanya kwenye meza huku ukitoa offer kwa wanaokuzunguka”

Ndicho alichokifanya Mussa pale Club

This was his grave mistake

What a coincidence!

Ilitokea kuwa pale Club yule mhudumu wa Bank aliyemhudumia Mussa naye alikuwepo.

Naam alikuwepo pale akipata kinywaji na jamaa yake mmoja ambaye ni “njagu”

Njagu huyu alikuwa meza moja na yule mhudumu pamoja na manjagu wenzake.

Hivyo wakati Mussa anamwagilia Moyo kwa “bia msitu” na wakati manjagu wale wanavutiwa naye walianza kumjadili mbele ya yule Mhudumu.

Mhudumu bila kujua akasema Mussa ana kisu cha kutakata kwani ni yeye alibadili pesa zake.

Akasema anatokea Nachingwea na Lodge aliyofikia

Naam!

Mhudumu akawaambia Mussa amefikia SADINA hotel

Mhudumu aliyasema yale “in good faith” bila kujua kama anauza ramani ya vita kwa wale manjagu.

Mussa akaondoka muda ukiwa umeenda sana kurudi lodge kwake.

Bila ya kujua tayari kuna manjagu yamemuundia mkia.

Majira ya saa 7 kwenda saa 8 usiku Mussa akashangaa mlango wa chumba chake unagongwa kwa fujo.

Alipofungua wakaingia watu waliojitambulisha kuwa wao ni polisi na yuko chini ya ulinzi.

Alipouliza kosa lake hakutajiwa akaambiwa anahitajika kituoni.

Manjagu wakasachi chumba chake lakini wakaishia kukuta milioni 2.5 pekee.

Hii haikuwaridhisha!

Wao walikuwa na story nzima kutoka kwa mhudumu wa benki kuwa Mussa kaondoka na kiasi gani.

Walikuwa wanajua pia kuwa Mussa alibadili kiasi tu cha pesa kati ya pesa aliyokuwa nayo.

Mussa alipohojiwa kilipo kiasi kingine alikana kabisa kuwa na pesa nyingine.

Mussa seemed to be a very brave young boy.

He might have hidden the rest of the “package” somewhere within his room.

Mussa alipokaidi akachukuliwa na kupelekwa korokoroni Mtwara Central police.

Sasa unajua mtu anapoingia kituoni ni lazima aandikwe kwenye Detention Register kuwa anaingia ndani kwa kosa gani.

Askari wale wakaandika kuwa Mussa anashikiliwa kwa kosa la Wizi wa pikipiki.

Musa akalala korokoroni siku hiyo.

Sasa msomaji inabidi uelewe kitu kimoja,

Kulala korokoroni usiku mpaka asubuhi sio issue

Issue ni kuwa ikifika kesho yake asubuhi mpaka mchana swala lako linakuwa nje ya waliokukamata.

Swala linaanza kupata “nzi” wengi kwani mwenye kituo “OCS” ni lazima ajue umeingiaje.

Ukiacha “OCS” mwingine ambaye ni lazima ajue ni mkuu wa upelelezi “OC- CID” na lazima mkuu wa polisi wa wilaya OCD lazima ajue idadi ya mahabusu wake wilayani ili aweze kutoa ripoti kwenye “morning brief” kwa mkuu wa wilaya ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati ya usalama wilayani.

So mpaka inafika kesho yake asubuhi Swala la Mussa lazima tayari lilishafika kwenye Meza za vigogo wa polisi niliowataja.

(Save for the DC kwani yeye anaweza kupewa “fabricated infos)

Lakini niliowataja kwa nyadhifa zao ni lazima walipata taarifa toka kwa wakamataji na Mussa.

Ni kwa sababu Mussa asingeendelea kukaa ndani bila maelezo yake kuchukuliwa.

Na ni lazima Mussa alijitoa kwenye kesi ya wizi wa Pikipiki na akaeleza uhalisia kuwa yeye ni nani, anatokea wapi, na kafata nini Mtwara hadi kuishia korokoroni.

Tuendelee

So wale wakamataji wakawashirikisha wakubwa wao kuwa issue ya Mussa inaweza kuwafanya waibuke na “donge nono”

Swala hili likawavutia wakubwa wale.

Wakubwa wakaona wa “adjust” vipimo vya kumuhoji Mussa

Then they started to “forgive” Mussa mpaka aseme pesa nyingine ilipo.

After a severe “forgiveness” Mussa akataja alipoficha pesa nyingine SADINA lodge.

Manjagu walipoenda kweli wakakuta pesa ikiwa imefichwa kwenye dari ya choo kwenye chumba alichokikodi Mussa.

What a Bingo!

Sasa manjagu wale wakaanza kuamini Story ya yule mfanyakazi wa Bank kuwa Mussa alimweleza kuwa anabadili nusu na pesa na nyingine angeenda kubadili sometimes afterwards.

Sasa bingo ikawa utamu kolea!

Wakapata hamu kwenda kuzifata Nachingwea.

Lakini kikaibuka kikwazo!

Yes kikwazo!

Wanaenda Vipi kufanya kazi wilaya nyingine huku wao wanatokea wilaya nyingine?

Wakaona hiyo haiwezekani without prior notice of RCO na RCIO

Ndio!

Wasingeweza kwenda bila kumjulisha mkuu wa Upelezi na Mkuu wa intelejensia wa Mkoa.

“Nzi” wakaongezeka kwenye chain

Naam!

Ilibidi hawa nao wafahamu swala la Mussa kinaga ubaga kama kweli wanazitaka zile pesa.

Baada ya watu hawa kuwekwa sawa na baada ya mussa kuwa ametepeta wakapiga simu Nachingwea.

Namba ya simu wasingeipata kokote zaidi ya kuitoa kwa Mussa.

Namba ile ilikuwa ni ya Mama yake Mussa

Ndugu Msomaji, nakurudisha nyuma kidogo

Yule mjomba wake Mussa anayefanya kazi kituo cha mabasi cha MKANALEDI pale Mtwara alishangaa ukimya wa mpwa wake tangu jana yake.

Huku akiwa hapatikani kwenye simu.

Katika jitihada za kumtafuta ndio akawa ameenda hadi kituo cha polisi kumuulizia kama labda alikamatwa kwa shida yoyote.

Hisia zake zikazaa matunda.

Akabaini Mussa yuko pale kituoni kwa siku mbili nzima.

Akaambiwa kesi ya Mussa ni nzito ya wizi wa pikipiki so hawezi kumuona.

Kipindi hicho namba ya Mama wa Mussa imeshachukuliwa.

Yule mjomba wake akamtafuta mzee mmoja maarufu kwa jina la Ng’itu asaidie kumnusuru mpwa wake

Kweli yule mzee akampambania Musa lakini huku akifata anayoelekezwa na wale Manjagu.

Siku ya tatu toka Mussa ashikiliwe Manjagu wakampa yule Mzee namba ya Mama Mussa aitwaye Hawa Ally ili aipige na walishamwambia cha kusema.

Yule mzee akampa maelezo mama yule kuwa Mussa amekamatwa na inahitajika shilingi laki tatu kwa ajili ya dhamana.

Mama wa watu na mmewe(Baba wa Mussa wa kufikia) wakajichanga wakatuma ile laki tatu ili kumsaidia Mussa apate dhamana.

Hawakuuliza sababu ya kukamatwa kwake

Wao walichojali ni mtoto wao awe huru.

Wakamnunulia Mussa Uhuru tunaoambiwa ulishapatikana mwaka 1961

Let’s pause at this juncture ndugu msomaji.

just imagine,

Hawa manjagu tayari walishapata pesa nyingi tu kutoka kwa Mussa pale Mtwara mjini.

