Mpenzi au mke wako akibakwa...

Mbu

Kuna wengine usikute wanachangia kwa vile wanatajiriba husika.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
kuna familia ambayo ni kama jamaa zangu wa karibu, walivamiwa na majambazi usiku, mke na watoto wa kike walibakwa mbele ya baba mwenye nyumba. it was so sad, haielezeki. but cha ajabu, after a week baba alihama nyumba akaenda kuishi sijui wapi, lakini baada ya miezi miwili the same baba akafa kwa pressure.
watu walijiuliza maswali bila majibu, lakini ndivyo ilivyokua. This was about 10 year ago. The same familia iliyobaki, wanaishi kwa mashaka na vichwa vyao havijatulia hadi leo, mabinti wako watatu ni wakubwa wanapaswa kuolewa na kua na watoto, lakini hakuna hata mmoja amehabatika. na sijawahi kusikia hata kuna mwenye mahusiano. Ni Maisha magumu kusema kweli.
 
Mbu

Kuna wengine usikute wanachangia kwa vile wanatajiriba husika.

tajiriba nm uzoefu mtu alionao katika kutenda jambo.

....inasemekana kati ya watu 50% mpaka 90% tunakabiliwa na post traumatic stress disorder ya aina fulani,
wasiwasi na wahka, woga, kutojiamini, nk ni viashiria kwamba huko udogoni mpaka umri tulionao kuna vitu vili trigger hizo reactions...ndio maana nimesema reaction ya mtu itakuja iwapo tu akishakumbana na hali hiyo....

kuna watu reaction yao ya kwanza kwenye trauma ni kukimbia, wengine kilio, wengine kuzimia, wengine ugomvi, wengine kuzubaa mpaka wakurupushwe na kofi..., nadhani la kuhofia zaidi ni reaction ya pili (secondary reaction) itayofatia baada ya maamuzi ya awali (primary reaction)... ogopa sana watu walio na uwezo mkubwa wa kuficha hisia zao.
 
Hii imenikumbusha kipindi nimeitm f6 miaka kadhaa nyuma mpenzi wangu alibakwa na mwl wake kulikopelekea yule mwl kufungwa kiukweli ni ngumu sana kuendelea na mahusiano hasa jambo linapokuwa wazi kwa jamii nilikuwa nikimpenda sana yule binti ila mahusiano yaliishia pale sikuwa na amani naye tena sikuwa na furaha tena kwa sababu uhusiano wetu ulikuwa wazi so may be inadepend na m2 ila kikawaida ni ngum sana
 
kwa kweli mi sielewi itakuwaje maana sijui kamaa nitweza kumwambia au nifiche
 
Hili ni jaribu kubwa sana na gumu sana, katika hali ya kawaida ni ngumu kulitolea majibu, mungu aepushie mbali.
 
Dah....Hii ni sawa na Kugongewa Tu halafu Unalazimishwa Kusamehe...Hakuna Jinsi, utachukulia poa, mtapima ht kwa psyschologist mtaenda ila Dah...aseeeee....Epusha.......Mapenzi yanaweza Badilika sana...
 
Katika hiyo nyekundu, mtu akibakwa na ikithibitika aliembaka ana HIV, kuna tiba inaitwa Post Exposure Prophylaxis (PEP) inatolewa karibu na health centres zote... It has to be administered with 78 hrs tokea hilo tukio litendeke. Hivyo one should also think of that ili tusifikie kutengana vyumba baadae.

Then hiyo ni sababu nyingine ya msingi ya kutoficha the incident ya kubakwa! Ule msemo wa "sema shida yako usaidiwe" ndio unaapply hapo; maana ukificha waweza ficha ugonjwa!
 
Kuna jirani yetu walivamiwa na "majambazi" wakaondoka na mkewe. Wakampeleka wanakokujua wakambaka. Mama akalazwa hospital for days. But the way I see them they are still in love.

Watu wanadai ni business partners wake walimfanyizia sijuhi aliwadhulumu; maana walikuwa wamepania kweli. Sijawahi kusikia wezi wanaondoka na mke wa mwenye nyumba nadhani ni kweli ni kisasi.
 
