Mohamed Dewj mzalendo halisi!

Sisi hapa tunamzungumzia Mohammed Dewji kama mtu binafsi na haituizungumzii jamii yake. Maendeleo ya kweli ni yapi? huoni kuwa kwa kutumia soka tunaweza pia kuongeza pato la nchi kwenye utalii au hata kuboresha maisha ya vijana mbalimbali ambao wanaweza kuisaidia taifa lao kwa kuchangia kwenye pato la Taifa. Ukianza kujumuisha jamii yake utakuwa unakosea, sisi tunamzungumzia yeye kama mtu binafsi na michango yake mbalimbali. Je Mushi wewe ni Mzalendo? na umechangia nini kwenye Taifa lako?
Ndio ndio......kuna watu kila wakiona sura za wahindi wanakasirika.........hii thread inaonekana ina elements vya chuki dhidi ya wahindi......
 
Inaweza kuwa sio Wahindi-Watanzania wote wana mapenzi ya kweli na Tanzania. Lakini bila ya shaka kuna baadhi yao ni wazalendo kutushinda waasili wenyewe.

hayo maneno hapo juu binafsi sina wasiwasi nayo hata kidogo. ukisoma historia ya kupigania uhuru wa nchi hii kuna waasia waliotoa mchango wa maana kudai uhuru wa nchi hii. baadhi yao walikuwa karibu na viongozi wetu enzi zile.
wakati huohuo hawakukosekana weusi wenzetu ambao walikuwa 'hawauhitaji uhuru huo'. hawakuunga mkono jitihada za kudai uhuru.

Kweli kuna sababu ya kuwa na wasiwasi na uzalendo wa Mohamed Dewj kama anavyoonekana kwenye picha hizi mbili (attached)? Aliacha shughuli zake muhimu na kujitokeza kushangilia ushindi wa Taifa stars. Ushindi ambao hauna faida wala maslahi yoyote kwa Mhindi ambaye hana mapenzi ya kweli na Tanzania.

Hakika huyu ni mmoja wa Wahindi wenye 'damu ya Kitanzania.'

mi naona mtu anaweza kuwa na mapenzi na mpira pekee. kama anazimikia mpira lakini taifa kama taifa to hell with it? sisemi kuwa this is the case with 'MO'. mwaka ujao anaweza kuhamishia biashara zake uganda. timu yao ya taifa inaweza kushinda pia. akienda akavua shati na kucheza ngoma za kiganda tutakuja kusema nini? mshabiki wa mpira au mzalendo halisi?
Jacob Zuma wa bondeni hupenda sana kuimba na kucheza kiasili. kwa njia hiyo chati yake inapanda ktk jamii.
hata hivyo nimesikia mara nyingi akisaidia sana mchezo wa mpira hapa nchini. kwa hilo nampa hongera 'MO'. mpira si tu burudani bali ni ajira kwa watu wengi tu!
 
Nasikia huyu kijana ni mafia. Bidhaa zake nyingi ni substandard.

Kuna wakati alipelekeshana sana na Z.Meghji alipokuwa Waziri wa afya wati wa Mzee Ruksa pale MeTL walipoingiza Ngano ambao haufai kwa matumizi ya binadamu. Dewji alimvimbia pale alipokataa kuteketeza ngano hiyo Zakia Meghji akasema kama haitateketezwa basi atajiuzulu uwaziri, ngoma ilikuwa tamu hatimaye Dewji akanywea na ngano ikateketezwa
 
MAcho huona yanachotaka kuona, masikio yanachotaka kusikia. Umekwisha msikia akiongea kiswahili??? Ni mzalendo gani anaongea hivyo??? akisafiri nje hasemi yeye mtanzania akiwa jukwaa la siasa ndio mzalendo!!!!!!!!!!!
Mzalendo wa kweli hubaki mzalendo akiwa Masukulu kule Tukuyu, Maruku kule Bukoba, Mahiwa kule Lindi au Stokes kule Manchester, au Akiabara kule Japan.
Huyu ni mfanya biashara anatumia nafasi yake kujenga jina lake. Panda nusu kilo ya mahindi uvune kilo 500 baada ya miezi mitano. Tusiwe na haraka haraka ya kupongeza mtu anayetupa karoti huku nyuma ameficha fimbo kubwa!!!!!!!!!!!
 
