MORE PRESSURE: CDM Wasiposhinda Arumeru East Uongozi mzima wa Taifa LAZIMA Ujiuzulu

Nakubaliana na wewe Mwanakijiji lakini tusisahau, kuwa pamoja na kushindwa, kuna mafanikio makubwa Chadema imeweza kuyapata katika hizo chaguzi.


Hili halina mjadala lakini haya mafanikio yanasaidia vipi CDM zaidi ya kuongeza matumaini kuwa siku moja mkono wa mwanadamu utaanguka? Kwa mfano, Nassari akipata 20,000 zaidi ya 17,000 alizopata lakini bado akashindwa na mgombea wa CCM ambaye atapata 24,000 (less 10,000 za alizopata Jeremiah Sumari) tunaweza kusema kuwa CDM imefanikiwa?

BInafsi naamini tuanze kupima mafanikio kwa kuanglaia kushinda uchaguzi kwanza vitu vingine vyovyote ni secondary. I mean kama chama ni maarufu, kina wanachama wengi, na kinapendwa lakini hakishindi uchaguzi kinafaa nini kwenye kuleta mabadiliko? NI kweli kinagusa nyoyo za watu, kinawapa watu matumaini, kinafichua mafisadi lakini hata kwenye majimbo ya mafisadi wenyewe chama hakishindi bado tunaweza kusema ni mafanikio?
 
MMM,

Unachokisema wewe may be kitakuwa aplicable baada ya kupatikana Katiba mpya...

Swali Ndogo tu kwako ni kwamba unafikiri hawa viongozi hawatimizi wajibu wao au wananchi hawawapigii kura au ?

Nadhani uko ndani ya nchi hii na unafahamu kila kinachoendelea, Chadema na viongozi wake wanatimiza wajibu wao ila CCM, UWT, NEC, JWTZ, POLISI, TAKUKURU na pengine mahakama ndiyo wanaowahujumu CDM na watanzania kwa ujumla.

Ndiyo maana sahivi wabunge karibu wote wa CDM wa kuchaguliwa wote wana Kesi mahakamani ambazo hazina Msingi wowote.

Katika mazingira haya nadhani si vizuri kuwashinikiza viongozi wa juu wote wame play part yao na wananchi wana ply part yao ila hizo taasisi nilizozitaja hapo juu ndiyo wahujumu wakubwa wa wananchi.

Mfani ni swala la kutumia daftari la wapiga kura la 2010 kwenye uchaguzi wa 2012 huu ni usanii nafikiri wa kwanza kujiuzulu ni Jaji lubuva kwa kukataa kuwandikisha wapiga kuwa wapya Arumeri na CDM.

Na kuhusu wapambanaji wote wa CDM kugombea ubunge 2010, Nadhani unaona mchango wa hawa wabunge uliowataja bungeni mfano Mbowe, Tundu lisu, Zito Myika, Lema etc... Hawa ndiyo waliofanya mchakato wa katiba mpya kuanza na ni kutokana na ujasiri na uwezo wao.... Embu fikiria CDM ingewatuma wabunge lelemama kama wale wa CCM kingetokea nini? nafikiri jibu unalo.

Nadhani huu ni wakati wa kuelekeza mashambulizi kwa wahujumu kura za wananchi na si kuanza kulaumiana..


Nawasilisha.
 
Matukio ya ndani ya hivi karibuni yamenifanya niamini zaidi kuwa niliyoasema hhapa ni sasa. WAKISHINDWA NI LAZIMA WAJIUZULU!
 
CHADEMA itashinda vipi wakati tunasoma kuwa akaunti ya uchaguzi ni 0, yes zero! fedha imekopeshwa kwa Slaa kujengea nyumba yake Kunduchi! na nyingine inalipiwa posho za Josephine na hausigeli wao kwa ajili ya Junior apate malezi mema, na nyingine zinalipa walinzi wa Kanisa analokwenda Josephine. Aliyepewa fedha za kufanya "study" ya uchaguzi Arumeru alikuwa South Africa ambapo hakuna mawasiliano, huku kampeni zinaendelea! Kwi kwi kwi teh teh teh!

Kuna kuwashinda CCM hapo? hapo kuna mchezo wa kuigiza tu.

uchaguzi umeisha wana arumeru wamesha amua
 
Back
Top Bottom