Lakini hawakuridhika!

Wakamkamua pia mama wa watu shilingi laki tatu.

With due respect, these cops were animals.

Tuendelee

So baada ya muda Mzee yuleyule akapiga simu na kumwambia kuwa Mussa ameshaachiwa.

Lakini,

Mzee yule akamwambia Mama Mussa kuwa kwa mujibu wa maelezo ya Mussa ameeleza kuwa ana pesa nyingine kaacha kule nyumbani so polisi wanaenda kuzifata.

Baada ya simu ile baba wa kambo wa Mussa akaona ule ni ushenzi,

Akaingia kwenye chumba cha Mussa na kuanza kusaka pesa zile popote zilipo.

Nia yake ilikuwa azichukue azifiche ili polisi wakifika wasizikute.

Katika msako wake baba yule akabahatisha kuzikuta pesa zile kwenye begi la nguo za Mussa.

Zilikuwa bideni zipatazo 31,500

Mzee akahamisha pesa zile na kuzificha anakopajua.

Mida ya jioni Polisi kutoka Mtwara wakafika na gari lao Nachingwea nyumbani kwa kina Mussa.

Naam!

Walikuwa wameambatana na Mussa akiwa kapigwa pingu chini ya ulinzi mkali kama wamekamata gaidi hatari.

Ukiwaona unaweza kusema wako serious kumbe wako kwenye armed robbery.

The people we entrusted with our lives and properties, were now conspiring and executing armed robbery shamelessly in a broad daylight.

Mussa akashushwa garini

Wazazi wake wakishangaa kulikoni

Manjagu wale hawakuwa na maneno mengi wakawataka wazazi wale wajitambulishe.

Wazazi wale wakasema wao ndio baba na mama wa “gaidi” aliyepo mbele yao.

Funny but not funny

Manjagu wake wakasema wako pale kwenye mission moja tu ya kuhakikisha Mussa anawaonyesha alikoacha fedha nyingine pale nyumbani.

Nafikiri manjagu wale walikuwa kwenye zoezi la malezi wakiwasaidia wazazi wake kumlea Mussa.

Labda waliona kwa umri wake hapaswi kuwa na fedha zile kwani zingeweza kumharibu kwenye makuzi.

Kweli Mussa alikuwa Mdogo,

Mussa alizaliwa mwaka 1996

Basi bwana Mussa akaingia kwenye chumba chake huku akiwa chini ya ulinzi.

Akaongoza moja kwa moja kwenye begi lake la nguo alikokuwa kaacha pesa zile.

Musa akabaki na mshangao kama anasoma talaka baada ya kuzikosa pesa zile!

Akawaambia manjagu kuwa aliziacha pale lakini anashangaa hazipo.

Wale manjagu wenye njaa kama wametoa mimba hawakutaka kuelewa lolote.

Njagu mmoja akamulekezea Mussa bunduki kisogoni na kumwambia asilete mzaha kwani atakuwa anaiweka roho yake kwenye kamali kwa dau dogo.

Sura za manjagu wale zilikuwa mbali kabisa na masikhara na yote haya yalifanyika huku wazazi wa Mussa wakishuudia.

Uchungu wa mwana aujuaye Mzazi!

Mama Mussa akapiga magoti kuwasihi manjagu wale wasimzuru mwanae.

Mama akaanza kuropoka huku akimwambia mmewe awaonyeshe pesa ziliko.

Akasema mmewe ndio alizihamisha ili kunusuru nafsi ya mwanae.

Dear reader,

Despite the fact that it is me who is jotting down this thread, this captivating and hollow scene didn’t exonerate me from sobbing.

Naomba nimnukuu Mama Mussa

“Wakamuuliza hela umeweka wapi, akasema kwenye begi, wakamuonyesha bunduki, maana walikuja na bunduki. Kwa hiyo kwa kuona mimi nina uchungu wa mtoto wasimpige wasimuue wakati mimi niko pale, ndipo nikamwambia (mume wangu) katoe hela uwape. Ndipo wakapewa, wakazichukua wakawa wanazihesabu, mimi nilikuwa nalia kwa sababu ya uchungu, mtoto ametiwa pingu.”

Polisi walipozipata pesa zile hawakuridhika.

Wakaanza kuangalia chochote chenye thamani pale nyumbani kwa kina Mussa.

Wakaona battery ya solar na Inveter ndio vyenye thamani navyo wakavibeba.

Vitu hivi Mussa alikuwa amemnunulia mama yake baada tu ya kupata pesa zake.

Lakini navyo vikabebwa.

Njaa! Njaa! Njaa!

Kama watoto wa Mamba.

Si unajua mtoto wa mamba hanyonyi?

Baada ya kupata bingo kwa mara ya pili manjagu wale wakamrudisha Mussa kwenye gari lao kisha wakamchukua na baba yake aliyekuwa ameficha pesa zile wakisema anaenda kuisaidia polisi wakaenda nao Kituo cha polisi Nachingwea.

Pale Kituoni wakamwacha yule mzee arudi kijijini bila hata nauli.

Hata kazi ya kuisaidia polisi hawakumpa tena kama walivyoahidi.

Kisha gari ikaunganisha mpaka Kituo cha polisi Mtwara wakiwa na Mussa.

Pale kituoni Mtwara manjagu wakamwambia Mussa kosa lake ni kukutwa na Dola za Marekani.

Lakini wakamkataza kutangaza suala hilo.

Badala yake wakampa kesi ya wizi wa pikipiki.

Wakamruhusu aondoke na wakampatia laki Moja kama “chenji” ya kukutwa na kosa la kumiliki dola wakati yeye ni mmatumbi.

Akaambiwe asionekane pale mjini na arudi tarehe 6 Nov kuangalia status ya kesi yake.

Mussa akarudi Nachingwea akiwa na laki moja tu akiwa kapauka.

Siku hazigandi,
 
Part 2

Tarehe 6 Novemba ikawadia, Mussa akarudi kituoni pale lakini akaishia kufukuzwa na akaambiwa kama hajitaki arudi tena.

Mussa akarudi tena Nachingwea.

Namnukuu tena mama yake;

“Alipotoka nyumbani, yule mtoto akaanza kuumwa, aliumwa sana, nimezunguka naye hospitalini ili atulie. Hospitali wakasema mara BP (shinikizo la damu), mara sijui UTI, mara typhoid. Nilipokwenda kwa waganga wa kienyeji wakasema ni BP kwa kufikiria vitu alivyonyang’anywa,”.

His mother did everything a mother is obligated to do to his son unfruitful.

Musa akawa ananyong’onyea kwa dhuluma aliyofanyiwa.

Yule Mzee aliyekuwa anamsaidia wakati yuko kituoni akawapingia simu wazazi wa Mussa na kuwashauri Mussa atumie mwanasheria kupata haki zake.

Mussa akapata mwanasheria wa Lindi mjini.

Lakini siku aliyopanga kwenda kwa mwanasheria, wale polisi wakampigia simu aende Kituoni Mtwara akachukue vitu vyake.

Mussa akamjulisha habari hizi yule mwanasheria.

Mwanasheria akamshauri asiende huko bila kupitia Lindi mjini akachukue barua ya kisheria aliyokuwa ameiandaa awapelekee.

Musaa na Mwanasheria wake hawakujua mipango waliyokuwa wamepanga watu hawa.

Polisi hawa hawakuwa na nia ya kumrudishia Mussa pesa zake kama walivyojinadi.

Ni kwamba siku zote tangu Mussa alipoonyesha amenuia kurudishiwa pesa zake, Manjagu wale wakaanza kumuona Mussa ni kama kijiwe kidogo kilichomo ndani ya kiatu hivyo kumsumbua aliyekivaa.

