Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Fuatilia yatakayojiri kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo Dkt. Salaa, Askofu Mwamakula pamoja na Mawakili Mwabukusi na Madeleka watakuwa wazungumzaji wakuu, leo Julai 12, 2023 saa 4:00 asubuhi.

Ni kuhusu suala la DP World.

IMG_7986.jpeg


===



===

MKUTANO UMEANZA

Askofu Mwamakula anazungumza
Juni 6, 2023 baada ya kusikia minong'ono ya mkataba kuwa na miaka 100, nilichukua jukumu la kuishairi serikali itoke kufafanua suala hili, baadae Bunge lilitoka kusema mkataba ungejadiliwa Bungeni.

Baadae Mkuu wa Mkoa wa DSM alitoa kauli kumuonya Dkt. Slaa, baadae Dkt. Nshala katishiwa maisha, baadae Wakili Mwabukisi naye katishiwa maisha.

_116993364_4683814a-dadb-447e-a3b7-50a9d5d522eb.jpg

Askofu Emmaus Mwamakula wa kanisa la Uamsho la Moravian
Tumeona pia jeshi la polisi limemuita Dkt. Nshala kumhoji kuhusu matamshi ya mkataba, tulidhani watamhoji ili awape ushirikiano kuhusu suala lake la kutishiwa maisha.

Mimi kama Askofu natoa tahadhari, mtanzania yeyote anayetoa maoni kuhusu mtakaba, kama akidhurika, akitekwa au kuuawa kwa namna yoyote viongozi waliotoa maoni ya kutisha pamoja na Serikali watawajibika. Mungu atawafedhehesha watu hao kuanzia aliyetoa wazo, anayepanga mkakati, anayetoa amri na ayetekeleza amri ya kuwadhuru watu wanaoongea, kulalamika na kudhurika kuhusu mkataba huu.

Kanisa linaangalia, lakini haliridhiki na yanayoendelea japo sio kila Askofu atasimama kama mimi kusema. Tuache kuteka na kufedhehesha watu wanaotoa maoni kuhusu jambo hili.

Wakili Peter Madeleka anazungumza
Mambo yanayoendelea nchini kwa sasa hasa hili suala la Mkataba wa DP World hayavumiliki. Hakuna mjomba wala shangazi kutoka nchi nyingine atakuja kutimiza wajibu huu (wa kulinda rasilimali).

20220421_064652.jpg

Wakili Peter Madeleka
Bunge la JMT lilikubali kuridhia ile nyaraka, kwa mujibu wa kilichofanyika Bungeni, ule ni Mkataba sio Makubaliano kama inavyosema. Bunge limepewa mamlaka ya kujadili mkataba, sio makubaliano.

Mtu akija kuwaambia kuwa ule sio mkataba bali ni makubaliano mkataeni mtu huyo bila kujali cheo au jinsia yake. Muongo ni muongo tu.

Kuthibitisha kuwa ni sheria, baada ya Bunge kuridhia, kinachofuata sasa ni Bunge kutunga sheria na ndio maana kwa kutambua hilo, Bunge la JMT limepokea muswada wa kubadili sheria mbalimbali zinazoleng kufanikisha utekelezaji wa mkataba huu.

Wanaotetea kuwa ni makubaliano waulizeni kwanza taaluma yao ni ipi? maana unaweza kuwa unabishana na mtu ambaye hana hata uelewa wowote kuhusu sheria.

Mtu asiye na elimu ni sawa sawa na mtu aliyekufa. Tupo hapa kuwapa elimu adhimu hasa ya mkataba huu unaohusu maslahi ya Taifa.

Sophia Mjema alitoa tarifa ya maazimio ya NEC iliyoongozwa na Rais Samia, na mojawapo ya maazimio ni kuipongeza Serikali ya JMT kwa kutekeleza vyema ilani ya CCM. Naiheshimu NEC lakini nayo imejidanganya, hakuna sehemu kwenye ilani yao walisema wataleta mwekeaji au kubinafsisha bandari kwa njia waliyoenda nao wao.

