MORE PRESSURE: CDM Wasiposhinda Arumeru East Uongozi mzima wa Taifa LAZIMA Ujiuzulu

Madai yako hayana justification ya kuwalazimisha viongozi wa juu wajiuzulu. Ume-draw conclusion kwa kutumia sample ndogo sana. Tume huru ya uchaguzi ikipatikana unaweza uka-draw hiyo conclusion ila sio kwa mazingira ya sasa.
 
Huko kwenye suala la uchaguzi hujaona hoja zinazoelezea ununuzi wa vitambulisho vya kura, kutokuboreshwa daftari la wapiga kura na uchakachuaji wa matokeo. labda macho yako yanaona unayopenda kuona?

Ukiendaa kucheza mpira ukichezewa rafu ukaja kushindwa husingizii nilichezewa rafu, vaa shin guard. Hayo malalamiko unayoyasema tunayasikia hata CCM wanalalamika. Mwisho wa siku, umelambwa magoli.

Sasa wewe unasema nini kuhusu Josephine kuwa kinara makao makuu mpaka "software za mahesabu" kuweka yeye? walinzi wa kanisa lake kulipiwa na chama, posho ya hausigeli wake kuliko yako. Halafu anadanganya umma kuwa mkewe, hata akiwa mkewe ndyo yafikie hayo? hapo hajaolewa bado, akiolewa?
 
Mwanakijiji nafikiri ulichokisema ni sahihi,mi nakumbuka jinsi Mh zitto alivyoshinda kule kigoma kask,ilikuwa ni pamoja nakutambua kura zake kupitia kuratibu watu wenye vitambulisho wote,hivyo akawa anafahamu watu wote watakaompigia KURA, na hata mtu akihama kambi tayari mnapunguza idadi yenu ya kura..kinachotakiwa kufanyika ni kuwatumia vijana wa kila kijiji kuratibu zoezi hilo kwa vijijin watu wanafahamiana sana..hii itawezekana kufahamu idadi ya watu watakaompgia kura Nassari kijana wangu pale Tabora school.Pia inatakiwa kila siku wakutane nakutoa ripoti kama kuna mabadiliko ya idadi.....Jana nilikuwa naongea na rafiki yangu ambaye ni mkazi wa Arumeru ananiambia hali sio nzuri kwa uoande wa CCM ila akasema kuwa vijana wengi hawna IDs za kupigia kura....
 
Mwanakijiji nisikufiche
nilikuwa nafikiria hili swala ila nadhani nilipungukiwa na ujasiri. Wewe umeweka standard ya juu sana.

Wakishindwa wajiudhuru, Ili tupate viongozi wengine wakutupeleka kwenye next level ya mashtaka yetu.Ni lazima tufikie mwisho, tunakoelekea ni kwenye kuzoea harakati, malalamiko na chaguzi zisizo kwisha, itafikia wakati tutasahau hata tunachokipagania ni nini.

Mwanamke gani huyu asiyezaa. Tusipopata mtoto sasa uondoke.

Yaani mnataka na Zitto Kabwe wetu aondoke!!......wewe kweli ni CHADEMA au Agent wa CCM? usikate tawi la mti uliyokaria bandugu.
 
Mzee Mwanakijiji nimependa jinsi ulivyo "dare devil" kutoka zile makala za "utopia" into reality!.

Nilipopinga Dr. Slaa kususia matokeo nilieleza baadhi ya hizi hoja ulizo kuja nazo kuhusu Chadema kusaini "rules of the game", na kwamba watacheza fair play in "playing by the rules" na wakati wanatambua wazi "the playing field is not level" walitegemea nini?.

Nimezisoma kwa makini hoja zako zote, Arumeru is the same game played by the same players using the same rules and the same field!. Tusubiri matokeo ndipo nitayamalizia ya kwangu, nisije nikayasema sasa nikaonekane nawachuria watu bure!.

Uchaguzi wa Arumeru ni litmus paper ya 2015 ili kubaini acidity au alkalinity ya reactors zetu!. Chadema wakishinda Arumeru, moto wa mageuzi utakolezwa rasmi na the wind of change will sweep accross Tanzania!. There will be no turning back ni mbele kwa mbele mpaka Magogoni!. CCM ikishindwa huu utakuwa ndio mwanzo wa mwisho wa utakoloni wa CCM, na kitakachobakia ni kufungasha tuu virago vyake taratibu na kujiandaa kuitwa Chama Kikuu cha Upinzani!.
 