Ilikuwa ni lazima kijiwe hiki kitolewe kwenye kiatu kama Mvaaji anataka kuendelea kuvaa kiatu kile.

Ukasukwa mpango kabambe wa kuhakikisha Mussa hatasumbua tena.

Naam!

Mussa kuendelea kuwa hai ilikuwa inawaweka tumbo juu wale wote waliokuwa kwenye Chain.

Hasa wale wakubwa!

Ndipo yakahitajika maoni ya daktari.

Kwamba “what injection can be administered to human body that can cause rapid death?

Yes that was the opinion these culprits were in search off.

Wakajikuta ni lazima hapa mtu mwingine aingie kwenye chain.

Huyu si mwingine bali mganga mkuu wa zahanati ya Majangu pale Mtwara Inspector John Msuya Mganga.

Infact baada ya mtaalamu huyu kuingizwa kwenye deal na kuombwa opinion yake juu ya hilo, alitoa presentation nzuri sana.

Daktari akasema ipo dawa ambayo huwa inatumia kwa ajili ya Euthanasia.

Neno hili lisikuchanganye msomaji

Tupo hapa kwa ajili ya kujifunza na kuongeza maarifa.

Euthanasia ni kifo cha hiyari. Kwenye mataifa ya wenzetu wameruhusu mtu kama kuishi kwake duniani ni mateso basi anaweza kuuwawa kwa hiyari ili apumzike.

Watu wenye magonjwa mfano Alzeimers huteseka sana maishani mwao kama ugonjwa umefikia kuwa critical. Mara nyingi ugonjwa huu huwapata wazee kwa kuanza kuzalishwa protini bandia (Neurofibrillary Tangles) ndani ya seli za ubongo.

Wagonjwa hawa hupoteza kumbukumbu. Imagine mzazi anamsahau mwanae au jirani yake, akitoka kwenda matembezi anasahau nyumbani kwake na kupotea.

Ili kuwahepushia mateso haya wenzetu huwapumzisha wagonjwa hawa kwa Euthanasia baada ya kujaza ombi la kisheria.

Sasa dawa inayoumika kwanza humpoteza mgonjwa fahamu, husimamisha upumuaji na mwisho husababisha cardiac arrhythmia ambapo mfumo wa umeme wa moyo hupata hitilafu na kusababisha mapigo ya moyo yabadilike ama kwa kupanda au kushuka kuliko kawaida.

Ukifikia hatua hii hiyo walatini wanaita Adios Amigo yaani kwaheri rafiki.

Actually dawa hii anayopewa mtu wa kufa kwa hiyari ni mchanganyiko (cocktail) ya dawa tatu ambazo ni Pavulon yenye kazi ya kupalarize misuli hivyo kusimamisha upumuaji , Potassium Chloride inayosimamisha moyo na Midazolam ambayo inatia ganzi na kulaza usingizi(sedation)

So ule msemo wa Kill me softly hapa ndio unapata matumizi yake kwani unakufa kwa raha kabisa huku unabembelezwa na usingizi.

Haya niliyoyaeleza hapa inawezekana yalikuwa ni sehemu ya presentation ya yule daktari mkuu wa zahanati ya polisi Mtwara.

Na Inaonekana presentation hii ilikuwa imepita bila kupingwa kwa ajili ya utekelezaji na watu wale.

Ndio Mussa akapigiwa simu akafate pesa zake.

Mussa akiwa hana fununu zozote za mipango iliyokuwa imepangwa dhidi yake akajaa tunduni.

Yes!

The bird was in its nest

Mussa akafata barua kwa Mwanasheria wake Lindi.

Tarehe 5 January Mussa Akaenda Mtwara ambapo, akampitia mjomba wake pale stand ya mkoa Mkanaledi, wakaongozana kwenda polisi kudai vyao.

Walipofika pale Mussa akaingizwa ndani ya kituo na Mjomba wake akaambiwa amsubiri nje kwani wanafanya mahojiano na Mussa.

Mjomba wake alijaribu kubisha lakini akadhibitiwa akabaki nje.

Hii ndiyo ilikuwa mara ya mwisho Mussa kuonekana tena.

Alipotelea ndani ya kituo kama sindano ndogo inavyoweza kupotea kama mazingaombwe.

Mussa akaendelea kukaa ndani kwa Muda mrefu bila kutoka huku mjomba wake akimsubiri.

Baadaye kupitia namba ya simu ya Mussa, mjomba wake akapokea ujumbe mfupi kwenye simu yake ukisema:

“Wewe nenda mimi nakuja”

Lakini taa za full zilibaini baadae kuwa ujumbe ule haukutumwa na Mussa mwenyewe.

Ujumbe ule ni lazima ulitumwa na mmoja wa nyamela ndani ya gwanda za kinjagu ili mjomba yule asilete kiwingu kwenye mipango yao ya kumpa Euthanasia cocktail Mussa.

Ilikuwa imeshafika jioni.

Baadae jua likaona aibu kushuhudia kifuatacho.

Huo ulikuwa ni muda sahii wa kufanya Mussa awe mahabusu aliyezidiwa hivyo apelekwe zahanati ya polisi ili “kutibiwa”

Ikafanyika hivyo!

Lakini hakutakiwa kufika zahanati, hiyo ilikuwa ni njia tu ya kumtoa pale kuhadaa polisi wasiojua lolote.

Kule zahanati daktari angejua angecheza vipi na swala la Mgonjwa kutofika.

They were acting so blindly without knowing how to hide the traces.

Then in between Mussa akawa injectect Euthanasia Cocktail.

Mwili wake ukasafirisha usiku huo huo na kwenda kutupwa kwenye pori lililoko kijiji cha Hiari nje kidogo ya Mtwara mjini.

Siku ya pili, mjomba alirudi polisi kujua hasa mpwa wake alikopelekwa, lakini hakupata majibu sahihi.

Hali hii ilipelekea kutoa taarifa NACHINGWEA na hapo familia ikaenda kwa Mkuu wa wilaya ya NACHINGWEA ili wapatiwe msaada wa kumpata ndugu yao huyo.

Taarifa zilifika mbali zaidi ambapo sasa uchunguzi ulifanyika kubaini nini tatizo halisi.

Sasa togwa likawa tayari limeingia nzi

Mkuu wa wilaya Nachingwea akawasiliana na mkuu mwezake wa wilaya ya Mtwara.

Mkuu huyu wa wilaya Mtwara sasa ndio akawa ameanza kupata fununu juu ya mkasa wa Mussa ambazo awali alikuwa akifichwa.

Na zaidi ya yote Kilichomshtua mkuu wa wilaya Mtwara ni alipoambiwa kuwa askari wake walivuka mipaka ya wilaya yao na kwenda kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha Nachingwea.

Mkuu huyu wa wilaya akaanza kuwasha taa za full kwani sasa swala hili lilishaonyesha picha ya wakubwa wa polisi ndani ya mkoa kulijua jambo hili.

Kuna kitu kimoja naomba mkijue kuhusu Mtwara.

Mkoa wa mtwara kwenye makao yake makuu ambayo ni wilaya ya Mtwara, tunaweza kuiita wilaya hii kama wilaya ya Kijeshi.

Mkurugenzi wa wilaya ni kanali wa JWTZ ndugu Michael Mwaigobeko.

Pia mkuu wa mkoa ambaye naye yuko pale pale Mtwara ni Brigedia Jenerali wa JWTZ ndugu Marco Gaguti

Mkuu wa wilaya akaona amshitikishe swala lile Mkurugenzi wake ili wamalizane kijeshi.

