Mnyika ashinda kesi dhidi yake; Hawa Nghumbi atakiwa kulipa gharama za kesi!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Hali ya mambo ni nzuri watu hawana munkari kama ilivyotarajiwa hasa wale wa Chadema ndio wengi na wanaonyesha wana matumaini ya Ushindi,

Hukumui haijaanza kusomwa tunaelezwa itaanza mida ya saa 3 hivi,

Polisi kwa mida hii sio wengi sana kwa hesabu hawafiki 50. Kwa ujumla hali ni ya amani kabisa!

Tutawajuza hatua kwa hatua moja kwa moja toka ukumbini!

Updates:

- Basi aina ya coaster lililobeba mashabiki wa chadema ndio linaingia huku likishangiliwa na watu kwa alama ya vidole viwili alimaarufu Amani na Upendo!

- Naaaaam vijana wakazi (FFU) ndio wanaingia kwenye eneo la tukio wakiwa wamevalia kikazi yani kama Baghdad lakini wapo kwa usalama tu hakuna dalili ya vurugu yoyote hali ni yaamani tu!

- Kuna mabishano ya hapa na pale kati ya wananchi na wahudumu wa mahakama, watu wanalalamika kuwa mbona mda unakwenda na hawaruhusiwi kuingia mahakamani! Lakini wamefanikiwa kuwasihii na wananchi wametuliza munkali

- Tunaendelea kusubiri mda ufike tuanze kufuatilia kesi hii!

- Naaaaam tumeshaingia ukumbini tayari kuanza usikilizaji wa kesi hii uendelee! Tumeambiwa tuzime simu lakini MIMI sitazima mwanzo mwisho!

- Tunasubiri jaji aingie na jopo la mawakili wa pande zote wapo tayari!

UPDATES:
Kuna kichekesho kimejitokeza hapa, yani wakati wakuingia ukumbini kuna mbinu iliyotumika na mashabiki wa CDM kuwabana mlangoni wale wa Magamba na wakashindwa kupata siti kilichofuata ni afande kuwatoa nje, wakati wakitolewa nje kuna mwanachadema mashuhuri akaingia ukumbini na afande akataka kumuunganisha na wana ccm kutoka nje, unaambiwa ukumbi umelipuka na kusema huyo siti ipoo!

Naaaaaaaaaaam Mh Mnyika ndio anaingia ukumbini anashangiliwa kwa makofi na Pipooooooozi Pawaaaaaaaaaaaaaa!

Updates:
Wakili wa Mnyika ndugu Mbogolo ndio anaingia anasalimiana na mnyika waapiga picha wanaendelea kupiga picha!
Sasa kilichobaki ni kumsubiri jaji tu aingie ukumbini!

Updates:
Jambo la kufurahisha ktk kesi hii nikuwa Mh Mnyika na Hawa Ng'umbi wamekaa pamoja na wanapiga stori kweli, hata alipotokea afisa usalama akataka kuwatenganisha mnyika amemwambia haina tatizo watu pipoooooooooooz!

UPDATES:

M/Kiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe aka Sauti ya Zege ndio anaingia anashangiliwa ile mbaya pipooooooozi


UPDATES:
Mpaka dakika hii saa nne kamili bado Jaji haja ingia ukumbini, tunaendelea kumsubiri!

UPDATES:
Naaaam jaji ameingia na hukumu inaanza rasmi,

Jaji anaomba radhi kuwa ataisoma hukumu kwa lugha ya kitumwa! Twendeleeee!

Updates:
Jaji anaendelea na mapitio ya mwenendo wa kesi nzima tangu ilipoanza na mpaka ilipo, kimsingi ameanzia kwenye historia ya kampeni,uchaguzi, uhesabuji kura na utangazwaji wa mshindi, sasa anaingia kwenye malalamiko makuu ya mlalamikaji,

Vuteni subira naripoti kwa kificho maana tumeambiwa tuzime simu na kamera zote za wanahabari!

Mtanisamehe nitaripoti yale muhimu tu, longolongo za jiji sitaziripoti mda wa kutafsiri lugha ya kitumwa sina!
Jaji mwenyewe inamsumbua kusoma ana nasanasa tu wakati anaisoma kwenye karatasia utadhani kaambiwa aisome kichwani!

Bado anaendela kusoma mwenendo wa kesi! Hajaingia kwenye vifungu halisi vinavyosubiriwa!