Kingine ni kuepusha tuwapendao na mazingira hatarishi yanayopelekea kubakwa. Hii ni pamoja na kuwapa elimu mabinti wadogo kwani hao ndio target kubwa ya wabakaji.
 
Kwa mfano, mtu amebakwa alikuwa ameenda kwenye semina na warsha huko na akapewa kinywaji na kuchukuliwa; huyo anaweza kweli kusema alibakwa au anaweza kujikuta anahalalisha na hivyo hasemi lolote?
 
Kwa mfano, mtu amebakwa alikuwa ameenda kwenye semina na warsha huko na akapewa kinywaji na kuchukuliwa; huyo anaweza kweli kusema alibakwa au anaweza kujikuta anahalalisha na hivyo hasemi lolote?

Naamini ukibakwa katika mazingira hayo au katika kipindi mume/mpenzi kasafiri kumhadithia inakuwa ngumu. Unaweza mwanamke kuchukua hatua zote kama kwenda kupatiwa hizo dawa au kuwashtaki polisi (hapa kwa mtu mwenye strong will kweli kweli), lakini suala la kuhadithia kwa mume/mpenzi gumu sana kwa kuogopa shutuma.
 
Ndio maana nimesema kuna mazingira hatarishi ambayo wanawake tunajiingiza wenyewe either kwa kujua au bila kujua. Mwanaume ambaye si ndugu yako hupaswi kuwa naye faragha iwe kwenye warsha au mko college.

Kwa mfano, mtu amebakwa alikuwa ameenda kwenye semina na warsha huko na akapewa kinywaji na kuchukuliwa; huyo anaweza kweli kusema alibakwa au anaweza kujikuta anahalalisha na hivyo hasemi lolote?
 
Afu mwanakijiji mtu mzima akibakwa inakuwa ngumu kuaminika. Labda wale waliovamiwa na majambazi. Yani na utu uzima huu kweli nibakwe. Ngumu aisee kuna many treaks za kujinasua including kujifanya ume give in afu unang'ta hiyo mic. Labda wanichangie watu kadhaa; ila mmoja hawezi kunibaka ng'o.

Tatizo naloliona ni kwa wanawake walevi. Hao ni rahisi sana kubakwa.

Kwa mfano, mtu amebakwa alikuwa ameenda kwenye semina na warsha huko na akapewa kinywaji na kuchukuliwa; huyo anaweza kweli kusema alibakwa au anaweza kujikuta anahalalisha na hivyo hasemi lolote?
 
Ndio maana nimesema kuna mazingira hatarishi ambayo wanawake tunajiingiza wenyewe either kwa kujua au bila kujua. Mwanaume ambaye si ndugu yako hupaswi kuwa naye faragha iwe kwenye warsha au mko college.

Shutuma kama hizo hasa ndizo zinazomfanya mwanamke asihadithie likimkuta. Ataambiwa ilikuwaje ukafungua mlango na wewe uko peke yako? Your colleague anaweza gonga mlango akitaka some certain documents. Hutafungua mlango?

In reality mtu huwezi kuwa conscious kuzuwia hatari wakati wote. Na kama zinavyotokea ajali nyengine, ndio zinavyotokea hizo.
 
Nilikuwa napitia hii ripoti ya UNICEF kuhusu sexual violence kwa watoto Tanzania; nikaona kuwa wengi sana wanafanya kitendo cha kwanza cha mapenzi bila kuwa na hiari - yaani wanalazimishwa. Yaani, wengi ya wasichana wanavunjwa bikira katika mazingira ya kubakwa. Sasa kitu kingine ambacho nimekiona ni kuwa baada ya tukio hilo la ubakaji hao hao mabinti wanaweza kujipeleka kwa mbakaji (mara nyingi ni boyfriend) na baadaye wanaanza mahusiano "halali".

Kwanini mabinti katika mazingira hayo hawatoi taarifa za kuwa wamebakwa?
 
Kwa mfano, mtu amebakwa alikuwa ameenda kwenye semina na warsha huko na akapewa kinywaji na kuchukuliwa; huyo anaweza kweli kusema alibakwa au anaweza kujikuta anahalalisha na hivyo hasemi lolote?

Huyo kajibakisha.
Na anaweza kukaa kimya maana anajua kafacilitate kubakwa kwake.
OTIS.
 
Back
Top Bottom