Mlioko kwenye ndoa naomba ushauri hasa wanawake: Nilifumaniwa na mtoto wangu wa kiume

Habari za jioni.
Mimi ni mama mtu mzima nina watoto 4 kwa mume wangu wa ndoa kabisa.

Niende kwenye mada.
Miaka 10 iliyopita nilifumaniwa na mtoto wangu wa kiume(my first born). Sikuamini kilichotokea nilishituka sana kwa hile
Kama umevumilia miaka yote hiyo Kumi na yeye mwanao ashafika umri wa kuwa na familia yake usisubutu kufungua mdomo wako kwa mumeo labda kama unataka kutubu na ndoa iishie hapo sawa ila kama unaitaka ndoa ww endelea kukakaa kimya na usitumie nguvu sana kuweka mambo sawa kwa mwanao ataoa mda si mrefu anaelewa kuwa kwenye ndoa huwa Kuna kipindi Cha tope vumbi na Kila aina ya rangi na ww utabakibna mumeo maisha yatasonga kosa lako lilikuwa kutumia nguvu mtoto akusamehe au muelewana tena huyo ndio mzuri hajawa mnafiki kwako wala kwa baba yake vinginevyo mngerekebisha na mzee angejua ndio ungekuwa balaa kwa wote ww na mwanao mwanao amekusadia kukaa mbali na maujinga Yako ww muheshimu kwa Hilo unavyotaka awe ni kuwa mwanaume mjinga mtoto wa kiume anayejitambua na anatajia kuwa baba kesho hawezi kumsaliti baba yake kijinga kwa makosa ya mama yake
 
Tubu kwa Mungu wako pekee,usiliseme hili kwa mchungaji au yeyote anaekufahamu.

Amua kubadilika kitabia,matendo yako,na chochote unachoona hakimpendezi Mungu,muombe akupe kibali Kwa mwanao kurudisha mapenzi kwako.

Ila yote yatawezekana kama ukiwa muaminifu na kukubali kubadilika na kuachana na makandokando yako.

Kwa MUNGU yote yanawezekana,ila kwetu binadamu utaishi kwenye maumivu zaidi kama ukilitoa nje. Naamini mpaka leo mwanao hajaliongea popote
 
Acha kumchuza mwenzako

Hapo cha kufanya tafuta watu wenye hekima au wa kanisani, mwaga ukweli kama ulivyomwaga hapo, wakae waongee na mumeo naye ajue. Usubirie kitakachotokea, mume akikubali kukusamehe basi mtamjumuisha na mtoto kwenye mapatano hayo, nadhani hii itasaidia kuliko kukaa nayo moyoni, huenda ukaibua makubwa zaidi
Hapo mtoto pia umeshamuatjiri kisaikolojia.
 
Habari za jioni.
Mimi ni mama mtu mzima nina watoto 4 kwa mume wangu wa ndoa kabisa.

Niende kwenye mada.
Miaka 10 iliyopita nilifumaniwa na mtoto wangu wa kiume(my first born). Sikuamini kilichotokea nilishituka sana kwa hile tukio lilotokea.

Mimi nafanya kazi kwenye wizara moja hivi nipo hapa dsm mpaka sasa. Miaka iliyopita niliingia mahusiano na Baba mmoja hivi anafanya kazi wizara nyingine tofauti na yetu nilikutananae kwenye kikao vya ofisini.
Mimi ni kawaida yangu kumcheat mume wangu, japo hajawahi kunitilia hofu kama nimewahi kumcheat maana mara nyingi navizia akiwa safarini ndo ninafanya hivyo. Maana ninajua kumcheta mwanaume ni hatari sana kwani wanaume wanawivu sana na hasira, kama mume wangu namfahamu ni mtu mwenye hasira sana , so nilijitahidi asijue kabisa.

Sasa kuna siku mimi nilienda kwenye duka langu maana kwenye duka langu kabla jioni ijafika lazima niwepo ndo nifunge na wafanyakazi waondoke pale. Sasa kipindi tunamaliza yule Baba alinipigia simu nikamwambia nipo sehemu falani , nikamuelekeza akafika na alipofika wafanya kazi wangu nao wakawa wanaondoka mda huo huo. Mimi nikamkaribisha mchepuka ndani , sasa kwenye duka **** ofisi kwa ndani si nikaenda nae mapaka kwenye ofisi katika kuongea kama 20 minutes, kwa sababu ni mchepuka tukajisahau akaanza kunishika na kuanza kukiss each other katika kunishikashika nikajisahau.

Kumbe mtoto wangu wa kwanza alikuja pale dukani aliingia baada ya kuona mlango wa flemu moja ujarudishiwa mpaka chini kabisa so akajua kuna mtu ndani.
Aliingia moja kwa moja mpaka ofisini kwenye ndani ya duka, na mlango wa ofisi sikufunga , nilishituka sana mpaka kumtuja (mmiliki wa vyote) ile siku nilitetemeka pale pale , isitoshe mapaja yangu yote yalikuwa nje , japo nashukuru hatukufika ile stage ya kusexy.
Nilitetemeka sana na moyo kwenda mbio kwani yule ni mtoto wangu wa kumzaa. Alituangalia afu akaondoka, mchepuko akaniulize yule ni nani nikamwambia mwanangu, yeye mwenyewe alishituka. Akanishahauri kuwa tulia tuu tuongee tuyamalize nikamwambia subiri niende home kwani namjua atakuwa anaenda home. Akili iliruka siku ile. Nikafunga duka.

