Msaada: Natafuta mila za kijita, kikara, kikerewe, kikwaya

Kisanduku

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
284
482
Kwa miaka mingi nimekulia kwenye mazingira ya haya makabila tajwa.

Kila familia niliyoishi au kuona nimeona mambo kadhaa ambayo binafsi nimekuwa nashindwa kupata ufafanusi wake lakini naishiwa kuambiwa kuwa kimila yanafanywa hivyo.

Mfano, sehemu kadhaa hapa nchini utasikia wanasema "baba akijamba basi mkiulizwa mtoto ndiyo ujitokeze ili isionekane baba ndiye katoa ushuzi".

Nimekaa na wajita nikasikia desturi kwamba baba au mama yako akikasirika kisha akikuvulia nguo na kubaki uchi basi ni lazima upate laana.

Girfriend wangu ni mchaga wa Marangu. Siku moja aliniona ninachoma pad za bleed yake akanikasirikia siku nzima. Mimi sikujua chanzo na nilipomwuliza akaniambia kuwa kuchoma pad (pamba) ni kukaribisha mkosi! Mimi si mchaga nikashangaa!

Kwa wakerewe, wajita, nilikoishi muda mrefu nimeona desturi kwamba inapopakuliwa nyama ya kuku basi watoto kamwe hatukuruhusiwa kura firigisi! Kwamba firigis ni mzee mwenye mkubwa kuliko wote!

Sisi wajita msichana akiolewa basi haruhusiwi kutaja jina la baba mkwe. Ajabu tunapoolewa waume zetu wanayatumia majina ya baba zao kama surname na msichana anaitwa Mrs. Surname ile. Hii imewapa tabu mama na dada zetu lakini tukaambiwa ndiyo mila zenyewe. Kwa wajita kuita jina la baba mkwe kunaitwa "kutogola".

Pia tumekuta desturi kwamba mtoto wa mjomba anaweza kuwa mume au mke wako.

Hizo ni baadhi tu ya ninayoendelea kukusanya niyaweke kwenye collection moja.

Ninafanya hivyo kwa sababu ninajua makabila yote nchini ya desturi hata kama tunatofautiana. Lakini wengi hatujayaandika mahala fulani kama reference na ndiyo maana huwa unazuka ubishi kuhusu nini kinatakiwa kufanyika.

Makabila yana mila na desturi lakini kiswahili si kablia na hivyo sijui mila na desturi za kiswahili. Ninachojua ni kwamba sisi wajita tunazo na wengine wanazo.

NImepata idea kwamba ikitokea mila na desturi hizi zikandikwa basi itasaidia sana kuwa kama reference. Kwamba hata kama huzipendi walau una cha kupinga kwamba mila ile si nzuri na huitaki. Kuliko ilivyo sasa hivi, hakuna zilipohifadhiwa na hivyo kila mmoja anaweza kujitamkia maadamu anajua kipengele cha mila kinaweza kumnufaisha.

Mfano, nimeona magomvi mengi kama baba au mama kuingilia na kutaka kuvunja ndoa ya mtoto anayejitegemea. Inapojulikana badala ya baba au mama yule kuomba radhi wanakuambia "mkubwa haombi samahani!".

Hivyo, nashauri kama kuna anayezifahamu tuzijadili, tuzkusanye kama reference na wanaozipenda wazitetee kwa hoja. Hata kama watachekwa na makablia mengine basi hiyo ndiyo gharama ya kupenda na kukiamini chako.

Mimi ningependa za makabila niliyotaja hapo juu.

Saidia.
 
Mh mie ni mkerewe sidhani kama watoto kutokula firigisi ni mila ya kikerewe. Tofautisha labda mila na desturi. Lakini nafikiri mambo mengi yalikuwa yakifanywa ili watoto waji-behave vizuri hasa pale wanapokula na wageni. Swali kwa nini firigisi na si nyama nyingine. Watoto walikuwa wanapewa maini (ya kuku). Ukifuatilia kwa undani utaona labda ulaini na ugumu wa nyama yenyewe ndo ulidetermine nani ale nini. Lakini haya mambo si yameshapitwa na wakati? Kwenu bado kuna mila za KUSOMBOKA? (Baada ya mmoja wa wanandoa kufariki?). Je majina ya kina Lusato, Nansato, Magonzi etc kuitwa watoto eti kwa kuwa chatu aliuliwa au kaonekana amekufa sehemu bado zinafanya kazi? Bahati mbaya au nzuri wakerewe hatuna mila za kumwoa binamu maana kule hatuna binamu mtoto wa mjomba ni mjomba au mama na mtoto wa shangazi ananiita mjomba sasa utamwoaje mtu unamwita mama?
 