Mwanakijiji  nafikiri  ulichokisema ni sahihi,mi nakumbuka  jinsi  Mh zitto   alivyoshinda  kule  kigoma kask,ilikuwa ni pamoja nakutambua kura  zake kupitia  kuratibu watu  wenye vitambulisho  wote,hivyo  akawa   anafahamu  watu wote watakaompigia KURA, na hata  mtu  akihama  kambi tayari  mnapunguza  idadi yenu ya kura..kinachotakiwa kufanyika  ni kuwatumia  vijana  wa kila  kijiji  kuratibu zoezi hilo  kwa  vijijin watu wanafahamiana sana..hii itawezekana  kufahamu idadi  ya watu watakaompgia  kura Nassari  kijana  wangu  pale Tabora  school.Pia inatakiwa  kila siku  wakutane nakutoa  ripoti  kama kuna mabadiliko  ya idadi.....Jana nilikuwa naongea  na rafiki  yangu ambaye ni mkazi wa  Arumeru  ananiambia hali  sio nzuri  kwa uoande wa CCM ila akasema  kuwa  vijana wengi hawna IDs  za kupigia kura....
 
Madai yako hayana justification ya kuwalazimisha viongozi wa juu wajiuzulu. Ume-draw conclusion kwa kutumia sample ndogo sana. Tume huru ya uchaguzi ikipatikana unaweza uka-draw hiyo conclusion ila sio kwa mazingira ya sasa.

Kwi kwi kwi, teh teh teh! tume ya uchaguzi ilikuwa huru au ilikuwa livu pale mlipopata kiti kimoja kwenye chaguzi ndogo?

Maji yamewafika shingoni Arumeru, mnajuwa hakuna ushindi, mnaanza kuja na kila sababu. CCM wanasema kwa sasa hawataki mchezo, kama ni "upiganaji" basi vita mbele!

Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeezzzzzzzz Pwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Mwanakijiji  nafikiri  ulichokisema ni sahihi,mi nakumbuka  jinsi  Mh zitto   alivyoshinda  kule  kigoma kask,ilikuwa ni pamoja nakutambua kura  zake kupitia  kuratibu watu  wenye vitambulisho  wote,hivyo  akawa   anafahamu  watu wote watakaompigia KURA, na hata  mtu  akihama  kambi tayari  mnapunguza  idadi yenu ya kura..kinachotakiwa kufanyika  ni kuwatumia  vijana  wa kila  kijiji  kuratibu zoezi hilo  kwa  vijijin watu wanafahamiana sana..hii itawezekana  kufahamu idadi  ya watu watakaompgia  kura Nassari  kijana  wangu  pale Tabora  school.Pia inatakiwa  kila siku  wakutane nakutoa  ripoti  kama kuna mabadiliko  ya idadi.....Jana nilikuwa naongea  na rafiki  yangu ambaye ni mkazi wa  Arumeru  ananiambia hali  sio nzuri  kwa uoande wa CCM ila akasema  kuwa  vijana wengi hawna IDs  za kupigia kura....

Hayo ma nbsp ndio madudu gani sasa? kama hauna kifaa cha uhakika cha kuingia nacho mtandaoni si bora ungetafuta internet cafe kuliko kutuwekea mavitu ya kuchafua nyuzi?
 
Mzee Mwanakijiji,
Hivi unategemea kweli viongozi wa Chadema wakishindwa uchaguzi Arumeru Mashariki wajiuzulu...
 