Mkataba huu ni mbovu, Rais Samia alimpa nguvu kisheria Waziri Mbarawa kusaini mkabata unaompa mamlaka kamili kwenye Nchi 2 za Dubai na Tanzania, inawezekanaje Rais Samia awe na nguvu ya kufanyia kazi masuala ya Dubai wakati yeye sio Rais wa huko?

Pia Dubai sio nchi, ni mojawapo ya sehemu za UAE, wameungana 7 kutengeneza nchi 1 kwa mujibu wa katiba ya UAE. Mfano ni Zanzibar, uliwahi kusikia wapi kuna balozi wa Zanzibar wanasaini mkataba kwa niaba ya Serikali ya JMT? Dubai haina uwezo kisheria wa kuingia mkataba wa kimataifa maana sio nchi, tumetapeliwa.

Mkataba huu hata ikitokea kitu gani kilicho nje ya uwezo wa Binadamu hauvunjiki, na suluhu yake inatafutwa kwenye mahakama ya Uingereza. Sheria ya Uingereza inatambua majanga ya asili mfano vita, njaa na mabalaa mengine ambayo ni ukuu wa Mwenyezi Mungu, lakini mkataba huu unasema hata ziwepo sababu hizo hauvunjiki. Mahakama za Uingereza itabidi zivunje sheria za mkataba huu.

Viongozi wetu sio malaika, ni watu kama sisi, wanakosea kama sisi. Hatuwasemi kwa nia mbaya, tunataka maoni haya yasikilizwe ili mambo yabadilishwe.

Rais Samia ajue kuna watu wanamfitini, CCM wenzie wanamsifia sana bila kumuonesha mapungufu yake ya kibinadamu. Watu hawa watamgeuka baadae, kama Rais uliyekuja kwa mapenzi ya Mungu tafakari makukusudi ya Mungu wewe kuwa Rais bila kupigiwa kura ni yapi?

Rekodi ya Samia itakayodumu milele ni kuleta katiba mpya na kufuta mkataba wa Dp World hata kama CCM wenzake watamchukia, na CCM sio wazazi wa Rais Samia.

Bunge linakwenda kubadili Sheria za Nchi maana tayari kuna muswada huo wa Ulinzi na usimamizi wa Rasilimali za Nchi. Sheria mama inakataza rasilimali za nchi kujadiliwa nje ya mipaka yetu, lakini muswada huu unaenda kuifuta, maana yake sasa kesi zote za rasilimali zetu zitajadiliwa kwenye Mahakama za nje. Kama muswada huu utapita, tutakwenda kuupinga Mahakamani.

Waziri Masauni ana mamlaka ya kisera huhusu vyombo chibi ya wizara hiyo, sio mambo ya kiutendaji. Masauni anathibitisha kuwa hafahamu majukumu yake kupitia kauli anazotoa, hajawahi kuwa mgambo au sungusungu. Kila idara ina wakuu wake na wapo trained kutekeleza makukumu yao (Mfano IGP), wao wanajua ni wakati gani wanapaswa kukamata watu.

Wakili Mwabukusi anazungumza
Watanzania tuna wajibu wa kikatiba wa kulinda rasilimali za nchi hii. Waziri Masauni na Nape waaxhe kutisha watu, nipo tayari kupambana nao kisheria. Huu mkataba ni wa kijambazi, hatutaruhusu aina hii ya mkataba kufanya kazi nchini.

Hakuna mwenye risasi ya kuua mawazo na dhamira zetu, kwa njia yoyote watakayoamua kutukabili, kila tendo ovu watakalopanga dhidi yetu litajibiwa kwa njia ileile, mimi sio mhaini, nitaripoti polisi (wameniita) na nimesoma katiba, kila anayesapoti mkabata huu ni mwizi.

F0aWT2HXsAE_-A9.jpg

Wakili Mwabukusi
Kuna watu wanasema kesi ipo mahakamani, kilichopo huko ni kutafsiri mkataba, huku mtaani tutaendelea kuwawajibisha waachie ngazi. Sisi tumekuja kwa kuungaunga hapa, hatujahongwa na mtu yeyote, kama yupo wamtaje.

