Mrema aitolea uvivu CHADEMA

hivi kweli mkuu bado unasoma gazeti la UHURU??
MREMA = GAZETI LA UHURU.
GAZETI LA UHURU = CCM.
 
Mrema hana ubavu hata wa kufukuza kuku! The man is down on his and now begging live on National TV apewe mafao ya ustaafu of kwa cheo ambacho hakipo constitutionally!
 
anakaribia kufa kwa maradhi na umri unaanza kusogea, IQ yake imeshuka sana
mrema1.jpg
 
Achana na Mrema mbona ni CCM by PROXY!, We uliona wapi gazeti la CCM likampatia page mpinzani?
 
Mrema aidai serikali mafao ya ubosi wake

"Nilipeni posho hiyo ili niendelee kuwatetea (serikali) bungeni. Msione simba kalowa maji mkadhani nyani. Mimi najua mambo mengi nchi hii, mmenifundisha wenyewe. Nipeni haki yangu niwasaidie kutetea hoja zetu hapa bungeni," alisema.

Kizitto Noya, Dodoma
Saturday, 25 June 2011 10:04
MWANANCHI

MWENYEKITI wa TLP Augustine Mrema, ametoa mpya bungeni kufuatia hatua ya kuidai serikali mafao ya kutumikia nafasi ya Naibu waziri mkuu.Akichangia mjadala wa hotuba ya Waziri Mkuu jana bungeni, Mrema aliitaka serikali impe mafao yake ya kutumikia nafasi ya Naibu Waziri Mkuu wakati wa Serikali ya Awamu ya Pili.

Katika mchango wake, Mrema aliitaka serikali imlipe angalau asilimia 20, kama serikali inaona hastahili.Katika kipindi hicho, Mrema alikuwa Naibu Waziri Mkuu akimsaidia John Malecela ambaye ndiye aliyekuwa Waziri Mkuu.
"Kama Sheria ipo kwamba Waziri mkuu mstaafu anatakiwa kulipwa mafao ya asimilia 80 ya mshahara wa waziri mkuu aliyeko madarakani, kwanini mimi sipati. Nipeni basi angalau asilimia 20,"alisema Mrema na kuendelea:

"Nilipeni posho hiyo ili niendelee kuwatetea (serikali) bungeni. Msione simba kalowa maji mkadhani nyani. Mimi najua mambo mengi nchi hii, mmenifundisha wenyewe. Nipeni haki yangu niwasaidie kutetea hoja zetu hapa bungeni," alisema.

Mrema aliendelea kuhoji imekuaje mawaziri wakuu wote wastaafu walipwe posho hiyo na yeye asipewe.Awali katika mchango wake kwenye hotua hiyo ya waziri mkuu, Mrema alitumia muda mwingi kuzungumzia umuhimu wa amani kwa Taifa akibeza maandamano ya mara kwa mara yanayoandaliwa na wanasiasa.

Akitumia gazeti la Mwananchi, ambalo lilichapisha habari za athari za maandamano na ukosefu wa amani nchini Misri, Mrema alisema Tanzania itafikia hali hiyo kama wanasiasa wataendelea kuwatumia vijana kupinga serikali kwa maandamano.

"Misri leo haikaliki, ndicho tunataka Tanzania, Machafuko nchini Madagascar, Libya yalianza hivyo hivyo. Ndivyo tunavyotaka Tanzania iwe, Tunisia nako machafuko tunayoyaona leo yalianzia kwenye maandamano ya kutaka kuiondoa serikali. Ndicho tunachotaka," alihoji.

"Kenya nako maandamano yaliua watu 1000 na baadaye Kibaki (Mwai-Rais wa nchi hiyo) na Odinga (Laila-Waziri mkuu wa Kenya ), wakakaa huyu hapa na mwenzeke pale mezani, maisha ya watu waliokufa kwenye maandamano hayo yalimsaidia nani," aliendelea kuhoji.

Mrema aliwatahadharisha wanasiasa kuacha kuandaa maandamano yasiyokuwa ya lazima na kwamba kama lengo ni kuiondoa serikali iliyoko madarakani, hilo linaweza kufanyika kwa namna mbadala.

"Hawa vijana wasiokuwa na kazi tunaowahamasisha kushiriki maandamano, tukiwadekeza nchi itaingia kubaya. Ni afadhali tukawahamasisha kwenda kupiga kura kuliko maandamano, mwaka jana waliojiandikisha kupiga kura walikuwa watu 20 milioni lakini waliojitokeza kupiga kura ni milioni nane tu, hili ndilo tatizo la msingi."

"Hatuwezi kuibadilisha serikali kwa hoja ya maandamano bali kwa kupiga kura. Mheshimiwa waziri mkuu nakupongeza sana katika hotuba yako unaposema amani inahatarishwa na maandamano," alihitimisha Mrema.
 
Unafiki ndiyo unaomsumbua hakuna kingine, mbona hadai madai ya kukuia chama cha NCCR Mageuzi?
 