UPDATES:
Naam Hoja ya kwanza ndio inaelekea ukingoni kuna dalili za jaji kuitupa nje! Pamoja sanaaaa!

HOJA zenyewe ni hizi:
1)Kwamba Mnyika alimtuhumu kuuza nyumba za UWT
2)Kutumia Laptop za Mnyika Kuhesabu kura
3)Kuingia watu wengi wa CHADEMA ktk chumba cha kuhesabia kura
4)Kuzidi kwa kura hewa 16,000
5)Kukosewa kwa karatasi za kujumulisha kura (form)


- Hoja ya kwanza imetupwaaaaaaa!

- Hoja pili inaendelea na kunadalili za kutupwa nje kwani jaji tayari keshasema hazikutumiwa ila lilikuwa kama ombi tu baada ya kuona za tume zipo slow! Bado anaendelea kufafanua juu ya hoja hiyo!

- Shtaka la 4 la laptop binafsi limetupwa mbali. Bado moja na la mwisho la Idadi kubwa ya watu kituo cha kuhesabia kura

UPDATES

Hoja zote tano zilizo wasilishwa mbele ya mahakama zimetupwa na jaji amemtangaza Ndugu Mnyika kuwa Mbunge halali wa Jimbo la Ubungo, na kumtaka mlalamikaji hawa Ng'umbi kulipa gharama zote za kesi hii!

Tumeshindaaaaaaaaaaaaaaa samahani kwafuraha nimeshindwa kuwajuza mwishoooooo!
Pipooooooooozi Powaaaaaaaaaaaaa!
 
Nashukuru upo eneo la tukio na umeanzisha uzi, uendelee kutujuza sisis tulio mashenzini ambao kwetu JF ni kila kitu.
 
UPENDO HILLARY MSUYA (Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania)



*Jaji No. 40 (J.40) kulingana na nafasi ya uteuzi wake (Seniority) kwa Majaji Mahakama Kuu ya Tanzania waliopo sasa (bila kumjumuisha Jaji Kiongozi FAKIHI ABDALLAH RHENO JUNDU)

*KANDA/Kituo cha Kazi: DAR ES SALAAM (Kama ilivyohakikiwa tarehe ya April 5, 2012. Kituo hiki cha kazi na pia namba ya Jaji huyu ki-mpangalio kwa uteuzi wake, vyaweza kubadilika pasipo sisi kuwa na taarifa. Tafadhali fanya uhakiki binafsi. Hatutawajibika kwa kutohakiki kwako huko katika jambo hilo na mengineo yaliyoandikwa humu)

*Maamuzi ya Mh. Jaji UPENDO MSUYA yanapatikana katika Mahakama Kuu ya Tanzania; Mahakama ya Rufaa ya Tanzania (hasa yanapokatiwa Rufaa hapo); machapisho ya Sheria, maktaba za wanasheria na pia katika blog ya Case Lawyer
 
Tunakutegemea Kamanda na hata hivyo usisahau picha angalau!

Kila la Kheri Chama makini kwa wanainchi wake!
 
Kwa nchi hii chochote chaweza kutokea hata kile ambacho macho ya binadamu hayawezi tegemea eti. Tunasubiri updates toka kwenu mlioko karibu.
 
Walishiriki dhambi ya kumzuia nakumpoka ushindi mwaka 2005 mungu akampa uvumilivu na subira. Akajenga sana hamasa kubwa kwa vijana kupenda siasa na kujitoa kugombea nafasi kubwa kama Ubunge, Vijana wakaanza kufikiria mageuzi na mapinduzi ya mifumo ndani na nje ya chama tawala. Mwaka 2010 wananchi kwa wingi wa ajabu na kwa kishindo wakampa ridhaa ya kuwatumikia na kuwa msemaji wao. Wanajaribu tena kumpoka ushindi kwa mamlaka zao walizo zitengeneza wao na wanadai ni Huru na Haki ila maamuzi wanayaingiliwa na kuwahadaa majaji. Mungu yu mwema atasimama na wengi atasimama na wenye haki ndani na nje ya Mahakama

Leo furaha ya Ushindi na mageuzi ya Kura itapatikana, Leo furaha ya Ushindi na mageuzi yaweza kuporwa ila hakika wakifanya hivyo watakuwa wanajenga hamasa na ushawishi mkubwa zaidi kwa watu kuunga mkono mageuzi.
 
Back
Top Bottom