Mohamed Dewj mzalendo halisi!

Unajuaje hana mapenzi na nchi yake na pia unajuaje hatokuwa tayari ku-serve katika jeshi?

Rejea posting yangu ya mwisho..Lakini iko hapo chini again...Je huyu ndugu ame speak out kuhusiana na direction ya Taifa ambayo ni unwise na unjust?
Ama ni mambo ya cherry picking..Nilisema publicity mkabisha...

Others argue that a true patriot speaks out when convinced that their country is following an unwise or unjust action.
 
Inaweza kuwa sio Wahindi-Watanzania

Haya Bwana,
Kama ndio kiwango cha kufikiri ndiohiki, inaonyesha tunahitaji miaka 500 kubadilika kutoka hapa tulipo.

Du, job true true!
 
Tatizo hapa ni Mohammed Dewji kuitwa 'Mzalendo halisi'..Mods nadhani ni vizuri kubadilisha heading kama ilivyopendekezwa hapo juu ili wanajamii twende pamoja
 
Sawa. Ili kuondoa utata, labda pengine niwaombe maMods warekebishe heading ili iwe "Mohamed Dewj ameonyesha element ya uzalendo." kama ulivyopendekeza.

Na hasa ukizingatia mtoa hoja Mkuu QM ameridhia kubadilisha heading kama inavyoonekana hapo juu
 
Rejea posting yangu ya mwisho..Lakini iko hapo chini again...Je huyu ndugu ame speak out kuhusiana na direction ya Taifa ambayo ni unwise na unjust?
Ama ni mambo ya cherry picking..Nilisema publicity mkabisha...

Je unakubaliana na nilivyokwambia mwanzo kuwa wazalendo wanakuja katika nyanja tofauti, kwa hiyo unataka kuniambia wale wote wanaojitolea na kuipigania nchi yetu katika sehemu mbalimbali lakini wakawa kimya ku-speak out kuhusiana na muelekeo wa nchi si wazalendo?? Sidhani ku-speak out ni kipimo pekee cha uzalendo au ni kipimo kikuu unapomzungumzia mzalendo.
 
Je nilivyokwambia mwanzo wazalendo wanakuja katika nyanja tofauti, kwa hiyo unataka kuniambia wale wote wanaojitolea na kuipigania nchi yetu lakini wakawa kimya katika ku-speak out kuhusiana na muelekeo wa nchi si wazalendo??

Mkuu Geeque sijasema hivyo naomba urejee mchango wangu kwenye thread hii.
Nimeainisha kwamba hatuwezi kusema Dewji ni mzalendo halisi kwa kutumia vigezo vya soka na mdundiko.
Nakubaliana na wewe kuwa wazalendo wanakuja kutoka nyanja tofauti lakini sidhani kama ni sahihi kusema eti nyanja yake ya mdundiko na soka ndio kuwa eti ni mzalendo halisi...Again i still believe ni publicity tu kucheza na emotions za watanzania.
 
Hapo chini nimeweka sentensi uliyoitumia hapo juu kuhusu uzalendo...Dewji ame support...Lakini unasahahu kuna ku "Love and prepared to serve"Hatuwezi kugawa uzalendo kiulaini tu kwa kigezo cha kusapoti soka na mdundiko....Uelewe hata ku serve inavyozungumziwa ni pamoja na jeshi nk...Kupigana kwa ajili ya Taifa.

Na kwenye sentensi ya mwisho kabisa kwenye paragraph ya definition ya patriotism...Nimeipenda hii na hapo ndipo napopasimamia kwenye mjadala huu...

Patriotism is a love of and loyalty to one's country. A patriot is someone who loves, supports, and is prepared to serve their country.