Hali yake bado ni mbaya sana, wachaga walimpa nafasi ya ubunge ili apate pesa kwa ajili ya matibabu, kwani walidai kuwa hata hali hiyo aliyo nayo iko hivyo kwa sababu ya siasa. Debe tupu haliachi kutika!
 
Ijumaa iliyopita Mrema alizungumzia amani na kuyapinga maandamano ya Chadema kuwa
yatavuruga amani wakati akichangia hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mrema alikariri makala ya kimataifa ya gazeti moja akidai kwamba maandamano
yamezorotesha uchumi wa nchi za Tunisia, Misri, Libya, Madagascar na Kenya.


Akitoa mfano wa madhara ya maandamano kwa mujibu wa makala hiyo, Mrema alidai kwamba
sekta ya utalii imeathirika vibaya nchini Misri kwa sababu watalii hawaendi. "Misri leo haikaliki,
ndicho tunataka Tanzania? Machafuko nchini Madagascar, Libya yalianza hivyo hivyo. Ndivyo
tunavyotaka Tanzania iwe? Tunisia nako machafuko tunayoyaona leo yalianzia kwenye maandamano
ya kutaka kuiondoa serikali. Ndicho tunachotaka?" Alihoji.

Mrema aliendelea: "Kenya nako maandamano yaliua watu 1000 na baadaye Kibaki na Odinga,
wakakaa huyu hapa na mwenzeke pale mezani, maisha ya watu waliokufa kwenye maandamano
hayo yalimsaidia nani?"


Imegundulika kwamba kelele za Mrema zilikuwa na ajenda nyuma yake na alikuwa muwazi
alipoitaka serikali impe mafao yake ya kutumikia nafasi ya Naibu Waziri Mkuu wakati wa Serikali
ya Awamu ya Pili:
"Nilipeni posho hiyo ili niendelee kuwatetea (serikali) bungeni. Msione simba kalowa maji mkadhani
nyani. Mimi najua mambo mengi nchi hii, mmenifundisha wenyewe. Nipeni haki yangu niwasaidie
kutetea hoja zetu hapa bungeni."
 
Ijumaa iliyopita Mrema alizungumzia amani na kuyapinga maandamano ya Chadema kuwa
yatavuruga amani wakati akichangia hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mrema alikariri makala ya kimataifa ya gazeti moja akidai kwamba maandamano
yamezorotesha uchumi wa nchi za Tunisia, Misri, Libya, Madagascar na Kenya.


Akitoa mfano wa madhara ya maandamano kwa mujibu wa makala hiyo, Mrema alidai kwamba
sekta ya utalii imeathirika vibaya nchini Misri kwa sababu watalii hawaendi. "Misri leo haikaliki,
ndicho tunataka Tanzania? Machafuko nchini Madagascar, Libya yalianza hivyo hivyo. Ndivyo
tunavyotaka Tanzania iwe? Tunisia nako machafuko tunayoyaona leo yalianzia kwenye maandamano
ya kutaka kuiondoa serikali. Ndicho tunachotaka?" Alihoji.

Mrema aliendelea: "Kenya nako maandamano yaliua watu 1000 na baadaye Kibaki na Odinga,
wakakaa huyu hapa na mwenzeke pale mezani, maisha ya watu waliokufa kwenye maandamano
hayo yalimsaidia nani?"


Imegundulika kwamba kelele za Mrema zilikuwa na ajenda nyuma yake na alikuwa muwazi
alipoitaka serikali impe mafao yake ya kutumikia nafasi ya Naibu Waziri Mkuu wakati wa Serikali
ya Awamu ya Pili:
"Nilipeni posho hiyo ili niendelee kuwatetea (serikali) bungeni. Msione simba kalowa maji mkadhani
nyani. Mimi najua mambo mengi nchi hii, mmenifundisha wenyewe. Nipeni haki yangu niwasaidie
kutetea hoja zetu hapa bungeni."

Njaa na tamaa ni kitu kibay sana, tangu Mrema apelekwe India kwa matibabu na serikali ya kikwete alikatwa makali.
Hivyo kwa sasa "Mrema ni toothless bull"
 
Jamani kwani huyu Babu ni wa kumjadili pia? si anajulikana kuwa anatumika na CCM kufifisha vyama vya upinzani, kwa malipo kidogo! mi nimeshawahi kumuona mara kadhaa kwenye jengo la White house ya CCM pale DOM, wwakati wa vikao vya CC, na ndo yakawa matokeo ya NCCR kudumaa, na tlp kupoteza directions, so now hana jipya, najua wanasiasa wanamjua! na CDM inabidi tuwe na mbinu za kumdhofisha asitusumbue!
 