mwanakijiji ni ukweli kwamba article yako umeianalyse sana theoroticaly and not practialy, wanafalsafa huwa wanasema kwamba'' ukisahau historia ya maisha yako basi wewe utakuwa ni mtumwa wa maisha yako''
hivi tungeweza kupata uhuru kweli kama waasisi wetu wakina jk nyerere, nkwame nkurumah, nelson mandela etc wangejiuzulu kizembe zembe kwa makosa ya mkoloni mwenyewe/ mfano mkoloni alitunga sheria au katiba kandamizi ambayo ilikuwa ikikwamisha na kuchelewesha ukombozi wa mwafrika, but licha ya vikwazo vyote hivyo waasisi wetu hawakujiuzulu na badala yake wakaendeleza mapambano kwa kuishinikiza serkali ya mkoloni ktk mambo mbalimbali mpaka kikaeleweka, kwani kama waasisi wetu wangeweza kujiuzulu eti kwa sababu ya ubaya wa katiba ya mkoloni basi wangekuwa tayari washajitangazia kushindwa na hatimaye wangekuwa wamempa mkoloni nafasi ya kuendelea kutawala milele.
so hata kwa viongozi wajuu wa chadema hawana hata chembe ya hatia ya kujiuzulu kwani tatizo silao bali tatizo lipo ubovu wa katiba hii na tume ya uchaguzi, na kama tukisema wajiuzulu kwa sababu ya hoja zako nyepesi basi ujue kwamba viongozi wa chadema watakuwa wameshajitangazia kushindwa na hapo moja kwa moja watakuwa wameipa nafasi ccm kutawala milele, jua kwamba uongozi wa juu ya chadema upo imara sana kuliko hata jinsi ww unavyofikiria zas y kila siku wan ccm na awtu wasioitakia mema chadema wanafanya kila jitihada kuwachafua viongozi wa chadema kwa sababu wanajua kwamba ukishawaua kisiasa slaa, mbowe , zitto etc ndio utakuwa mwanzo na mwisho wa chama makini chadema.
my take.
ni kwamba uchaguzi wa arumeru ndio mwanzo mwingine wa ccm kujichimbia kaburi lake kama endapo chadema itashinda huu uchaguzi kwani chadema itakuwa imeyatangazia maeneo mengine ya tz ikiwemo na kwetu tabora kuwa mabadiliko na ushindi vimewadia pia ushindi huo wa chadema ndio utakuwa mwanzo mwingine mpya wa migogoro mikubwa ndani ya ccm ambayo itakuwa ni advantage kwa chadema.
pia endapo ccm itashinda arumeru basi utakuwa ni mwanzo mkubwa tena katika kupata tume huru ya uchaguzi na na katiba mpya iliotakasika kwa jasho la wapiganaji waliopigania kwa harakati zilizotokana na uchungu wa kuonewa na kukandamizwa na chama tawala kupitia ubovu wa katiba na tume ya uchaguzi.
 
Nimewahi kumwandikia Dr. Slaa kwenye wall yake kuwa wawe makini na voter's robbing wa ccm. Hawa kazi yao kubwa ndo inawafanya ccm waibuke kidedea na sie tubaki tunalia jamaa wanahaa kuhakikisha wanafanya uhakiki wa wapiga kura wao mapema na wanakuwa na uhakika wa watu hao kupiga kura. Chadema wanajaza watu kwenye mikutano yao ya kampeni na kudhani wamemaliza kazi kumbe wamesahau primary objective ambayo ni kumake sure watu wanawapigia kura kwa kila njia
 
"Siwezi kujiuzulu kwani mimi sikuwa mgombea wala mpiga kura, kwani nikijiuzulu ndiyo CHADEMA itatangazwa mshindi Arumeru?"
 
nimependa jinsi ulivyo ainisha taarifa yako ina leta maana na ni upembuzi yakinifu
 
CHADEMA, sasa hivi ni uchaguzi Arumeru Mashariki. Nguvu zote, akili yote, maarifa yote na sala zote zielekezeni huko. Stay focus. Muda wa kuongelea mfumo na uendeshaji wa chama utakuja, lakini kwa sasa barabara iko moja - Arumeru Mashariki Road.

Maoni yangu, wekezeni kwenye wakala, na ongeza juhudi kwenye field force ili watu wasiuze shahada zao na siku ya kura kila mtu aje na mwenzake. Mwenye maoni (specifically) kuhusu namna ya kuboresha campaign Arumeru na afanye hivyo, muda wa mfumo utawadia.
 
Hayo ma nbsp ndio madudu gani sasa? kama hauna kifaa cha uhakika cha kuingia nacho mtandaoni si bora ungetafuta internet cafe kuliko kutuwekea mavitu ya kuchafua nyuzi?

Hata mimi naona kuna nbsp humu ndani!! kweli "Jf never boring"
 
Pamoja na hayo yote Mzee Mwanakijiji uliyoeleza, bado CHADEMA wanayo kila sababu ya kujivunia mafanikio ya chama ambayo yameletwa na huu uongozi. Binafsi nawapongeza viongozi wa CHADEMA taifa kwa kazi kubwa wanayoifanya. Record ya CHADEMA katika chaguzi ndogo ni nzuri na ni ya kujivunia, tatizo ni hali wanayopambana nayo ya 'CHAMA DOLA'. tunajua hali ilivyokuwa BUSANDA na BIHARAMURO vitisho na kila aina ya hujuma zilifanyika ili CHADEMA isishinde. Huwezi leo hii kuwahukumu CHADEMA ili hali unajua uwanja wa mashindano hauko level!. Tuko kwenye tatizo la kikatiba! wasimamizi wote wa uchaguzi kwa sasa ni wateule wa mwenyekiti wa chama dola! hapa unategemea nini!.
 
