Mrema aitolea uvivu CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Wadau,

Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema ameyalaani vikali maandamano ya Chadema yanayoanza kesho nyanda za juu kusini. Mrema anadai kwamba CHADEMA wanaandamana kudai mambo ambayo tayari serikali inayafanyia kazi..ametoa mfano wa katiba mpya.

Mrema ameenda mbali zaidi na kusema kwamba CHADEMA wanataka kuvuruga amani na kuleta uchochezi ili nchi isitawalike. Amewasihi polisi wawazuie CHADEMA na kuvuruga mikutano na maandamano yao.

Mrema anajidai kusema kwamba eti yeye ndiye mwenye uchungu na nchi hii na ndio maana anakamata viongozi wa halmashauri wanaoendekeza vitendo vya ufisadi.

Hakika kila mtu aliyemsikia Mrema amejiuliza mara mbilimbili yeye ni nani hata aisemee serikali????
 
Kama anao uwezo wa kukamata, basi namshauri aende kuwakamata viongozi wa chadema watakao kuwa wanaongoza maandamano huko nyanda za juu kusini.
 
Hayo kuongelewa na Mrema ni mambo ya kawaida, huyu kesha rudi ccm siku nyingi na sio mpaka atangaze, mienendo yake ilionekena ha ta kabla ya uchanguzi uliopita na yuko chini ya ccm, TLP ni kivuli tu cha kumfichia aibu.
 
Msimpinge, muache Mrema apumzike.

Mwenye akili iliyo na afya hawezi kuwa na mgombea wa chama chake akampigia kampeni mtu wa cha chama kingne ili amuangushe aliyemsimamishe yeye,aya mambo yako ktk nchi ya kusadikika ya Mfalme Juha!
 
Kweli ana uchungu na nchi hii.....

babu mrema anaenda kuwakamata wananchi wilayani wanaopunguza bajeti ili waweze kupata mkate wa kila siku,akibaki kuchekelea mafisadi wanaoitafuna nchi,anafika hatua anamuomba mchakachuaji amteue awe waziri. Mrema is good for nothing to liberate the poor!
 
nafikiri kinachomsumbua ni njaa,halafu yule mzee mnafiki sana kama yeye alishindwa anataka wengine wasijaribu?
 
Naona historia yajirudia kwani mwaka 1991 alijaribu kuyazuia mageuzi kwa kulitumia jeshi la polisi (FFU) lakini hakufanikiwa. Wakati huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika serikali ya Mwinyi na alipoona mambo hayaendi alidandia gari la wanamageuzi. Leo, miaka ishirini baadaye, akiwa kachoka anaanza tena kuchangamkia makombo ya Kikwete kwa kuikandia Chadema - mambo yale yaleee ! Poor Mrema !
 
Heshima ya mwanaume ipo kwenye matumizi ya vichwa vyake viwili kimoja hupumzika uzee ukimtawala na cha pili huendelea kulinda heshima sasa huyu mzee vyote vimeharibika
 
Unajua Mrema amezeeka hadi akili......angejua angetulia tu na Posho za Ubunge maana Nyumbani kwake palikuwa pamechakaa sana angalau siku hizi panang'ara kidogo!
 
Taarifa ya habari ya leo nimesikia kuwa Mhe Mrema a.k.a Mzee wa Kiraracha akiwashauri Watanzania wasishiriki maandamano eti hayana faida wala hayatawaletea wananchi maendeleo.

Haki ya kuandamana ipo ndani ya katiba hivi walioiweka haki hiyo anaona wao ni wajinga, pili hii nikuwafanya watanzania kuwa hawana uwezo wa kufikiri kuwa kipi pumba na kipi mchele. Hawa jamaa MREMA+CHEYO na MBATIA kazi yao badala ya kufikiri kujenga vyama vyao wao wanafikiri kupambana kuibomoa CHADEMA kwa kuamua kuwa mavuvuzela ya CCM.

Mbaya zaidi ze la kiraracha ni mbunge wangu kule kijijini ila sikumchagua na wala sitakaaa kufikiri kuchagua mjinga kama huyu nasikia hata aibu kusema huyu ni mbunge wangu.
 
Wadau,

Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema ameyalaani vikali maandamano ya Chadema yanayoanza kesho nyanda za juu kusini. Mrema anadai kwamba CHADEMA wanaandamana kudai mambo ambayo tayari serikali inayafanyia kazi..ametoa mfano wa katiba mpya.

Mrema ameenda mbali zaidi na kusema kwamba CHADEMA wanataka kuvuruga amani na kuleta uchochezi ili nchi isitawalike. Amewasihi polisi wawazuie CHADEMA na kuvuruga mikutano na maandamano yao.

Mrema anajidai kusema kwamba eti yeye ndiye mwenye uchungu na nchi hii na ndio maana anakamata viongozi wa halmashauri wanaoendekeza vitendo vya ufisadi.

Hakika kila mtu aliyemsikia Mrema amejiuliza mara mbilimbili yeye ni nani hata aisemee serikali????

Jamani wanajf, mrema anafahamika toka enzi zile. Kapoteza mvuto wa kisiasa na kisura. Ni wakala makini wa magamba, kama walivyo baadhi ya wachungaji, mashehe na mapadri.
THESE PEOPLE INSIST ON PEACE BUT NEGLECTING HUMAN RIGHTS, this happen as their party ccm is being rejected in most areas.
 
Mrema analipa fadhira kwa lile lii-mprest alilopewa na JK kwenda India kutibiwa.Ana special assignment toka kwa JK YA KUHAKIKISHA ANAKISAIDIA CHAMA CHAMA MAGAMBA kwani kimemaliza mvuto kwa wenye nchi
 
ccm chama kubwa imekula sana kwangu-MREMA
Mrema anajua anachofanya , siku hizi wan-ccm B
nila kuipinga chadema wanakutema, hii ni mbinu ya kisayasi

Wadau,

Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema ameyalaani vikali maandamano ya Chadema yanayoanza kesho nyanda za juu kusini. Mrema anadai kwamba CHADEMA wanaandamana kudai mambo ambayo tayari serikali inayafanyia kazi..ametoa mfano wa katiba mpya.

Mrema ameenda mbali zaidi na kusema kwamba CHADEMA wanataka kuvuruga amani na kuleta uchochezi ili nchi isitawalike. Amewasihi polisi wawazuie CHADEMA na kuvuruga mikutano na maandamano yao.

Mrema anajidai kusema kwamba eti yeye ndiye mwenye uchungu na nchi hii na ndio maana anakamata viongozi wa halmashauri wanaoendekeza vitendo vya ufisadi.

Hakika kila mtu aliyemsikia Mrema amejiuliza mara mbilimbili yeye ni nani hata aisemee serikali????
 
Mrema alimpa nani kadi yake ya CCM alipoenda NCCR? Ukijibu hilo swali hutashangaa kauli yake?
 
Back
Top Bottom