Mnyika ashinda kesi dhidi yake; Hawa Nghumbi atakiwa kulipa gharama za kesi!

Nimeiona nguvu ya umma hapa posta full shangwe na ulinzi wa ffu juu nao wanashangilia kimya kimya
 
Huyu Mama Ng'umbi amenishangaza sana, kesi kubwa na muhimu kama hiyo ameweka Mashahidi watatu!
Ningeshangaa sana kama Jaji angekubali madai yake.
 
Jamani msikose kuja jangwani jumamosi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara wa chadema , viongozi wote wa CDM watakuwepo, nami nitakuwepo live nikirusha matangazo......
 
Tunawashukuru wapiganaji wote kwa kutujuza nadhani sasa hii ndio nguvu ya umma hakika mungu yuko upande wetu
 
kashinda mahakamani, je kwa wanachi waliomchagua mpaka sasa kawafanyia nini?
Tumwache aendelee tu kupiga bla bla zake...but ndio mwisho wake wa kuwa mbunge wa ubungo.

yule mama wa ukonga kafanya nini? Mbona wanataka kumng'oa wapiga kura wake. Umeshindwa vibaya mzee.
 
kashinda mahakamani, je kwa wanachi waliomchagua mpaka sasa kawafanyia nini?
Tumwache aendelee tu kupiga bla bla zake...but ndio mwisho wake wa kuwa mbunge wa ubungo.

pole sana . Najua wewe nigamba pole. Wacha sisi tushangilie ushindi wa haki vs dhuluma
 
Peoplesssssssssssssssss......pawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Kashinda mahakamani, je kwa wanachi waliomchagua mpaka sasa kawafanyia nini?
Tumwache aendelee tu kupiga bla bla zake...but ndio mwisho wake wa kuwa mbunge wa Ubungo.

Kwani wabunge wote wa CCM walioliongoza hilo jimbo la Ubungo tangu tupate uhuru wamewafanyia nini wananchi zaidi ya bomoa bomoa na kuhakikisha hawapati maji?
 
Pamoja sana mkuu,Tunashukuru kwa updates nzuri!
Hali ya mambo ni nzuri watu hawana munkari kama ilivyotarajiwa hasa wale wa Chadema ndio wengi na wanaonyesha wana matumaini ya Ushindi,

Hukumui haijaanza kusomwa tunaelezwa itaanza mida ya saa 3 hivi,

Polisi kwa mida hii sio wengi sana kwa hesabu hawafiki 50. Kwa ujumla hali ni ya amani kabisa!

Tutawajuza hatua kwa hatua moja kwa moja toka ukumbini!

Updates:

- Basi aina ya coaster lililobeba mashabiki wa chadema ndio linaingia huku likishangiliwa na watu kwa alama ya vidole viwili alimaarufu Amani na Upendo!

- Naaaaam vijana wakazi (FFU) ndio wanaingia kwenye eneo la tukio wakiwa wamevalia kikazi yani kama Baghdad lakini wapo kwa usalama tu hakuna dalili ya vurugu yoyote hali ni yaamani tu!

- Kuna mabishano ya hapa na pale kati ya wananchi na wahudumu wa mahakama, watu wanalalamika kuwa mbona mda unakwenda na hawaruhusiwi kuingia mahakamani! Lakini wamefanikiwa kuwasihii na wananchi wametuliza munkali

- Tunaendelea kusubiri mda ufike tuanze kufuatilia kesi hii!

- Naaaaam tumeshaingia ukumbini tayari kuanza usikilizaji wa kesi hii uendelee! Tumeambiwa tuzime simu lakini MIMI sitazima mwanzo mwisho!

- Tunasubiri jaji aingie na jopo la mawakili wa pande zote wapo tayari!

UPDATES:
Kuna kichekesho kimejitokeza hapa, yani wakati wakuingia ukumbini kuna mbinu iliyotumika na mashabiki wa CDM kuwabana mlangoni wale wa Magamba na wakashindwa kupata siti kilichofuata ni afande kuwatoa nje, wakati wakitolewa nje kuna kuna mwanachadema mashuhuri akaingia ukumbini afande akataka kumuunganisha na wanachadema kutoka nje, unaambiwa ukumbi umelipuka na kusema huyo siti ipoo!

Naaaaaaaaaaam Mh Mnyika ndio anaingia ukumbini anashangiliwa kwa makofi na Pipooooooozi Pawaaaaaaaaaaaaaa!

Updates:
Wakili wa Mnyika ndugu Mbogolo ndio anaingia anasalimiana na mnyika waapiga picha wanaendelea kupiga picha!
Sasa kilichobaki ni kumsubiri jaji tu aingie ukumbini!