Jamaa yangu umejaribu kuchambua ndio but unatakiwa uangalie pia hali ya chama katika jimbo husika kabla ya uchaguzi mdogo kufanyika na matokeo ya kura baada ya uchaguzi mdogo. Pia zingatia rafu zinazochezwa na CCM kwa maana kuwa wanaomba kura wakiwa tayari na kodi za wananchi mikononi mwao. Kwa mfano; Magufuli alipoenda Igunga aliwaapia wananchi kuwa atawajengea barabara kwani yeye ndiye waziri wa ujenzi. Na arumeru umesikia kwamba ambaye amepoteza kitambulisho hataruhusiwa kupiga kura ingawa jina lake na picha vinaonekana kwenye daftari la mpiga kura.
Mi naona mambo yataendelea kuwa hivi hadi tutakapopata katiba mpya. So usishangae chadema inaposhindwa. Haimaanishi kuwa inapoteza sifa yake ya kuwa chama makini.
 
Mkuu Mwanakijiji,

Kwenda kupoteza katika uchaguzi huu (Kitu ambacho kipo Obvious kwa asilimia takribani 55%) kitapunguza sana mvuto wa CDM.Ila kuna tatizo la msingi ,narudia tatizo la Msingi ni Tume ya Uchaguzi.INGEKUA BORA CDM wakaamua kuacha kupeleka mgombea ili ku resolve issues za daftari la kudumu la wapiga kura n.k. Wangeanzisha mgogoro ili daftrai lirekebishwe,Sidhani kama kuna sheria ina yo guide kwamba daftari lirekebishwe baada ya muda fulani.

CDM Imekua tumaini jipya hasa kwa vijana,vijana ambao in the next elections watakuwa ndio kundi kubwa la wapiga kura.CDM Inatakiwa ijipambanue katika uwajibikaji,ikiwapa moyo vijana kuna uhakika wa asilimia 80 CDM Kuchukua dola kukiwa na mazingira ya tume huru ya Uchaguzi na vijana wakipiga kura (SATTA Ameshinda kwa nguvu ya vijana).TUKISHINDWA Arumeru, KUJIUZULU kwa uongozi wa juu kuwe ni kama swala la uadilifu.Hii itaongeza credit kwa chama.Lakini kwa hili tunatakiwa kuwa makini zaidi kujua chanzo cha success au failure.
 
Unajitafutia wanachama wa CCK kwa nguvu zote! hii hatari kubwa sana, CCJ iliwalenga CCM, naona CCK imewalenga chadema, haya, yetu macho.
 
Huwa ninakukubali sana MMM ila leo natofautiana nao sana tu

Umetoa hamasa njema ya kuhakikisha CDM inashinda Arumeru. Na hilo ni jambo zuri ambalo ni very positive. Shida yangu ni hapo tu pa kujiuzuru kwa viongozi wote wa kitaifa.

Kwa mtizamo wangu nadhani hujaona negative implications ya viongozi wote kujiuzuru kwa maramoja kbu tu ya kusindwa chaguzi ndogo. Ingawa ni kweli CDM imeshindwa chaguzi nyingi ndogo na kushinda 1 tu. But I challenge you kuwa hujatizama upande wa pili wa kuwa hiki chama kimefanya mambo mawili au hata matatu au zaidi kwa wakati mmoja.
1. kukifanya chama kiweze kukubalika kwa wananchi na hili hata ww unakubali kuwa si siku nyingi sana chama hiki kilikuwa kidogo tu na cha kawaida sana, ila kimejengwa kwa kasi kubwa sana ndani ya miaka isiyozidi 4-5 hivi, hili tuwapongeze hao viongozi wa kitaifa na hadi wa matawini.
2. Viongozi wa kitaifa wameweza kuja na mbinu ya kujenga ngome imara na zenye watu wengi: K'njaro, Arusha, Mwanza, Mara, Kagera, Shyinyanga, Mbeya, Iringa na sasa tunaona Songea, Tabora (Igunga), Dar kwa sehemu kubwa tuu, Pwani (Kibaha), Moro (Ulanga nadhani kama siyo Kilombero), Tanga, n.k Hapo ni jitihada za kuwa na ngome, tuwapongeze jamani!!!
3. Njia mbadala za mbinu za kampeni ambazo hata ccm wameiga toka cdm. Mbinu pekee ya ccm wanayo ni ya kuchakachua matokeo pale ambapo wameshindwa kihalali na unajua cdm ni vigumu kuwa na fursa hiyo kimundo wa vyombo vyote kuwa chini ya ccm, na hii MMM unajua sana kuwa yanatokea na si mara moja
4. cdm wamejipambanua kuwa chama mbadala chenye kuweza kuleta tumaini jipya kwa tz hilo liko wazi sana na hii ni ndani ya miaka michache ya karibuni na ni kupitia viongozi haohao wa kitaifa ambao MMM unawahitaji wajiuzuru wakishindwa Arumeru!!
5. cdm imeweza kuwaonyesha vijana tumaini jipya na kuwapa fursa za kuonyesha vipaji vyao vya uongozi kwa lugha nyingine wanalea na kuwaandaa vijana kuchukua nnchi hivi karibuni na kuleta maendeleo yanayohitajika tz tuwapongeze!!