Tangu nianze kusoma sheria, huu ni mkataba mbovu zaidi kuanzia mwanzo wake hadi ukurasa wa mwisho wa saini yake. Hata slow learner akiona atagundua tu.

Angalia Bungeni wanavyojichanganya, wanasema makubaliano, mara mkataba. Katiba inasema Bunge linajadili Mkataba sio makubaliano, njia rahisi ya kutuaibisha ilikuwa ni kutuita watusikilize na sio kukimbilia kupitisha.

Wameshaharibu, dhambi ni dhambi haina maana nyingine. Hii sio Tanzania waliyoizoea, tumechoka kudanganywa na kupuuzwa. Vitisho vyao vinatunyegesha tu (stimulate).

Watanzania sasa wanataka uongozi, Wazee mtuongoze kwa maneno na vitendo, sisi tutauwa mbele. Ikibidi kufa, tutaendelea kufia wizi huu. Tukiamua kuandamana itakuwa bila kikomo kama mkataba wenyewe ulivyo, Polisi tutawapa taarifa.

Hansadi za bunge zipo wazi, Bungeni kule walituambia mkataba huu wa Rais Samia. Tunapoitisha uwajibikaji hatuna malaika sehemu, tunataka na Rais naye ajipime. Serikali haiogozwi kwa imani, inaongozwa kwa katiba na sheria.

Tuna kazi moja ya kuzungumza lugha watawala watakayoelewa, lugha yenyewe ni nguvu ya Umma.

Mdude anazungumza
Tumeiajiri Serikali, ilikuwa na wajibu wa kutujibu bila kutisha. Level ya kutishwa ilishapita, Nape wa kututisha kweli?

_106898358_a0bb4379-9853-47dc-83a4-cd012e1c1f08.jpg

Mdude Nyagali
Mimi nawaaambia kwenye hili jambo, tumeanza maandalizi ya maandamano. Nitaongoza maandamano ya vijana nchi nzima na vijana kukataa huu mkataba.

Kwenye hili jambo hatutaka kimya. Serikali wakubali wametuuza maana hatuwezi kukubali kusikia kuwa walikuwa hawajui kilichomo ndani. Enzi za Nyerere waliosaini mkataba huu wangenyongwa.

Balozi Dkt. Slaa anazungumza
Dunia ya leo imebadilika, imetuonyesha jinsi mlivyoshindwa kuongoza nchi hii. Kwa kutumia psychology yangu ya miaka 7 seminarini, natambua saikolojia yangu na ndio maana siku nimetoa press yangu wote mlikuwa na heading moja, mlikubali maelekezi ya mabwana zenu. Wote mlitakiwa kufutwa kuwa waandishi, sisi tutawaambia watanzania waache kununua magazeto yenu, tutawaambuia kuna magazeti bandia.

Sisi hatupingi mkataba, tunapinga aina ya masharti ya mkataba na ndio hoja yangu niliyosema siku ya kwanza. Wanaosikiliza hata wale wa majaliwa na yule Msigwa asiye na akili (naweza kutoa uhahidi mahakamani kama ataenda) nataka wasikie.

H.E_Dr_Willibrod_Peter_Slaa.jpg

Dkt. Wilbroad Slaa, Balozi Mstaafu
Na Rais aache kuajiri machawa, wanatupandishia tozo, TBC mjitafakari pia mliwahi kunikatisha mawasilinano na Msigwa alikuwa anatoa maelezo wanikatie.

Hoja ya kwanza, namuomba Majaliwa rafiki yangu sana, na nampemda sana, ajitafakari na kujiuliza kwa kisomo chake kuwaambia hawa watanzania waendelee kuelimishwa (kuhusu mkatab) basi tutafakari aina ya elimu tuliyonayo. Asiendelee kupotosha watanzania kuhusu mkataba huu.