Updates:
Jambo la kufurahisha ktk kesi hii nikuwa Mh Mnyika na Hawa Ng'umbi wamekaa pamoja na wanapiga stori kweli, hata alipotokea afisa usalama akataka kuwatenganisha mnyika amemwambia haina tatizo watu pipoooooooooooz!

UPDATES:

M/Kiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe aka Sauti ya Zege ndio anaingia anashangiliwa ile mbaya pipooooooozi


UPDATES: Mpaka dakika hii saa nne kamili bado Jaji haja ingia ukumbini, tunaendelea kumsubiri!

UPDATES:
Naaaam jaji ameingia na hukumu inaanza rasmi,

Jaji anaomba radhi kuwa ataisoma hukumu kwa lugha ya kitumwa! Twendeleeee!

Updates:
Jaji anaendelea na mapitio ya mwenendo wa kesi nzima tangu ilipoanza na mpaka ilipo, kimsingi ameanzia kwenye historia ya kampeni,uchaguzi, uhesabuji kura na utangazwaji wa mshindi, sasa anaingia kwenye malalamiko makuu ya mlalamikaji,

Vuteni subira naripoti kwa kificho maana tumeambiwa tuzime simu na kamera zote za wanahabari!

Mtanisamehe nitaripoti yale muhimu tu, longolongo za jiji sitaziripoti mda wa kutafsiri lugha ya kitumwa sina!
Jaji mwenyewe inamsumbua kusoma ana nasanasa tu wakati anaisoma kwenye karatasia utadhani kaambiwa aisome kichwani!

Bado anaendela kusoma mwenendo wa kesi! Hajaingia kwenye vifungu halisi vinavyosubiriwa!

UPDATES:
Naam Hoja ya kwanza ndio inaelekea ukingoni kuna dalili za jaji kuitupa nje! Pamoja sanaaaa!

HOJA zenyewe ni hizi:
1)Kwamba Mnyika alimtuhumu kuuza nyumba za UWT
2)Kutumia Laptop za Mnyika Kuhesabu kura
3)Kuingia watu wengi wa CHADEMA ktk chumba cha kuhesabia kura
4)Kuzidi kwa kura hewa 16,000
5)Kukosewa kwa karatasi za kujumulisha kura (form)

- Hoja ya kwanza imetupwaaaaaaa!

- Hoja pili inaendelea na kunadalili za kutupwa nje kwani jaji tayari keshasema hazikutumiwa ila lilikuwa kama ombi tu baada ya kuona za tume zipo slow! Bado anaendelea kufafanua juu ya hoja hiyo!

- Shtaka la 4 la laptop binafsi limetupwa mbali. Bado moja na la mwisho la Idadi kubwa ya watu kituo cha kuhesabia kura

Tumeshindaaaaaaaaaaaaaaa samahani kwafuraha nimeshindwa kuwajuza mwishoooooo!
Pipooooooooozi Powaaaaaaaaaaaaa!
 
Hizi hoja zilikuwa DHAIFU mno. Haihitaji kuwa na hata Kajicheti ka sheria kung'amua hilo. Sijui ni kwa nini Supreme court imekubali kudharauliwa kiasi hiki.
 
Chadema hongereni kwa kushinda KESI, hatahivyo tunatafakari ikiwezekana tutaenda Mahakama ya RUFAA, yule jaji hatujamuelewa kipengele cha laptop kwa nini hakikumweka Mnyika Kitanzini????
 
HONGERA MHESHIMIWA MNYIKA

Nami naungana na wapendwa wengine wanachama wa chadema na wapenzi wa chadema na Mnyika mwenyewe kumshukuru Mungu kwa ushindi alioruhusu uendelee kwake Mnyika.
Mungu ibariki chadema na Tanzania na mheshimiwa hakimu aliyetoa HUKUMU ya haki
Amina
 
Silaa amkana Lema hadharani adai kauli ya Lema ni ya kwake mwenyewe kuhusu anaodai vigogo wanaotaka kuhama CCM movie ya Kidosi bado inaendelea

Kama 'Inauma' muombe achomoe. Silaa ndio kitu gani gamba wewe?

Au unaweweseka baada ya mama yenu kuambiwa na jaji umbea wake apeleke saluni?
 
Tusaidiane kwa hili. Ni uhuru wa Mahakama au hofu ya CCM kurudia chaguzi ndogo hasa maeneo ambayo CHADEMA ina nguvu sana?
 
Back
Top Bottom