Afanyeje huyu?

Swenailie

JF-Expert Member
Feb 15, 2016
240
228
Habarin wapendwa,

Mimi nina rafiki angu wa karibu anamsongo wa mawazo nafikia point namuhurumia. Nimemfaham tangu tunasoma kidato cha tano. Tangu tunafahamiana wote hatukuwahi kuwa na uhusiano. Ila tulipanga tukimaliza kidato cha sita Ni wakat mzuri wa kuwa na uhusiano.

Kipindi hicho Kuna rafiki wa kiume alikuwa anawasiliana nae alikuwa anasoma shule ya kivulana jirani na shule tuliyosoma sisi. Basi yule ndo akawa kawekwa pending kwamba tukimaliza form six atakuwa mchumba. Kipindi hicho yeye alitutangulia darasa Moja. Tulipomaluza shule na kurejea majumban haikupita mda akaniambia tayar amemkubal huyo kaka wanaanza mausiano hivo mkaka kasema atatoka chuoni aende kumsalmia. Mapenzi yao hayakudumu kwani kwa bahati mbaya yule kaka alifariki kwa ajali miezi miwili baada ya kuwa na uhusiano. Rafk angu aliumia sana.

Mda ukaenda tukajiunga na chuo. Baada ya mda kupita kidgo aliamua kuwa na mtu mwingine kwakweli aliweka moyo upya alimpenda sana yule kaka. Yule kaka alikuwa fundi umeme mwenye diploma anapiga dili zake tu mjini maisha yanaenda. Kama mjuavyo uhusiano haukosi changamoto yule dada aliingia kwa nia kabisa ya kumfanya mtu wa baadae ila inaonekana kaka bado alikuwa anapita. Dada kahangaika sana hadi sa nyingine tunamfokea maana kapenda kupitiliza.

Kavumilia mengi kanakwamba tayar kaolewa. Mwanaume anatumia kilevi mwanamke hatumii tykienda club tunajitwandika yey walaaa kweli aliniudhi sana kipindi hicho. Mwanaume alikuwa mlevi sana ila msichana aliweza kumcontrol. Akamshawish anunue kiwanja mwanaume akawa hana mda.

Kuna siku viwanja vilikuwa vinatangazwa na halmashauri yule dada alimdanganya bwana ake Ada yake imepelea na hajatumiwa anaomba ampe lak saba afu akitumiwa atamrudishia. Yule mwanaume akasema hana hela. Akakaa sku mbili akamwambia nimepata lak nne naomba Tatu mwanaume akampa. Yule dada akaenda halmashauri akalipia Kila kitu na kupata namba ya kiwanja ambapo akapewa mda wa kumalizia malipo.

Inshu ikawa atasemaje? Alipoona karibia mwisho unafka ikabidi aseme yule mwanaume alimfokea utafanyaje jambo ka Hilo mm sitaki kuishi hapa ntaka nijenge Dar. Basi yule dada akaomba msamaha ila ndo mtu kakasirika. Akamfata rafk wa karibu akamueleza. Rafk alienda kumuambia bwana ake akamwambia shukuru kupata dem wa kukufanyia hivo. Pale ndo akili zkamjia akajirudi. Wakaendelea vizuri.

Kwa kipindi hicho kumbe yule kaka alikuwa anacheat kilichotokea akampa ujauzito mdada mwingine Bila rafiki yang kujua. Nilianza mm kujua ila nkaogopa kumuambia maana najua jinsi gani angeumia na alikuwa anampenda sana. Mara nying huyu dada hakuwa anajua sana tabia za bwanaake hapendi kukagua sm and sa nyingine bwana alikuwa anaenda kwenye pombe anafanya yake. So hata tulipokuwa tunamtonya tabia za mpenz wake alikuwa anatusikiliza anasema sawa ila kesho utawaona pamoja. Hadi nikawa nakasirika.

Badae tulipokaribia kumaliza shule Inshu ilitibuka rafk angu akajua kuwa Kuna mwenzie mjamzito. Alilia sana Lakin cha kushangaza yule mwanaume sijui alimueleza nini akasamehewa wakakubaliana mwanamke atajifungua atalea mtoto akikua watamchukua. Imeenda hivo kiroho safi nafikia naona huyu karogwa.

Baadae 2014 tukiwa tumemaliza shule tunasubiri graduation mdada alimshaur mkaka waanze kujenga yeye hana kaz ila mwanaume anashughuli zake za Kila siku. Kimchezo mchezo wlianza. Wameenda vizuri saana mtoto alizaliwa wakaendeleza makubaliano hata mama wa mtoto alielewa kwani wnadai uhusiano wao haukuwa na ahadi za kuishi pamoja ndo wakajikuta wamepeana mimba tu.

