Mkutano wa CCM Jangwani: Nape anawatukana UAMSHO na kuwaita Wezi wakubwa na Majambazi...

Status
Not open for further replies.
nape hujui kama ni mkiristo? wakiristo wote ni lao moja. angalia hapa JF tu

Hii ni kauli ya CCM unaihusisha vipi na ukristo? pamoja na kuvunja na kuchoma makanisa na kuiba mali za makanisa huko Zanzibar uliwahi kusikia kiongozi yoyote wa kanisa akiwatukana Uamsho kwa kuwaita wezi au majambazi? Je Nape ni kiongozi wa kanisa? hapana sasa pambaneni na CCM na Nape acheni wakristu! Najua mnatafuta kwa dhati sana ugomvi na wakristu lakini hamtaupata maana sisi mungu wetu sio wa visasi wala jihad! Tumeamriwa tusamehe saba mara sabini na mtu akikupiga kofi kulia mgeuzie na kushoto!
 
miaka hamsini wameshindwa kugusa maisha ya mtanzania leo wanagusa, hiyo ni ndoto mkuu, CCM hawawezi tena na wala hawana nia ya kufanya hivyo, kama wewe una nia nzuri fanya haraka hamia CHADEMA mapema tukawakomboe watanzania, kama unaendelea na gamba lako subiria tukukomboe 2015
 
Mkutano wa CCM Jangwani: Nape anawatukana UAMSHO na kuwaita Wezi wakubwa na Majambazi..

Hayo maneno anayasema muda huu Jangwani LIVE ITV yaani kwa Ujumla kageuka Lusinde. Cha kujiuliza je Matusi ni sera ya CCM?

Mbona huyu Nape anaporomosha matusi jukwaani pale Jangwani Chadema Square.


Source: Live ITV.

Matusi/kebehi/kukosa busara ni jambo la kawaida sana kwa viongozi wa ccm wanayoiunda Serikali hii,,aibu aibu yao
 
wakati mwingine muwe mnaangalia content ya issue anayoiongelea na si kushika neno moja na kulikuza wakati maana nzima ya speech umeiacha.
yeye kazungumzia kama watuhumiwa wengine na hajawaita waislam majambazi
 
hoja hapa si uislamu au ukristo, acheni uvivu wa kufikiri, kila mtu ana dini yake au aweza kuwa mpagani, hoja yetu ni kwamba ccm wametufanyia nini zaidi ya kuhubiri amani na utulivu ambao haupo? ziko wapi rasilimali zetu, ziko wapiu huduma za afya, elimu bora, maji, barabara, uchumi endelevu n.k wako wapi walioba fedha benki kuu mchana kweupeee?
kama ningekuwa kiongozi wa ccm nisingeitisha mkutano jangwani leo, ningekuwa natenda zaidi kwa sababu dola wanayo, mikutano ningewaachia wapinzani ambao wanastrugle kuchukua dola, ningewajibu kwa vitendo, mawaziri wangekuwa vijijini wakisikiliza matatizo ya watu, lakini nyinyi magamba kweli sasa nimeuona mwisho wenu! you are gone!
 
Nape ametumia maneno yenye ncha kali yasiyo na staha kwa jamii ya watanzania kwa kutoa lugha ya kuudhi na kukashifu viongozi wa kundi la kidini la uamsho kwa kuwaita majambazi.

Viongozi wa uamsho ambao karibuni wote ni waislamu hawakuwa wakifanya ujambazi kama dhana ya ujambazi kwa maana na mapana yake inavyo weza kusadifu. Kitendo cha kuwaita viongozi wa kiimani majambazi ina maana hata mahubiri yao yalikuwa ya kijambazi, na kimantiki hata walio kuwa wanahudhuria walikuwa wanapata mapokeo ya kijambazi.

Huu ni uzalilisha na dharau kwa viongozi wa uamsho ambao ni waislamu na hivyo kuchafua taswira ya uislamu na wafuasi wake kwa kuwafuata na kuwasikiliza majambazi.

Natumaini viongozi wa uamsho hawata kaa kimya bali kumkanusha na kumtaka Nape afute kauli yake yenye kuwadhalilisha na kuudhalilisha uislamu. Lakini pia Nape awe muungwana kwa kuona kuwa ulimi uliteleza na kuwaomba radhi viongozi wa uamsho ambao kimsingi walifanya uamsho kwa kupata baraka na kibali cha serikali ya Zanzibar.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kwa hiyo kawaita waislamu majambazi......hilo timbwili mbona litakuwa kubwa balaa au anadhani watakaa kimya kama alinyo watukana wachaga...kazi unayo Nape.....................
 
Sauti ya Nape ni sauti ya kikwete..by Kikwete........kwa hiyo wakiandamana waende Ikulu maana magizo kapewa na Kikwete kuwa kaaambie waislamu ni majambazi
 
Kwa hiyo na serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa kuisajili uamsho nao ni majambazi kwa sababu walisajili kundi la majambazi.
 
ndugu yangu osokoni unanipa hasira sana, kwa sababu nape haliwakilishi kanisa anaiwakilisha ccm, je unasemaje kuhusu waislamu walioko ccm nao lao ni moja na hao wakristu wakina nape? je watoke waende chama gani TZ kisicho na wakristo? wewe ni mdini ila bado una nafasi ya kujirekebisha maana nia na dhamira yetu sasa ni kutafuta maendeleo huku tukiwa na amani yetu! fujo za zanzibar zinasababishwa na serikali kuzembea pamoja na intelligensia yao ambayo macho na masikio yako chadema tu!
 
CDM mnajisumbua bure,hata mpotoshe mambo lakini ukweli uko pale pale, waislamu wako upande wa CCM na wanajua wazi kuwa CCM peke yake isio na udini. Muislamu punguani tu ndio anaamini kuwa uamsho inamwakilisha.
 
Sauti ya Nape ni sauti ya kikwete..by Kikwete........kwa hiyo wakiandamana waende Ikulu maana magizo kapewa na Kikwete kuwa kaaambie waislamu ni majambazi
Nyie si mlisema JK mdini? Sasa imekuwaje atukane dini yake mwenyewe?
 
Mkuu majebere acha kupotosha!
Kiongozi wa dini yako akitoa matamko au mawaidha yanayo husu imani yako ya dini amekuwakilisha.
Hivi mfano leo Papa akisema mapadri ruksa kuoa utasema haja gusa imani yako na kanisa lako kuhusu ndoa?
 
nape hujui kama ni mkiristo? wakiristo wote ni lao moja. angalia hapa JF tu

hacha unafki, hakuna mkristo aliye furahia njia aliyo itumia nape,tulitegemea atoe tamko la kutafuta suruhu ya matatizo. Kwani hujui matusi ndio huwa matamko ya nyinyiemu? Si kila mkristo ana akili kama za nape, uliona mapadri wametumia lugha aliyo itumia nape.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom