Mo Ibrahim: CCM awamu ya nne yavunja record utawala bora

Huwa haisaidii sana na sio vema kwa baba mwenye nyumba kusifiwa na majirani/watu wa nje kuwa ni BABA bora wa familia wakati watoto wake na familia wanamuona kama ni baba dhaifu na kumuogopa kama kituo cha polisi...Baba wa aina hii inabidi ajaribu kutafakari tatizo ni nini watoto wake mwenyewe hawana furaha wakati nje wanaonyesha picha tofauti???
 
Taarifa ya utawala bora iliyotolewa na taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Ibrahim Mo imemtaja Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuvunja record ya utawala bora kwa kuiingiza Tanzania kwa mara ya kwanza katika nafasi ya 10 bora kati ya nchi zaidi ya 50 za Africa.

Kati ya nchi hizo, ni Tanzania pekee kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati.

My take:
Watanzania tuzitambue na kuthamini juhudi anazozifanya rais wetu kama vile mafanikio ya kujenga barabara zenye urefu wa km 18,000 ndani ya miaka nane tu ikilinganishwa na km 11,000 alizozikuta, daraja la kusini, la kigamboni, mradi wa mabasi yaendayo kasi, reli ya tanga to musoma+bandari ya musoma itakayoanza hivi karibuni, ufumbuzi wa tatizo la umeme, uvumilivu alionao, uhuru wa kutoa maoni bila mipaka, uhodari wa kutatua matatizo kama uchochezi wa wanasiasa n.k. Hata hivyo tusipozitambua juhudi hizo, watu wa mataifa mengine watazitambua na kumpongeza kwa uwazi kabisa.

Tutabaki tunalalamika kuwa Kikwete hivi Kikwete vile lakini ukweli utabaki kuwa J.K is a super president ever happened in TZ.!

Mwenyekiti wa Mo Ibrahim bado ni Salim A. Salim? Then what to expect from that **** NGO? Fadhila za Salim ndo hizo kapewa umakamu tume ya katiba........Gimme a break!
 
...maendeleo ya kweli ya nchi hayapimwi kwa vitu bali yanapimwa katika watu,je watu wameendelea?...vyote hivyo ulivyorodhesha hapo juu kama mafanikio ya JK,havina maana yoyote ile kama watu wanaotakiwa kunufaika-navyo haviwasaidi kujiretea maendeleo...
 
Hivi ni chama gani ambacho vingozi wao hawajaandaa watoto wao? Hebu kitaje nikuorodheshee ndugu na jamaa na vimada walivyopangana.

nyani haoni kundule, wanayaona mabaya tu ya wenzao, hawaoni zuri hata moja wala mabaya yao hawayaoni.

Nenda kaangalie kwenye majimbo yao kama kuna mazuri matupu, ni madudu tu wala hakuna ya kujivunia.
 
...maendeleo ya kweli ya nchi hayapimwi kwa vitu bali yanapimwa katika watu,je watu wameendelea?...vyote hivyo ulivyorodhesha hapo juu kama mafanikio ya JK,havina maana yoyote ile kama watu wanaotakiwa kunufaika-navyo haviwasaidi kujiretea maendeleo...mimi napendekeza hata hii ripoti ya Mo Ibraim iinginzwa kwenye maajabu 7 ya dunia kwa kuiweka Tanzania kwenye top 10 wakati watanzania wakikabiliwa/wakitaabika na hali ngumu sana ya maisha...
 
Hii taasisi nilidhani ipo serious!kumbe nayo ni walewale.waje wachukue ripoti za tume ya binadamu na REPOA ziwasaidie kufanya maamuzi.Au ndo maandalizi ya 2015?....TAFAKARI..................................................
 
well, mimi nasubiri hiyo 2016 angalau na sisi tupate hayo mamilioni kama aliyopata Joachim Chissano baada ya hii miaka yote kukosa 'kiongozi bora' barani Afrika.
 
Hivi ni chama gani ambacho vingozi wao hawajaandaa watoto wao? Hebu kitaje nikuorodheshee ndugu na jamaa na vimada walivyopangana.

we MKALI MOTO jibu hoja zote kama kweli we ni GT acha kukurupuka mtetezi wa mafisadi weee
 
Kwenye kuendeleza Barbara na miundo mbinu I agree. Tatizo Hilo la utawala bora halipo. Ni udini na makundi mwanzo mwisho.
 
Ni kweli kikwete ni kiongozi ambaye tz haijawahi kupata kama yeye.Alitakiwa aongoze zaidi ya miaka 10,angeiacha nchi mbali sana.Kuna watu wanamchukia kwa sababu zao za kiimani na si kingine kwa sababu hatuoni hoja zaidi ya matusi,hasira na chuki.

Wamejaribu kumchokoza lakini hachokozeki,wamechochea vurugu lakini wameshindwa na nia yao ili kutia dosari uongozi wake.Sasa ripoti mbalimbali zinazotolewa na taasisi za kimataifa juu ya mafanikio ya uongozi wake zimekuwa zikiwakera na kuwaumbua,wanachotaka ionekane nchi imemshinda jambo ambalo si kweli.

