Mnyika, Balille, Rostam Aziz na kisa cha sms!

yaani nyika ungekuwa karibu ningekununulia bia ya tusker kwa jinsi ninavyoipenda! huyu ni fisadi, tena hayawani na mhaini. alitaka kutumia magazeti yake kulitumbukiza taifa kwenye vita na ghasia halafu, akimbilie kwake huko uajemi. nani asiye kuwa na hasira dhidi ya bwege rostam azizi? naomba na miye simu yakew nimpashe......kudadeki
 
Sijaona Mantiki ya Ndugu yangu Zitto kwenda kumtete Bwana Mbowe katika jukwaa la wahariri.Kama anaona Mbowe anapendwa kule Tarime basi angebaki ahudhulie Mazishi kama alivyobaki yeye Zitto.There is something wrong which this guys wanna hide to us.Siyo kwamba Chuki ilipandikizwa na CCM ila baada ya Wangwe kusimamishwa CHADEMa kuna watu walichukizwa hasa wale watu wa kemakorere na ndiyo walikuwa na sumu waliyonyeshwa toka zamani ya Ukabila.

Mkuu Gembe,

usiwe mgeni kwenye siasa, hasa za Afrika! Mkuu wa usalama na vyombo vyake wanapokuambia kuwa havina uhakika wa kukupa ulinzi nadhani unajua nini wanamaanisha ...

Hata pale ZANU-PF walipoona wanashindwa kwenye kampeni za mara ya pili, walitumia Afisa Usalama na Polisi kumweleza MDC leader Tsvangirai kuwa hawana uhakika na usalama wake! maana "lolote" linaweza kutokea (la kupangwa ama la) na wao (Maafisa usalama) si wakulaumiwa kwani walishawaeleza.

Ukiwa na washauri wazuri uamuzi ni mmoja tu, kubali yaishe ONDOKA! Na nadhani una mfano hai wa Bwana Tsvangirai tangu tangazo hilo hakushiriki tena kampeni! Na huo ndio ulikuwa msimamo wa washauri wa Mbowe/ CHADEMA.

Siasa za Afrika ni sawa na punguwani! Kutoa Roho ni kitu cha kawaida!
 
[
rostam azizi hawezi kwenda mahakama yeyote katika nchi hii labda huko kwake uajemi. hawezi kwenda kwa kuwa ataingia mahakamani mikono yake ikiwa inavuja damu, kila mtu atamshangaa muuaji anayekana kuwa si muuaji akiingia mahakani huko amebeba kichwa cha aliyemuua, na huko mkono mmoja amenyoosha akiapa kuwa hakuua!
 
Twende mbele turidi nyuma; Chama Cha Mapinduzi kama "Chama/Taasisi" kimekomaa sana. Vitendo hivi vya Chadema nidhahiri kabisa kuwa hawa wenzetu hawako tayari kuongoza nchi yetu. Nasikitikika sana kukubaliana na ukweli huu...!!

Mkuu YY,

vuta pumzi kisha fikiri, CCM itaachaje kukomaa wakati wana Televisheni (TBC) na Radio (RTD) vyote vya Umma viko kwa ajili yao! Na bado kuna vyombo vingine binafsi ambavyo vinakwenda na usemi wa Mh. sumaye ".. ukitaka mambo yako yakunyookee ..."

Sasa hapo fairness iko wapi? Kutokana na hayo hapo juu hata kama chama tawala ni CHAUSTA bado kingeonekana ni CHAMA KOMAVU SANA!
 
nadhani wachangiaji wengi hapa jf, hamjui impact ya propaganda za rostam aziz kuhusu kifo cha wangwe na athari zake kwa taifa hili, muda mfupi tu tangu kuandikwa habari ya kuwa wangwe kauuwa, tayari kulkuwa na tension kali sana katika miji ya tarime na moshi, mjini moshi ambako nilikuwa wakurya walikuwa na wasiwasi sana, kama wachaga walioko tarime wangeshambuliwa, nasikia maduka ya wachaga tarime yalifungwa siku nzima. wakati huo rostam azizi alikuwa yuko bize akichochea vita, na hali anayo ticket ya ndege ya kukimbilia ughaibuni, na mamilioni ya dola ya kula mpaka afe, yale aliyioiba pale benki kuu

kuna lugha gani ya kuongean na hayawani, punguani, zandiki, nduli, mpuuzi, fala, mnafiki, kama huyu? nisiikosee bure jf kwani ningemkuta ningemzaba kibao na tusi kama.....
 
