MNEC ASAS Achangia Shilingi Milioni 15 Ujenzi wa Bweni la Chuo Kikuu cha Iringa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduz (MNEC) na Mfanyabiashara wa Makampuni ya ASAS, Salim Abri Asas amechangia zaidi ya Tsh. milioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la Wanafunzi wa Chuko Kikuu cha Iringa lenye uwezo wa kuchukua Wanafunzi zaidi ya 40 kama sehemu ya kuunga mkono shughuli za elimu katika Mkoa wa Iringa .

Akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi Salim Abri Asas, Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Iringa Asunta Nombo amesema Chuo hicho kinakabiliwa na changamoto ya malazi ikiwemo ukosefu wa mabweni ya kutosha “Chuo kinapokea Wanafunzi wengi na tayari ujenzi wa bweni umeanza na umaliziaji unagharimu zaidi ya Tsh. milioni 35 na bweni likikamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua Wanafunzi wengi”

Akiongea wakati wa sherehe hizo za ukaribisho wa Wanafunzi wapya waliojiunga na Chuo hicho katika kozi mbalimbali, Asas amesema Serikali kwa upande wake inafanya kazi kubwa katika Sekta ya Elimu jambo ambalo linatia moyo kwa Taasisi mbalimbali na Watu binafsi kuunga mkono juhudi hizo.

“Kwenye ujenzi wa bweni hili kwanza nitahakikisha litakamilika kwa viwango vizuri kwasababu najua bweni hili limepewa jina la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hivyo nitahakikisha linakamilika na hata kuanza kuweka vitu vinavyostahili ndani ya bweni hilo kama vitanda, viti, meza n.k hivyo nitahakikisha kwa kushirikiana jengo hilo litakamilika ili kusiwe na shida hii tena”

GDLZ8tyWIAAGbCb.jpg
GDLZ8tvWwAEBDYf.jpg
GDLZ8tpWUAAcHoR.jpg
WhatsApp Image 2024-01-07 at 14.12.56(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-07 at 14.12.57.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-07 at 14.18.51.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-07 at 14.18.52.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-07 at 14.18.53.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-07 at 14.18.53(1).jpeg
 
Anatafuta ubunge huyo na kwa huu utawala atazawadiwa tu

Akishakuwa mbunge iringa itaharibiwa km morogoro ilivyoharibiwa
 
#Don.
Ally Happy alikuwa anampiga hela sana huyu jamaa na baadhi ya wafanyabiashara wa Iringa, alikuwa anawaundia tu story eti JPM anahitaji kiasi kadhaa.

Kuna mmoja aliingizwa chaka eti JPM anahitaji mbao kadhaa, kumbe kajamaa kanapeleka kwenye ujenzi wake Dsm
 
Back
Top Bottom