Bandari yetu ina gati 12, tumejenga wenyewe. Leo unatuambiaje kuwa mwekezaji ni lazima? Hatukatai wawekezaji, kama mnataka kubinafsisha kila kitu basi binafsisha Samia na Serikali, na magereza. Kaeni pembeni, wenye uwezo waingie.

Wamenitishia na mimi, na ubalozi wamesema watauchukua. Chukueni hata sasa hivi. Taifa likiwa kwenye msiba linakaa kujadili, Rais Samia kaliingiza Taifa kweye msiba kwa kujua au kutokujua.

Nchi hii Mungu kaibariki, watanzania hatukuomba kuzaliwa hapa. Hakuna nchi duniani ina Tanzanite, tulileta mwekezaji kule, Watanzania wakawa wanavuliwa hadi nguo mwanamme mzima unabaki na chupi. Hatuna shida na uwekezaji, isipokuwa mnavunja sheria za nchi. Serikali ni mwalimu wa kuvunja sheria, hakafu mnataka watanzania waheshimu sheria.

Mwadui karibia almasi yote inaisha, kuna mtu yeyote kanufaika? Miaka 40 iliyopita, Norway ilikuwa maskini kama Tanzania, Norway kagundua mafuta na gesi na kutumia maji ya mserereko, wakatengeneza umeme leo watu wote wanalipwa.

Waandishi piganieni haki nanyi mlipwe kwa haki, msiwakandamize watanzania mtapata laana.

Kubabidhi bandari ni mauaji, pita DSM mtaona kila nyumba ina geti. Katika Sheria hii inaruhusu DP World kusafirisha vitu vyake kutoka nje ya nchi, hivi ikitokea akaamua kupitisha silaha zikaenda kwa maadui, si watakuja hapa tupigane?

Kwa hatua ya sasa siamini kama Serikali pekee ndio ina haki ya kutoa elimu kwa watanzania, sasa sisi pia tunaanza kutoa elimu sahihi kwa watanzania ambao ndio wenye nchi.

Sauti ya Watanzania imechangia pesa za press hii na Julai 22, 2023, kupitia sauti ya Watanzania inayohusisha watanzania wa ndani na nje tutafanya mkutano mkubwa. Nyie mna tozo na kosi, sisi hatuna hayo yote ila tunachanga.

Sasa tunaaza kufuatilia vyombo vya habari vya nchi hii, kuna kamati inafuatilia, wale mnaoripoti kwa kuhongwa tutawashawishi watanzania kuwapuuza kwa njia yoyote.

Julai 22, 2023, kutakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara na maandalizi yanaendelea vizuri. Sehemu na muda vitatangawa, lakini uwezekano wa kwanza ni Zakhiem, tumesema mapema maana polisi huwa wanafanya hujuma tunapopeleka barua kuwa sehemu tayari imechukuliwa.

Tunaomba ushirikiano wa kila mmoja wetu katika kulinda maslahi ya nchi yetu.

===

MASWALI NA MAJIBU
Wakili Mwabukusi: Akijibu swali lililohoji kuwa haogopi kuitwa na Bungeni kujibu shutma za kulidharirisha amesema kuwa haogopi na yupo tayari kufika kwenye kamati hiyo. Pia yeye siyo mbunge, hana hofu yoyote

Kuhusu suala la Utanganyika na Uzanzibari, Mwabukusi amesema huo sio ubaguzi bali mkataba wenyewe ndio umetaja mambo hayo. Yeye ni mtanganyika kwanza kisha Tanzania, na Tanganyika ilibakwa na kama kungekuwa na maoni basi wengi wasingekubali muungano uwepo. Watanganyika wasifundishwe hofu.

Amesema atamfikisha mahakamani Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kutoa kauli mbaya za kumshambulia na watamjibu kwa kadri ya shambulizi lake ili iwe fundisho kwa wakuu wengine wa mkoa wenye tabia kama zake.

Askofu Mwamakula: Akijibu swali lililotaka kufahamu kama walioripoti kwake kutishiwa maisha walienda pia polisi amesema yeye amefanya kazi yake ya kiaskofu na amesisitiza kuwa mamlaka za nchi zinapaswa kujitenga na watu wasiojulikana ambao kama Serikali itakaa kimya, itaonekana wapo pamoja nao.

