Dan Zwangendaba
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 5,482
- 7,459
Mo Ibrahim Leadership Prize ni tunzo anayopewa kiongozi msataafu aliyetumikia nafasi ya juu kabisa ya uongozi miongoni mwa nchi za Kiafrika, na katika uongozi wake aliheshimu na kuruhusu demokrasia, akasimamia utawala bora na kuondoka madarakani kwa kuheshimu mihula ya kiuongozi na kukabidhi madaraka kwa anayemfuatia.
Mpaka Sasa, Rais Samia ni miongoni mwa marais wachache katika Afrika ambaye ameweza kuweka mizania nzuri ya kusimamia mabadiliko ya kiuchumi, demokrasia, utawala bora na uimrishaji wa huduma za jamii. Kama ataendelea hivi na kuruhusu uchaguzi huru na wa haki hapo 2025 na akaondoka madarakani kwa misingi hiyo, bila shaka atakuwa kiongozi wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashabiki na Kati kutwaa tuzo hiyo.
Hapana ubishi kuwa kasi ya Samia katika ujenzi na uimarishaji wa huduma za kijamii hususan elimu, maji na afya haina mfanowe kwa Sasa. Maudhui ya taarifa za habari hususan ITV katika kipindi takribani mwaka Sasa, ni juu ya utekelezaji au uzinduzi wa miradi mbalimbali ya elimu, afya na maji.
Chapa Kazi mama, kazi iendelee.