Zijue maana za alama tofauti za mitandao ya simu (G, E, 3G, H/H+, 4G, 5G, VoLTE)

Itscharlie

JF-Expert Member
Apr 15, 2022
3,794
15,772
ZIJUE MAANA ZA ALAMA TOFAUTI TOFAUTI ZA MITANDAO YA SIMU

(G, E, 3G, H/H+, 4G, 5G, VoLTE)

Hizi alama najua umewahi kuziona sana kwenye simu unapokua maeneo tofauti tofauti ya dunia na una uzoefu na speed ya ya internet kutokana na alama husika iliyopo.

G (GPRS)
Yenye kirefu cha General Packet Radio Service hua na kawaida ya kutoa internet yenye kasi ndogo sana katika huduma ya 2G GSM teknolojia hii hupatikana kwenye vifaa vya zamani sana na ni mara chache sana kuiona tena labda uende sehemu za vijijini ndani ndani huko.

E (Edge)
Kama hautapata 3G au 4G mara nyingi utapata hii E ambayo kiujumla tu ni enhanced GPRS ikimanisha ni GPRS iliyoboreshwa lakini bado haina speed kubwa sana unaweza browse kwa shida shida na unaweza kuangalia video YouTube kwa shida shida hivo hivo speed yake ni 300kbs.

3G
E na G zilimaanisha 2G na 3G inasimama yenyewe hapa sasa ndo kidogo tukaanza ku experience ile speed ya ya kasi ya internet baada ya kugunduliwa kwa hii teknolojia nchini japan mwaka 1998 na ikaenea bara la Europe.

H/H+
Hii ni aina ya 3G iliyoboreshwa zaidi ndio maana mara nyingi sana utaona H/H+ badala ya 3G na kuonesha kwamba ni 3G iliyoboreshwa ni zinaitwa 3.5G
,H imesimama badala ya neno High speed packet access (HSPA) na hii data transmission speed yake ni 21mbs ukilinganisha na.

4G/LTE au LTE-A
Ni kama ilivo 3G ,4G pia ina LTE Yenye kirefu cha neno Long term Evolution hii speed ya data transmission ni kubwa kuliko zote zilizopita ambayo ni 150mbs.

5G
Hii ndio unayoiona ambayo vodacom wa mara ya kwanza wameizindua Tanzania ,ndio teknolojia ya kisasa na inayotoa internet ya kasi zaidi duniani ambayo data transmission speed yake ni 40gbs ingawa kikawaida haiwezi fika hio yote ,kwa sasa kwa baadhi ya kampuni.

VoLTE
Kama unaongea na simu na umewasha 4G Service na ukaona alama ya volte ujue ni HD audio calling ambayo hua inatolewa kupitia huduma ya 4G maana 4G hainaga default support ya huduma ya kupiga ,kwaio ukipiga mara nyingi hua inashuka kwenye 3G au chini ya hapo.



Source:CXSTOREtz
20220921_135821.jpg
20220921_140155.jpg
20220921_140152.jpg
20220921_140143.jpg
20220921_140140.jpg
20220921_140129.jpg
 
KAMA UNATUMIA TIGO NICHEKI NIKUUNGE HUDUMA YA POSTPAID UPATE GB NYINGI KWA GHARAMA NDOGO SANA‼️

GB15 KILA MWEZI KWA MIEZI 24 BEI 15000 TU!
GB35 KILA MWEZI KWA MIEZ 24 BEI 35000 TU!
GB48 KILA MWEZI KWA MIEZ 24 BEI 40000 TU
GB75 KILA MWEZI KWA MIEZI 24 BEI 60000 TU.
HUDUMA NI YA UHAKIKA HAKUNA UTAPELI HUNITUMII HELA HATA MIA NAKUELEKEZA TU UNAJIUNGA MWENYEWE MOJA KWA MOJA! (nikishakupa maelekezo unaweza kupiga no 100 ukaulizia ili kujirizisha Zaid)

Niambie nikuelekeze zaid au nipigie au txt kwa no 0717700921
 
Back
Top Bottom