Cha kushangaza baadae wamekaa hivo mwanaume akaanza game ya mara huku mara kule. Kitendo hicho kilimboa sana rafk angu.walihitalfiana sana. Angali wako kwenye misukosuko hiyo rafk angu alipata kaz akitakiwa aende kigoma. Kabla hajaenda kigoma aliniambia nimejipa mda nijitafakari naweza endelea na huyu bf Au siwezi. Alikaa takriban mwezi na hawana mawasiliano mazuri. Akapata jibu haiwezekani kuendelea. Kwa miaka yote hiyo na misukosuko hakuwahi kusema imetosha ila nilimskia kwa mara ya Kwanzaa akaniambia.

Tar 23 December aliamua kumwambia mpenz wake kwamba imetosha sikuhitaji tena. Pale ndipo shida ilianza kumbe yule kaka alikuwa kashapanga kumuoa sasa sijui alikuwa anasumbua nini. Kwa kipindi chote Kuna mtu alikuwa anawasiliana na rafk angu kawaida hasa kipindi cha campen za uchaguz ndo walikuwa karibu na urafiki wao ulidumu. Basi
naona urafiki wao ulidumu hadi wakafkia kuwa wapenzi.

Hapo safari nyingine akaianza January mwaka huu. Uhusiano mpya sasa nimeshindwa kuelewa nifanyeje mm ka rafiki ake wa karibu. Alinieleza vizuri juu ya uhusiano na alidai mwanaume alionekana nimtu. Sasa sijui alijudge mwanzon Au laa. Wameenda ila changamoto ndgondgo hazikosekan.

Mwanzon nilijua uhusiano wao utakuwa na shida kwani hana iman tena na mtu aneitwa mwanaume hivo nilijua italeta shida kiasi. Ila waliendelea vizuri ingawa uhusiano ulikuwa wa mbali mwanaume Dar mwanamke kigoma. Mungu saidia mwanaume Akapata kaz geita kidgo ikawa karibu matamanio yao waishi karibu hata ka sio pamoja Basi isiwe mbali mdada nae akafyt kupata kaz mwanza na Mungu akamskia.

Changamoto ilianza hapa sijui nini kimetokea mdada anadai mwanaume kachange alikuwa ana attention nae ila kabadilika akimuuliza anamjibu dry anaumizwa na hicho Kitendo na yeye anawish wawe pamoja waongee rugha Moja. Akimuuliza kosa hajibu. Simu zile za mara kwa mara zimepotea ule ukaribu haupo hafurahii tena uhusiano. Sasa Kahama kigoma awe karibu na mtu ila ndo hivo tena. Kabla hajareport alienda kwa bwana ake ila anadai still sio yule amebadilika.

Mdada aliondoka kuenda kureport kaz huku anaumia amefika amekaa siku mbili mawasiliano ya shida mwanaume busy na Simu usku akiuliza anasema ndgu yake. Mwanaume hana mda tena wa kuwasiliana na yeye anaweza kuta missed call asimtafute wala nini. Kibaya zaidi katika makubaliano yao walikubaliana wafanye mahusiano ya waz hivo Kila mtu ajue mwanzon dada alisita badae akaona inaweza ikawa anakosea akakubali. Ila katika kipind kifup Mdada aliweka dp ya mchuchu wake Kuna mtu akaona akamwambia huyo Ni shemeji yake kwa mtoto wa mamdgo. Akashangaaa mbona huyu tumeongea na bado naskia haya.

Sasa kwa kitendo hicho dada alitaka amuulize mpenz wake siku amempigia hakupokea akamtumia meseji naomba ukiwa free tuongee mwanaume hakujali kumtafuta siku mbili Mdada amejiuliza afanye nini akakaa kimya anachoniambia anamuomba Mungu tu mapenz yake yatimizwe hataki tena uhusiano wa kusumbuka. Week ya pili hii hawana mawasiliano na hata huyo mwanaume hajamtafuta. Imefikia hatua rafk angu anasema anamuomba Mungu ampe hekima ya kutambua udhaifu wake kwani amechoka kuwa kwenye uhusiano wakuumizana.

My take: Ni kweli hawa watu walikubaliana kuwa na mahusiano na kama ndio iweje wote wakose interest za kumtafuta mwenzie week mbili. Je Ni kweli huyu mwanaume anampenda Au alitaka apite tu. Je Ni kweli huyu rafk angu alimpenda huyu Au alitaka mtu wa kuondolea stress. Je hivo anavosema ajichunguze madhaifu yake huku wakiwa wamechuniana Ni njia sahihi?

