Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni; Bravo JK

Hivi IMF wana msaada gani tanzania kazi yao ni kumonitor monetary systems na hawatupi hata senti moja hela zilizoibiwa sio zao. Lets wait for the real donors and see what they will say to their tax payer.
 
Aloo pole, pole sana. Kama unampongeza Kikwete kwa swala la EPA naona kidogo umekosea.Naomba ujiulize maswali yafuatayo halafu ukishapata majibu ukae chini utulie:
*Nani aliibua suala la EPA
*Kwanini serikali ya CCM siyo iliyoibua swala la EPA,wakati ndiyo yenye
wabunge wengi bungeni
*Raisi Kikwete na watendaji wake walikuwa wapi, huku nchi ikionekana
kwa dhahiri kwamba inateketea?
*Watuhumiwa wamechukuliwa hatua gani mpaka sasa
*Hata kama inaonekana kuna hatua zinachukuliwa, kwanini muda mrefu kiasi
hicho umepita?
*Kwanini watuhumiwa hawajachukuliwa hatua,za kuridhisha mpaka sasa?
Naomba hawa IMF au World Bank wasikutishe, hawa ni wadau tu katika ufisadi.
 
Tuko pamoja kichuguu. Si hotuba wala maamuzi ya Prezda yanaonesha usiriazi katika kushughulikia mafisadi wa epa.
 
Quote:

Mwakyusa:Natafakari ushauri wa kujiuzulu

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, amesema ushauri wa kutakiwa kujiuzulu kufuatia matatizo yaliyojitokeza ya watoto kuzirai baada ya kupewa dawa za chanjo ya kichocho na minyoo, amelipokea, lakini bado anautafakari.

Mkuu, sidhani kama huyu ataachia ngazi maana itampa kazi nyingine tena JK ya kupangua baraza la Mawaziri. Inadaiwa huwa analalama kazi hiyo ni ngumu sana :)
 
Ni kawaida hata kwenye msafara wa mamba na makenge huwa wamo ndani yake. Lete hoja na si vinginevyo.

pundamilia,

Umenena mwenyewe kwamba mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Hii ni kweli sana kwa sababu mbele ya mamba, kenge huonekana mnyonge. Na hivyo hivyo mbele ya MAFISADI wananchi tulio wengi tunakuwa wanyonge lakini haki yetu tupeni. Umeamua kwa sababu zako kuvaa miwani waivaayo watu wa aina yako na kuona mafanikio hata pale palipo dhahiri kuwa hamna lolote. Hivyo si ajabu Tanzania, nchi iliyojaaliwa kila aina ya utajiri inajikuta miongoni mwa mataifa masikini na ombaomba. Raisi wetu ameweka rekodi duniani ya kutembeza bakuli kukicha kama mzee Matonya hapa mtaa wa Samora.

Raisi wetu hatulii nyumbani kwa sababu matatizo aliyoapa kuyapa ufumbuzi yamemzidi kimo. Raisi wetu anakuwa bubu mbele ya MAFISADI wenzake kwa sababu wanamzidi kete kwa kuwa ndio waliotumia pesa zao kumweka madarakani. Raisi wetu anasifiwa na na nchi matajiri kwa kuwapa hazina yetu na kuwawezesha kula bila kunawa katika meza ambayo tulimchagua atuandalie sisi wananchi wake. Raisi wetu anakula na kunywa na maadui ambao wananchi walimpa ridhaa ya asilimia 80% awashughulikie. Raisi wetu anafunga milango ya Ikulu na kuwaacha wazee, wanaodai haki yao huku wakizidi kudhoofika kiafya, wakisota nje ya LANGO LA IKULU.

Pundamilia, pamoja na kwamba umeniita kenge kwenye kundi la mamba, ndiyo nakubali. Lakini wewe unayempa sifa huyo Raisi nikuite nini na kwenye kundi la nani. Nafikiri jibu ni rahisi na ninakuachia hilo jibu ulitafute wewe mwenyewe. Toka umetoa mada yako, nathubutu kusema umeona wananchi wazalendo walivyokushukia kama linyundo la chuma. Jiunge nasi tuikomboe nchi.
 
Nadhani sasa umepoteza dira, wewe umedai kuwa mimi ni mwanachama wa chama cha mafisadi. Nimekufahamisha kuwa hoja yako umeijenga kutokana na hisia kwani hunifahamu na huna ushahidi kwamba mimi ni mwanachama wa chama cha mafisadi. Zaidi ya hapo nikakueleza kuwa sijawahi kukisikia chama kinachoitwa chama cha mafisadi, sasa unataka nikueleze kitu gani ambacho mimi sikifahamu? Samahani kwa kutengua ubashiri na hisia zako kuwa ni za kufikirika na zisizokuwa na ukweli wowote. Please lete hoja za kweli na siyo za kupandikiza.

Hata siku moja siwezi kupoteza dira. Sichangii chochote hapa kwa kumchukia mtu yeyote yule bali nachukia sana viongozi ambao wanaiangamaiza Tanzania kwa kufanya maamuzi mbali mbali ambayo hayana maslahi na Tanzania. Hakuna hoja ya kupandikiza hapa. Unaishi nchi ya kusadikia ndiyo maana hujasikia chama kinachoitwa chama cha mafisadi, vingineyo ungekuwa unafahamu chama cha mafisadi ni chama kipi. Nimetoa na data za kuonyesha kwamba huyo njemba unayemsifia si lolote si chochote wewe unasifia kama kipofu tu na kuimba kama kasuku hata ukiulizwa maana ya wimbo unaouimba hujui maana yake. Nitakuwekea tena data hizo ili kukuonyesha kwamba siandiki mambo ambayo siwezi kuyathibitisha kama ulivyo wewe na kuimba nyimbo kama kasuku. Zipitie tena data hapo chini halafu ujaribu kuzijadili moja baada ya nyingine.

1. Ahadi za kupitia mikataba ya madini ambayo haina maslahi kwa Watanzania zilikuwa nyingi mno wakati wa kampeni, kilichofanyika hadi hii leo unakijua au kwa kukumbusha tu ni sifuri, zero, ZILCH.

2.Ahadi za maisha bora kwa kila Mtanzania hakuna chochote, bali tunachokiona ni ahadi za maisha bora kwa kila fisadi.

3. Fisadi Mkapa kakupua Kiwira mchana kweupe mgodi ambao unathamani ya shilingi bilioni 4. Amejiuzia kwa shilingi milioni 700, lakini kalipa shilingi 70 milioni tu. Juhudi zetu Watanzania kuhakikisha mgodi huu unarudishwa chini ya miliki ya Watanzania hadi hivi sasa zimegonga ukuta. "Viongozi" wanajifanya kama hawaelewi yale tunayoyazungumza.

4. Ahadi za ari mpya, nguvu na kazi mpya hatuoni chochote bali midebwedo tu kila kukicha, usanii na uVDG.

5. Ufisadi wa rada, mpaka leo hii Watanzania tuko gizani kuhusiana na pesa zetu shilingi bilioni 12 walizolipana mafisadi katika ununuzi wa rada hiyo akiwemo mzee wa vijisenti aliyekuwa na vijisenti katika bank account ya nje ya nchi.

6. Kwa kifupi hakuna chochote kilichofanywa ambacho kinamhamasisha Mtanzania yeyote yule mwenye mapenzi ya kweli na Tanzania kumpigia kura JK, lakini kwenye chama cha mafisadi bado huyu ni mwenzenu anayestahili kuchaguliwa tena 2010 na si ajabu hata kubadilisha katiba ili aendelee kuwepo madarakani mpaka 2025!!! Halafu mnadai mna mapenzi ya kweli na Tanzania pamoja na kuona nchi inaangamia!!!!! kumbe mnatumia madaraka yenu kujitajirisha na kuwalinda mafisadi wenzenu!!!!
 
Sasa kafanya nini kizuri katika EPA! Kusema kakamata passport wakati watu wanasafiri bado!!!! Wanasafiria za bandia au? Kakufurahisha wapi wewe wakati anashughulikia suala la jinai kama vile la madai!!!!!!! Ikifika November akawapeleka mahakamani wahusika kwa kesi ya madai kutakuwa na tofauti gani na kesi za akina manji na mengi, au mengi na ze comedy, au mtikila na wengineo wanaodaiana mabilioni huko mahakamani!!!!! Zuri liko wapi sasa! Yaani, umetumwa-umetumwa na kama hujatumwa basi wewe ni jamii ya akina Kigunge!

Mimi huwa situmwi, ninajituma na niko huru kutoa mawazo yangu kwa yale ambayo ninaamini kuwa ni sahihi na nitaendelea kusimamia mawazo ambayo ni sahihi wakati wote.
Hata kama ningekuwa na tofauti zozote na Kikwete kama rais au vinginevyo, hainizuii hata kidogo kusema kuwa 'hapa Mh. Rais amefanya kazi nzuri'. Hili ninaweza kumpongeza mtu yeyote, sina uchoyo inda wala wivu. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
grrr yani nyumbani kwako watoto wamevaa nguo zimechanika,wana njaa na nyumba ni mbavu za mbwa,hali ya hapo inatisha na kila siku unacheka cheka unawaambia msihofu eeeh nipeni muda mambo yatakuwa mazuri. Ukienda kujiweni unasema aah kwangu mambo mazuri sanaaa, basi kijiwe kizima kinakusifu aisee we kiboko wa kutunza familia. Jirani yako ilhali akijua kabisa wanao wana njaa na nyumba yavuja anaenda nae kujiweni kusema aisee mzee wa jirani mambo yake safi?
does it even click on ones mind hali yetu ilivyo,shillingi yaendelea kuanguka,mafuta juu, rushwa ya viongozi juu, wezi wanafichwa. Hivi kuna asieona? wakati mwingine nahisi akili zetu hazina akili basi.Au tukiona tope tunaona ni chocolate cake?
What a wastage of resources and time kufanya maandamano kuunga mkono hotuba? hata kijana wangu wa form 1 aliuliza mbona sisi wajinga?
Nashindwa kabisaa kuelewa nini hasa kilikuwa special kwenye ile hotuba? eti kafanyaje?ooh punda just spare my breath, u know very well whats cooking? you know very well the money revolves among them, huyo huyo anayetangaza nawapa hadi novemba knows exactly kuna nini? tusipende kupotosha umma,amehandle vema wakati ukata wa maisha unazidi.
kweli tunahitaji uamko wa fikra otherwise tupo kama brainwashed vile.

Nimesikia kilio chako, Je unadhani wizi wa pesa za EPA ndiyo suluhisho la matatizo yaliyopo? Je unataka kuniambia kuwa so far hatua ambazo zimekwishafikiwa ni za kubeza? Kipindi hiki cha kufikia Nov 1, ni wakati ambapo tunataka wale wote waliochotewa hizo fedha warudishe ili ziende kuwafaidisha wakulima kama ilivyoagizwa, je hujaona kuwa hili ni jambo jema? Yatakayo fuata baada ya Nov 1, mimi na wewe tumekwishaambiwa kuwa wahusika watafikishwa katika vyombo vya sheria, hilo pia hujaliona?
 
Nasikia hotuba ya KIKWETE ina makosa na hivyo inabidi irekebishwe. Sasa hata haya ya EPA unaweza kukuta yanamakosa. Wanaokaa na kusifu kazi ya Kikwete kwa hili wakati HOTUBA INAMAKOSA, wanafikiria sawasawa?
Duuu, nilifikiri PUNDAMILIA SI PUNDA.

NB: Niongozeni kwenye listi ya watu wanaoona Muungwana hajafanya kitu na EPA.
CCM inatembeza U-SODOMA, inatulaaa!!! Mafisadi na Wawekezaji nao kwa sana tu.

Unasikia? Endelea kusikia!!!!
 
Hivi IMF wana msaada gani tanzania kazi yao ni kumonitor monetary systems na hawatupi hata senti moja hela zilizoibiwa sio zao. Lets wait for the real donors and see what they will say to their tax payer.

'A wishful think'
 
Mimi huwa situmwi, ninajituma na niko huru kutoa mawazo yangu kwa yale ambayo ninaamini kuwa ni sahihi na nitaendelea kusimamia mawazo ambayo ni sahihi wakati wote.

Hata kama ningekuwa na tofauti zozote na Kikwete kama rais au vinginevyo, hainizuii hata kidogo kusema kuwa 'hapa Mh. Rais amefanya kazi nzuri'. Hili ninaweza kumpongeza mtu yeyote, sina uchoyo inda wala wivu. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Afadhali unatambua kuwa uko huru kutoa mawazo yako kulingana na unavyoamini. Kwa hiyo, haya ni mawazo yako tu kulingana na imani yako, na wala hayana ukweli wowote ule.