Mh mie ni mkerewe sidhani kama watoto kutokula firigisi ni mila ya kikerewe. Tofautisha labda mila na desturi. Lakini nafikiri mambo mengi yalikuwa yakifanywa ili watoto waji-behave vizuri hasa pale wanapokula na wageni. Swali kwa nini firigisi na si nyama nyingine. Watoto walikuwa wanapewa maini (ya kuku). Ukifuatilia kwa undani utaona labda ulaini na ugumu wa nyama yenyewe ndo ulidetermine nani ale nini. Lakini haya mambo si yameshapitwa na wakati? Kwenu bado kuna mila za KUSOMBOKA? (Baada ya mmoja wa wanandoa kufariki?). Je majina ya kina Lusato, Nansato, Magonzi etc kuitwa watoto eti kwa kuwa chatu aliuliwa au kaonekana amekufa sehemu bado zinafanya kazi? Bahati mbaya au nzuri wakerewe hatuna mila za kumwoa binamu maana kule hatuna binamu mtoto wa mjomba ni mjomba au mama na mtoto wa shangazi ananiita mjomba sasa utamwoaje mtu unamwita mama?

Mkuu nakupata sana.

Binafsi ninashindwa kutibitisha kwamba yamepitwa na wakati kwa sababu tunaoyakataa hatujui tuliyakataa lini. Nimeguswa kutafiti haya kwa sababu bado wengi wana influence nayo hasa wakati wa matukio kama harusi na msiba.

Mfano, hadi leo huwa ninaona bibi harusi anakataa kutoka ndani hadi apewe senti fulani kutoka upande wa bwana. Hii ni nje ya ile mahali. Mimi ni msomi mzuri tu. Shida yangu si kuyarudisha. Bali shida yangu ni kuwa nayo kama reference ili hata ninapoyapinga niwe ninakuwa na uhakika kuwa hicho wanachokitetea wanakisadiki vipi.

Na nilianza kuwa hivi baada ya kufiea na shemeji yetu miaka michache nyuma ambako tukasikia tetesi kwamba inabidi dada yetu atafute jamaa wa kujamiiana naye walau kwa nusu saa. Nadani huko ndiko unakoita KUSOMBOKA.

Tulibishana sana pale msibani hata kufarakana maana ndiyo kwanza nilikuwa ninaisikia hiyo. Leo nikitizama ubishi ule ninaona hatukuwa tumebuni njia nzuri ya kuyapinga yaliyo machafu. Kwa mfano kama msibani pale ningekuwa na kitabu kilichojaa hizo mila na desturi basi ingekuwa rahisi kwetu kuwaambia ubaya na uzuri wa desturi moja baada ya nyingine.

Kwa ujumla vikikusanywa na kuwekwa kenye kitabu kimoja, basi ni rahisi hata walioziamini kuuona kweli kwamba ni rahisi kusambazwa na kusomwa pengi na hivyo wako responsible na sifa au dharau inayotokana na kusambaa huko.

Lakini hata kama ni kweli kuwa kila kitu kimepitwa na wakati, je rekodi iko wapi kwa ajili ya kihistoria tu?

Vilevile ninaposoma Kanuni za Bune ni kwamba Spika huwa anaapa kulind katiba, sheria na mila na desturi. Sasa hapa ndipomfano mzuri. Tunaongea kiswahili lakini hakuna kablia la kiswahili. Mimi ni mjinta na wewe ni mkerewe. Sasa kwa kesi kama yangu Spika atalinda mila na desturi zipi kama hazijaandikwa kwenye kitabu kama reference.

Na tunapotetea kuwa tusiige desturi za kigeni, je, za kwetu ni zipi kama hakuna mahala tulipoziandika tunaishia kupayuka mojamoja mdomoni?

Zidi kunihabarisha.
 
Kuna ukoo flani unaitwa wazigaba (wajigaba?) hawali naskia utumbo wa mbuzi ama ng'ombe.
 
kuna wale ambao mwanamke akifumaniwa wanamsunda limti huko chini,
hivi ni wa kabila gani hawa.
 
ngoja nyamtondo aje
Edson,

Siga naike mchijita. Ni Nyamtondo wendaki. Niwe ulya Nyang'omboli aga namwmba ati "Mbe Nyamtondo, nalola linyoni. Esemwene nakamaga amata".

Pai go?Milimo?
Milimu echikora, anye ntakwenda chilabwire buli chinu. Munane jimila nibe najo. Ntakusanila. Enijenda ntaja jilabwira.

Mwanawasu waika kutiki go???
Nanako ebili norwo esatu. Oundi akanana etano enibha nakingiswe munana.
 
Back
Top Bottom