Movement for change (m4c) imeishia wapi?

Makyomwango

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
322
79
WANA BODI
Wakati wa uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, CDM walianzisha mpango maalum wa watanzania kujikomboa kwa kupewa elimu ya uraia mijini na vijijini. Ili kufanikisha mpango huu watanziniawaishio arusha na sehemu nyingine walialikwa katika hotel moja huko arusha kwalengo la kuchanga fedha za kugharamia mpango huo.

Wengi tuliupokea mpango huo kwa furahana tukidhani ni endelevu, lakini sasa naona siku zinakwenda tu bila kutaarifiwa nini kinaendelea juu ya mpango huo wa kuwakomboa watu wetu hususan wa vijijini.

Nawaomba viongozi wa CDM watoe utaratibu wa kuutekeleza mpango huo kwa kila mkoa ili wale wote wenye nia njema na nchi hii wajiandae kwa hali na mali kuwakomboa watu wao chini ya ukoloni mamboleo wa magamba kupitia mpango huo.
 
Wanabodi tunaunga mkono hoja yako ila pia kuna watu wameanza kuhoji mapato na matumizi.
Ni vyema pia tukapata mrejesho wa jinsi michango yetu ilivyotumika ili kuweka uwazi zaidi. tusije kuonana wabaya bure!
 
Huwa hatukurupuki kuanzisha vitu, sisi siyo ccm, kila jambo lina wakati wake wa kufanyika, ratiba ilivyokaa sasa baada ya uchaguzi mdogo ni kurudi ofisini na kujipanga, kuna kikao cha bunge, baada ya hapo kamati kuu itakaa na itatoa ratiba ya shughuli za chama. Kuwa na subira.
 
Mshituko wa kunyang'anywa ubunge Arusha mjini umepotezea dira

Wanachama, Wapenzi na washabiki wa magamba (CCM) wako katika makundi mawili
  1. Kundi la kwanza ni lile linalofaidika na mfumo uliopo sasa bila kujali athali zinawapata watangayika wengi ambao wakosa elimu, matibabu na huduma nyingine nyingi muhimi. Kundi hili limejaa watu wabinafsi kupita kiasi na lijumuisha watu kama mwigulu nchemba, lusinde, Nape, Sita n. k.
  2. kundi la pili ni wale wote wanaoshabikia magamba bila kujijua na hawana sababu ya kuipenda na kushabikia CCM. Hawa wapowapo tu na wanapelekwa pelekwa kama vile mchungaji wa ng'ombe anavyowapeleka peleka ng'ombe wake machungani

Je wewe mama porojo ukiwa shabiki mkubwa wa magamba upo katika kundi gani kati ya hayo mawili?
 
WANA BODI
Wakati wa uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, CDM walianzisha mpango maalum wa watanzania kujikomboa kwa kupewa elimu ya uraia mijini na vijijini. Ili kufanikisha mpango huu watanziniawaishio arusha na sehemu nyingine walialikwa katika hotel moja huko arusha kwalengo la kuchanga fedha za kugharamia mpango huo.

Wengi tuliupokea mpango huo kwa furahana tukidhani ni endelevu, lakini sasa naona siku zinakwenda tu bila kutaarifiwa nini kinaendelea juu ya mpango huo wa kuwakomboa watu wetu hususan wa vijijini.

Nawaomba viongozi wa CDM watoe utaratibu wa kuutekeleza mpango huo kwa kila mkoa ili wale wote wenye nia njema na nchi hii wajiandae kwa hali na mali kuwakomboa watu wao chini ya ukoloni mamboleo wa magamba kupitia mpango huo.

Naona leo umetimiza kamwaka kamoja kamili toka ujiunge na JF. Hongera kwa haka kanyimbo ka birthday. M4C ipo Dodoma kaka.
 
Kweli mkuu nakuunga mkono LEMA akabidhiwe uchangishaji maana hali ya kiuchumi ilikuwa si njema baada ya kutemwa kwenye ULAJI.
Nauunga mkono LEMA aongoze M4C

kaka umesoma? Maana ya M4C sio michango,ni mpango wa cdm kuzungka kuwapa elimu watz like operation sangara..kiazi una pupa wewe mbona?
 