Likawa ni swala dogo tu kwa Mkurugenzi huyu kumtaarifu afande wake mkuu wa mkoa kwani yeye ndio mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa.

Naam!

Sasa kiraka kilikuwa kimeshang’olewa kwenye jeans ya bishoo tena bishoo matata.

Zile habari za kulindana kuzima hili sakata zikawa dhahili zimeanza kwenda Mrama.

Nafikiri damu ya Mussa ilikuwa bado ikilalamika kwa dhuruma iliyofanyiwa kule kwenye pori la Hiyari ulipofukiwa mwili wake.

Mkumbuke kitu kimoja,

Wakati Mussa akiwa ameshanyang’anywa pesa na kuachiwa, akiwa kwao Nachingwea (wakati anaumwa) alishaenda kwa mganga wa kienyeji na kusomewa dua.

Aliyafanya haya yote ili waliomfanyia haya waweze kumuita wenyewe na kumrudishia pesa yake.

Huko kwenye dua akawa anayataja hadi majina ya waliomfanyia ubaya.

Kweli baada ya muda ndio kweli Mussa akawa ameitwa.

Naye akaamini inawezekana zile dua ndio zimetoa majibu.

Siwezi kuingia kwa undani lakini labda inawezekana pia ni dua hizi zilizofanya swala la Mussa lisizimike.

Hapa najiuliza swali,

Je ni wangapi wanaweza wakawa wamepotezwa kwa njia hizi na wakakosa mtu wa kuwasemea?

Tuendelee

Sasa likawa ni swala dogo tu kwa Mkuu wa mkoa Brigade general Gaguti kumtaka RPC ampe majibu ya swala la Mussa haraka iwezekanavyo.

Yakatoka na maelekezo ya kuwatia ndani na kuwahoji wote waliokuwa kwenye Chain.

Likafatia tukio la kama movie inayoanzia mwishoni na kuendelea na matukio ya nyuma (flashback)

Swali la kwanza aliloulizwa RPC ni nani alitoa kibali cha askari kwenda Nachingwea.

Hapa akatajwa mkuu wa Intelejensia wa mkoa (RCIO) Assistant Superintendent Nicholaus Kisinza pamoja na Mkuu wa upelelezi wilaya ya Mtwara Superintendent Gilbet Kalanje.
 
Part 3

Huyu naye alipohojiwa akadai alitoa kibali kile baada ya kupewa taarifa fiche na Inspector Shiraz Makupa kuwa kuna kijana wanayehisi anamiliki pesa ambayo inashukiwa kuwa ni zao la uharifu na pesa hizo zipo Nachingwea. Ndipo akatoa idhini askari waende.

Inspector Shiraz Makupa ikabidi naye ahojiwe yeye taarifa ya pesa hizo katoa wapi?

Inspector akasema alipewa taarifa zile na askari aliyemkamata Mussa Usiku akiwa hotelini kwake. Askari huyu alikuwa na cheo cha Corporal aitwaye SALIMU JUMA MBALU

Naam!

Things were now unfolding themselves.

Ikajulikana jinsi Mussa alivyokamatwa na kulala ndani tangu mwezi October mwaka jana.

Ushiriki wa mkuu wa Kituo OCS ukabainika. Hivyo mkuu wa kituo ASP Charles Onyago akaitwa mbele ya kiti cha kunesa nesa cha Brigedia Jenerali Gaguti.

Issue hapa ilikuwa ni MUSSA YUKO WAPI?

Wakati kamata kamata hii imeshika hatamu, Mhusika mmoja alianza kutazama swala lile kwa jicho la tatu.

Tuseme sio mpaka kamata kamata ilipoanza.

Hapana!

Huyu alikuwa ameshaanza kukosa usingizi kwa mambo ambayo aliyashuhudia usiku wa tarehe 5 January.

Huyu hakuwa mwingine bali ni ASP GREYSON MAHEMBE
 
Sasa huyu mkuu wa upeleleziwilaya ya Mtwara ndiye wananchi wengi walikuww wanamchanganya na yule askari aliyewahi kumtolea bastora Waziri Nape Nnahuye maarufu kwa jina la Kisanduku.

Ukweli ni kwamba hawa ni watu wawili tofauti na si kama ilivyowahi kuripotiwa na gazeti la Mwananchi.
IMG-20221023-WA0150.jpg
IMG-20221023-WA0147.jpg
 
Part 4
Huyu naye alipohojiwa akadai alitoa kibali kile baada ya kupewa taarifa fiche na Inspector Shiraz Makupa kuwa kuna kijana wanayehisi anamiliki pesa ambayo inashukiwa kuwa ni zao la uharifu na pesa hizo zipo Nachingwea. Ndipo akatoa idhini askari waende.

Inspector Shiraz Makupa ikabidi naye ahojiwe yeye taarifa ya pesa hizo katoa wapi?

Inspector akasema alipewa taarifa zile na askari aliyemkamata Mussa Usiku akiwa hotelini kwake. Askari huyu alikuwa na cheo cha Corporal aitwaye SALIMU JUMA MBALU

Naam!

Things were now unfolding themselves.

Ikajulikana jinsi Mussa alivyokamatwa na kulala ndani tangu mwezi October mwaka jana.

Ushiriki wa mkuu wa Kituo OCS ukabainika. Hivyo mkuu wa kituo ASP Charles Onyago akaitwa mbele ya kiti cha kunesa nesa cha Brigedia Jenerali Gaguti.

Issue hapa ilikuwa ni MUSSA YUKO WAPI?

Wakati kamata kamata hii imeshika hatamu, Mhusika mmoja alianza kutazama swala lile kwa jicho la tatu.

Tuseme sio mpaka kamata kamata ilipoanza.

Hapana!

Huyu alikuwa ameshaanza kukosa usingizi kwa mambo ambayo aliyashuhudia usiku wa tarehe 5 January.

Huyu hakuwa mwingine bali ni ASP GREYSON MAHEMBE
 
Part 5

Ilitokea mara mbili swala la Mussa linapitia mikononi mwake.

Just kama coincidence tu!

Mwezi October 2021 wakati Mussa anakamatwa kwa mara ya kwanza, askari huyu alikuwa ndiye incharge wa Charge room CRO usiki ule.

Na ndiye aliyepewa maelezo na askari mkamataji kuwa Mussa anaingia korokoroni kwa kesi ya wizi wa pikipiki.

Alijaribu kuhoji wasifu wa pikipiki iliyoibiwa ni aina gani na namba zake za usajili. Pia akahoji kama kesi hiyo ilishawahi kufungukiwa huko nyima na mlalamikaji alikuwa nani?

Maswali haua yalikosa majibu usiki ule, naye kwa kuamini labda mkamataji yupo Kwenye mchakato wa “kumchekecha” Mussa ajipatie chochote hakutilia maani.

Lakini askari huyu wakati anamaliza zamu, akatoa maelekezo kwa askari mmoja wa chini aliyeingia asubuhi afatilie swala la Mussa kisirisiri ajue sababu halisi ya kukamatwa kwake amjuze.

Musssa alipoendelea kukaa kwa siku tatu ikabidi jamaa huyu anuse nuse na akabaini kinachoendelea nyuma ya pazia.

Askari huyu akawa anafosi aingizwe kwenye deal naye ajipatie chochote.

Lakini wahusika wakamtoa kwenye picha na akashangaa tu yanakuja maelekezo aende Morogoro kikazi.

Na Usiku ule ambapo Mussa alishikiliwa mara ya pili, ni yeye alikuwa tena CRO(ASP MAHEMBE).
IMG-20221023-WA0149.jpg
 
Part 6

Mussa alipotolewa kwa minajili ya kumpeleka “zahanani” ni yeye aliyetakiwa kuidhinisha kwa kwenye nyaraka za pale Charge room.