Je nifanye nn ili nimfanye huyu rafk angu arudishe moyo kwamba bado anaweza kupata mtu wakapendana maana navohis hata changamoto za hapa bado Kuna vitu vya alikotoka Vinamsumbua. Huyo Mungu anaemuomba anapendezwa na ukimya? Huyo mwanaume kama na yeye alimuhitaji huyu dada angeweza kukaa weekmbili hajamtafuta Kuna upendo kweli kati yao???

Na je niongee Na huyo kaka Au niache? Nilitaman niongee nae nimsihi kama anaweza play role ya kumuaminisha kwamba Kuna maisha nje ya kuumizwa so ajirudi. Nifanyeje?
Ana msongo wa mawazo.

Je huu usemi wa destiny is destiny kwamba haya yanatokea ili warudiane na mpenz wake Au nini maana yule mwanaume anabembeleza msamaha Kila sku warudiane mdaada hataki.
 
Dah!ndefu aisee,mpe pole sana Dada huyo lakin mm nahis chanzo cha yote huyo Dada anamuamin mapema sana mwanaume kias cha kukutana kimwili soon tu baada ya kuwa pamja. Wanaume weng wanaokuwa wanapita huwa wakifanya sex tu thamn ya mwanamke inapopunguwa kwa kisingzio kuwa hakuna kipya aschokijua so anatakiwa kuwa mvumilivu sana na pia apate mda wa kumjua boyfriend wake
Hata hivyo uhusiano wa mbali lazma uwe na changmoto kamà hizo hasa pale mmja wao au wote hawana hofu ya Mungu ktk mioyo yao
 
ushauri mwepesi mwambie huyo dada akae pemben kwanza ili aweke focus kwenye kazi maana kuna wengne hua tuko vizur kwenye urafik tukbadl status we cant keep the relation thing....

kingine kuhusu yule kaka wa mwanzo asiwe na wazo la kumrudia kwa maana tayar ana mtoto so Ampe ruhusa alee mwanae na yule mwanamke mwengine

swali la msingi tu vip kile kiwanja walichoanza kujenga kimeishia wapi?
 
U

unataka ukakinunue nn
 
Inaonekana kwa sasa mdada hajui anachokitaka, hajui anataka nini kwenye mahusiano. Ukijua unataka nini kwenye mahusiano, inakuwa rahisi kutafuta na kuanza mahusiano na mtu atakayekidhi matarajio yako. Mwambie kwanza ajiweke pembeni kabisa, ajipe muda wa kutosha kabla hajaanza mahusiano mapya, ajipe muda ili ATAFAKARI NA AJIULIZE anataka nini katika maisha yake, ajiulize anataka aina gani ya mahusiano kwa mwanaume, yaani asiingie katika mahusiano mpaka awe na uhakika kwamba anataka nini kwenye mahusiano, na hata akiingia katika mahusiano na mambo yasipoenda kama alivyotarajia hataumia sana kwasababu atakuwa ameshajua anachokitaka
 
Mpe pole sana huyo rafikiako. Maoni yangu ambayo yanaweza yawe ni sehemu ya ushauri wako kwake ni kwamba:

1. Achukulie hilo linalomtokea kama changamoto ya kawaida katika mapenzi. Yeye sio wa kwanza na wala hatakuwa wa mwisho.

2. Hana option zaidi ya kuanza upya. Hao wanaume wote wanacheza na hisia zake. Hawampendi kama anavyostahili. Bahati mbaya wanajua udhaifu wake na wana-take advantage. Yeye amekuwa ni easy prey kwao. Kwa mtazamo wangu wote hawamfai...hata waombe misamaha. Mimi ninaamini katika kujenga historia ya kimapenzi ambayo naona ni foundation muhimu sana ya kutengeneza a sweet and lasting love. Msingi ukiwa positive bila ya nyufa kama hizo inasaidia pale ambapo changamoto ya kimapenzi imejitokeza huko baadae. Simaanishi kuwa hawawezi kuoana. Hapana. Ila ukweli ni kwamba hawajaanza vizuri. Uzuri ni kwamba bado ana muda atulie..all will eventually be well !!

3. Anaonekana ni mwanamke mzuri kwa kumuoa na kumwita mke. Ila nafikiri tatizo lake ni kwamba yuko so desperate. Kwa wanaume wengi hii ni deal breaker. Anatakiwa ajifunze kupitia haya yanayomtokea.

