Kwa miaka mingi nimekulia kwenye mazingira ya haya makabila tajwa.
Kila familia niliyoishi au kuona nimeona mambo kadhaa ambayo binafsi nimekuwa nashindwa kupata ufafanusi wake lakini naishiwa kuambiwa kuwa kimila yanafanywa hivyo.
Mfano, sehemu kadhaa hapa nchini utasikia wanasema "baba akijamba basi mkiulizwa mtoto ndiyo ujitokeze ili isionekane baba ndiye katoa ushuzi".
Nimekaa na wajita nikasikia desturi kwamba baba au mama yako akikasirika kisha akikuvulia nguo na kubaki uchi basi ni lazima upate laana.
Girfriend wangu ni mchaga wa Marangu. Siku moja aliniona ninachoma pad za bleed yake akanikasirikia siku nzima. Mimi sikujua chanzo na nilipomwuliza akaniambia kuwa kuchoma pad (pamba) ni kukaribisha mkosi! Mimi si mchaga nikashangaa!
Kwa wakerewe, wajita, nilikoishi muda mrefu nimeona desturi kwamba inapopakuliwa nyama ya kuku basi watoto kamwe hatukuruhusiwa kura firigisi! Kwamba firigis ni mzee mwenye mkubwa kuliko wote!
Sisi wajita msichana akiolewa basi haruhusiwi kutaja jina la baba mkwe. Ajabu tunapoolewa waume zetu wanayatumia majina ya baba zao kama surname na msichana anaitwa Mrs. Surname ile. Hii imewapa tabu mama na dada zetu lakini tukaambiwa ndiyo mila zenyewe. Kwa wajita kuita jina la baba mkwe kunaitwa "kutogola".
Pia tumekuta desturi kwamba mtoto wa mjomba anaweza kuwa mume au mke wako.
Hizo ni baadhi tu ya ninayoendelea kukusanya niyaweke kwenye collection moja.
Ninafanya hivyo kwa sababu ninajua makabila yote nchini ya desturi hata kama tunatofautiana. Lakini wengi hatujayaandika mahala fulani kama reference na ndiyo maana huwa unazuka ubishi kuhusu nini kinatakiwa kufanyika.
Makabila yana mila na desturi lakini kiswahili si kablia na hivyo sijui mila na desturi za kiswahili. Ninachojua ni kwamba sisi wajita tunazo na wengine wanazo.
NImepata idea kwamba ikitokea mila na desturi hizi zikandikwa basi itasaidia sana kuwa kama reference. Kwamba hata kama huzipendi walau una cha kupinga kwamba mila ile si nzuri na huitaki. Kuliko ilivyo sasa hivi, hakuna zilipohifadhiwa na hivyo kila mmoja anaweza kujitamkia maadamu anajua kipengele cha mila kinaweza kumnufaisha.
Mfano, nimeona magomvi mengi kama baba au mama kuingilia na kutaka kuvunja ndoa ya mtoto anayejitegemea. Inapojulikana badala ya baba au mama yule kuomba radhi wanakuambia "mkubwa haombi samahani!".
Hivyo, nashauri kama kuna anayezifahamu tuzijadili, tuzkusanye kama reference na wanaozipenda wazitetee kwa hoja. Hata kama watachekwa na makablia mengine basi hiyo ndiyo gharama ya kupenda na kukiamini chako.
Mimi ningependa za makabila niliyotaja hapo juu.
Saidia.