Je unatamabua vile vile kuwa imani yako inaweza kuwa si sahihi hivyo ukatoa mawazo yasiyo sahihi?

Je unatamabua kuwa siyo vyema kulazimisha watu wengine wakubaliane na mawazo yako. Ukiona wengi hawakubaliani nawe, ama nyamaza uachane nao au kubaliana nao; lakini kujaribu kulazimisha ili mawazo yako yakubalike ni kupoteza muda bure. Ni afadhali ungetuelimisha ambao hatujaona ya kusifia kuliko kutulazimisha tusifie lislokuwepo. Hii tabia ya kufuata mkumbo kama vile kuandamana eti kuunga mkono hotuba ya raisi ni kati ya mambo yayoturudisha nyuma sana kimawazo.
 
chikira;277796]Aloo pole, pole sana. Kama unampongeza Kikwete kwa swala la EPA naona kidogo umekosea.

Nina kuhakishia kuwa sijakosea kumpongeza Mh Rais, ni haki yangu na niko huru kufanya hivyo

Naomba ujiulize maswali yafuatayo halafu ukishapata majibu ukae chini utulie:
*Nani aliibua suala la EPA
Serikali ndiyo iliyoibua suala la EPA (Rejea hatua na maagizo ya serikali yaliyoagiza akaunti ya EPA ikaguliwe baada ya Gov Kuwa amekataa)

*Kwanini serikali ya CCM siyo iliyoibua swala la EPA,wakati ndiyo yenye
wabunge wengi bungeni

Nimekujibu hapo juu (inaonekana kuwa swali lako umelichanganya na kushindwa kujua bunge ni nini na serikali ni nini)

*Raisi Kikwete na watendaji wake walikuwa wapi, huku nchi ikionekana
kwa dhahiri kwamba inateketea?

Fafanua swali lako vizuri una maanisha nini?

*Watuhumiwa wamechukuliwa hatua gani mpaka sasa
Je, ulisikiliza hotuba ya Mh Rais pale bungeni ambayo ndiyo chanzo cha mada hii? kama hujui ni hatua gani zimechukuliwa je umewezaje kuchangia hapa na kupinga pongezi zangu?

*Hata kama inaonekana kuna hatua zinachukuliwa, kwanini muda mrefu kiasi hicho umepita?

*Kwanini watuhumiwa hawajachukuliwa hatua,za kuridhisha mpaka sasa?

Inaonesha you are not sure either!

Naomba hawa IMF au World Bank wasikutishe, hawa ni wadau tu katika ufisadi.[/QUOTE]

Hakika, huenda you are not in the picture.
 
pundamilia,

Pundamilia, pamoja na kwamba umeniita kenge kwenye kundi la mamba, ndiyo nakubali. Lakini wewe unayempa sifa huyo Raisi nikuite nini na kwenye kundi la nani. Nafikiri jibu ni rahisi na ninakuachia hilo jibu ulitafute wewe mwenyewe. Toka umetoa mada yako, nathubutu kusema umeona wananchi wazalendo walivyokushukia kama linyundo la chuma. Jiunge nasi tuikomboe nchi.

Kama umeshakubali kuwa wewe ni kenge, unataka nini tena, yamekwisha tusonge mbele!
 
Hata siku moja siwezi kupoteza dira. Sichangii chochote hapa kwa kumchukia mtu yeyote yule bali nachukia sana viongozi ambao wanaiangamaiza Tanzania kwa kufanya maamuzi mbali mbali ambayo hayana maslahi na Tanzania. Hakuna hoja ya kupandikiza hapa. Unaishi nchi ya kusadikia ndiyo maana hujasikia chama kinachoitwa chama cha mafisadi, vingineyo ungekuwa unafahamu chama cha mafisadi ni chama kipi. Nimetoa na data za kuonyesha kwamba huyo njemba unayemsifia si lolote si chochote wewe unasifia kama kipofu tu na kuimba kama kasuku hata ukiulizwa maana ya wimbo unaouimba hujui maana yake. Nitakuwekea tena data hizo ili kukuonyesha kwamba siandiki mambo ambayo siwezi kuyathibitisha kama ulivyo wewe na kuimba nyimbo kama kasuku. Zipitie tena data hapo chini halafu ujaribu kuzijadili moja baada ya nyingine.

