Dullo
JF-Expert Member
- Oct 24, 2009
- 251
- 64
Mzee Mwanakijiji nimependa uchambuzi wako lakini ujue kwamba CDM bado ni taasisi inayotegemea nguvu za watu bado haijawa na rasilimali zake za kukifanya kijiendeshe chenyewe.
Kumbuka kuwa hata ruzuku wanayoipata haitoshi kuendesha chama nchi nzima hivyo ukisema uongozi ujiuzulu kwa kushindwa uchaguzi mdogo huoni kama utakuwa unabariki kufa kwa chama sababu ya kushindwa katika uchaguzi mdogo? Nakumbuka humu ndani kuna mtu alishawahi kusema watu wanarundikiwa vyeo wakati ni wabunge badala ya kuwaajili vijana ambao wako katika chama na hawana kazi za kufanya, wakatokea viongozi wa CDM wakatoa ufafanuzi na kutuambia uongozi ndani ya CDM ni wa kujitolea na chama hakina vyanzo vya fedha zinazoweza kuajili watu na kuwalipa mishahara.
Mfano unasema wakishajiuzulu ufanyike uchaguzi na atakayeta kugombea kama ni mbunge aachie ubunge wake ndiyo apewe uongozi, hapo MM unakutaka kuwaonea bure kwani huo ubunge kuupata mbele ya CCM sio kazi rahisi sasa leo aache ubunge ili atumikie chama wakati wameshasema hawana vyanzo vya kupata pesa.
Kuna mengi umeshauri lakini ushauri wako umewahi sio wa 2012 ni labda wa 2017 maana bado wako katika kukijenga chama na tusiwapuuze kuna kila jitihada wanazifanya ikiwemo kuwa tayari hata kugharimu maisha yao kwa ajili ya kukitetea chama.
Kwa ushauri wa kuwafikia wnanchi wa mikoa ambayo bado haina mwako hilo naliunga mkono kwani mikoa kama Lindi, Mtwara, Tanga mingine ambayo mwako ni mdogo inabidi wawekeze nguvu zaidi.
Zaidi inabidi tuendelee kuwaunga mkono hawa jamaa kwani wanajitahidi sana sana kupenya katika mishipa iliyobana katika jitu linaloitwa CCM