Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,554
- 19,420
Sijadiliani hapa kwenye forum kwa kutumia hisia, kwahiyo sijadai kuwa ni msemaji wa watanzania walio wengi, zaidi ya hapo siwezi pia kuwa msemaji wa familia yangu katika suala la EPA.
Sitakushawishi wala kukulazimisha umsifie Mh Rais kwani hiyo siyo kazi yangu. Mimi nipo hapa kujieleza yale ambayo ninaamini ni ya kweli na hata taasisi na watu wengi wameona kama nilivyoona mimi.
hujaona upungufu ulionao katika hii mada uliyoanzisha mwenyewe? mimi situmii hisia bali ninataka kujua waliohusika na wizi wa EPA wamechukuliwa hatua zipi za kisheria. Nchi hii inaendeshwa kwa sheria siyo kwa longo longo nyingie yoyote ile, na serikali ndiye msimamizi mkubwa wa sheria. Kama wewe unajitenga na familia yako katika mambo ya kitaifa basi wengine tunashirikiana na familia zetu.