Akahoji mbona mahabusu mwenyewe anaonekana buheri wa afya?

Lakini kwa kuwa ilikuwa ni amri ya mwenye kituo (OCS) ikabidi atekeleze.

Zaidi ya yote alitakiwa kutoa jina la Mussa kwenye orodha ya mahabusu waliokuwa wanashikiliwa siku hiyo.

Tayari Kengere ya hatari ilikuwa inavuma kichwani mwa askari huyu.

Lakini hakuwa anajua ni hatari gani. Akajiuliza, kama “wamemalizana” na Mussa na kuamua kumwachia, kulikuwa na haja yoyote ya kufuta taarifa zake? Kulikuwa na haja ya kumtoa kwa mgongo wa kwenda zahanati?

Jamaa akamwachia Mussa lakini akamshirikisha jambo lile askari mmoja mdogo (anahifadhiwa) kwa kuwa alikuwa zamu pale usiku aende na Mussa zahanati.

Askari yule alipojiunga na “timu” ya wanamkakati alipomfikisha zahanati akawa anataka kufatilia swala la matibabu ili amrudishe Mussa “Makwaya”.

Wanamkakati wakampa amri yule askari dogo aindoke kwani pale kuna askari wengine.

Dogo huyu akaondoka kinyonge kwani kichwani mwake aliamini kama kuna deal la pesa lilikuwa linaendelea lazima angeshirikishwa na hivyo kujipatia chochote.

Kwa hiyo kwa taarifa za kituo dogo huyu ndiye aliyejulikana kuwa aliondoka na Mussa Kituoni.

Si Msala huu!

Masikini ya watu dogo hakuwa anajua lolote na hakushirikishwa lolote.

INAENDELEA

Note: Kuna askari (simtaji) ndani ya huu mkasa, alikamatiwa akaachiwa. Nitapiga naye Michapo Jumamosi (kaahidi) Pia Mganga ambaye Mussa alienda kwake ana mengi ya kueleza. Mussa alimtajia hadi majina ya wabaya wake. Akamtajia hadi alivyopata pesa zile. Ilikuwa ni lazima aeleze ukweli ili “atibiwe”

Jinsi Mussa alivyopata pesa pia ni story ya kustaajabisha. Sio madini kama ilivyosemwa naye anaupande wake wa pili wa “giza”

Utulivu wenu ndio utanipa ufatiliaji Mzuri
IMG-20221023-WA0148.jpg
 
A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

KILLINGS IN CUSTODY

Hit me!

Jab Me!

Make me say I did it.

When you pour Cold water on me,

I’ll Sign the Paper.

This is a two in one Thread

Yes!

Huu ni Uzi wenye mikasa miwili

Naanza kwa kunukuu Barua ya rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi (Kipindi akiwa ni waziri wa mambo ya ndani), aliyomwandikia Rais Julius Nyerere kumtaarifu nia yake ya kujiuzuru baada ya mauaji ya wananchi mikononi mwa polisi Mwanza na shinyanga Mwaka 1977

“Polisi ni chombo cha kulinda amani,mali na maisha ya watu wake. Si chombo cha kuwaua.”

“Pia polisi ni chombo cha kuhifadhi na kudumisha usalama na haki. Si chombo cha kudhulumu, kuonea na kuwatesa wananchi wale wale wanaogharamia kukiweka”

Barua inaendelea

“Kwa bahati mbaya,maovu kama haya ndiyo haswa yalitendwa na vyombo vya serikali huko mikoa ya Shinyanga na Mwanza”

Mwinyi akaendelea

“Kijinai, mimi binafsi nisingehusika kwani sikushiriki wala sikushauri, Sikuagiza wala kuelekeza mambo yale yafanywe kama hivyo yalivyofanywa”

Mwinyi akaonyesha uungwana

“Hata hivyo,kisiasa nakiri kuwa nahusika. Siwezi kukwepa kwa sababu dhamana yangu ya uwaziri inaambatana na wajibu unaonitaka nijue yanayotendeka wizarani na pia niweze kudhibiti na kuhakikisha mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi.”

Mwinyi akanukuu msaafu

“Msaafu unatuusia kwa kusema “WALA HATABEBA MZIGO WA MWINGINE”

“Kisiasa MZIGO HUU NI WANGU NA NAKUBALI KUUBEBA KWANI HAKUNA MWINGINE WA KUUBEBA”

Then Mwinyi threw the towel

“Kwa hiyo,Mwalimu nakuomba mambo matatu.Kwanza naomba radhi mimi nafsi yangu na pia naomba radhi kwa niaba ya askari wote wema walipo. Pili naomba vilevile uelewe sehemu yangu katika kosa hili.Tatu kwa fedheha hii,naomba unikubalie kujiuzuru”.

Mwinyi akawa amemaliza barua yake.

Naiita barua hii kama barua ya kiungwana na ya Kihistoria.

Ni barua pekee ya Kiongozi wa Taifa letu aliyejiuzuru huku akikubali makosa bila kumtupia mzigo mtu mwingine.

Barua hiyo ilifuatiwa na kustaafishwa kwa manufaa ya umma, Director wa Tiss, Mzena, IGP, Pundugu, na maofisa kibao.

Mtiti huu ukahamia Mwanza kulikotokea vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, Masanja Makhula Mazengenuka na Issack Mwanamkoboko.

RC wa Mwanza, Peter Kisumo,
RSO Andrew Mayalla, DSO Ihuya, RPC Mkwawa, na OCD, wakastaafishwa kwa manufaa ya umma, kisha wakapandishwa kizimbani kwa Kesi ya Mauaji Mwanza. Washitakiwa wote walikutwa na hatia, isipokuwa Andrew Mayalla aliyekuwa akitetewa na wakili Murtaza Lakha.

Je Tangu mwaka 1977 mpaka leo, ni matukio mangapi yametukia kwa watu kuuwawa wakiwa mikononi mwa polisi?

Je, alishawajibika kiongozi yeyote wa kisiasa?

Alishawajibishwa kiongozi yeyote kwa ngazi ya RPC, RSO, RCO nk?

Sasa nakukaribisha katika uzi huu kuyaangazia matukio mapya

Sheria inasema

“When a person in in trusted as a custodian of a suspect or convict. He or she will be liable of anything that might befall to that suspect /Convict”

Kwa tafsiri isiyo rasmi maneno hayo yanamaanisha”

“Mtu aliyeaminiwa kumshikilia mahabusu au mfungwa atawajibika kwa lolote litakalomtokea mahabusu au mfungwa wakati yuko chini ya uangalizi wake”

Tuendelee

Nianze na mkasa wa kwanza

Mkuu wa gereza la Liwale mkoani Lindi alikuwa amesafiri kikazi kwenda mkoani Dar Es salaam.

Huko nyuma katika gereza lake kukawa kuna kazi ya kuvuna mahindi katika shamba la gereza.

Wafungwa wakifanya kazi hiyo chini ya usimamizi wa askari Magereza

Baada ya kuvuna ikafata kazi ya kusomba mahindi hayo kupeleka kwenye ghala la gereza na mengine yalipaswa kupelekwa nyumbani kwa Bwana jela ACP Gilbert Sindani ambaye kwa wakati huo alikuwa safarini Dar es salaam.

Mkuu wa gereza akiwa bado yuko Dar es salaam akapigiwa simu na “vichomi” wake kuwa katika mahindi yake yaliyovunwa kuna mengine yameibiwa.

Mkuu wa gereza akarudi Liwale.

