Wana Nyanda za Juu Kusini Tutamlinda Salim Abri ASAS-MNEC Iringa

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
Utendajikazi, Upole, Ustamilivu, Subra, Busara, Huruma na Mapenzi ya MNEC Iringa Ndugu Salim Faraj Abri ASAS Kwa wanaIringa na Wana-Nyanda za Juu Kusini, Imekuwa ikijenga taswira njema ya Chama kwa Wananchi wote.

Tabia ya kujitoa, Kusaidia na kushika Mkono jamii ya Wana-Nyanda za Juu Kusini imeendelea kuwa sababu moja kuu ya Wananchi kuendelea kukiamini Chama.

Pamoja na mambo mengi mazuri ya kujitoa kwake Kwa jamii, Pia Mzee Salim Abri ASAS amekuwa faraja ya watu wanyonge na wananchi wenye uhitaji.

Wana-Iringa na Wana-Nyanda za Juu Kusini wanajivuna sana na uwekezaji wake anaojitoa nao katika sekta za Afya, Elimu, Miundombinu, Mitaji ya Wafanyabiashara wadogo(Machinga), Vijana na Kinamama, Lishe Mashuleni, Michezo na Matamasha ya Kijamii.

Hakika MNEC Iringa amekuwa nuru ya wananchi wa nyanda za Juu Kusini kwa Mikoa yote ya Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Songea kwani katika maeneo haya yote ameacha Alama ambayo imewapa tumaini Wananchi na Tabasamu.

Huyu ni mdau wa kweli wa maendeleo ya kimkoa, Kanda na Kitaifa.

Kwa kifupi, Mzee Salim Abri Faraj ASAS ni brand ya nyanda za Juu Kusini na Kiongozi wa Mfano kwa sasa.

Wananchi pamoja na wanaCCM tushtuke Kwa pamoja Kwa watu wasiojua faida ya mdau huyu Kwa jamii.

Kuna jambo ambalo uenda lisionekane kwa macho ya kawaida lakini ni lazima tujue kupitia michango mikubwa ya ASAS wapinzani na watu wenye nia ovu na serikali lazima waumie na wachunike mioyo yao kwa kuwa MNEC Iringa ametekeleza Kwa vitendo dhima ya Uongozi bora na wamfano.

Kupitia MNEC Chama kimezidi kuwa Imara na kuendeleza heshima kwani MNEC Iringa ameziishi vyema Ahadi za mwanachama wa CCM;
Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni Moja
" Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote ", " Nitajitokea nafsi yangu kuondoka umasikini, Ujinga, Magonjwa na Dhuluma ",
" Nitashirikiana na wenzangu wote kujijenga nchi yetu ",
" Nitakuwa mwanachama muaminifu wa CCM na Rais mwema wa Tanzania na Afrika "

Hakika MNEC anaziishi na kuzitendea haki AHADI za mwanachama Kwa VITENDO.

Tuwalinde Viongozi wenye Mfanano wa MNEC Iringa, Tuzuie maneno yasiyofaa Juu Yao na Tuwasaidie kuifikia jamii kubwa zaidi uwepo wao ni faida Kwa jamii.

Tunampa Kongole MNEC Iringa - Salim Faraj Abri ASAS kwa kuwawezesha Wananchi wa Nyanda za Juu Kusini katika nyanja za Afya, Elimu, Miundombinu, Uwezeshaji Kiuchumi, Michezo.

Tunaomba Mungu akulinde na Akutunze Kwa Faida kubwa ya Sasa na Badae.

*Kalamu ya Mzalendo
 
Mwanaume anasifiwa hivyo?
Badala ya kuwaambia vijana wawe na akili za kujituma ila umekazana kumsifia mwanaume aliepambana
 
f7ffb173a75407a3e4cbefb764c1eb5b.jpg
 
Back
Top Bottom