Nilikimbilia nyumbani ili kumuwahi mtoto maana Baba yake alikuwa Bagamoyo anarudi kesho , nilifikili ataenda kupiga simu ya nyumbani na kumwambia mume wangu, nilipofika home nilimkuta hajafika bado nilimsubiri alilofika. Nilimuita nje nikaongea nae sana. Nikajua yameisha.
Kesho yake nikamwambia unataka nini nikununulie akasema hataki chochote .

Yule Baba akanipigia simu tukaongea sana akaniambia njoo uchukue pesa tumpe mtoto atajamaza tuu , yule Baba alinila 1,000,000 nimpe mtoto wangu niliasiseme nilimpa zile pesa nikajua yameisha.

Sasa kadri siku zinazidi kwenda mtoto wangu alikuwa aninichukia sana kuna kipindi alikuwa hata kunisalimia hataki kabisa. Nikimtuma hataki kabisa hata kwenda. Ila mimi niliewa kuwa ni lile tukio.
Kuna siku alinisikia namuita mume wangu kipenzi, kijana wangu si akasikia aliniangalia sana.
Mpaka mimi nikashituka, na nikajua yeye jinsi anavyo jisikia.

Kuna kipindi nililazwa hakuja hata kuniangali hospital.
Mara nyingi tukiwa pekeetu nakuwa nakaa nae naongea nae namwambia mimi ni mama yako naomba unisahame nimemkosea Baba yako, nimeacha sijarudia tena. Ila hanijibu chochote ananyamaza tuu. Najitahidi kumfanyia mambo mazuri ilimradi nirudishe mahusiano na mtoto wangu. Lakini inashidikana.
Kuna siku namwambia unapenda nikufanyia nini mwanangu hanasema tuu mimi nipo sawa mama.
Tangu lile tukio niliacha kucheat.

Ki ukweli ananichukia sana mimi mama yake uwa nakaa ne mara nyingi naongea nae ila inashindikiana.
Mwaka juzi nilimuona kuna rafiki yake anagari , na mimi nikasema ngoja nimnunulia kagari mtoto wangu , kwa vile mimi nimeajiriwa na nina mshahara mzuri, nilijikusanya na kuchukua pesa baadhi kwenye biashara zetu na mume wangu, mwaka jana mwezi wa 8 nikaenda mlimani pale nikanunua gari , nikamfanyia kama surprise hivi alisema tuu Asante akachukua ,
Ila nilishangaa aliendesha kama 2 weeks baadae alilirudisha nyumbani na kuweka funguo mezani ajariendesha mpaka leo, mume aliniuliza gari vipi nikazuga zuga tuu.
Nilishangaa sana nilimuuliza kuwa unajua mimi ni mama yako nimekosa ila kumbuka mimi ni mama yako. Yeye sasa anaumri wa miaka 26.

Sasa wiki 2 zilizopita mume wangu aliniambia kuwa ninaona wewe na first born hamna mahusiano mazuri nawafatilia mda mrefu sana sijajua shida ni nini. Nimeshituka sana kwani sitaki mume wangu hajue hii ishu japo ilitokea 10 years ago ila baada ya kujiambia hivyo niliishiwa nguvu kabisa. Juzi nilijaribu kumuuita mtoto wangu niongee nae lakini still bado anahasira nami.

SASA JAMANI Naomba msaada wenu kimawazo nideal vipi na hii kesi. Najua hawezi kumwambia Baba yake ila na mimi nikikaa kinywa , mume wangu atajua tuu **** something tunamficha maana hata juzi katoka kusema shida yenu ni nini nimemrukaruka tuu.
Mtoto wangu hataki kabisa kunisikiliza.

Nilitaka kushirikisha kiongozi wa dini mmoja ni mwanamke , tumuite ili tuongee nae ila naona haitakuwa siri tena inatavuja tuu.
Msaada wa mawazo . Nahitaji.
Chai
 
Hizi thread za kuwacheat waume zenu mkikamatwa mnakuja kulia lia humu mbona nyingi sana siku hizi? Ni kama mko proud na mnachokifanya sio?

Kiukweli pambaneni na hali zenu, binafsi sinaga ushauri kwenye mambo kama haya.
Bora nawe umenotice,. Wanatuletea trend uchwara tu hapa.
Wanafanya vijana wa watu waone wake wa siku hizi ni hamna kitu.

Kwa kweli wakomae na shida zao
 
Mimi nafanya kazi kwenye wizara moja hivi nipo hapa dsm mpaka sasa
Kuna haja gani we mama mtu mzima new member??
Mwambie mumeo mtoto anakuchukia sababu alikukuta unataka kuliwa dukani. Lol

Mama mtu mzima kwanini hujaja na Id yako ya zamani??
Kuna marioo gani hapa unamtega? 😂😂

Ukute uko na kende 2 hapo ila wajifanya wakike. Mweeh.
 
Back
Top Bottom