Akamuita msaidizi wake na kumhoji juu ya taarifa mahindi yake kuibiwa.

Msaidizi akakubali ni kweli tuhuma hizi amezipata lakini bado hajazichunguza hivyo bado hakuna yeyote aliyetuhuniwa kuiba mahindi au kupokea mahindi ya wizi.

Taarifa hii haikumridhisha mkuu wa gereza.

Kesho yake tarehe 8 june 2022 Mkuu huyu akawaita Nyampala wa gereza pamoja na “Kiherehere” wake,

Usishangae ndugu msomaji,

Kiherehere ni cheo gerezani na huyu huwa ni mpambe wa Nyampala na muda wowote anaweza kupanda cheo kuwa Nyampala.

Nyampala alikuwa ni mfungwa namba 70/2020 ABDALAH NGATUMBALA

Kiherehere alikuwa ni mfungwa namba 76/2021 SIABA MBONJOLA

Hawa wote waliitwa na mkuu wa gereza na kuhojiwa akiwataka wampe taarifa kamili juu ya wizi wa mahindi yake.

Wawili hawa wakakana kujua lolote.

Baada ya majibu hayo Palepale Mkuu wa gereza akaanza kuwapiga akiwataka wamtaje aliyechukua mahindi na amechukua kiasi gani.

Alipochoka Mkuu wa gereza akawaita askari wawili;

1.SGT.YUSUPH SELEMANI

na

2.CORPORAL FADHILI MAFOWADI

wamsaidie kuwapiga hadi watakapotaja wezi

Kipigo hicho hakikuwafurahisha askari wengine ambao waliwazuia Sajenti Yusuph na Koplo Fadhili wasiendelee kuwapiga, wakihoji iwapo wana uhakika kweli kuna wizi umetokea?

Wengi waliamini kuwa uchache wa mavuno ya mwaka huu ndiyo sababu ya kudhani kwamba wizi umefanyika.

Mkuu wa gereza alipobaini kuwa wafungwa wale wameumizwa sana, akaondoka.

Muda mfupi baadaye akarudi na kuwapakia kwenye gari kuwapeleka hospitalini hospitali ya wilaya Liwale.

Pale hospitali kwa kuwa walipelekwa wakiwa na hali mbaya madaktari wakashauri kwanza wapatiwe Form ya polisi namba 3 PF3 ndio waendelee na matimabu.

Wakati haya yanaendelea mmoja ya Wagonjwa alimfahamu Nyampala Ngatumbara

Akampigia simu ndugu yake aitwaye SAID MOHAMED

Baadaye madaktari wakabaini kuwa tayari Nyampala Ngatumbala alikuwa amekwisha kufariki dunia.

Na kwa kuwa hali ya kiherehere ilizidi kuwa mbaya wakamwandikia rufaa akimbizwe hospitali ya Mifupa Moi

Ndugu wa Nyampala akiambatana na diwani wao Nassoro wakaenda hospitali ya liwale lakini wakazuiwa kumuona mgonjwa wao (marehemu) bila ya kibali cha mkuu wa gereza.

Wakampigia simu Mkuu wa wilaya aliyewataka waende ofisini kwake.

Walipofika Mkuu wa wilaya akawaeleza kuwa tayari ana taarifa hizo na kwamba ameshawasiliana na mkuu wa Mkoa ili atume timu kuchunguza sakata hilo.

Kesho yake Mkuu wa gereza akawapigia simu diwani na ndugu wa marehemu waende Kipute (liliko gereza la Liwale)

Walipoenda wakamkuta Mkuu wa gereza akiwa na Mkuu wa gereza wa mkoa wa Lindi (RPO)FELSCHEME MASSAWE

Mbele ya RPO mkuu wa gereza akawaeleza kuwa ndugu yao amefariki kutokana na maradhi ya shinikizo la damu.

Ndugu hawakuridhika na maelezo hayo ambapo wakaomba postmortem ifanyike

Ripoti ya daktari ikabainisha kuwa marehemu alikuwa kavunjika mguu mmoja, mshipa wa nyuma wa mguu mwingine umechanika huku damu ikiwa imeganda maeneo ya mikononi.

Ripoti ikahitimisha kuwa marehemu alifariki kwa kipigo na sio shinikizo la damu.

Mfungwa huyo aliyeuwawa alikuwa akitumikia kifungo cha miaka mitano tu jela baada ya kukutwa na hatia ya kukamatwa na nyama pori ya nguruwe.

Lakini askari hao wakaamua kubadilisha adhabu yake kugeuka kuwa ya kifo.

Mfungwa huyo aliyeuwawa alikuwa akitumikia kifungo cha miaka mitano tu jela baada ya kukutwa na hatia ya kukamatwa na nyama pori ya nguruwe.

Lakini askari hao wakaamua kubadilisha adhabu yake kugeuka kuwa ya kifo.

Katika nusa nusa ndipo ikabainika kuwa Mfungwa huyu aliuwawa kwa bahati mbaya tu Wakati watu wakitaka kutekeleza visasi vyao.

Nanukuu

“Kuna watu ambao Mkuu wa Gereza hapatani nao. Kuna askari anawatafutia sababu awafukuzishe kazi. Ni bahati mbaya kuwa askari hao hawakutajwa na Marehemu Ngatumbara na mwenzake,”

Quoted from a source within, under anonymity conditions

Hili sio tukio la kwanza kwa mfungwa kufia mikononi mwa askari Magereza.

Mwaka 2010 Mfungwa namba 214 Khassim Kumchaya aliuwawa na askari wanne mwenye namba B 5147 WDR Swalehe, A 854 Sajenti Mohamed, 4264 Sajenti Jason aka Machozi na askari mwenye namba A 5294 Sajenti Shaibu.

Mfungwa huyu aliuwawa katika gereza la Lilungu mkoani Mtwara.

Mwaka 2019 askari wa gereza la Kilombero walimuua mfungwa Basiri Makungu.

Mnahisi nimemaliza?

Hapana ndio naanza!

Sasa Nageukia tukio la mauaji ya Kijana mfanyabiashara wa madini aliyeuwawa na Polisi mkoani Mtwara.

Ilikuwa hivi;

Mussa Hamisi alikuwa akijishughurisha na biashara ndogo ndogo ikiwemo kuuza mitumba katika kijiji cha Luponda wilayani Nachingwea mkoani Lindi.

Baadae Mussa akaondoka kijijini Luponda Kwenda kwenye machimbo ya dhahabu kijiji cha Mpiruka B hukohuko Nachingwea.

Mungu amtupi mja wake na penye nia pana njia.

Mwezi october 2021 Mussa akapata bahati ya kengewa baada ya shimo lao kutema.

Baada ya kusafisha dhahabu musa akapata dhahabu ya kutosha kubadili maisha yake.

Madalali wakamuunganisha Mussa na mnunuzi wa dhahabu yake raia wa kigeni

Kweli biashara ikafanyika!

Mussa akiibuka na kiasi kikubwa cha pesa ambayo hakupata kuiota.

Naam!

Alilipwa kiasi kikubwa cha dola za Kimarekani yapata 31,500 usd

Ukikileta kikwetu kwetu ni sawa na milioni 74 na ushee.

Musa akaondoka machimboni na kurudi kijijini kwao Luponda.

Kule akamnunulia mama yake Battery Solar na Inverter

Kichwani akipanga kupabadilisha kabisa pale nyumbani kwao.

Akaficha nusu ya pesa ile pale nyumbani.

Akaondoka na nusu ya pesa kwenda kuibadilisha Mtwara mjini.

Alipofika Mtwara akamjulisha mjomba wake aitwaye SALUM NG’OMBO kuwa yuko Mtwara.