Kusema eti Chadema, itakufa kwa sababu Mnyika amieita spade a spade ni mawazo mufilisi, na kama ni kweli basi hakukuwepo na chama ikabisa from the beginning, sometimes tunamkuza mno Rostam,

However, Chadema waache spin, Mwenyekiti wao hakuhudhuria mazishi kwa sababu wananchi wa huko wasingekubali, hii ni fact na political reality, kama vile Muungwana akiwa waziri alivyokataliwa kwenye mazishi ya mke wa Mangula, hizi spin zingine haziwezi kuongeza wala kupunguza umaarufu na uwezo wa chama cha siasa kukubalika kwa wananchi,

Kama ni jimbo la Tarime, tunajua kuwa CCM haiwezi kushinda huko hata kwa bunduki, nina dada anayeolewa na mkulu wa kutoka huko Tarime, aliyeniambia in advance kuwa mwenyekiti wa Chadema, hawezi gusa huko kwenye mazishi spinzingine hazina maana ni waste of time!

Bravo tena kwa Mnyika na salute juu!
 
niliwahi kuandika hapa kuwa linapokuwa swala la taifa tuweke vyama vyetu na itikadi zetu pembeni, hapa point ni moja hayawani mmoja kwa jina rostam azizi alitaka kulitumbukiza taifa letu kwenye damu, kisha alale mbele. namna ya kumshughukilia huyu

1.fungia magazetu na media zote anazomiliki

2. zuia paspoti yake asije akaanzisha vita akatoroka

3. kamata wote walioandika ule uppuuzi choma ndani, nyangana leseni zao za uandishi wa habari

4. magazeti yale yaombe msamaha
 
Sijaona Mantiki ya Ndugu yangu Zitto kwenda kumtete Bwana Mbowe katika jukwaa la wahariri.Kama anaona Mbowe anapendwa kule Tarime basi angebaki ahudhulie Mazishi kama alivyobaki yeye Zitto.There is something wrong which this guys wanna hide to us.Siyo kwamba Chuki ilipandikizwa na CCM ila baada ya Wangwe kusimamishwa CHADEMa kuna watu walichukizwa hasa wale watu wa kemakorere na ndiyo walikuwa na sumu waliyonyeshwa toka zamani ya Ukabila.

Siyo kwenye siasa ndugu yangu. Kwenye siasa common sense inasema lazima ujibu kiwingu chochote kinachoelekea kukukosanyisha na wapiga kura. Ningeshangaa na ningewalalamikia sana viongozi wa chadema kama wangekalia kimya umafia huu wa vyombo vya habari. They did the right thing, absolutely the right thing..na ndio maana wahariri wameiona hoja na sasa wameamua kuunda kamati ili ukweli uwekwe wazi, in a non partisan manner.
 
Wanabodi,

Ebu tuwe wawazi kwanza na kutoa solution ambazo zinaweza kubeba uzito sawa na hayo aliyosema Mnyika..
Ikiwa wewe umewekwa kati kama Mnyika ni njia gani ungeitumia kupambana na magazeti ambayo yamekusudia kuharibu jina lako na la chama chako wakati unafahamu fika ni UONGO na mtu aliye nyuma ya kashfa hizi unamfahamu.
Nambieni bila kuzunguka mngefanya nini bila kuharibu wakati huo huo ujumbe wako umefika kwa mhusika na kutoa tahadhali kwake kutoendelea na mchezo mchafu wa Siasa..