1. Ahadi za kupitia mikataba ya madini ambayo haina maslahi kwa Watanzania zilikuwa nyingi mno wakati wa kampeni, kilichofanyika hadi hii leo unakijua au kwa kukumbusha tu ni sifuri, zero, ZILCH.

2.Ahadi za maisha bora kwa kila Mtanzania hakuna chochote, bali tunachokiona ni ahadi za maisha bora kwa kila fisadi.

3. Fisadi Mkapa kakupua Kiwira mchana kweupe mgodi ambao unathamani ya shilingi bilioni 4. Amejiuzia kwa shilingi milioni 700, lakini kalipa shilingi 70 milioni tu. Juhudi zetu Watanzania kuhakikisha mgodi huu unarudishwa chini ya miliki ya Watanzania hadi hivi sasa zimegonga ukuta. "Viongozi" wanajifanya kama hawaelewi yale tunayoyazungumza.

4. Ahadi za ari mpya, nguvu na kazi mpya hatuoni chochote bali midebwedo tu kila kukicha, usanii na uVDG.

5. Ufisadi wa rada, mpaka leo hii Watanzania tuko gizani kuhusiana na pesa zetu shilingi bilioni 12 walizolipana mafisadi katika ununuzi wa rada hiyo akiwemo mzee wa vijisenti aliyekuwa na vijisenti katika bank account ya nje ya nchi.

6. Kwa kifupi hakuna chochote kilichofanywa ambacho kinamhamasisha Mtanzania yeyote yule mwenye mapenzi ya kweli na Tanzania kumpigia kura JK, lakini kwenye chama cha mafisadi bado huyu ni mwenzenu anayestahili kuchaguliwa tena 2010 na si ajabu hata kubadilisha katiba ili aendelee kuwepo madarakani mpaka 2025!!! Halafu mnadai mna mapenzi ya kweli na Tanzania pamoja na kuona nchi inaangamia!!!!! kumbe mnatumia madaraka yenu kujitajirisha na kuwalinda mafisadi wenzenu!!!!

In fact sioni wapi pa kubadilisha pamoja na maelezo yako marefu ndiyo umezidi kuharibu na kuonesha kwa kiasi gani umepoteza mwelekeo. Tafuta mtu atayeweza ku-refresh your mind.
 
kichuguu;278338]Afadhali unatambua kuwa uko huru kutoa mawazo yako kulingana na unavyoamini. Kwa hiyo, haya ni mawazo yako tu kulingana na imani yako, na wala hayana ukweli wowote ule.
Je unatamabua vile vile kuwa imani yako inaweza kuwa si sahihi hivyo ukatoa mawazo yasiyo sahihi?

Na wewe hayo hapo juu pia ni mawazo yako siyo lazima yawe na ukweli wowote.

Je unatamabua kuwa siyo vyema kulazimisha watu wengine wakubaliane na mawazo yako.

Hakuna mahali popote nilipoandika kuwa ninalazimisha ukubalianae na mawazo yangu, kama ipo nitafurahi kama utanionesha.

Ukiona wengi hawakubaliani nawe, ama nyamaza uachane nao au kubaliana nao; lakini kujaribu kulazimisha ili mawazo yako yakubalike ni kupoteza muda bure.

Unachekesha sana, itabidi hii kauli yako tuwapatie wana-demokrasia waliobobea waifanyie kazi.
Sidhani kamakutokukubaliana na mtu kimawazo suluhisho ni kunyamaza? Ninyi ndiyo mliyoifikisha nchi hii hapa ilipo kwa vile hamkukubaliana na CCM basi mkanyamaza!!!

Ni afadhali ungetuelimisha ambao hatujaona ya kusifia kuliko kutulazimisha tusifie lislokuwepo. Hii tabia ya kufuata mkumbo kama vile kuandamana eti kuunga mkono hotuba ya raisi ni kati ya mambo yayoturudisha nyuma sana kimawazo.[/QUOTE]

Sioni uhusianao wowote wa kitendo changu cha kumuunga mkono Mh Rais na kukurudisha wewe nyuma kimawazo
 
Back
Top Bottom