Kwa haya yanayotokea kwa mafanikio ya uongozi wake,na hila mbalimbali zinazofanywa kutia dosari mafanikio yake,naungana na wale waliosema Jakaya Kikwete ni CHAGUO LA MUNGU.
 
Mambo ya kipuuzi tu hayo, utawala bora unapimwa kwa 'uhuru wa kutoa maoni kwenye social media'??? Wale 'mbwa' wake wanavyoua raia hovyo mbona hawajasema, au hivyo si vigezo? U-dini aliouanzisha na kuulea mbona hawajazungumzia?? Kilo ya unga wa mahindi kufika 1,300 mbona hawaoni?? Shwaini tu hawa...
 
Taarifa ya utawala bora iliyotolewa na taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Ibrahim Mo imemtaja Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuvunja record ya utawala bora kwa kuiingiza Tanzania kwa mara ya kwanza katika nafasi ya 10 bora kati ya nchi zaidi ya 50 za Africa.

Kati ya nchi hizo, ni Tanzania pekee kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati.

My take:
Watanzania tuzitambue na kuthamini juhudi anazozifanya rais wetu kama vile mafanikio ya kujenga barabara zenye urefu wa km 18,000 ndani ya miaka nane tu ikilinganishwa na km 11,000 alizozikuta, daraja la kusini, la kigamboni, mradi wa mabasi yaendayo kasi, reli ya tanga to musoma+bandari ya musoma itakayoanza hivi karibuni, ufumbuzi wa tatizo la umeme, uvumilivu alionao, uhuru wa kutoa maoni bila mipaka, uhodari wa kutatua matatizo kama uchochezi wa wanasiasa n.k. Hata hivyo tusipozitambua juhudi hizo, watu wa mataifa mengine watazitambua na kumpongeza kwa uwazi kabisa.

Tutabaki tunalalamika kuwa Kikwete hivi Kikwete vile lakini ukweli utabaki kuwa J.K is a super president ever happened in TZ.!

Kama kweli ameisaidia Tanzania ikaingia top ten je ni vigezo gan tuzo ya mo ibrahim inaviangalia? Kama kweli Tanzania imeingia top ten basi ni kwa kukiuka misingi ya utawala bora maana kama kila siku raia wanauliwa na polisi, mafisadi wanazidi kutuibia na hawachukuliwi hatua yeyote unafikiri ni utawala upi tunaoungelea
 
Kwa uwelewa wangu mdogo ni kuwa daraja la kusini liwe la Umoja ama daraja la Mkapa limejengwa enzi za Mkapa . Barabara unazosema zilianzwa kujengwa enzi za Mkapa na fedha zilishatengwa .Cha kustaajabisha kasi ilianza kupungu alipoingia baba Riz kwa kuzipeleka ndiko siko -kuzurura dunia nzima .

Hizo tuzo za Mo Ibrahim ni usanii mtupu ,zinawafaa kina Diamond na Wema
 
Lakini hao hao MO IBRAHIM wamesema mwaka huu hakuna nchi ama kiongozi atakae pata tuzo kwasababu hakuna aliefikia vigezo vyao..kwahiyo bwana zumbukuku kutuingiza top 10 ni blah blah tu hamna kitu hapo

Tuzo za Mo Ibrahim wanapewa marais wastaafu tu, kwani JK si bado yuko pale magogoni? haja qualify kupata tuzo so, si blah blah! its real!
 
amewatuma watu wamuue ulimboka wakakosea,akawaacha watu waue mwndishi bila kuchukua hatua,akawaacha huru polisi walioua waandamanaji pale arusha,akazidi kuidumisha demokrasia kule morogoro plisi walipoua raia,ametumia mabomu jana tu pale zanzibar hali iliyopelekea kifo cha askari polisi,anaongoza kama raisi ambae mawaziri wake kuumwa na kupata ajali za ajabu ajabu kwa kweli anastahili tuzo na jinsi ambavyo anaendelea kusaini mikataba,viva presdaaa.
 
Taarifa ya utawala bora iliyotolewa na taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Ibrahim Mo imemtaja Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuvunja record ya utawala bora kwa kuiingiza Tanzania kwa mara ya kwanza katika nafasi ya 10 bora kati ya nchi zaidi ya 50 za Africa.

Kati ya nchi hizo, ni Tanzania pekee kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati.

My take:
Watanzania tuzitambue na kuthamini juhudi anazozifanya rais wetu kama vile mafanikio ya kujenga barabara zenye urefu wa km 18,000 ndani ya miaka nane tu ikilinganishwa na km 11,000 alizozikuta, daraja la kusini, la kigamboni, mradi wa mabasi yaendayo kasi, reli ya tanga to musoma+bandari ya musoma itakayoanza hivi karibuni, ufumbuzi wa tatizo la umeme, uvumilivu alionao, uhuru wa kutoa maoni bila mipaka, uhodari wa kutatua matatizo kama uchochezi wa wanasiasa n.k. Hata hivyo tusipozitambua juhudi hizo, watu wa mataifa mengine watazitambua na kumpongeza kwa uwazi kabisa.

Tutabaki tunalalamika kuwa Kikwete hivi Kikwete vile lakini ukweli utabaki kuwa J.K is a super president ever happened in TZ.!

Na ingekua si kijobi-lion kuchafua hewa tungekua juu zaidi!
 
Back
Top Bottom