Jamani nachokiona hapa ni hali halisi ya Udanganyika - WOGA hasa kuogopa wenye fedha na nguvu ya mtu kama Rostam. Hivi kweli nyie Wadanganyika mnaogopa kumwita ROSTAM - FISADI wakati mmeweza kumwita Lowassa aliyekuwa waziri mkuu!..Kumbe kuna uwezekano mkubwa mkiambiwa simameni na kumwita Lowassa mbele ya macho yake kuwa ni Fisadi hamuwezi isipokuwa mnaweza sana kuandika humu ktk majina yenu ya kujificha!...
Then kazi ya Ukombozi wa nchi yetu ni kubwa sana kuliko nilivyofikiria, as a fact narudi tena ktk hisia zangu za awali kwamba Wabongo huwa tunasema sanaaaa lakini inapofika ktk vitendo utabakia peke yako! wote wataingia mitini..
To prove me wrong nambieni nyie mnge deal vipi na swala kama hili!
 
nadhani wachangiaji wengi hapa jf, hamjui impact ya propaganda za rostam aziz kuhusu kifo cha wangwe na athari zake kwa taifa hili, muda mfupi tu tangu kuandikwa habari ya kuwa wangwe kauuwa, tayari kulkuwa na tension kali sana katika miji ya tarime na moshi, mjini moshi ambako nilikuwa wakurya walikuwa na wasiwasi sana, kama wachaga walioko tarime wangeshambuliwa, nasikia maduka ya wachaga tarime yalifungwa siku nzima. wakati huo rostam azizi alikuwa yuko bize akichochea vita, na hali anayo ticket ya ndege ya kukimbilia ughaibuni, na mamilioni ya dola ya kula mpaka afe, yale aliyioiba pale benki kuu

kuna lugha gani ya kuongean na hayawani, punguani, zandiki, nduli, mpuuzi, fala, mnafiki, kama huyu? nisiikosee bure jf kwani ningemkuta ningemzaba kibao na tusi kama.....

Mkuu mwikimbi
Mimi ninakubaliana na wewe, huyu fisadi RA hana ubinadamu kabisa,. Yaani hata kabla Wangwe hajalazwa mahali pake pa milele yeye anaanza kufanya campaign za kuchukua jimbo la Tarime kwa kutumia habari za uongo bila kujua madhara yanayoweza kutokea kwa Taifa?. Nafikiri CCM hilo jina la "King Maker" walilompa litawafanya siku moja wajutie na kumwita "King Terror". Sifa wanazompa zitaliingiza Taifa katika majuto makubwa huko tuendako. Huyu Jamaa halitakii mema Taifa letu, au kwa kuwa ana uhakika kuwa yeye atapewa hifadhi na ulinzi wakati watu wakiuwawa. Hakuna adui mkubwa katika ulimwengu kama uchonganishi, maana mpaka ithibitike kuwa ni uwongo roho za watu wangapi zitakuwa zimetoka?, Je Huyu fisadi pamoja na kutuibia hela zetu anaweza kulipa gharama ya amani? au atatuachia manyoya na kutafuta safe haven nje ya nchi huku sisi tukiuwana wenyewe?, Mi nafikiri sasa huu ni wakati wa watanzania wenye uchungu na nchi yao kusema NO kwa Mamluki kama akina ROSTAM AZIZ.
 
Rostam ni Mbunge na anakiapo cha jamhuri hana sababu ya kwenda mahakamani.

Mnyika atashitakiwa na jamhuri sawa na mtu aliyemzaba kibao DC au RC. Nikweli viongozi wetu wamekuwa assulted kwa sms mno, tumeshampata Mnyika na ameshakiri kuwa alimtusi! tunaanza nae, sawa jamani?

BAKITA ndio offical body ya kutafsiri kiswahili, kamusi ya kiswahili inasema fisadi ni mtu mzinifu, Rostam hawezi kuwa basha waMnyika kamwe, ila sina uhakika kama Mnyika sio shoga! sheria ichukue mkondo wake tu.

mwikimbi! Habari kuwa wangwe kapigwa risasi mbili kichwani zilianzia jf sio RAI, habari ya chenge kunywa sumu zilianzia jf sio Rai, kama kuna upotoshwaji basi ulianzia jf. pia Kwa nini tumsakame rostam wakati kuna mhariri mtendaji wa Rai?

Kuhusu EPA, zitto ambaye ni bosi wa Mnyika ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali hivyo anajua zaidi nani mhusika. Kwa mfumo wa Bunge M'kiti wa PAC anatoka upinzani. Wakati Uhuru Kenyatta akiwa M'kiti wa PAC ali-account kila single senti ya serikali ya kenya, Ng'ombe atatokaje bandani wakati funguo tunazo mfukoni? tujiulize.

Ati Rwanda! radio muhabura ilikuwa sawa na jf haikujulikana inatangazia kuanzia wapi na mpaka leo mitambo yake haijulikani iliko.
 