Huyu mjomba wake alikuwa ni dalali wa kwenye mabasi akifanyia kazi yake kituo cha mabasi MKANALEDI pale pale Mtwara Mjini.

Mussa alamjuza sababu ya ujio wake na akamuomba amsindikize kwenda Bank

Wakaona benki ya BMN (code) ndiyo ingefaa kutumika kubadilisha Biden kuwa Samia.

Mussa akazama BMN bank Mtwara

Pale Bank akahudumiwa na mdada flani hivi

Biden wakageuka Samia kama milioni 30 hivi

Baada ya kubadili yule dada akamuuliza anaishi wapi?

Mussa akasema kuwa anaishi Nachingwea na anapanga kuondoka siku ile ile.

Mdada akamshauri kuwa sio salama kusafiri na pesa ile kuwa kuwa muda umeenda.

Akamshauri aende nyumba ya wageni aliyomtajia ili kesho mapema arudi Nachingwea

Mussa Akakubali kiroho safi

Jioni Mussa akatoka kujivinjari na akaenda kwenye Club maarufu pale Mtwara Kama Triple V

Sasa hapa ndipo ndugu msomaji inabidi nirudie kauli moja ambayo niliwahi kumnukuu Kachero mmoja wakati “tunabadilishana kahawa”

Nanukuu

“Makachero huwa tunavutiwa sana na mtu anayekunywa “bia msitu” awapo bar... Sio kwamba tunamuonea wivu.. Hapana! Bali huwa ni msingi mkubwa wa kuanza kuwa suspicious kutaka kujua anafanya kazi gani inayompa kipato cha kunywa “bia msitu””.

Hapa bia msitu anamaanisha ile tabia ya kuagiza vinywaji vingi kwa wakati mmoja na kutapanya kwenye meza huku ukitoa offer kwa wanaokuzunguka”

Ndicho alichokifanya Mussa pale Club

This was his grave mistake

What a coincidence!

Ilitokea kuwa pale Club yule mhudumu wa Bank aliyemhudumia Mussa naye alikuwepo.

Naam alikuwepo pale akipata kinywaji na jamaa yake mmoja ambaye ni “njagu”

Njagu huyu alikuwa meza moja na yule mhudumu pamoja na manjagu wenzake.

Hivyo wakati Mussa anamwagilia Moyo kwa “bia msitu” na wakati manjagu wale wanavutiwa naye walianza kumjadili mbele ya yule Mhudumu.

Mhudumu bila kujua akasema Mussa ana kisu cha kutakata kwani ni yeye alibadili pesa zake.

Akasema anatokea Nachingwea na Lodge aliyofikia

Naam!

Mhudumu akawaambia Mussa amefikia SADINA hotel

Mhudumu aliyasema yale “in good faith” bila kujua kama anauza ramani ya vita kwa wale manjagu.

Mussa akaondoka muda ukiwa umeenda sana kurudi lodge kwake.

Bila ya kujua tayari kuna manjagu yamemuundia mkia.

Majira ya saa 7 kwenda saa 8 usiku Mussa akashangaa mlango wa chumba chake unagongwa kwa fujo.

Alipofungua wakaingia watu waliojitambulisha kuwa wao ni polisi na yuko chini ya ulinzi.

Alipouliza kosa lake hakutajiwa akaambiwa anahitajika kituoni.

Manjagu wakasachi chumba chake lakini wakaishia kukuta milioni 2.5 pekee.

Hii haikuwaridhisha!

Wao walikuwa na story nzima kutoka kwa mhudumu wa benki kuwa Mussa kaondoka na kiasi gani.

Walikuwa wanajua pia kuwa Mussa alibadili kiasi tu cha pesa kati ya pesa aliyokuwa nayo.

Mussa alipohojiwa kilipo kiasi kingine alikana kabisa kuwa na pesa nyingine.

Mussa seemed to be a very brave young boy.

He might have hidden the rest of the “package” somewhere within his room.

Mussa alipokaidi akachukuliwa na kupelekwa korokoroni Mtwara Central police.

Sasa unajua mtu anapoingia kituoni ni lazima aandikwe kwenye Detention Register kuwa anaingia ndani kwa kosa gani.

Askari wale wakaandika kuwa Mussa anashikiliwa kwa kosa la Wizi wa pikipiki.

Musa akalala korokoroni siku hiyo.

Sasa msomaji inabidi uelewe kitu kimoja,

Kulala korokoroni usiku mpaka asubuhi sio issue

Issue ni kuwa ikifika kesho yake asubuhi mpaka mchana swala lako linakuwa nje ya waliokukamata.

Swala linaanza kupata “nzi” wengi kwani mwenye kituo “OCS” ni lazima ajue umeingiaje.

Ukiacha “OCS” mwingine ambaye ni lazima ajue ni mkuu wa upelelezi “OC- CID” na lazima mkuu wa polisi wa wilaya OCD lazima ajue idadi ya mahabusu wake wilayani ili aweze kutoa ripoti kwenye “morning brief” kwa mkuu wa wilaya ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati ya usalama wilayani.

So mpaka inafika kesho yake asubuhi Swala la Mussa lazima tayari lilishafika kwenye Meza za vigogo wa polisi niliowataja.

(Save for the DC kwani yeye anaweza kupewa “fabricated infos)

Lakini niliowataja kwa nyadhifa zao ni lazima walipata taarifa toka kwa wakamataji na Mussa.

Ni kwa sababu Mussa asingeendelea kukaa ndani bila maelezo yake kuchukuliwa.

Na ni lazima Mussa alijitoa kwenye kesi ya wizi wa Pikipiki na akaeleza uhalisia kuwa yeye ni nani, anatokea wapi, na kafata nini Mtwara hadi kuishia korokoroni.

Tuendelee

So wale wakamataji wakawashirikisha wakubwa wao kuwa issue ya Mussa inaweza kuwafanya waibuke na “donge nono”

Swala hili likawavutia wakubwa wale.

Wakubwa wakaona wa “adjust” vipimo vya kumuhoji Mussa

Then they started to “forgive” Mussa mpaka aseme pesa nyingine ilipo.

After a severe “forgiveness” Mussa akataja alipoficha pesa nyingine SADINA lodge.

Manjagu walipoenda kweli wakakuta pesa ikiwa imefichwa kwenye dari ya choo kwenye chumba alichokikodi Mussa.

What a Bingo!

Sasa manjagu wale wakaanza kuamini Story ya yule mfanyakazi wa Bank kuwa Mussa alimweleza kuwa anabadili nusu na pesa na nyingine angeenda kubadili sometimes afterwards.

Sasa bingo ikawa utamu kolea!

Wakapata hamu kwenda kuzifata Nachingwea.

Lakini kikaibuka kikwazo!

Yes kikwazo!

Wanaenda Vipi kufanya kazi wilaya nyingine huku wao wanatokea wilaya nyingine?

Wakaona hiyo haiwezekani without prior notice of RCO na RCIO

Ndio!

Wasingeweza kwenda bila kumjulisha mkuu wa Upelezi na Mkuu wa intelejensia wa Mkoa.

“Nzi” wakaongezeka kwenye chain

Naam!

Ilibidi hawa nao wafahamu swala la Mussa kinaga ubaga kama kweli wanazitaka zile pesa.

Baada ya watu hawa kuwekwa sawa na baada ya mussa kuwa ametepeta wakapiga simu Nachingwea.

Namba ya simu wasingeipata kokote zaidi ya kuitoa kwa Mussa.

Namba ile ilikuwa ni ya Mama yake Mussa

Ndugu Msomaji, nakurudisha nyuma kidogo

Yule mjomba wake Mussa anayefanya kazi kituo cha mabasi cha MKANALEDI pale Mtwara alishangaa ukimya wa mpwa wake tangu jana yake.

