Kwako Lusinde na Kenani; Dkt. Bashiru aliwahi kusema maneno haya akiwa Katibu Mkuu wa CCM. Je, hamkumuelewa enzi zile?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
KWAKO MH LUSINDE NA MH KENANI;DK BASHIRU ALIWAHI KUSEMA MANENO HAYA AKIWA KATIBU MKUU WA CCM,JE HAMKUMUELEWA ENZI ZILE!?

Leo 17:50hrs 20/11/2022

1. "Nimekuta wizi wa kutisha kwenye chama chetu cha CCM na wengine nikiwataja hamtanielewa. Wanajifanya ni waheshimiwa kumbe ni wezi,mijizi,wameiba magari, wameiba ardhi. Ukiwaskia nje wanabwatuka unawezakudhani ni wazalendo kumbe ni mijizi na kwenye vikao mkikaa hata kabla hamjafikia maamuzi, mijizi hiyo inatoka nje".

2. "Mijadala ndio namna ya kuendeleza nchi yetu, mijadala ndiyo inatufanya tujisahihishe. Hatuwezi kusonga mbele bila mijadala. Tumekosea sana katika nchi yetu, tumepotea sana katika nchi yetu. Mbaya zaidi tumeanza kuogopa kusema ukweli, lazma tubadilike".

3. "Tuambizane ukweli; kuanzia sasa CCM haitachukua tena wanamuziki kwaajili ya kampeni za chaguzi. Hivi wananchi mkiishapewa kofia na fulana halafu nyimbo za "mbele kwa mbele" zikapigwa, huwa mnapata nafasi ya kuhoji sifa za mnayetaka kumchagua? Wanamuziki wanakichaji chama fedha nyingi na wanafaidika wao na matumbo yao. Hivyo, kuanzia sasa hakuna tena kitu kama hicho";

4. "Wapigakura wajanja wameanza tabia ya kudharau chaguzi. Wanabaki nyumbani kwani wanaona chaguzi ni kituko, ni mchezo wa kuigiza. Ndio maana leo kupata watu wa kwenda kupiga kura imekuwa shida. Note CCM tunakoshinda ni chini ya 30%, chini ya 40% . hakuna mahali ambako wapigakura wamejitokeza kwa 50%. na mwaka 2010 ulitia fora. Watu wengi walijiandikisha kumbe walikuwa wanataka kile kiparata (kitambulisho cha mpigakura) kwasababu huwa kinatumika polisi kumwekea mtu dhamana. Wakiishakipata wanaingia mitini. Kwa mara ya kwanza katika historia nchini, mwaka 2010 tukapata serikali ambayo haina uhalali wa kisiasa kwasababu 50% ya wapigakura walibaki nyumbani".

5. "Msimu wa uchaguzi umekuwa msimu wa rushwa. Imefika mahali wagombea wanauza adi nyumba. Wengine wanaomba sana michango. Usipomchangia anakuwa mkali na kununua uso utadhani anakwenda kutibiwa,akiishazikusanya fedha anakwenda kuwanunua mawakala, nao wanawanunua wananchi. Wananchi mnachotakiwa kufanya ni kubomoa soko la kura".

6. "Napenda kuwafahamisha kwamba Hussein Bashe sio mkorofi bali ni miongoni mwa wabunge wa CCM wadadisi,kuna tofauti kubwa kati ya mdadisi na mkorofi,Bashe na Nape Nnauye ni miongoni mwa wanachama wetu wadadisi na wanasaidia kulichangamsha bunge ila wanatofautiana katika udadisi wao. Nape kidogo ana joto zaidi kuliko Bashe. Wote nawafahamu vizuri hivyo msidanganywe kuwa Nape na Bashe ni watukutu. Sio watukutu, ni wadadisi na wamewezesha mawaziri kufikiri kabla ya kutenda. Kutenda kila mmoja anawezakutenda, hata mwendawazimu anaweza kutenda lakini ili uweze kutenda kwa ufanisi na tija lazma ufikiri. Michango ya Bashe bungeni inafikirisha".

7. "Mimi ninachosisitiza ni nidhamu na si kunyamazisha watu. Tutapata wapi fikra mpya bila kuhojiana, bila kujadiliana na bila kudadisi? Tusipofanya hivyo, Chama Chetu cha Mapinduzi kitakuwa chama mfu".

8. "Nilikuwa Morogoro na akatajwa Waziri kuwa anamiliki hekari 1000. Watu wanatakakujua amezipataje na mi ntamwita waziri huyo nimuulize kusudi nikawajibu walioniuliza. Hatuwezi kuwa na viongozi ndani ya chama kinachojitambulisha kama chama cha wanyonge halafu baadhi yetu tunapora ardhi ya wanyonge. Ni suala la kuchagua kati ya kuwa Kiongozi wa CCM au kuwa Mporaji wa ardhi".

9. "Na hii habari ya "Dar Es Salaam ya Makonda" sio sahihi. Hakuna "Dar es Salaam ya Makonda" ni "Dar we Salaam chini ya Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Makonda". Kuna wakati huwa namsikia Makonda akasema "Wananchi wangu", nani kamwambia ana wananchi wake? Hakuna wananchi wako,hakuna kiongozi anamiliki wananchi, ni "wananchi wenzangu". Mwalimu Nyerere aliwahi kuonya juu ya ubinafsi .."mkianza kusema- mimi, wewe, sisi au wao hamfiki". Vongozi vijana mnapaswa kuwa wanyenyekevu na kuacha papara. Vinginevyo mtapotea kama walivyopotea viongozi wengine vijana waliopewa madaraka wakakosa unyenyekevu" .

10. "Nawashukuru sana watanzania. Nawashukuru watanzania kwa kunisomesha kwa kodi zao na hatimaye nikaweza kupata shahada zote tatu, kamwe sitawasahau watanzania,nina deni kubwa la kulipa utumishi uliotukuka. Kazi niliyopewa ya kuwa Mtendaji Mkuu katika chama ni kubwa mno".

Kwa hakika, nukuu hizi kuntu zinamtanabaisha Mh Daktari Bashiru alikuwa ni mwanadamu wa aina gani,na alidhamiria kuifanya CCM iwe chama cha aina gani,"Nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko" tulifundishwa hivyo na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

-Hofu yenu iko hapa.

Mnasema huenda he is ready for the worse !! Come what may ! Che guevara alisema “ its better to die standing than to live kneeling “. !!

Shida nyingine ndani ya chama,Vigogo ndani ya chama wanajua kabla haujaanzisha vita na kamati kuu ya chama,hakikisha kwanza una back-up ya kutosha kupitia wenyeviti wa mikoa na wilaya,ukiisha kusanya hiyo support ndio twende sasa na ‘twanga, nikutwange’ mpaka ndani ya vikao vya ndani,mifano ni minyukano ya Chama tola ile dhana ya kuvua gamba hadi uchaguzi wa 2015.

Niseme tu kama mwanazuoni,maneno ya Daktari Bashiru ni Phd in delivery,Daktari Bashiru ni freemind, hategemei hisani kama ninyi, ndio maana pamoja na kupewa ukatibu mkuu wa CCM na Rais Magufuli ila bado alikuwa anaongea maneno yenye ukakasi mno dhidi ya CCM na Rais Magufuli aliyachukua hayo kama feedback na kuyatafutia solution.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.

-Bachelor of Business Administration in International Business

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Niseme tu kama mwanazuoni,maneno ya Daktari Bashiru ni Phd in delivery,Daktari Bashiru ni freemind, hategemei hisani kama ninyi, ndio maana pamoja na kupewa ukatibu mkuu wa CCM na Rais Magufuli ila bado alikuwa anaongea maneno yenye ukakasi mno dhidi ya CCM na Rais Magufuli aliyachukua hayo kama feedback na kuyatafutia solution.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Kama Mungu asingemuita kwake, 2025 ilikwa ni Dr. Bashiru!. Pascal Mayalla amchambua Dkt. Bashiru, adai aliandaliwa kuwa Rais 2025

Unaweza kuusikiliza uchambuzi huu kutoka DW
P
 
Mungu Bado ana watu wake ndani ya Taifa hili.
Ni ukweli usiopingika kama Hawatakuwepo watu aina ya Dr. Bashiru, Tundu Lisu, Mnyika ,Dr. Slaa, Polepole, Jaji Warioba, God bless Lema, Mch. Msigwa , Antony Mtaka, Askofu Bagonza,Askofu Shoo, Askofu Mwamakula, Mpina n.k. basi nchi hii itakua Mali ya Shetani kama zilivyo nchi nyingi za Ulaya ya Leo yenye kizazi kilichopotoka na Sasa Ulaya inaporomoka na kuondoka kwenye ushawishi wake kidunia. Tanzania inakwenda kuwa na watu wa hovyo na watawala watakua ni mapandikizi ya Wala rushwa ,mashoga, wauza madawa ya kulevya, wafanyabiashara walaghai wa kitaifa na kimataifa, nchi yenye vifo vingi vya magonjwa ya kutengeneza, wawekezaji wezi wanaokuja na makaratasi wanaondoka na mabilioni ya Dola ,wasagaji, watoto wahovyo wasio na maadili,nchi isiyojali maadili ya kifamilia na kiutumishi.

Watanzania tukidhani hii nchi ni ya mtu mmoja na wale anaowapenda na kuwapa madaraka tutakua wendawazimu na Leo wameanza kutangazia Dunia kuwa watanzania wengi wengi ni wagonjwa wa akili. Maana yake ni kwamba Kuna siku watakua wanawakamata watu na kuwafunga pingu za miguuni na mikanoni na kutangazia ulimwengu kuwa huyu ni kichaa tunampeleka Mirembe.

Wameshiba na watoto wao lakini Bado wanatuchagulia viongozi waovu na wabaya wasiofaa ,wezi na wahuni Kwa sababu wametudharau bila kujua kuwa dharau zao ni Kwa sababu ya maskini na sio utajiri wao. Ndio,ni Kwa sababu ya watoto wa maskini wanaowalinda huku wao na watoto wao wakistarehe na kuwatukana na kusema kuwa wanakula kutokana na urefu wa kamba zao.

Ipo siku watoto wa maskini watajua kuwa hawana kesho ya watoto na wajukuu zao kama wataendelea kuwalinda wezi na wahuni.

Dr.Bashiru ni Sauti ya wanyonge ole wake mtu atakayepingana na sauti ya Wanyonge.
Wakulima Mmesahau kuwa Hawa wanaowaletea Mbolea wameshapiga dili zao kwenye miamala na Mbolea ni geresha ndio maana hata Mungu amewanyima mvua? Hiyo Mbolea labda muweke kwenye pesa za Mikopo labda zitaota na kuzaa Dola. Mvua ni Chache sana. Na wale mliowekeza kwenye kilimo Cha umwagiliaji Sasa ndio mmeambiwa marufuku kutumia maji ; mana wameshindwa kutafuta vyanzo vya maji Kwa ajili ya maji ya kunywa Dar es Salaam Jiji linalokaribiana na mito mikubwa kama Ruvu, Wami, na Rufiji, Mito inayohitaji tu uzalendo kuongeza uzalishaji na sio mvua.
Ukiwauliza mbona maji kwenye Mito hiyo Bado yanaingia Baharini hawana majibu zaidi ya kukaa ofisini na kalamu na kuandika dodoso za vikao na kulipana posho na Sasa Wanakwenda Tanga kucheza michezo ya kuvuta kamba na kukimbiza Kuku Kwa pesa za Mikopo Toka Oman , Falme za Kiarabu na Kwa Wale watetezi wa ndoa za jinsia Moja na nyingine zisiyo na Ziwa kubwa kama Ziwa Victoria Wala ardhi kubwa kama tuliyonayo lakini Wana uzalendo TU na akili zao wamezitumia vizuri kuliko wanyama.

Shame on you .Mmebaki kumshambulia Dr.Bashiru ; mnataka awalambe nyayo zenu zilizokanyaga jasho la wanyonge.
 
Kama Mungu asingemuita kwake, 2025 ilikwa ni Dr. Bashiru!.
P
Hii nchi ngumu saana, kwa kipindi alichokuwa katibu mkuu wa CCM, Kuna hatua zozote aliwachukulia hao watu aliowaita majizi?

Au aliishia kutoa speech tu na biashara ikaendelea kama kawaida, lakini tukiweka takwimu sawasawa huyu aliwahi kusema huwezi kuwa na dola halafu ukashindwa uchaguzi, lakini saizi kwa sababu amezungumza maneno ya kukosoa Serikali iliyopo madarakani na kwa kuwa yeye hayupo anaonekana shujaa.

Huyu ndiye yule aliyesema Hataki cheo kingine ukatibu mkuu wa Chama ndio cheo chake cha mwisho, hata kubali hata ateuliwe cheo kingine, lakini leo ni mbunge viti Maalum.
 
Huyu nduli mnafiki ndio alikuwa Engineer wa wizi wa kura mkubwa kuwahi kutokea Tanzania uliofanywa na CCM, waliiba viti vyote vya ubunge wa upinzani na kuwabambikia kesi na wengine kufungwa bila sababu, yote chini ya huyu mwehu, sasa hana sponsor wenzake wamemgeuka mirija ya vyeo na pesa imekatwa hana tofauti na wahuni kama Sabaya na Makonda, roho mbaya inalipa
 
Back
Top Bottom