Ukitaka kummaliza nyoka bila madhara sharti umkate kichwa au ponda ponda kichwa chake.Tatizo lililo mbele yetu sasa haijulikani nani kichwa nani kiwiliwili na nani mkia kati ya RA, JMK na EL kama hawa wakiondoka nchi hii inaweza kurudi kwenye mstari.
 
Pamoja na kuwa sikuwa na nia ya kuchangia katika hatua hii kwa sababu zinazoeleweka, lakini nadhani lazima nimpongeze Dogo Mnyika kama ilivyoitwa. Tofauti na aliyedhani ndiyo mwisho wake kisiasa, nadhani wakati wa siasa za maficho sasa umepitwa na wakati. Ufisadi hauna dawa nyingine isipokuwa kupigwa vita wazi. Wenye uwoga ni wale wasiojiamini. Yaliyoandikwa na Magazeti yaliyotajwa hayahitaji lugha nyingine isipokuwa kukemewa na wale wote wenye kupenda ukweli katika nchi hii. Nilikuwepo mimi kama mhusika mmojawapo, nilivyopokelewa na nilivyoagwa ni ishara tosha kuwa vyombo vilivvyoandika yaliyoandikwa yalikuwa na agenda tofauti kabisa na msiba uliotupeleka Tarime. Cha kutisha zaidi ni TBC1 chombo cha Taifa, kinachoendeshwa kwa kodi ya Watanzania wa makabila yote, itikadi zote inapoanza kuchukua sura ya uchochezi badala ya kujenga umoja wa kitaifa, na hasa kuwa na 'deliberate biased reporting'. Ningependa kuichallange TBC ilipatwa na kigugumizi gani baada ya mbinu yake kukwama? Sasa ndiyo ninaanza kutambua kwanini hotuba yangu siku ya TAMISEMI/Waziri Mkuu haikutangazwa. Sote tu watu wazima, wasomi wa kutosha hata kama hatujui sana IT kwa maana ya ufundi wa kurusha habari. TBC1 lazima ije clear katika hili. Hii haina maana ya kwamba naingilia hatua ya Jukwaa la Wahariri. Lakini kwa ujumbe Jukwaa lifahamu kuwa wadau tupo, na tunamaoni ya kutoa iwapo watahitaji katika jitihada za kutafuta ukweli. Naomba radhi kulazimishwa kutoa 'comment yangu' wakati tuko bado kwenye maombolezo. Maslahi ya Taifa yanahitaji ukweli bila kuchelewa, na ikilazimu vitabu vitakatifu vinajieleza vya kutosha kuhusu hatua yangu hii.
 
Rostam ni Mbunge na anakiapo cha jamhuri hana sababu ya kwenda mahakamani.

Mnyika atashitakiwa na jamhuri sawa na mtu aliyemzaba kibao DC au RC. Nikweli viongozi wetu wamekuwa assulted kwa sms mno, tumeshampata Mnyika na ameshakiri kuwa alimtusi! tunaanza nae, sawa jamani?

BAKITA ndio offical body ya kutafsiri kiswahili, kamusi ya kiswahili inasema fisadi ni mtu mzinifu, Rostam hawezi kuwa basha waMnyika kamwe, ila sina uhakika kama Mnyika sio shoga! sheria ichukue mkondo wake tu.

mwikimbi! Habari kuwa wangwe kapigwa risasi mbili kichwani zilianzia jf sio RAI, habari ya chenge kunywa sumu zilianzia jf sio Rai, kama kuna upotoshwaji basi ulianzia jf. pia Kwa nini tumsakame rostam wakati kuna mhariri mtendaji wa Rai?

Kuhusu EPA, zitto ambaye ni bosi wa Mnyika ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali hivyo anajua zaidi nani mhusika. Kwa mfumo wa Bunge M'kiti wa PAC anatoka upinzani. Wakati Uhuru Kenyatta akiwa M'kiti wa PAC ali-account kila single senti ya serikali ya kenya, Ng'ombe atatokaje bandani wakati funguo tunazo mfukoni? tujiulize.

Ati Rwanda! radio muhabura ilikuwa sawa na jf haikujulikana inatangazia kuanzia wapi na mpaka leo mitambo yake haijulikani iliko.

