Ni kabila gani familia ikipata mgeni inabadili kanuni za kila siku ili ziendane na tabia ya mgeni?

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,496
37,789
Tunaambiwa Tanzania ina zaidi ya makabila 120 yenye Mila, tamaduni na desturi mbalimbali tofauti. Kwa bahati mbaya sijabahatika kufanya utafiti wa makabila hata 50 Kati ya hayo 120+.

Kwa vile humu JF naamini ina Wawakilishi wa makabila yote na hata toka nje ya Nchi, nisaidieni kulijua kabila hata moja àmbalo mgeni ukiwatembelea Kwa Muda hata wa wiki moja familia inalazimika kubadili kanuni zào ili ziendane na tabia yako wasikukwaze mgeni.

Yaani kama famili nzima inalazimika Kula pamoja saa 7 mchana basi wewe hata kama uko nyumba ya pili unacheza bao watakusubiri Hata ukirudi SAA 10 ndo chakula kiwekwe mezani.

Usiku hata ukirudi saa 7 umelewa shemeji yako ambaye ni Baba mwenye nyumba atakufungulia na kukupa pole huku akikuuliza kama hujajikwaa njiani au kushambuliwa na Wahuni?

Halafu masuala ya chakula gani kipikwe Kwa siku inabidi usubiriwe wewe uamke hata ukiamka saa 5 asubuhi sababu ya mning'inio utakuta hawajapika hata chai mpaka useme wewe kwanza?

Ni kabila gani kama lipo? Ni;
Wanyiha?
Wanyamwezi?
Wanyaturu?
Wandamba?
Wakurya?
Wasubi?
Waha?
Au
Wakonongo?
Wafipa?
Wanyantuzu?
Wajita?
Itakuwa ni;
Wakerewe?
Wahaya?
Wamwera?
Wangoni?
Au basi ni;
Wanyakyusa?
Wapangwa?
Wairaqwi?
Wanyiramba?
Washirazi?
Wahehe?
Ahhhh!
Wakinga?
Wachaga?
Basi labda ni!!
WAGOGO?

Yaani mgeni anakuja, Baba na mama na watoto wanaitana kutengua kanuni za familia ili kutomkwaza mgeni.
Wandewa

Nisaidieni ni kabila gani Wakulungwa?
 
Kabila la wenyeji wa Kizimkazi ndiyo Wana tabia hiyo. Wanataka kubadilisha sheria iendane na matakwa ya DPW
 
Makabila yote yanayopenda kukirimu mgeni hapo hata chakula kitakuwa safi hata kama hawana pesa ,utaona nyama ya kuku safi na mambo mengine mpaka anaondoka.
 
Wewe utakuwa na shida kwenye ubongo,ni jukumu LA mgeni kuendana na tabia za wenyeji na sio wenyeji kuendana na mgeni.
Hayo ndio mambo yamefanya Afrika kuwa nyuma kwa kila kitu,tumeiga wazungu kuanzia dini,lugha,elimu mpaka life style-sa hivi tumebaki kulalamika watu kukosa maadili kumbe tuliiga mpaka mambo ya hovyo.
 
Tunaambiwa Tanzania ina zaidi ya makabila 120 yenye Mila, tamaduni na desturi mbalimbali tofauti. Kwa bahati mbaya sijabahatika kufanya utafiti wa makabila hata 50 Kati ya hayo 120+.

Kwa vile humu JF naamini ina Wawakilishi wa makabila yote na hata toka nje ya Nchi, nisaidieni kulijua kabila hata moja àmbalo mgeni ukiwatembelea Kwa Muda hata wa wiki moja familia inalazimika kubadili kanuni zào ili ziendane na tabia yako wasikukwaze mgeni.

Yaani kama famili nzima inalazimika Kula pamoja saa 7 mchana basi wewe hata kama uko nyumba ya pili unacheza bao watakusubiri Hata ukirudi SAA 10 ndo chakula kiwekwe mezani.

Usiku hata ukirudi saa 7 umelewa shemeji yako ambaye ni Baba mwenye nyumba atakufungulia na kukupa pole huku akikuuliza kama hujajikwaa njiani au kushambuliwa na Wahuni?

Halafu masuala ya chakula gani kipikwe Kwa siku inabidi usubiriwe wewe uamke hata ukiamka saa 5 asubuhi sababu ya mning'inio utakuta hawajapika hata chai mpaka useme wewe kwanza?

Ni kabila gani kama lipo? Ni;
Wanyiha?
Wanyamwezi?
Wanyaturu?
Wandamba?
Wakurya?
Wasubi?
Waha?
Au
Wakonongo?
Wafipa?
Wanyantuzu?
Wajita?
Itakuwa ni;
Wakerewe?
Wahaya?
Wamwera?
Wangoni?
Au basi ni;
Wanyakyusa?
Wapangwa?
Wairaqwi?
Wanyiramba?
Washirazi?
Wahehe?
Ahhhh!
Wakinga?
Wachaga?
Basi labda ni!!
WAGOGO?

Yaani mgeni anakuja, Baba na mama na watoto wanaitana kutengua kanuni za familia ili kutomkwaza mgeni.
Wandewa

Nisaidieni ni kabila gani Wakulungwa?
Acha ujinga hakuna kabila la Wanyantuzu unatukosea sana Wasukuma!
 
Back
Top Bottom