Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
- Thread starter
- #21
Mwanakijiji madai yako yana msingi sana lakini binafsi yangu nimeona vitu viwili vikubwa ambavyo vinaiangusha CDM katika chaguzi nyingi.
1.0 Wafuasi wake wengi ni vijana ambao walikuwa hawajapata hamasisho la kujiandikisha. Hawa ndiyo wanakiangusha sana chama.
2.0 Tume kuwa biased kabisa. Yaani imekaa kuhakikisha CCM inashinda huku ikijivuna nguvu ya jeshi endapo itavurunda. Na kwa tanzania bado hatujafikia hatua ya kujitoa mhanga kudai haki zetu. Kwa mbali madokta wameonyesha njia.
Hivyo huwezi kukilaimu sana chama, kwa matokeo mabovu.
Mwisho chama bado kina safari ndefu kabla ya kukabidhiwa watu wengine. Bado sina imani sana na baadhi ya watu pale juu naona wamekaa kimamluki lakini.
Kwangu hilo la pili silijali sana kwa sababu tayari liko presumed. Hilo la vijana ni suala la mikakati tu. Kwanini CDM inaenda kushiriki chaguzi abazo inajua ngome yake - vijana - hawana kadi za kupigia kura? Uchaguzi huu unafanyika zaidi ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu kwanini hakukuwa na zoezi la kuandikisha wapiga kura wapya? Well.. "You go to war with the army you got" alisema Rumsfeld.