Dkt. Slaa: Akijibu swali la Mwandishi aliyetaka kujua kama tayari kaingia kwenye active politics baada ya kuondoka CHADEMA amesema waandishi wanapaswa kusoma katiba ili waache kuuliza maswali mepesi na kujiaibisha kama haya maana yeye ni raia wa nchi hii na anao wajibu wa kuzungumza.

Amedokeza pia kuwa suala la katiba mpya ni sasa, yanayofanyika sasa wala sio kesho, yanayofanika sasa ni mchezo na haihitaji kibali cha Rais. Rais anaajiriwa na watu na lazima awasikilize.
 
Wacha ukweli uendelee kuwafikia watanganyika, Samia lazima atambue yeye ni mtumishi wetu, sio bosi wetu nasi watumwa wake hivyo kujiona anaweza kutupeleka atakavyo, hilo halipo.

Samia ni mjinga naamini kabisa hakusoma ule mkataba, naamini hivyo kwasababu tabia yake ya kuwaagiza watendaji wake "na hili mkalitazame" ndio imetufikisha hapa, au pia aliusoma, lakini kwa upeo wake wa kuunga unga akaona ule mkataba wa hovyo hauna shida, taifa limepata hasara.

"Tukiamua kuandamana, itakuwa bila kikomo kama mkataba wenyewe ulivyo" -Adv. Mwabukusi, nampa cheo cha Rais wa Tanganyika, kuanzia sasa.
 
Fuatilia yatakayojiri kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo Dr. Salaa, Askofu Mwamakula pamoja na Mawakili Mwambukusi na Madeleka watakuwa wazungumzaji wakuu, leo Julai 12, 2023 saa 4:00 asubuhi.

Ni kuhusu suala la DP World.

View attachment 2685517
Ni vyema wasiwe na maneno mengi sana ya kusema leo hii kwani maneno mengi kuhusu suala hili tayari yamesemwa na wasemaji mbalimbali. Kinachotakiwa ni wao kutoa "mwelekeo mzuri" wa kuweza kuhitimisha jambo hili kwa vitendo ili Jambo hili sasa lifike kikomo na Watanganyika kuweza kupata nafasi ya kufanya mambo mengine ya maendeleo.
 
Ni vyema wasiwe na maneno mengi sana ya kusema leo hii kwani maneno mengi kuhusu suala hili tayari yamesemwa na wasemaji mbalimbali. Kinachotakiwa ni wao kutoa "mwelekeo mzuri" wa kuweza kuhitimisha jambo hili kwa vitendo ili Jambo hili sasa lifike kikomo na Watanganyika kuweza kupata nafasi ya kufanya mambo mengine ya maendeleo.
Jambo hili halifiki mwisho mpaka waliolianzisha walirudishe walikolitoa lianze upya. Warekebishe mapungufu yote ndo Watanganyika tutaridhika. Vinginevyo HATUDANGANYIKI safari hii. Si umeona wameanza kujichekesha na machakato wa Tume huru? Waendelee nayo lakini bandari zetu tunazitaka.
 
Ni vyema wasiwe na maneno mengi sana ya kusema leo hii kwani maneno mengi kuhusu suala hili tayari yamesemwa na wasemaji mbalimbali. Kinachotakiwa ni wao kutoa "mwelekeo mzuri" wa kuweza kuhitimisha jambo hili kwa vitendo ili Jambo hili sasa lifike kikomo na Watanganyika kuweza kupata nafasi ya kufanya mambo mengine ya maendeleo.
Nyinyi endeleeni kuwasikiliza tu wenzenu wanalipwa na makampuni yanayowatuma yanayoelekea kupoteza ulaji bandarini nyinyi mmebaki kukesha mitandaoni kuwasikiliza badala ya kwenda mashambani na kwenye shughuli zitazokuingizieni kipato na familia zenu.
 
Back
Top Bottom