Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
Mada hii imeshajadiliwa na wenzetu kabla. Hata hivyo kutokana na umuhimu wake ni muhimu kuijadili katika vipembe vingine kuzidi kuifahamu
Microsoft wameshatangaza kuwa toleo la windows 10 liliopo sasa litafikia ukomo ifikapo oktoba 2025.Watumiaji wake wataachwa kujikongoja na toleo hilo na kupata muda wa kufanya mabadiliko kuhamia toleo jipya mpaka 2028.
Watakaoshindwa kufanya mabadiliko hayo ambayo yatakuwa ya gharama basi itapelekea mamia ya mamilioni ya kompyuta duniani kutokuwa na kazi tena.
Pamoja na kuwa uamuzi huo utaongeza tatizo na kuongezeka kwa plastic duniani ambazo haziozi lakini hilo litakuwa lazima kwa kampuni hiyo ya microsoft ili kufikia malengo yake ya ifikapo mwaka 2030 kuwa carbon negative.
Haya wataalamu wa mambo ya electronic na mawasiliano ya kimtandao tupeni elimu zaidi kutuepusha na hasara.