Tena fadhali hata ya Dewj amefit kwenye "supports." Wakina sisi tunafit kwenye "loves" only. Ukweli ni kwamba, wengi wetu hatu "support" wala hatuko tayari "serve." Tumebaki kuimba wimbo wa mapenzi yetu kwa Bongo, lakini ikija kwenye 'kusupport' tunatafuta uchochoro. Na kwa sababu hatusupport, sidhani kama tutakuwa na nia ya kuserve pale tutakapohitajika.

Kwa hiyo, angalau 'mgeni' wetu Dewj anafanya kile ambacho wengi wetu hatufanyi hata kama tuna uwezo wa kufanya hivyo.
 
Mkuu Geeque sijasema hivyo naomba urejee mchango wangu kwenye thread hii.
Nimeainisha kwamba hatuwezi kusema Dewji ni mzalendo halisi kwa kutumia vigezo vya soka na mdundiko.
Nakubaliana na wewe kuwa wazalendo wanakuja kutoka nyanja tofauti lakini sidhani kama ni sahihi kusema eti nyanja yake ya mdundiko na soka ndio kuwa eti ni mzalendo halisi...Again i still believe ni publicity tu kucheza na emotions za watanzania.

Na kama umenisoma saa zote sijazungumzia uchezaji wake wa mdundiko kama kipimo cha uzalendo, mimi kwa muda wote hapa nimezungumzia mchango wake kwenye medani ya michezo pale nchini. Mdundiko kila mtu anaweza kuucheza lakini moyo wa kusaidia kitu fulani kwa taifa lako sio kila mmoja anao.

Kwa hiyo Mazee Mushi unakubaliana nami kuwa msaada wake kwenye michezo pale nchini ni kipimo cha uzalendo au kunaainisha kuwa ana chembe za uzalendo kwa taifa la Tanzania?? Nipe jibu kwa hili.
 
Haya Bwana,
Kama ndio kiwango cha kufikiri ndiohiki, inaonyesha tunahitaji miaka 500 kubadilika kutoka hapa tulipo.

Du, job true true!

Nakubali!

Vipi wewe ufikiri wako ukoje kuhusu kujitokeza kwa Dewj kwenye kushangilia Stars?
 
Nakubaliana na wewe kuwa wazalendo wanakuja kutoka nyanja tofauti lakini sidhani kama ni sahihi kusema eti nyanja yake ya mdundiko na soka ndio kuwa eti ni mzalendo halisi...Again i still believe ni publicity tu kucheza na emotions za watanzania.

Sawa Mushi, nimekosea. Sikuwa sahihi kutumia "mzalendo halisi" kuelekeza pointi yangu kuhusu Dewj. Kwa hiyo, naomba uendeleze uchambuaji kwa kutumia title mpya niliyowaomba Mods waiweke. Waweza fanya hivyo?
 
Mods bana....yani mmekuwa fast kuihamisha hii mada kwenda kwenye Celebrity Forum, lakini mnachelea kubadilisha title yake kama nilivyoomba?

Na kwanza sidhani kama hii ni 'Celebrity Forum' mada. Kwa sababu, haimzungumzii 'Dewj', bali tendo la 'uzalendo' halilofanya... Kwa hiyo ni 'uzalendo' ndio unaojadiliwa hapa na sio 'Dewj' as a person.
 