WANA BODI
Wakati wa uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, CDM walianzisha mpango maalum wa watanzania kujikomboa kwa kupewa elimu ya uraia mijini na vijijini. Ili kufanikisha mpango huu watanziniawaishio arusha na sehemu nyingine walialikwa katika hotel moja huko arusha kwalengo la kuchanga fedha za kugharamia mpango huo.

Wengi tuliupokea mpango huo kwa furahana tukidhani ni endelevu, lakini sasa naona siku zinakwenda tu bila kutaarifiwa nini kinaendelea juu ya mpango huo wa kuwakomboa watu wetu hususan wa vijijini.

Nawaomba viongozi wa CDM watoe utaratibu wa kuutekeleza mpango huo kwa kila mkoa ili wale wote wenye nia njema na nchi hii wajiandae kwa hali na mali kuwakomboa watu wao chini ya ukoloni mamboleo wa magamba kupitia mpango huo.

Kinachofanyika Dodoma ni mwendelezo wa mpango wa M4C umeisoma kaka?
 
Wanabodi tunaunga mkono hoja yako ila pia kuna watu wameanza kuhoji mapato na matumizi.
Ni vyema pia tukapata mrejesho wa jinsi michango yetu ilivyotumika ili kuweka uwazi zaidi. tusije kuonana wabaya bure!
Ujinga utakuua siku si nyingi, mambo ya CHADEMA yanakuhusu nini wewe mpumbavu? nenda Zanzibar kanyapalie kuvunja muunguna fisadi usie na haya!
 
Binafsi nawapongeza sana CHADEMA kwa kuibuka na kauli mbiu hii mwanana kwa watanzania wenzao, Movement for change!!

Kwa hali ya mambo inavyoendelea hapa nchini mwetu ni lazima tufanye mabadiliko. Lakini kama jamii ni lazima tujue aina ya mabadiliko tunayoyataka, tunayapataje mabadiliko hayo na athari chanya na hasi za mabadiliko hayo ni zipi. Mabadiliko yetu yasiwe ya kivyama, kikabila, kidini au kijinsia. tunataka mabadiliko ya taifa letu kwa faida yetu na ya vizazi vijavyo.

Lazima tujue ni mabadiliko gani yanatakiwa kwenye nyanja ya siasa, elimu, Jamii, kiuchumi na kimahusiano baina yetu. Bila kujua aina ya mabadiliko tunayoyataka bila shaka tutaishia kupaka rangi mpya kwenye gari lenye injini ya zamani. Vyama vya siasa vituongoze (CHADEMA wameonyesha mfano) kwenye kuleta mabadiliko tunayoyatarajia lakini vyenyewe visijigeuze ndiyo mabadiliko.

Tunahitaji mabadiliko makubwa sana kwenye mihimili ya serikali yetu. Tunahitaji tuwe na Mahakama tunayoiamini, tunahitaji tuwe na dola linalojali maslahi ya Umma na bunge linalotunga sheria zenye kuleta ustawi wa jamii. Kwenye mijadala ya kuleta mabadiliko tusileta mauza uza wala mikingamo kwa faida ya vyama vyetu vya siasa.

Watanzania tuvuke kizingiti cha kubaguana kifikra kwa kuegemea dini zetu, vyama vyetu vya kisiasa au makabila yetu, tutumie fursa iliyopo mbele yetu kabla ya mwaka 2015 kuleta mabadiliko ya kweli kwa taifa letu kwa sasa na hata kwa vizazi vijavyo. Asitudanye mtu kwamba hali iliyopo hivi sasa ni shwari wala asitutishe mtu kwamba kufanya mabadiliko itakuwa dhahama kwetu. Pia wasizuke watu kusema bila wao mabadiliko si mabadiliko mpaka wao waone kama ni mabadiliko. Tanzania ni yetu sote!!

Tufanye mabadiliko kwa faida ya nchi yetu!!
 
Back
Top Bottom