Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu

Hatukufanikiwa kupata mtoto, ila gari ni replacement ya damage ya gari ambayo ni ya gari yangu ambayo nilinunua wakati hatujafunga ndoa. Anyway hata vikigawanywa pamoja wala sitojali ilimradi haki yangu ipatikani. Chanve ya yeye kuja mahakamani ni ndogo kwa sababu hakuweza kutoa ushirikiano ngazi ya familia na baraza la kata.
komaa naye huyo jamaa akupe portion yako kwenye nyumba. Mawaelewa wanaume ni watata sana hasa ukutane na mlafi wa mali. Mahakama itakupa guidence nini ufanye incase jamaa hata cooperate. Ni PM tu chat zaidi na tufahamiane zaidi. Mi mwenyewe yalinikuta hayo 4 yrs back. Komaa mpaka upate haki yako.
 
hivi huyu dada uselfish wake uko wapi????
Nyumba kamuachia mwanaume kapangisha...bila kukubaliana nae. Kwa lugha nyingine kodi kalamba yeye na hawara yake.

The gari alonunua kwa pesa yake pia kachukua anatumia na hawara yake....

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni






kwa hiyo huyu dada its okey kuondoka na begi lake la nguo tu???
ukichunguza sana huyo ni mwanamke mwenzake
 
Wanaume aliyeturoga kafa na huyo mwanamke wake anaona sawa kuvunja ndoa ya mwanamke mwenzake.

Na mbaya zaidi naona huyo mwanamke kaweka profile picture ya whatssup akiwa na huyu mwanume ameandika ''If you believe yourself anytyhing is possible''
 
Najifunza mengi sihangaiki tena kushirikiana na mtu nanunua sahani glass na vikombe siku akinitibua navunja vyote naondoka.
 
hiyo thread ya mwanzo niliipita tu bila kuifungua...ila kwa huu mrejesho...nakupa tu pole komaa akupe talaka yako muachane kisheria kabisa ili asije kukusumbua baadaye.
 
Ndoa ni mtihani wa mashaka. Maisha lazima yaendelee jipange upya mume sio ndugu yako songa Mungu atakupigania
 
Hata hvyo na wewe ni mvumilivu sana,na unaonekana una upole flani au niseme sijui ni ustaarabu umekujaa ndio maana mumeo kaamua kukutesa namna hii.kwa mwanamke mtata asingekubali kutoka kwenye hiyo nyumba wala kuruhusu huyo mwanaume aondoke na gari lake.
 
Umeona eeeh

Yaani pangechimbika kwa kucha....



Hata hvyo na wewe ni mvumilivu sana,na unaonekana una upole flani au niseme sijui ni ustaarabu umekujaa ndio maana mumeo kaamua kukutesa namna hii.kwa mwanamke mtata asingekubali kutoka kwenye hiyo nyumba wala kuruhusu huyo mwanaume aondoke na gari lake.
 
Ni mshenzi wa tabia huyo, wewe hakutaki gari lako analitaka....mfyuuuuu, Siku ya kesi kitu cha kwamza muombe hakimu huyo mwanah.....arudishe gari kwanza, asilete ujinga wake hapa.

Mdogo wangu, tulia kesi itaisha, taraka yako utapata, nakuhakikishia malipo ni hapa hapa duniani atarudi tena kwa magoti but atakuwa keshachelewa sana, All the best
 
Sasa ndio yametokea yote hayo, ndugu zake wanajua, serikali ya mtaa wanajua na kata wanajua so mimi sidanganyi na haya yametokea. Wazazi wake na ndugu zake upande wa baba wamemsusia wamesema niende mahakamani nikadai haki yangu na wako pamoja na mimi kwa sababu wananifahamu vizuri na jinsi nilivyohangaika na mtoto wao.

Hii ni messege aliyonitumia baba yake mzazi nanukuu ''Mama nakupenda sana hujanikosea hata siku moja hata kama mtaachana mimi usinitupe, kuhusu suala ya kusimamia huyo mwanangu mimi siwezi nimeshindwa, nenda serikali ya mtaa, polisi au mahakamani upate haki yako'' mwisho wa kunukuu. Hii messege ninayo mpaka sasa hadi nimeiprint kabisa

Komaa mamangu hadi kieleweke, hawa watu sio wa kuchekea kabisa
Kwanza aliondokaje na gari.....duh! yaani pangechimbika, sijui nani angekuja kuamua, uondoke na mali niliyoinunua kwa pesa yangu, tumeishi muda wote huna la maana ulilonifanyia zaidi ya kuninyanyasa leo uondoke na mali yangu? una huruma sana bidada, namuonea huruma sana huyo mkaka, kwani majuto ni mjukuu
 
Back
Top Bottom