Huyu kijana kama baba yake Gulam ni wafanyabiashara wajanja wanaotumia njaa ya watanzania kama njia ya kufanikisha malengo yao. Hawa wamekaa nakugundua kuwa wadanganyika wengi hasa vijana wanapenda mpira kwa hiyo kuwekeza katika mambo ya mpira italipa; itawapa publicity na Cheap "popularity". Wanafanya hivyo kwa kutumia fedha, walizotuibia toka enzi za Gapex hadi leo kwa ujinga wetu!! Huyu kijana alinunua ubunge kule Singida and as if that was not enough akaja kununua membership ya ccm NEC na kumuondoa Msindai!! Huyu kijana ni mbunge je umewahi kumsikia akichangia hata siku moja humo bungeni? Mbinu zao ni kuwahonga waandishi wa habari ili waandike habarizao vizuri. Uzalendo ni kupenda nchi yako na sio kuihujumu kwa kuimalisha corruption; huyu kijana na baba yake ni mafisadi wakubwa wanatumia sisa kam kinga. Kuuza na kutunia madawa ya kulevya yanayoharibu nguvu kazi ya vijana wetu ni hujuma kwa nchi yetu, na hayo yamefanywa na watu wa aina hhii tangu enzi za marehemu Gulamali ambaye nae alikuwa mbunge!! Makamba pia alitaka Manji awe mbunge bila kumtaja kinara wao RA..Wanatudanganya na ukarimu kidogo huku wanafilisi nchi ;wadanganyika tuamke!!
 
Wewe unakijua kiswahili?......hoja mufilisi....nina ndugu zangu wanyantuzu hawajui hata salamu ya kiswahili nao je?

mi naona wanyantuzu wako unyantuzuni huko. MO tuko nae mitaani mijini. akina MO mara nyingi wanakuwa wamezaliwa mijini. tofauti na wanyantuzu au makabila mengine yaliyo mbali na mijini.
mtu akitoka usukumani au ufipani au popote pale kule kijijini akifika mjini akiongea kiswahili mostly kitakuwa na lafudhi ya huko alikotoka. baada ya muda hubadilika na inakuwa vigumu kujua katoka wapi akiongea kiswahili.
huenda MO au akina MO hawafagilii kiswahili. au pengine ukijua kiasia/kihindi inakuwa vigumu kuongea kiswahili vizuri.
 
Kaka!

MO Dewji hata kiswahili hajui....halafu hapa tunaongelea uzalendo.

Mbona huwa namsikia akiongea Kiswahili(anapohojiwa na media),labda unifafanulie mkuu hajui Kiswahili kivipi???,je kampeni zake za Ubunge kwa wananchi wa Singida alizifanya kwa kutumia Lugha ipi??,alikuwa na mkalimani ama??,naomba unisaidie kwa hilo mkuu..Heshima mbele..Be blessed
 
mi naona wanyantuzu wako unyantuzuni huko. MO tuko nae mitaani mijini. akina MO mara nyingi wanakuwa wamezaliwa mijini. tofauti na wanyantuzu au makabila mengine yaliyo mbali na mijini.
mtu akitoka usukumani au ufipani au popote pale kule kijijini akifika mjini akiongea kiswahili mostly kitakuwa na lafudhi ya huko alikotoka. baada ya muda hubadilika na inakuwa vigumu kujua katoka wapi akiongea kiswahili.
huenda MO au akina MO hawafagilii kiswahili. au pengine ukijua kiasia/kihindi inakuwa vigumu kuongea kiswahili vizuri.
Kumbe huna uhakika.
 
