Bubu ataka kusema,
Wewe siyo msemaji wa 'Watanzania wengi' hizo zako ni hisia tu na ambazo hazijengi hoja ya nguvu katika majadliano. Ukweli unabaki kuwa JK amefanya kazi yake vizuri na anastahili pongezi kwa hilo. Tatizo ambalo amelitatua ni tatizo la nchi na wala siyo tatizo lake binafsi. Huenda wale ambao haitakii mema nchi yetu walitaka kuona kuwa suala EPA haliishi na liendelee kuwa ni ajenda kila kukicha, tutafika kweli? JK is smart and Intelligent!
Kwangu mimi pesa sio jambo la msingi sana, kwani hizo zinatafutwa tu na Tanzania ilivyotajiri tunazo, na kwa kweli kama Mungu angetufunulia kujua ni mabilioni mangapi yameibiwa TZ tungusema na kuthibitisha kuwa EPA ni cha mtoto. Jambo la msingi ambalo watanzania wengi walilitegemea ni hatua za kisheria. Kikwete kushindwa kuwapeleka wezi wa EPA mahakamani kama ambavyo wezi wa kuku wanavyopelekwa ni kielelezo tosha kuwa jamabo la EPA limemshinda. Kwa kweli mimi bado sijaona kama amefanya kitu mpaka sheria ichukue mkondo wake. Wapelekwe mahakamani hata kama hakuna hata shs 1 iliyorudishwa ili liwe fundisho kwa wengine. Kama hawa watarudisha kisha kusamehewa je wakitokea wengine wa namna hiyo itakuwaje? Bwana Pundamilia kuwa mzalendo halisi na uache ushabiki tu.
Historia itakuja kutuhukumu.