Why wazo la kujizuru si zuri:
1. Itatokea mshituko mkubwa ktk chama na kinaweza kupoteza mwelekeo kabisa. Kutakuwa na ombwe la uongozi la ghafla
2. Kutakosekana wazoefu wa kuongoza maana wote watakuwa wapya na mbinu mpya ambazo hatujui kumbuka, kama zitaleta ufanisi kiasi gani
3. Hatuna uhakika hao wapya wote kwa mara moja mamluki watakuwa ni wangapi maana ccm inatafuta fursa kwa udi na uvumba kupenyeza mamluki wa kutosha ili kuvuruga cdm
4.Tutakuwa tume wahukumu kwa kosa moja tu la kushindwa chaguzi ndogo na kusahau makubwa mengi mazuri ambayo viongozi wamefanya hadi cdm imekuwa tishio kubwa kwa ccm na kuwavuruga kabisa ccm hadi wanakosa sera majukwaani na kubaki na mipasho na kutegemea nguvu za dora, fadhila za NEC, n.k
5. Kosa haliwezi kuwa kwa viongozi pekee; na wanachama na wapenzi wanafanya nini kuhakikisha ushindi unatokea. Mfano kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura, kulinda kura zao, n.k

Nakubaliana nawe kuwa cdm inatakiwa ione kuwa sheria za uchaguzi, vyombo vya uchaguzi (NEC), dola na kanuni na mazingira ya hizi chaguzi ni zilezile so kama wanahujumiwa basi watarajie kuendelea kuhujumiwa hadi hapo hayo mazingira yabadilishwe.

Ushauri wangu:
1.Hata kama cdm itashindwa Arumeru (ingawa kushindwa arumeru ni fikra maana ushindi wenyewe uko wazi kabisa) viongozi wasijiuzuru. Au hata kama watashinda. Viongozi waje na shauri la kutaka mazingira ya uchaguzi yabadilishwe. Na hii wailete kwa wananchi kwa njia ya mikutano, maandamano ya nchi nzima, semina, kila mbinu hadi kieleweke
2. Wawe na timu kabambe ya mikakati ya uchaguzi, kueneza chama vijijini, ulinzi na usalama wa viongozi, namna ya kuhakikisha wapenzi wao wana kadi na wanazitunza kila mahali tz
3. Viongozi wa ngazi zote wawe kitu kimoja hasa wale wa kitaifa. Kama wanatofauti wazimalize kwa njia ya vikao vyao vya ndani. Hakuna haja ya kuleta mambo yao hapa JF kwa faida ya nani. Mfano Tuntemeke na wenzake, au la basi Tuntemeke hayuko cdm bali anapata information toka cdm na hivyo anawalipua tu bila kujali
4. Sisi wengine tuwape hizo mbinu mpya ambazo mfano wewe MMM unazo ili kufanikisha ushindi na ukuaji zaidi na wa kasi wa cdm. Tusiishie tu humu JF na hizo mbinu tuwape
5. Si kama viongozi wa kitaifa wabakie kuwa viongozi milele la hasha bali kufuatwe njia za kawaida kabisa na katika mazingira ya kawaida ya kubadilisha viongozi. Hata wote wanaweza kubadilishwa ila kwa hatua tofauti tofauti na si wote kwa mara moja kama kunahitajika hilo
 
Back
Top Bottom