Mbona huwa namsikia akiongea Kiswahili(anapohojiwa na media),labda unifafanulie mkuu hajui Kiswahili kivipi???,je kampeni zake za Ubunge kwa wananchi wa Singida alizifanya kwa kutumia Lugha ipi??,alikuwa na mkalimani ama??,naomba unisaidie kwa hilo mkuu..Heshima mbele..Be blessed
Bora wewe uongee..........
 
...Ubunge una heshima yake. Unapovua shati kwenye kadamnasi na kuruka ruka tumbo wazi ndio tukujue kuwa wewe ni mzalendo sanaa, ama?? You must hand it to him, though. The guy knows how to hog some cheap publicity from unsuspecting Bongomites!!
 
Wewe nawe!!!!hata kama ubunge una heshima yake,kwani Mbunge anapovua shati kwa lengo la kuonesha furaha yake(bila kufanya mambo mengine ya ajabu)anakuwa kakosa heshima???,mbona mara kibao Timu yao ya wabunge inapocheza baadhi ya wabunge huchojoa tu mashati kwa lengo la kushangilia ama wanapobadilisha wachezaji ama hata baada ya mechi..Hata hivyo MO hana kitambu so mwache ajiachie mwanawane..Heshima mbele mkuu...Be blessed
 
Yaani pamoja na kuomba, lakini Mods wamegoma kabisa kubadilisha heading ya hii mada!!!

Oh well, huenda wana sababu zao......
 
....Unapovua shati kwenye kadamnasi na kuruka ruka tumbo wazi ndio tukujue kuwa wewe ni mzalendo sanaa, ama??.....

Ukisoma hii sentensi katikati ya mistari utagundua jinsi gani watanzania tulivyo na roho za "kwa nini".

Hii line ya "unapofanya....... ndio tukujue kuwa wewe ni...... sanaa/saana," inatumika sana miongoni mwetu.
 
Huu ni ukereketwa, uzalendo au mananii yalizidi!! Ni kweli kabisa kila Mtanzania mpenda maendeleo amefurahia ushindi wa Taifa Stars. Lakini nimeshangaa kuona hii picha hapo chini na kuona Mh. Dewji akionyesha BOXER yake. Kwa kiongozi wa jamii kuonyesha kitu kama hicho kwa mtazamo wangu haileti picha nzuri. Tusianze tukajikuta tunaanza hata ku-promote vitu ambavyo havina maana kwa jamii, mfano mitepesho n.k

Haya ni maoni yangu, wewe mwenzangu unasemaje? Angalia hiyo picha hapo chini. Bonyeza palipoandikwa Dewji hapo chini...
 
Attachments

  • Dewji.JPG
    Dewji.JPG
    52.4 KB · Views: 94
Msamehe Mnyaturu huyo..

Mambo ya EPA yanapozidi unasikia mtu kakimbizwa hospitali ooh mara Nairobi mahututi. Mhh wasanii nchi hii, anyway utamu bado wamsubiri. Wananchi watamsamehe mara atakapotumikia kifungo kisichopungua miaka 20. Hapo wananchi ndo wanaweza kufikiria fikiria kumsamehe.
 
Huu ni ukereketwa, uzalendo au mananii yalizidi!! Ni kweli kabisa kila Mtanzania mpenda maendeleo amefurahia ushindi wa Taifa Stars. Lakini nimeshangaa kuona hii picha hapo chini na kuona Mh. Dewji akionyesha BOXER yake. Kwa kiongozi wa jamii kuonyesha kitu kama hicho kwa mtazamo wangu haileti picha nzuri. Tusianze tukajikuta tunaanza hata ku-promote vitu ambavyo havina maana kwa jamii, mfano mitepesho n.k

Haya ni maoni yangu, wewe mwenzangu unasemaje? Angalia hiyo picha hapo chini. Bonyeza palipoandikwa Dewji hapo chini...

Mkuu ni kweli jamaa kiasi fulani ame cross boundary, lakini ni nafuu huyu hata akivua shati anaonekana ni mtu wa mazoezi. Hivi angekuwa yule mbunge yule mkuu wa TOT, nanihii yule...mnamjua, ana tumbo za bia ingekuwaje?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom