Isenye, usirudie tena kunichosha kusoma utumbo wa Uhuru. Koma kabisa.
Ijumaa iliyopita Mrema alizungumzia amani na kuyapinga maandamano ya Chadema kuwa
yatavuruga amani wakati akichangia hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mrema alikariri makala ya kimataifa ya gazeti moja akidai kwamba maandamano
yamezorotesha uchumi wa nchi za Tunisia, Misri, Libya, Madagascar na Kenya.
Akitoa mfano wa madhara ya maandamano kwa mujibu wa makala hiyo, Mrema alidai kwamba
sekta ya utalii imeathirika vibaya nchini Misri kwa sababu watalii hawaendi. "Misri leo haikaliki,
ndicho tunataka Tanzania? Machafuko nchini Madagascar, Libya yalianza hivyo hivyo. Ndivyo
tunavyotaka Tanzania iwe? Tunisia nako machafuko tunayoyaona leo yalianzia kwenye maandamano
ya kutaka kuiondoa serikali. Ndicho tunachotaka?" Alihoji.
Mrema aliendelea: "Kenya nako maandamano yaliua watu 1000 na baadaye Kibaki na Odinga,
wakakaa huyu hapa na mwenzeke pale mezani, maisha ya watu waliokufa kwenye maandamano
hayo yalimsaidia nani?"
Imegundulika kwamba kelele za Mrema zilikuwa na ajenda nyuma yake na alikuwa muwazi
alipoitaka serikali impe mafao yake ya kutumikia nafasi ya Naibu Waziri Mkuu wakati wa Serikali
ya Awamu ya Pili:
"Nilipeni posho hiyo ili niendelee kuwatetea (serikali) bungeni. Msione simba kalowa maji mkadhani
nyani. Mimi najua mambo mengi nchi hii, mmenifundisha wenyewe. Nipeni haki yangu niwasaidie
kutetea hoja zetu hapa bungeni."