Msaada kuhusu edge na gprs!!

Soki

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
1,303
279
Wadau, hapa niliko napata internet kwa namna mbili:

Kwanza, ni kupitia Airtel. Kwa line yao inasomeka kwamba napata EDGE lakini actual speed ni kama 15Kbps nikidownload
Pili, ni kupitia Voda. Kwa line yao napata GPRS lakini ninapodownload napata zaidi ya 40Kbps

Sasa inakuwaje GPRS wananipa speed kubwa kuliko EDGE wakati nilitarajia vice versa?
 
kwa hali halisi ya ki bongo bongo hasa ishu ya mitambo na locations usitegemee sana kila unachotangaziwa na mitandao yetu hii kipo kama wanavyotangaza....wewe unashangaa hiyo wakati saiz airtel wanatangaza 3.75G lakini kuna wakati unakuwa upo kabisa connected na hiyo 3G ila speed hufiki hata 10kbps...!! kuna factors nyingi sana za ku determine speed ya internet mfano ndo kama hizo nilizokwambia hapo juu!!
 
Speed ya airtel inaboa sana huku, ingawa inasomeka edge
 
Speed ya airtel inaboa sana huku, ingawa inasomeka edge
sio huko tu na wala sio aurtel tu....hili ni tatizo la kitaifa ndugu....kila kona kila mtandao!!! hakuna mtandao ulio 100% good ...kila mmoja una mazuri yake na mabaya yake kulingana na eneo husika...ushauri wangu ni kujaribu mitandao tofauti tofauti kwa nyakati tofauti ili upate ule utakaokuwa ahueni kulingana na eneo ulilopo!!
 
EDGE (yaani Enhanced Data Global Evolution) ilianzishwa ili ku-upgrade GSM ambayo ni bora kuliko GPRS. Kwa hiyo ni wazi kuwa speed ya EDGE inapita mbali GPRS.
Uwezo wa EDGE wa data speed ni 236 Kbps lakini makampuni ya simu yana configure EDGE isiyozidi 135 Kbps ili kubana matumizi ya spectrum resources.
Kwa hiyo suala la speed ya EDGE kuzidiwa hata na GPRS inategemea mambo mawili hasa:
  • configurated speed ya EDGE ambayo kampuni imeset na
  • afya ya connetion wakati unadownload inaweza ikaminya speed hata chini zaidi
.
 
Asante mkuu; lakini,
hapo red: Mimi speed ninayopata ni around 15Kbps while downloading. Sasa ukicompare na 135Kbps, tofauti ni kubwa sana

Kwenye blue: Sijui unamaanisha nini kwa 'afya ya connection wakati ninadownload', Lakini speed hiyo ya 15Kbps imekuwa ya siku zote si wakati fulani tu. Pia hapa nilipo ni eneo la mjini network ipo ya kutosha kabisa Mkuu!
 
Ninachomaanisha ni kwamba 135 Kbps ndio maximum ambayo makampuni yanatumia. Hivyo huwezi jua Airtel wanatumia ngapi, kama ni 10, 20, 40,70 nobody knows.
Kuhusu 'afya' ya connection namaanisha 'hali' (condition) ya connection.
 
Wenzetu wanafanya video calling, video conference bila shida, sisi bado tunadownload files kwa 6Kb/s - tutafika kweli? Sijui huo wimbo wa mkonga utaisha lini
 
Wenzetu wanafanya video calling, video conference bila shida, sisi bado tunadownload files kwa 6Kb/s - tutafika kweli? Sijui huo wimbo wa mkonga utaisha lini

Yaani we acha tu. Tatizo letu hapa maneno mingi.
 
aisee bora nyie mimi kimaajabu tigo ukifika 35mb kwa bundle ya standard napewa 25kbps hapo nipo Hspda
 
Mimi leo nimejaribu tigo nione spidi yao. Nikanunua muda wa hewani wa siku nzima kwa 700/= Speed ilikuwa almost kama ya voda ie around 40Kilobits/s. Cha ajabu ndani ya kama nusu saa, ikawa imeisha. Hawa nao sijui vipi!
 
Back
Top Bottom