Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,205
- 5,334
Ndoto ya jiji la Dar es salaam kuwa na jengo refu zaidi la ghorofa 40 ilivyotokomezwa na utawala wa serikali ya awamu ya nne:-
Hii ni kufuatia chapisho lililoandikwa na Martin Maranja Masese katika ukurasa wake wa mtandao wa X unaozungumzia taarifa kuhusiana na uliokuwa mpango wa ujenzi wa jengo refu zaidi Dar es salaam ambao ungekuwa ndiyo landmark ya jiji la Dar es salaam na Bwana Freeman Aikaeli Mbowe.
Nanukuu.."Architectural, Engineering consultants and master planners G+40 Bilicanas Tower on Mkwepu Street, Dar es salaam (perspective view),
Mradi huu ungelikuwa na ghorofa refu zaidi Dar es salaam, mali ya Freeman Aikaeli Mbowe, walikataliwa na serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete...hoja ilikuwa ni "mpinzani atajengaje the landmark of Dar es salaam!?"
Mwisho wa kunukuu.
Kama ni kweli hili lilifanyika kwa kigezo cha mambo ya kisiasa basi serikali iliwakosea sana watanzania ambao wanatamani maendeleo ya nchi yao na wangependa kuona wawekezaji wazawa wakipewa nafasi zaidi.
Hili jengo si kuwa tu lingeipendezesha Dar es salaam lakini pia lingezalisha ajira nyingi kwa watanzania, kuliko ilivyo hivi sasa baada ya kuibomoa iliyokuwa club ya Bilicanas (chanzo kingine kisicho rasmi pia kinadai ni sakata la kikodi kati ya wamiliki wa Billz na NHC ambalo liliamuliwa kimahakama)
Eneo hili lenye thamani kubwa katikati ya jiji hivi sasa linatumika kama parking ya magari yanayolipia sh.1000/= na hivyo kupoteza mapato na ajira nyingi ambazo zingeweza kutengenezwa na Bilicanas Tower endapo ingeruhusiwa iweze ku-exist.
Ombi langu kwa mwekezaji na Serikali kama kweli ilikuwepo azima hii nzuri kwa maendeleo ya Dar es salaam na Tanzania kiujumla warudi mezani na Serikali ya Mama Samia Suluhu naamini ni sikivu na inapenda wawekezaji.
Wayaweke sawa hili mwekezaji huyu aruhusiwe kuianza upya project yake maana mwisho wa siku watanzania tunachotaka kuona sisi ni maendeleo na ajira kwa watu wetu na siyo vinginevyo.
Maana hatuna haja ya kugombania fito wakati sote twajenga nyumba moja, tunatambua kuwa project zina maandalizi na gharama zake pamoja na muda wa utekelezaji ukishapita huwa umepita, pengine mwekezaji nae alishakata tamaa akaamua kuendelea na mengine,
lakini endapo Mbowe atakuwa na dhamira ya dhati ya kurejesha plan yake mezani na akaamua kuanza upya nafikiri hakuna mtanzania atakayepinga ujenzi wa jengo la namna hii katikati ya jiji letu pendwa la mzizima na itakuwa furaha kwetu kama wazalendo kuwa na mzawa mwenye kutuheshimisha kwa uwekezaji mkubwa wa namna hii ndani ya Tanzania.