Hapa watu wanabishana kama wako MAHAKAMANI. Mushi, nafikiri jamaa wanachokiongelea kinaonekana. Ila wee bado washikilia neno UZALENDO HALISI. Ondoa basi hiyo HALISI na bakiza uzalendo na habari ziendelee.
Hakuna kipimo cha Uzalendo. Karibu wote hapa tu-MAFISADI ila sema tu hatuna uwezo. Ndiyo maana dawa pekee ni kuweka sheria kali na ukaguzi wa mara kwa mara. Kiongozi akiwa anafanya kazi bila kuwa na MIIKO, basi atakuwa Dikteta, Fisadi, nk nk. Na hiyo miiko lazima ziwepo idara zinahakikisha miiko inaheshimika. Tatizo, hizo idara kwa Tanzania ziliuwawa, zikazikwa (azimio la Arusha, UWT nk), na hapo ndipo PEPO ya Mafisadi ikaanza. Hakuna mtu asiyetaka faida kama Mfanyabiashara. Mhindi ni binadamu wa kawaida kama sisi anayetaka na tuseme hata zaidi yetu sisi kupata faida. Kama wenyewe tunamfunulia, kwa nini asile? Kama tungelikuwa WAZALENDO kweli, basi Wahindi, Wazungu nk nchi hii wasingelipata kitu. Serikali tumejaa sisi, UWT ni sisi, POLISI ni sisi, Wizara zote ni sisi, kwenye migodi ni sisi, BoT ni sisi, bandarini ni sisi, TRA ni sisi sasa kama Mhindi ana-FISADI, mwenye makosa ni MHINDI au Sisi MIPINGO?? Kusema Wahindi ni MAFISADI kwanza ni kujidhalilisha. Ni sawa na kusema "Mitanzania haina akili". Imelala fofofo. Anakuja Mhindi/Mzungu na dola 1, baada ya miaka 5 anaondoka na dola milioni moja.
TUKOME kuwaita WAHINDI Mafisadi. Mafisadi ni SISI MIPINGO na ULAFI wetu. Hawa jamaa ni WATAFUTAJI tu. Ifike wakati tuanze kubeba misalaba yetu wenyewe. Mara ohh, Mwanamke, mara ohh, Wahindi, mara ohh Wazungu. Ningelikuwa RAIS, ningeliwafungulia Wahindi na kuwaomba Msamaha. Ila akina Yona, Mkapa, Mramba, Mary, Mahalu, Mboma nk hawa ndiyo wakushika na ku**&&^%$$$$$. Hapo sasa usubiri kama utaona kuna MHINDI au Mzungu anakuja KUFISADI Tanzania. Ua Mizizi na si matawi.
Narudia tena, WATANZANIA TUANZE KUBEBA MISALABA YETU WENYEWE.
 
Mo ameonyesha mfano mzuri kwa wengine na kama tuna question uzalendo wake basi nadhani neno uzalendo limepoteza maana yake au pengine ili uwe mzalendo lazima uwe na surname ya Mgonja, Yona, Mramba, Karamagi et al

Mkulu, Kwa ntaji huo, mie siutaki uzalendo!!!!!
 
Nakubali!

Vipi wewe ufikiri wako ukoje kuhusu kujitokeza kwa Dewj kwenye kushangilia Stars?

Wapo wenzi wapenzi wa Manchesta, chelse, madrid nakadhalika. Sidhani kuwa wapenzi wa timu hizo wakiwemo watanzania ni Wazalendo halisi wa nchi husika!
Tumewaona kina Manji sijui na yule mwingine alikuwa anaitwa Deuji waliokuwa wafadhili wakubwa wa simba na yanga.
Jambo la msingi ni kujua tu kuwa kuna upenzi na pia kuna msumkumo wa kiuchumi, kisiasa, kujamii n.k!

Sasa hapo ndo ngoma!
 
Vizuri!

Je unafikiri kuna maslahi gani ya kiuchumi, kisiasa, au kijamii Dewj anayopata kwa kucheza mdundiko kwenye 120 degrees...tena akiwa amevuwa shati nusu?

Tayari yeye ni mfadhili wa michezo anayejulikana sana tu. Unafikiri kutotokea kwake kungempunguzia nini katika maslahi yake yanayopatikana na ushiriki wake katika udhamini wa soka Tz?

Umemzungumzia Manji, yeye hakuonekana akicheza mdundiko. Je unafikiri maslahi yake ya kiuchumi, kisiasa, na kijamii yamepungua kwa kutokuonekana kwenye ushangiliaji huo?

Well, inabidi uingalie hizo picha kwa karibu kuweza kuona furaha yake jinsi inavyotoka ndani na sio ya kufake.
 
