Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Sasa b17 unabakiaje bongo tena?
Ni rahisi kuchukua ela ila uwa ni vigumu sana kuhamisha ela ukaitumia kihalali. Mfano uuze dawa za kulevya then uingize ela kwenye mzunguko, au uibe pesa bank bils kadhaa then usepe nazo nje ya nchi. Mafisadi tu viongozi wa serikali ndo uwa wanaweza hilo kirahisi.
 
Kama hakuwa na leseni tangu ameanza kufanya walikuwa wapi kwenda kumkamata hadi inafika miaka 3 ndio wanaenda kumkamata leo,walikuwa hawaoni kama anafanya makosa?
Serikali sio Mungu kwamba wajue kila kitu kwa wakati muafaka. Wanahitaji mpaka wapate taarifa aidha toka kwa walioathirika na kosa husika, au wapate taarifa za kiintelijensia toka kwa vyanzo vyao n.k. Na wakipata taarifa wanahitaji kujiridhisha pasi na shaka kuwa kweli kuna kosa limefanyika. Hapo ndipo uchunguzi/ upelelezi unapoingia. Kwahiyo kama taarifa hazijawafikia there is no way wanaweza kuchukua hatua yoyote.

Tukumbuke pia, mhalifu nae anajua anachokifanya kuwa ni haramu. Kwahiyo atatumia kila njia kuukwepa mkono wa sheria, na ndio maana inachukua muda mrefu kwa baadhi ya wahalifu kutiwa hatiani. Wote tunajua, kabla ya Anko Magu mtu alikuwa anafanya uhalifu na anatamba mitaani bila kukamatwa. Angalau sasa mambo yamebadilika, ni suala la muda tu - wahalifu hawana maisha marefu mtaani. It's not a rocket science.
 
Binafsi nadhani watu kama hawa sio wakuwa discouraged.. Kwanini wasinge mtengenezea mazingira ya kulipa kodi?

Alafu mbona sijasikia kama kunashitaka hata moja la malalamiko kutoka kwa wateja wake.. What is hidden behind this

Kama ni kweli biashara aliyofanya ilitimiza mahitaji ya wateja wake basi serikali imfanye mfano wa kuigwa sababu



Mfanyabiashara, Tariq Machibya (29) maarufu kama Mr. Kuku, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kufanya biashara ya haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za Umma zaidi ya Tsh. 17 bilioni.

Machibya ambaye ni mkazi wa Oysterbay amesomewa mashtaka yake leo 10/08/2020 na Wakili wa Serikali muandamizi mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Godfrey Isaya. Akisomewa mashitaka yake, mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi na 60/2020, kati ya mashitaka hayo 7 yapo ya kusimamia na kuendesha biashara haramu ya upatu, kupokea maingizo ya fedha za umma bila ya kuwa na leseni na kutakatisha fedha.

Mfahamu zaidi Mr. Kuku:
Mr. Kuku Farm ni aina mpya ya DESI?
Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku
 
Hahaha watanzania wanapenda sana hizi, waweke pesa mahala wao wakalale wakingoja faida.

Hakuna mtu wa kukufanyia kazi ukiwa umelala nyumbani, ona sasa pesa inaenda kutaifishwa na serikali na hamtalipwa, labda mfungue kesi ya madai.
Hata wafungue ya madai hawatapata kitu,wale wa Deci walianza kufuatilia mpunga wao wakashangaa tu wamewekwa ndani walivyotoka mpk leo hawaulizii tena mbegu zao walizopanda.
 
Handsome anavutia, kakunja nne mweyewe hana wasiwasi
Hata wakina Rugemalira na yule Mhindi mwanzoni walikua wanakunja 4 pale mahakamani ila kilichofuata sasa...
images-4.jpg
 
Ashakum si matusi. Tuwiane radhi, kawadhulumu wenye akili za kikuku.
Baada ya DECI, D9 na upumba.vu mwingi wa aina hiyo, watu bado hawakushituka ??

Kesho mwingine atakuja kwa staili nyingine na Ponzi scheme mpya na watu wataingia mkenge.

Hakuna hela ya short cut. Labda uibe, udhulumu nk.
Wajinga, wapmbv hawaishi wanazaliwa kila leo

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Huu unaoitwa utapeli na uharam wa biashara ya Mr Kuku umefanyika Kwa miaka minne na matangazo kwenye social media hadi Kwa radio.

Inakuwaje serikali inatazama watu wanapigwa hela kutoka bilion moja imekusanywa hadi bilioni 17 baada ya miaka minne ..ndo wanaamka na kusema
Hii biashara haram..

Serikali ilikuwa wapi Kwa miaka minne??? Hadi Joti anapewa kazi ya kutangaza?..
Waliopigwa hela waishitaki serikali Kwa uzembe huu???
 
Walikuwa bize na wapinzani kwanza. Any way, kibongo bongo vya muhimu havipewi kipaumbele, na vinavyopewa vipaumbele, vingi havina umuhimu.
 
Back
Top Bottom