Pia TLP hawamtaki but yeye anatamba ndiye mbunge pekee na mwenyekiti wa Chama,hivyo yeye ni bata anayetaga yai la SAABU(Dhahabu).What a Hopeless Man kutoka Dume la mbegu mpaka Jogoo mseng*
 
Nimesoma sociology....ninaelewa kuwa mwanadamu anaweza kuchange attitude towards jambo fulani lakini anapobadilika kuna mambo mawili ...kwanza kabisa kuna sababu iliyosababisha aamini jambo hilo na anapobadilika kuna jambo pia limetokea na kusababisha aamini kuwa alichokuwa anaamini awali kilikuwa na mapungufu kwaiyo haoni sababu ya kuendelea kuamini jambo hil katika mtazamo huo kwa iyo anaamua kubadilika.
Nikiwa kama mwanafunzi wa 'human geography' ninaamini pia katika role ya time and space katika maisha binadamu...kwa maana ya kuwa wakati fulani unaweza kukubaliana na jambo fulani na kundi fulani....lakini wakati mwingine unaweza kutokubaliana na watu wale wale hata ukiwa mahali palepale ila utategemea kwenye jambo gani...kama ni AJENDA ILE ILE uliyokubaliana nao awali then tunaweza kukuhoji sababu ya wewe kubadilisha mtazamo wako na itabidi uwe na majibu ya kutomung'unya ili tuelewe mwenzetu una ajenda gani.....kama utamung'unya mung'unya huwezi kuzuia watu kukuadhibu kwa kukupa label yaulichoonyesha .....

Nipo naangalia bunge hapa... Dr Augustine Mrema amepewa nafasi ya kuchangia katika hoja ya ujenzi...Mh mrema ametumia muda mwingi kuwalaumu watu wanaomuona kama kibaraka wa serikali....ametumia muda pia kujastifayi kwanini ana iunga mkono serikali and more specific JK...akitaja mazuri aliyotendewa katika jimbo lake nk. amesema pia si lazima awaunge mkono watu wa chama fulani na ajenda yao kuandamana kwa sababu yeye kwa uzoefu wake wa uwaziri/naibu waziri mkuu anajua athari ya uvunjifu wa amani....tena ameenda mbali zaidi kwa kudai kuwa hakutumwa na jimbo lake kutaka nchi isitawalike!!

Mh. Mrema ninaamini kuwa watanzania wanaokuita au kukuhisi kuwa kibaraka wa serikali hawafanyi hivyo from no where! wamekupima maneno na utendaji wako toka umekuwa kiongozi wa umma wa watanzania. Ukiwa kiongozi wetu ndani ya ccm uliweza kutetea watanzania kwa nguvu zako zote, bila woga wala TAHADHARI....ulisimama kidete kutetea rasilimali zetu mfano loliondo...ulileta msamiati wa WALAHOI kuonyeshwa kukerwa na gap ya umaskini kati ya walionacho na wasio nacho....ukiwa upinzani miaka ya mwanzoni pia uliendelea na mapambano...hukuchoka kusuta serikali na sisi hatukuchoka KUSUKUMA GARI LAKO KUKUUNGA MKONO....
Ni sisi wale wale tulikuwa tunakuona kama kimbilio ndio tunafikiri au zaidi ya yote kuamini kuwa umekuwa kibaraka kwani mtazamo wako juu yaleyale uliyokuwa unayakataa / SERIKALI ILIYO LIKIZO ISIYOTEKELEZA MAJUKUMU YAKE HATA RASILIMALI ZAKE KUIBIWA NA WANANCHI KUWA WALALAHOI UMEBADILIKA.......... LEO SOKOINE ANGEKUWEPO NA ANGEKUWA ANAWATETEA WAHUJUMU UCHUMI ALIOKUWA ANAWASAKAMA........AU LEO HII MWALIMU ANGEKUWEPO AKATETEA UBEPARI.. NA KUANZA KUELEZEA SEHEMU YA UZURI WAKE TUNGEHOJI...kwaninini...kwa sababu jambo lilelile waliokuwa wanalikataa na kubuni mbinu za kupambanana nalo usiku na mchana ...sasa wanalizungumza kwa kulitetea NA KUJARIBU KUTUONYESHA UPANDE WAKE MZURI BILA KUGUSA KABISA UPANDE WA HASARA YAKE.


Hata wanachama wa magamba wanasema hali si shwari (rejea, warioba, kitine)...hata mwl nyerere foundation wenye ccm yao wanatumambia si shwari...so haiwezi kuwa shwari kwa sababu ya vijineno vyako ...endelea kula ulichopewa kama vita ya mafisadi imekushinda waache wenye uwezo nao waitekeleze huna haja ya kuwasakama waache na sera zao…..
KWAME NKURUMA, MWALIMU NYERERE, SOKOINE, LUMUMBA,WARIOBA WATAENDELEA KUHESHIMIKA KAMA VIELELEZO VYA UZALENDO KWA MATAIFA YAO...HAKUNA KILICHOWATENGANISHA NA UPENDO WA MATATIFA YAO, IWE NJAA, IWE SHIBE, IWE NI WAKATI WAKIWA MADARAKAI AU LA, HAWAKUYUMBA WALICHOKIAMINI WALIKITETEA hata baadhi yao kuuawa
kwani walijua mwanadamu kula matapishi yake ni dalili ya uendawazimu hakuna jina lingine

UMEANDIKA HISTORIA KATIKA TAIFA LETU MREMA na ITAKUHUKUMU
 
Back
Top Bottom