4. Nikiangalia jinsi alivyojikuta yuko kwenye huu uhusiano wa sasa na huyu jamaa wa Geita ninapata picha moja kuwa rafikiako hayuko makini kwenye maamuzi yake. Lakini pia naona kuwa ni mwanamke anayeamini watu/wanaume kirahisi sana. Uwezekano mkubwa ni kuwa alimueleza huyu mwanaume matatizo yake ya kimapenzi aliyokuwa nayo na yule mpenzi wake wa mwanzo. Hapa ndio shida ilipoanzia. Jamaa akatumia fursa katika sura ya kumpa mdada a crying shoulder, upendo na huruma. Chui kwenye ngozi ya kondoo. Kwa sisi ambao in some way tunajihusisha na mambo ya kijamiii tumeona kuwa wadada wengi wanajikaangaga kwa mafuta yao wenyewe kwa mtindo huu bila kujijua. Wanakuja kushtuka wameachiwa manyoya tu. Bila kutafuna maneno mueleze tu kuwa hapa wa kulaumiwa ni yeye. But angalau imempa nafasi ya kujifunza...albeit in the hard way!!

5. Sio kila mwanaume anahuruma kwa mwanamke. Wapo ambao wanamchukulia mwanamke kama kiburudisho...kwa gharama yoyote ile. Mwambie rafikiako awe makini pale anapotaka kujiingiza kwenye mahusiano mapya. Achukue muda kumjua mpenzi wake kwa kiasi fulani. Hakuna muda maalum wa kum-study mpenzi na kumjua vizuri lkn anatakiwa ajiwekee viwango vyake mwenyewe bila kuwa pressured na circumstances. Asikurupuke kwa lengo la kuziba pengo au kupunguza stress au kukomoa mtu.

Of course akiamua kufanya vyovyote vile kwasababu yoyote ile ni haki yake lakini awe tayari ku-take responsibility ya matendo yake na sio kuanza kuwalaumu wanaume, Mungu au mapenzi yenyewe. Mapenzi matamu banaa...ha ha haaaah. Japo tunaumizwa sana. Na mara nyingi uzoefu wangu unanionyesha kuwa tunaumizwa na mapenzi kwa kutokuheshimu au kwa ku-ignore instincts zetu na obvious red-lights.

6. Kwasasa rafikiako yuko vulnerable kupita maelezo. Mshauri a-focus energy yake kwenye kazi yake, marafiki hasa wa kike ambao wako well-behaved na wenye mawazo chanya (awe makini na magumegume watamtumbukiza kwenye dimbwi la moto zaidi...ha ha ha), dini, kujisomea na activities nyingine ambazo zitamfanya awe na furaha and optimistic of a more brighter and meaningful future. Ajitahidi kuwa occupied kwenye vitu ambavyo ni more productive. Asiiweke furaha yake juu ya watu...she can easily be disappointed. This is too risky.

7. Tafadhali jitahidi kuwa karibu yake. Ongea naye mara kwa mara hata kwa simu na texts ili kuziba vacuum iliyopo kwa sasa as she transition.

Lakini pia usiwe rafiki mnafiki kwake. Akikosea mwambie ukweli hapo hapo. Najua wengi hawapendi kuambiwa ukweli...wanataka kusikia kile wanachotaka kusikia tu. Lkn utakuwa umetimiza wajibu wako kama a true friend. Akifanya jambo au uamuzi mzuri mpongeze pia. Kwa hali aliyonayo wengi wanapenda sana kupata attention na appreciation. Chukua hilo jukumu. It is a worthy investment kwake na kwako leo na hata kesho ukifa (kama unaamini kuwa kuna life after death).

Pole na kila la kheri kwenye kumsapoti rafikiako
 
Aisee asante sana yaani ushauri mzuri nimeelewa na ninaiman nitamsaidia. Yani nimejifunza mengi pia kupitia comment hiii.
 
daah hii issue yakupenda 98% na kumwamini mtu pindi unapokuwa naye ni chamgamoto tuko wengi! ila ajifunze kupunguza 47% ataweza kuhimili. nlishawahi kuwa na mtu kwa week ananiacha mara 5 na akiomba msamaha tu 4 minutes nshamsamehe! baadae ndo nkastuka amacjeza na akili yangu huyu
 
Mpe pole,lakini chamsingi kwanza atulize akili yake afanye mambo yake ya maisha,Wanaume atakutana nao makazini au kwenye mishe mishe nyengine,nadhani sasa amesha pata mkwaruzo au mikwaruzo ya moyo yakutosha ambayo itakua na somo kwake,usimshauri aurdi asipopataka alipokua anabwana alokua anamfanyia vitimbi hata wewe ulichukia ukamuona
mpumbavu sasa amesema basi muache, ila msihi sana wanasema usiachie tawi kabla huja shika tawi lakini sio kwenye mapenzi ni kwenye kazi tuu..
 
Back
Top Bottom