QM Huo mdundiko wataucheza kweli na shati nusu atavua lakini pa kwenda kulala ni tofauti sana.
Hulka yetu sisi waafrika haswa watanzania ni ukarimu...Na tunapoona kuna watu tofauti na sisi wanjichanganya kwenye jamii na kuzungumza lugha zetu nk basi jambo hilo huwa linatugusa sana na kutufanya tuwaone watu hao ni wa maana na wenye upendo sana na jamii yetu....Tatizo liko kwenye issue nyeti na muhimu sana kwa Taifa na si mambo ya michezo tu..Na ndio maana nikasema ni mapenzi yake kwenye kandanda na sidhani kama ni neccessarily uzalendo.

Dewji ni mtanzania mwenye asili ya kiasia...Na kwahiyo hatua aliyochukuwa inaonekana si ya kawaida kwa baadhi ya watu....Lakini nani hajui watu hao hao anaocheza nao mdundiko na kufadhili kandanda ndio watu hao hao ambao wananunuwa bidhaa zao ambazo zinanunuliwa kama njugu kutokana na umaarufu ulijengwa wa kishabiki...Sasa tunapogeuza mambo kama hayo kuwa uzalendo ndio hapo tunachanganya...Nakumbuka sana Abbas Gulamali(RIP) na yeye kiutani utani akaja akapata hadi ubunge,Dewji the same...Watanzania tunapenda soka na ni wazi kuwa tumekuwa tukiu husisha mchezo huo kama mojawapo ya utamaduni wetu na utambulisho wetu na hapo ni rahisi sana kugusu nyoyo za wananchi kwa kupitia michezo...Tumeona sana mifano kama hiyo hata kwenye basketball na Football hapa USA...Saa nyingine hata football ya wamarekani ndio kama aina flani ya mchezo unaoonyesha umarekani na hivyo kupelekea hisia za kizalendo pale inapokuja kwenye ushabiki.
Tuwe makini.
 
Tatizo la waswahili ndo hilo mnapenda sana kuchanganya Topic.Sisi tunachozungumzia hapa ni moyo wa kuijitoa na kuilaki timu ta taifa tofauti na viongozi wengine hasa wabunge ambao wao wanakuwa mstari wa mbele kujisifia pale maiki inapowekwa mbele yao tu.Msinchangaaye topic!nani asiye kua namakando kando!ebu jinagalienei nyie mnaoponda jinsi mlivyowachafu a mbaya zaidi wengine hamna msaada sio tu kwa jamii bali hata familia zenu na ndugu zenu pamoja na utajiri mlojilimbikia au mlorithi kwa wazazi wenu
 
Any way kwa vile anazo, na kakubali kujishusha na kuishangilia stars kama walala hoi wengine, nadhani anakitu tofauti ndani yake ambacho kwa mtazamo wangu yaweza kuwa mapenzi/ushabiki mkubwa wa football ama uzalendo. Kwani haipingiki kwamba jamaa anaonekana mwenye furaha sana!
 
Atauza sana bidhaa za viwanda vyake na kutangaza biashara zake zaidi na hii ndio inavyotakiwa kwa wafanyabiashara kitokezeni kudhamini na kutangaza biashara zetu au kazi zetu katika matukio kama haya
Hakuitaji kuvua shati na kurukaruka kwenye gari la wazi.Huyu mtu ni CEO wa METL ni mtu mkubwa kwa hulka ya wahindi hakuitaji kufanya yote hayo ili kupromote biashara yake.Tunajivunia kuwa WAZANEA lakini the fact is kuna WAZAWA pamoja na WAGENI wenye mapenzi ya dhati kwa nchi hii.Kuwa MZANEA sio kitu cha kujivunia/kushikamana nacho sana,cha muhimu ni kipi unaifanyia nchi yako.
MNYONGE MNYONGENI, HAKI YAKE MPENI.HIZO PICHA ZINAZUNGUMZA MENGI ZAIDI.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom