Mlioko serikalini msijione 'Special' sana. Mambo wakati mwingine hubadilika kwa kasi usiyoitarajia

Habari wana JF.

Kuna baadhi ya watumishi wa serikali, kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ngazi ya juu kabisa huwa wanajiona wao ni watu maalum sana.

Kama hujawahi kukutana na watu wa aina hiyo, basi nakuhakikishia iko siku utakutana nao. Wengi wao husahau ule usemi wa "cheo ni dhamana". Hao ndio wale ambao shida yako hata kama ilikuwa ni ya kutatuliwa kwa dakika moja (mfano kusaini document hakuhitaji muda mrefu), lakini utashangaa unaambiwa nenda utarudi kesho au mwezi ujao n.k.

Lengo la kuandika huu uzi ni kuwaasa watumishi wote wa serikalini kuanzia watendaji wa vijiji hadi kwa Rais, watambue kwamba wako pale kwa ajili ya kuwahudumia watu na siyo kuwanyanyasa au kuhudumia watu wa aina fulani kwa upendeleo. Na wanatakiwa wafanye hivyo huku wakijua kwamba wako wengi wenye uwezo kuliko wao, lakini hawakupata tu bahati ya kuwa pale walipo.

Naomba kuwasilisha.
Naunga mkono hoja
 
Leo kuna halmashauri fulani nienda kwa ajili ya kuomba documents fulani. Kwa nilicho kiona since naingia mpaka natoka zile office nilisikitija sana na kujisemea kua sisi wasomi hatulitendei haki taifa letu na huenda kwenda kufanya kazi halmashauri ndo mwanzo wa Kudumaza taaruma yako.
 
wanatakiwa wafanye hivyo huku wakijua kwamba wako wengi wenye uwezo kuliko wao, lakini hawakupata tu bahati ya kuwa pale walipo.
Mkuu hata hao wengine wakipata nafasi nao wanakuwa kama wao.
Malalamiko ya aina hii tunayo tangu zamani.
Watu wa ovyo wakistaafu wanaochukua nafasi zao wanakuwa na tabia zile zile.
Wafrika tuna roho za ovyo ambazo zinafanana.
Wasomi na maamuma wote wabinafsi.
 
Labda kijijini lakini mjini hakuna rangi hutoona. Halafu kuna vile umefika halmashauri una shida fulani wanaanza kukuzungusha mara nenda pale ukienda pale unaambiwa nenda kule ukienda kule unaambiwa rudi nyuma kidogo ingia kushoto ukiingia kushoto anakuambia nenda mbele kidogo ingia kulia mlango namba 2 ukiingia namba 2 unakutana na kidada kimechoka halafu sura ngumu halafu anachati. Ukimsalimia anaitika bila kuinua kichwa huku bado yuko kwenye simu. Unamueleza shida yako anakwambia muhusika hayupo na haijulikani atakuwepo lini na wewe umetoka mbali zaidi ya Km 100 na umetumia nauli kibao. Pumbav zenu!
Wapuuzi sana 🤣
 
Habari wana JF.

Kuna baadhi ya watumishi wa serikali, kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ngazi ya juu kabisa huwa wanajiona wao ni watu maalum sana.

Kama hujawahi kukutana na watu wa aina hiyo, basi
Unaweza kunitajia mtu yeyote ambaye hayuko serikalini?

Hata mfanyabiashara mdogoje :) , maadamu mfumo uleule ndio unampa kipato chake, basi kimsingi naye yupo serikalini.

Au nasema uongo ndugu zangu?

nakuhakikishia iko siku utakutana nao. Wengi wao husahau ule usemi wa "cheo ni dhamana". Hao ndio wale ambao shida yako hata kama ilikuwa ni ya kutatuliwa kwa dakika moja (mfano kusaini document hakuhitaji muda mrefu), lakini utashangaa unaambiwa nenda utarudi kesho au mwezi ujao n.k.

Lengo la kuandika huu uzi ni kuwaasa watumishi wote wa serikalini kuanzia watendaji wa vijiji hadi kwa Rais, watambue kwamba wako pale kwa ajili ya kuwahudumia watu na siyo kuwanyanyasa au kuhudumia watu wa aina fulani kwa upendeleo. Na wanatakiwa wafanye hivyo huku wakijua kwamba wako wengi wenye uwezo kuliko wao, lakini hawakupata tu bahati ya kuwa pale walipo.

Naomba kuwasilisha.
Umeandika point sana mkuu binafsi mi nimeshakutana na mtu wa namna hiyo yeye anafanyakazi mamlaka ya maji anaweza akapita nyumban kwangu akiwa na videm vyake utaskia ananichimbia bit eti ooh we umeshalipia maji, mara ooh nimetuma watu waje kukata maji kwenye nyumba yako

Sasa ukiangalia vitu vipo kwenye system sasa yeye anakuja kunihoji kijingakijinga

Mbaya zaid nyumban kwangu ndio imekuwa kama ofisin kwake

Utaskia nakusimamia hapa ili usiuze maji

Sasa jaman mtumishi wa namna hii ananitakia nini?

Kuna mpango nimemuandalia ili iwe fundisho kwa wafanyakazi wengine wangese kama huyu jamaa
 
Pole sana kwa chanamoto Mkuu..
Huyo wala hata haihitajiki kumpeleka kwa mjumbe. Siku akikuletea tena ujinga, mtandike makofi, halafu umripoti Polisi kwamba alikuja kufanya uvamizi. Maana anaingilia mambo yako yasiyomhusu kabisa!
 
Mkuu hata hao wengine wakipata nafasi nao wanakuwa kama wao.
Malalamiko ya aina hii tunayo tangu zamani.
Watu wa ovyo wakistaafu wanaochukua nafasi zao wanakuwa na tabia zile zile.
Wafrika tuna roho za ovyo ambazo zinafanana.
Wasomi na maamuma wote wabinafsi.
Ila kweli Mkuu
 
Back
Top Bottom