Asalaleeee! Kwa hiyo kile alichokitoa Dr Slaa kilikuwa ni orodha ya wazinifu? Na fisadi Rostam Aziz si alikuwepo kwenye orodha hiyo pia!

Asha
 
UFISADI ni mchanganyiko wa rushwa, wizi, ubadhirifu na maovu mengine ya jamii hiyo. Ndio corruption! Na neno hili limetumika sana Kenya na mwalimu Nyerere alikuwa akilipenda sana. Dr Slaa amelirudisha upya tu kwenye chati ya nchi yetu kupitia list of shame

Asha
 
Namuunga mkono Mnyika kwani unapopata audiance na fisadi inabidi umweleze ukweli kuwa yeye ni fisadi hakuna kumficha, hii tu ndo itawafanya wajue kuwa hali ni mbaya ndani ya tanzania na tunakaribia kuwakamua mapesa yetu yote waliyoiba.

Hakuna fitna kwa kumpongeza unapokluwa nae na kumtukana anapoondoka.
 
Rostam ni Mbunge na anakiapo cha jamhuri hana sababu ya kwenda mahakamani.

Mnyika atashitakiwa na jamhuri sawa na mtu aliyemzaba kibao DC au RC. Nikweli viongozi wetu wamekuwa assulted kwa sms mno, tumeshampata Mnyika na ameshakiri kuwa alimtusi! tunaanza nae, sawa jamani?

BAKITA ndio offical body ya kutafsiri kiswahili, kamusi ya kiswahili inasema fisadi ni mtu mzinifu, Rostam hawezi kuwa basha waMnyika kamwe, ila sina uhakika kama Mnyika sio shoga! sheria ichukue mkondo wake tu.

mwikimbi! Habari kuwa wangwe kapigwa risasi mbili kichwani zilianzia jf sio RAI, habari ya chenge kunywa sumu zilianzia jf sio Rai, kama kuna upotoshwaji basi ulianzia jf. pia Kwa nini tumsakame rostam wakati kuna mhariri mtendaji wa Rai?

Kuhusu EPA, zitto ambaye ni bosi wa Mnyika ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali hivyo anajua zaidi nani mhusika. Kwa mfumo wa Bunge M'kiti wa PAC anatoka upinzani. Wakati Uhuru Kenyatta akiwa M'kiti wa PAC ali-account kila single senti ya serikali ya kenya, Ng'ombe atatokaje bandani wakati funguo tunazo mfukoni? tujiulize.

Ati Rwanda! radio muhabura ilikuwa sawa na jf haikujulikana inatangazia kuanzia wapi na mpaka leo mitambo yake haijulikani iliko.

Unajua unaweza kufikiri watu wote wazima humu,kumbe wengine ...wamechelewa neno limeshakuwa na tafsiri yetu tuijuayo.Kam ndivyo walitakiwa waanza muda mrefu sana kuyashtaki magazeti yanayoandika neno fisadi yakiwemo ya serikali. EDDY HIVI WEWE SIO ROSTAM KWELI??

Waberoya
''wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo''
 
Suala afikishwe mahakamani au la niuamuzi wa DPP, kutoshitakiwa Dr.Slaa sio sababu ya Mnyika kutopanda kizimbani, sawasawa?
 
Eddy,
Mkuu ama kweli umenichekesha sana.. Sasa unataka vipi tafsiri ya neno Fisadi wakati wewe umeisha itoa?.. na iweje Fisadi kuwa tusi hali Uzinifu ni jambo ambalo asilimia 99 ya Watanzania tumepitia!..
Uzinifu maana yake ni kutembea kimwili nje ya ndoa yaani hata ukiwa na Girlfriend mkafanya hayo maswala basi nyie ni wazinifu. Leo iweje iwe tusi kiasi kwamba mnataka Mnyika aadhibiwe ati kampiga kofi DC.. Yaani nchi yetu ina sheria na haki kwa DC kumpiga kofi mwnanchi lakini sio kinyume!.. duh ama kweli tuna safari ndefu sana.
Fisadi mkuu ni mtu yeyote Mharibifu kwa kutumia hujuma, sasa kama Rostam hakutaka kuharibu jina la Mnyioka kwa kutumia vyombo vya habari mnaweza kutuambia ukweli ni upi?
 
Back
Top Bottom