Huku akiwa hapatikani kwenye simu.

Katika jitihada za kumtafuta ndio akawa ameenda hadi kituo cha polisi kumuulizia kama labda alikamatwa kwa shida yoyote.

Hisia zake zikazaa matunda.

Akabaini Mussa yuko pale kituoni kwa siku mbili nzima.

Akaambiwa kesi ya Mussa ni nzito ya wizi wa pikipiki so hawezi kumuona.

Kipindi hicho namba ya Mama wa Mussa imeshachukuliwa.

Yule mjomba wake akamtafuta mzee mmoja maarufu kwa jina la Ng’itu asaidie kumnusuru mpwa wake

Kweli yule mzee akampambania Musa lakini huku akifata anayoelekezwa na wale Manjagu.

Siku ya tatu toka Mussa ashikiliwe Manjagu wakampa yule Mzee namba ya Mama Mussa aitwaye Hawa Ally ili aipige na walishamwambia cha kusema.

Yule mzee akampa maelezo mama yule kuwa Mussa amekamatwa na inahitajika shilingi laki tatu kwa ajili ya dhamana.

Mama wa watu na mmewe(Baba wa Mussa wa kufikia) wakajichanga wakatuma ile laki tatu ili kumsaidia Mussa apate dhamana.

Hawakuuliza sababu ya kukamatwa kwake

Wao walichojali ni mtoto wao awe huru.

Wakamnunulia Mussa Uhuru tunaoambiwa ulishapatikana mwaka 1961

Let’s pause at this juncture ndugu msomaji.

just imagine,

Hawa manjagu tayari walishapata pesa nyingi tu kutoka kwa Mussa pale Mtwara mjini.

Lakini hawakuridhika!

Wakamkamua pia mama wa watu shilingi laki tatu.

With due respect, these cops were animals.

Tuendelee

So baada ya muda Mzee yuleyule akapiga simu na kumwambia kuwa Mussa ameshaachiwa.

Lakini,

Mzee yule akamwambia Mama Mussa kuwa kwa mujibu wa maelezo ya Mussa ameeleza kuwa ana pesa nyingine kaacha kule nyumbani so polisi wanaenda kuzifata.

Baada ya simu ile baba wa kambo wa Mussa akaona ule ni ushenzi,

Akaingia kwenye chumba cha Mussa na kuanza kusaka pesa zile popote zilipo.

Nia yake ilikuwa azichukue azifiche ili polisi wakifika wasizikute.

Katika msako wake baba yule akabahatisha kuzikuta pesa zile kwenye begi la nguo za Mussa.

Zilikuwa bideni zipatazo 31,500

Mzee akahamisha pesa zile na kuzificha anakopajua.

Mida ya jioni Polisi kutoka Mtwara wakafika na gari lao Nachingwea nyumbani kwa kina Mussa.

Naam!

Walikuwa wameambatana na Mussa akiwa kapigwa pingu chini ya ulinzi mkali kama wamekamata gaidi hatari.

Ukiwaona unaweza kusema wako serious kumbe wako kwenye armed robbery.

The people we entrusted with our lives and properties, were now conspiring and executing armed robbery shamelessly in a broad daylight.

Mussa akashushwa garini

Wazazi wake wakishangaa kulikoni

Manjagu wale hawakuwa na maneno mengi wakawataka wazazi wale wajitambulishe.

Wazazi wale wakasema wao ndio baba na mama wa “gaidi” aliyepo mbele yao.

Funny but not funny

Manjagu wake wakasema wako pale kwenye mission moja tu ya kuhakikisha Mussa anawaonyesha alikoacha fedha nyingine pale nyumbani.

Nafikiri manjagu wale walikuwa kwenye zoezi la malezi wakiwasaidia wazazi wake kumlea Mussa.

Labda waliona kwa umri wake hapaswi kuwa na fedha zile kwani zingeweza kumharibu kwenye makuzi.

Kweli Mussa alikuwa Mdogo,

Mussa alizaliwa mwaka 1996

Basi bwana Mussa akaingia kwenye chumba chake huku akiwa chini ya ulinzi.

Akaongoza moja kwa moja kwenye begi lake la nguo alikokuwa kaacha pesa zile.

Musa akabaki na mshangao kama anasoma talaka baada ya kuzikosa pesa zile!

Akawaambia manjagu kuwa aliziacha pale lakini anashangaa hazipo.

Wale manjagu wenye njaa kama wametoa mimba hawakutaka kuelewa lolote.

Njagu mmoja akamulekezea Mussa bunduki kisogoni na kumwambia asilete mzaha kwani atakuwa anaiweka roho yake kwenye kamali kwa dau dogo.

Sura za manjagu wale zilikuwa mbali kabisa na masikhara na yote haya yalifanyika huku wazazi wa Mussa wakishuudia.

Uchungu wa mwana aujuaye Mzazi!

Mama Mussa akapiga magoti kuwasihi manjagu wale wasimzuru mwanae.

Mama akaanza kuropoka huku akimwambia mmewe awaonyeshe pesa ziliko.

Akasema mmewe ndio alizihamisha ili kunusuru nafsi ya mwanae.

Dear reader,

Despite the fact that it is me who is jotting down this thread, this captivating and hollow scene didn’t exonerate me from sobbing.

Naomba nimnukuu Mama Mussa

“Wakamuuliza hela umeweka wapi, akasema kwenye begi, wakamuonyesha bunduki, maana walikuja na bunduki. Kwa hiyo kwa kuona mimi nina uchungu wa mtoto wasimpige wasimuue wakati mimi niko pale, ndipo nikamwambia (mume wangu) katoe hela uwape. Ndipo wakapewa, wakazichukua wakawa wanazihesabu, mimi nilikuwa nalia kwa sababu ya uchungu, mtoto ametiwa pingu.”

Polisi walipozipata pesa zile hawakuridhika.

Wakaanza kuangalia chochote chenye thamani pale nyumbani kwa kina Mussa.

Wakaona battery ya solar na Inveter ndio vyenye thamani navyo wakavibeba.

Vitu hivi Mussa alikuwa amemnunulia mama yake baada tu ya kupata pesa zake.

Lakini navyo vikabebwa.

Njaa! Njaa! Njaa!

Kama watoto wa Mamba.

Si unajua mtoto wa mamba hanyonyi?

Baada ya kupata bingo kwa mara ya pili manjagu wale wakamrudisha Mussa kwenye gari lao kisha wakamchukua na baba yake aliyekuwa ameficha pesa zile wakisema anaenda kuisaidia polisi wakaenda nao Kituo cha polisi Nachingwea.

Pale Kituoni wakamwacha yule mzee arudi kijijini bila hata nauli.

Hata kazi ya kuisaidia polisi hawakumpa tena kama walivyoahidi.

Kisha gari ikaunganisha mpaka Kituo cha polisi Mtwara wakiwa na Mussa.

Pale kituoni Mtwara manjagu wakamwambia Mussa kosa lake ni kukutwa na Dola za Marekani.

Lakini wakamkataza kutangaza suala hilo.

Badala yake wakampa kesi ya wizi wa pikipiki.

Wakamruhusu aondoke na wakampatia laki Moja kama “chenji” ya kukutwa na kosa la kumiliki dola wakati yeye ni mmatumbi.

Akaambiwe asionekane pale mjini na arudi tarehe 6 Nov kuangalia status ya kesi yake.

Mussa akarudi Nachingwea akiwa na laki moja tu akiwa kapauka.

Siku hazigandi,
Dah,inauma sana huu ukatili.

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom