Mkurugenzi Mkuu Tanesco Ajiuzulu

Mlm Nyerere nae asisahaulike ktk hili yeye nae anabeba lawama ktk maozo yote haya yanayoikumba nchi yetu leo, ingawaje hatupo nae tena.

Miaka 20 na ushee imepita yaani wewe bado unamlaumu Mwalimu? Yaani marais wote waliokuja na wabunge watunga sheria wote hadi awamu hii hawawezi kubadili hizo sheria kisa mwalimu. Absolutely stupid.
 
So Solution Board nayo iende lakini Muungwana hawezi kubeba haya matatizo yote kwa wakati moja, kuvunja baraza la mawaziri, Report ya BOT etc, CCM na matatizo yake, the hili la TANESCO.
Lakini kwa kweli Huyu Balozi naye tunafaa tumchunguze ndio hao hao wazee wa siku nyingi, na ni ndio hao hao ktk madili mengi kwenye Vitu vingi hapo Bongo. So inacho cheza hapo ni siasa na kulindana.
The key thing ni ku-review hiyo mikataba ilio shindikana, ya IPTL, Richmonduli, and the like.
Then kuweka Wataalamu hapo kwenye Board na kwenye Utendaji, especially Chairperson, na mkurugenzi.
Kama aliyekuwa VC Luhanga na wengineo ambao si wafahamu, but the system knows them.
 
Namshukuru Fundi Mchundo ameeleza vizuri. Sikuwa na mpango wa kujibu post yoyote leo, lakini nimefurahishwa na mchango wa fundi huyu. Kazi ya kwanza ya wanasiasa ni kutetea wananchi. Nchi zote zilizokuwa zimetawaliwa zimepata uhuru kutokana na mchango mkubwa wa wanasiasa, ki-uongozi na uhamasishaji. Na hata matatizo mengi hutatuliwa vyema wanasiasa wanaposhiriki kikamilifu (hii tunaita political will). Angalia maswala yanayohusu afya, mazingira nk, wanasiasa wanapoingia katika kushughulikia matatizo hayo, mabadiliko makubwa mazuri hutokea. Kampeni za chanjo na upandaji miti zimeleta manufaa makubwa sehemu nyingi duniani baada ya wanasiasa kuzibeba kama political agenda. Si lazima mwanasiasa aelewe taaluma inayohusika katika kuleta ukombozi, yeye anapaswa kuzingatia matashi ya ummat wake. Kwa hiyo mwanasiasa yeye anawa-challenge wataalamu walete maendeleo bila kuumiza wananchi unnecessarily. Ukitaka ku-fit kwenye madaraka hayo, lazima uwe versatile, usinganganie tu elimu yako ya darasani. CCM wametuahidi maisha bora kwa kila mtanzania. Huo ndio unaopaswa kuwa msimamo wa wanasiasa wa CCM. Sasa wataalamu wanaoajiriwa chini ya vision hii wanapaswa kuona hiyo ndio changamoto iliyo mbele yao, kutupatia maisha bora (ikiwamo umeme wa uhakika). Umeme sasa ni political agenda, lazima wanasiasa wasimamie hili. Na mtaalamu anapaswa kuichukua hii katika muktadha wa taaluma yake, kutatua changamoto iliyopo kwa kutumia rasilmali zilizopo. Ndiyo matumizi ya akili hayo. Fanya ujualo tupate umeme kwa wananchi kwa bei nafuu, ndio changamoto iliyo mbele ya TANESCO. Kama wanashindwa waondoke. Na huwezi kutenga siasa kwenye masuala yanayohusu wananchi wengi, tena maskini. Hivi wanasiasa wasipowatetea wananchi hawa, nani atawatetea? Hizo nadharia za uchumi wa kitabuni hatuzihitaji hapa, hazitusaidii kitu. Tunataka umeme kwa bei nafuu, huliwezi hilo, ONDOKA, basi. Elimu ya kukariri na kupata cheti haina maana yoyote, yenye maana ni ile ambayo unaweza kuitumia katika mazingira uliyopo kutatua matatizo at that level. Umesoma sana, tunakuheshimu, lakini kama huwezi kutumia elimu hiyo kutanzua changamoto zinazotukabili, basi pisha mwingine. Kabisa! Na wengine wa namna hiyo huko TANESCO na kwingineko kama bado wapo jamani nao wajiondoe, basi!
 
Domokaya,

Naona sasa utaamini kuwa JF ni MBELE KWA MBELE:

“Dk. Rashid alisema shirika haliwezi kuendeshwa kwa kuwavumilia watu au viwanda vinavyotumia umeme bila kulipa, akaona kama hilo nalo haliwezekani, bora ajiuzulu,” kilisema chanzo chetu. Kwa uamuzi huo, kuna habari kwamba jana jioni umeme ulirejeshwa katika kiwanda hicho, hatua inayoashiria kwamba ilikuwa ni pigo na kiashirio cha kwamba mapendekezo yake yalikuwa hayakubaliki kwenye bodi."

Ndio maana nilikwambia AMINI NDUGU YANGU TUNATOA KWANZA MAGAZETI YANAFUATIA

Nimeamini ndugu yangu.
 
Kitila,

Mimi ni mmojawapo wa wanaoamini kuwa MAWAZIRI hawatakiwi wawe wanasiasa.

Ninaamini kama tungekuwa na waziri wa fedha mwenye taaluma hiyo (uchumi/fedha) hazina isingekuwa tupu.

Utazungumzia washauri, YES, but u need to think! Angalia Dr Feki Nagu anavyobwabwaja hovyo kwa kutofahamu anachokiongoza!

Tukubaliane kutokubaliana.

Sawa; but why should we think kwamba kila mtu mwenye akili nzuri inabidi awe mwanasiasa. Yaani kuwa waziri ndiyo siasa yenyewe hiyo mzee whether umeingia through bunge au otherwise. Ministers all over the world are politicians! Anyway, ngoja tukubaliane kutokubalina kama ulivyosema.
 
No matter what are the reasons behind Dr Rashid's resignation,amefanya kile ambacho viongozi wetu wengi wameshindwa kukifanya.I salute his bravery!!!!

Kina Mbilinyi si walijiuzulu? au umekusudia ndani ya Tanesco, angalia kwa kuweka hadidu rejea sawa:confused:
 
Mlm Nyerere nae asisahaulike ktk hili yeye nae anabeba lawama ktk maozo yote haya yanayoikumba nchi yetu leo, ingawaje hatupo nae tena.

Kijakazi una personal grudge na Mwalimu au?
Yeye aliweka foundation, sasa ni juu yetu kuweka ukuta na Paa, wengine watakuja ongezea vitu vingine na kama ku-polish au kungarisha na nakshi mbali mbali, sio kuubomoa hata huo msingi alio weka.
It tantamount na Mzee wako akupeleke shule halafu unataka ukufanyi na mtihani.
 
Mfwatiliaji, naona unataka kuniumbua! Basi nitajiumbua. Mimi sikubold. Nilichukua jumla jumla bila kuangalia wapi pamekuwa bolded. Nilisoma zamani na hivi vitu vyenu vinanipa matatizo. Naomba mnivumilie tu.
Logic ya huyu Dr. ndiyo inanisumbua. Kwani ni Tanga cement peke yao ndio hawalipi umeme? Na wamekuwa hawalipi kwa muda gani? Hatua gani za awali zilichukuliwa katika kukabiliana na hali hii?Mimi naona vigumu kuamini kuwa shirika kama hili wanaweza kufanya hayo wanayodaiwa kuyafanya bila sababu za msingi. Athari kwa credibility yao hapo watakapogundulika ni kubwa mno. Ninavyoelewa (naomba mnisahihishe kama nimekosea) ni kuwa walikuwa na dispute kuhusu sehemu ya madai. Na yeyote aliyewahi kudeal na Tanesco ( na zamani TTCL nao) hili si jambo la kushangaa. Sasa kwaida ya vyombo vyetu ni kusema,lipa kwanza, tujadiliana baadae. Kitu ambacho si haki. Ndiyo maana nahisi kwamba kuna mengi ambayo hayajaongewa katika hii saga. Kilichopo ni spinning tuu. Kama alitempa na mita kwa sababu za kutaka kukwepa kulipa, ningemtoza faini (kama sheria inaruhusu hilo) na kumpeleka mahakamani kama akizidi kukaidi. Hatua ya kukata umeme na kuweka seal ingekuwa ya mwisho. Ningefanya hivyohivyo kama jambo kama hili lingetokea kwenye hospitali ya Muhimbili. Kuna sehemu inabidi kuangalia the big picture kabla ya kuchukua hatua yoyote.
 
The key thing ni ku-review hiyo mikataba ilio shindikana, ya IPTL, Richmonduli, and the like.
Then kuweka Wataalamu hapo kwenye Board na kwenye Utendaji, especially Chairperson, na mkurugenzi.
Kama aliyekuwa VC Luhanga na wengineo ambao si wafahamu, but the system knows them.

Hapa kupata solution ni ni kama ulivyopendekeza ila nasikia huyu jamaa alikuwa ameonyesha kuleta mwamko ndani ya TANESCO.

Pili nafikiri mirija iliyowekwa Tanesco ni mzigo mzito kwa mtu yeyote ambaye atakuwa Managing Director. Huwezi kufanya kazi nzito halafu unawalipa wengine.

Kweli mtu kama Luhanga ukimuweka pale Tatizo atawasha moto, sijui kwa nini serikali haitumii kichwa hiki. Au wenye data yuko wapi sasa hivi?
 
Namshukuru Fundi Mchundo ameeleza vizuri. Sikuwa na mpango wa kujibu post yoyote leo, lakini nimefurahishwa na mchango wa fundi huyu. Kazi ya kwanza ya wanasiasa ni kutetea wananchi. Nchi zote zilizokuwa zimetawaliwa zimepata uhuru kutokana na mchango mkubwa wa wanasiasa, ki-uongozi na uhamasishaji. Na hata matatizo mengi hutatuliwa vyema wanasiasa wanaposhiriki kikamilifu (hii tunaita political will). Angalia maswala yanayohusu afya, mazingira nk, wanasiasa wanapoingia katika kushughulikia matatizo hayo, mabadiliko makubwa mazuri hutokea. Kampeni za chanjo na upandaji miti zimeleta manufaa makubwa sehemu nyingi duniani baada ya wanasiasa kuzibeba kama political agenda. Si lazima mwanasiasa aelewe taaluma inayohusika katika kuleta ukombozi, yeye anapaswa kuzingatia matashi ya ummat wake. Kwa hiyo mwanasiasa yeye anawa-challenge wataalamu walete maendeleo bila kuumiza wananchi unnecessarily. Ukitaka ku-fit kwenye madaraka hayo, lazima uwe versatile, usinganganie tu elimu yako ya darasani. CCM wametuahidi maisha bora kwa kila mtanzania. Huo ndio unaopaswa kuwa msimamo wa wanasiasa wa CCM. Sasa wataalamu wanaoajiriwa chini ya vision hii wanapaswa kuona hiyo ndio changamoto iliyo mbele yao, kutupatia maisha bora (ikiwamo umeme wa uhakika). Umeme sasa ni political agenda, lazima wanasiasa wasimamie hili. Na mtaalamu anapaswa kuichukua hii katika muktadha wa taaluma yake, kutatua changamoto iliyopo kwa kutumia rasilmali zilizopo. Ndiyo matumizi ya akili hayo. Fanya ujualo tupate umeme kwa wananchi kwa bei nafuu, ndio changamoto iliyo mbele ya TANESCO. Kama wanashindwa waondoke. Na huwezi kutenga siasa kwenye masuala yanayohusu wananchi wengi, tena maskini. Hivi wanasiasa wasipowatetea wananchi hawa, nani atawatetea? Hizo nadharia za uchumi wa kitabuni hatuzihitaji hapa, hazitusaidii kitu. Tunataka umeme kwa bei nafuu, huliwezi hilo, ONDOKA, basi. Elimu ya kukariri na kupata cheti haina maana yoyote, yenye maana ni ile ambayo unaweza kuitumia katika mazingira uliyopo kutatua matatizo at that level. Umesoma sana, tunakuheshimu, lakini kama huwezi kutumia elimu hiyo kutanzua changamoto zinazotukabili, basi pisha mwingine. Kabisa! Na wengine wa namna hiyo huko TANESCO na kwingineko kama bado wapo jamani nao wajiondoe, basi!

Kithuku,
Kaazi kweli kweli! Siasa ndo hizo zimeifikisha TANESCO hapo ilipo- ina madeni kibao- bei nafuu na wengine wanaachwa hawalipi ndo hayo!
Cut your coat according to your cloth!
Mwanauchumi Dr. Idris (PhD- Boston) anakuambia haiwezekani- this way we can not run TANESCO. Options:
i)Serikali itoe ruzuku kubwa zaidi na kupunguza matumizi mengine or
ii)Kuongeza bei ya umeme! (Dr. Idris ameongeza bei)- serikali inaweza kupunguza for option i) above
iii) TANESCO ipunguze matumizi yake kuongeza productivity- hii nasikia TANESCO tayari wameanza -sijui tu kwa kiwango gani!

This is simple Economics na siyo Rocket Science! Electricity Energy in Tz is expensive commodity- it is a necessity but someone somewhere must pay for it!

NB Kumbuka pia bei ya mafuta iko juu sana kwa sasa na miji mingi Tz bado TANESCO wanatumia diseli!
 
Profesa Lipumba alihojiwa na waandishi wa habari baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 kutangazwa. Alisema, kama CCM imeshinda kwa kishindo pamoja na madudu yote wanayofanya hapa nchini na Watanzania wenyewe wakiishi katika lindi la umasikini wa kupindukia, basi haina haja ya kuwahurumia. Yaani kwa kifupi, hawabbebeki. Watanzania siyo watu wa kuhurumiwa!

Nami naungana na Prof Lipumba!

Kweli kabisa kabisa na kabisa!! Na 2010 wakija wakishinda tena watu wakishangaa imekuwakuwaje nitawatukana mimi. Kwa jamii yoyote iliyo "erevuka" (sina uhakika kama ni neno la kiswahili hilo) CCM ingekuwa imeshawekwa benchi loongi tu. Na jamii hiyo ingekuwa haina huruma utawala wowote ule elio mbovu uwe wa Chadema, CCM, mgombea binafsi n.k.
 
Duh! mheshimiwa anayemlaumu Mwalimu bado kaniacha hoi sana.Baada ya miaka 22!Duh!
Lakini leo nimesoma kwenye Citizen,na linasema Dr Idriss haja resign.The heading read thus"POWER DISCONNECTION COSTS GOVT,FIRM SHS 540M A DAY" Then the small print reads "AS TANESCO MANAGING DIRECTOR DR IDRIS RASHIDI DISMISSES REPORTS THAT HE HAS RESIGNED"
 
Ripoti zilizotoka ndani ya kikao cha board ya Tanesco zilisema KAJIUZULU.

Wananchi, hapa isije kuwa amri imetoka juu jamaa aendelee, na maamuzi ya board yakapigwa chini, msisahau kuwa board nayo inapo inapotakiwa kuripoti.

Kujiuzulu alijiuzulu, kama kakataliwa au ameombwa aache hasira au aliyoyataka yamekubaliwa hio ni hoja nyingine.
 
Kajiuzulu, labda aseme kuwa barua yake aliyoandika jana kaifuta vinginevyo ni mwongo .

Pili kuna mkono wa EL kuhusu uchunguzi unaoendelea juu ya Richmond.

Kuna taarifa kuwa wafanyakazi sita wa makao makuu wamepewa barua za kuhamishwa vituo vya kazi, na kama hili ni kweli basi hapa kuna kuficha ushahidi juu ya richmond.

Jana gazeti la mtanzania liliandaliwa kwa ajili ya kupewa taarifa hiyo kwa umma .

Mwenye simu ya Said Nguba mwandishi wa PM ampigie usikie atasemaje juu ya hilo ama Karamagi pia,
 
Sasa hii ndiyo mimi huwa nashangaa, yaani katika ile nchi ukifanya kazi vizuri basi unatakiwa uwe mwanasiasa? yaani hakuna kitu cha maana unachoweza kufanya isipokuwa siasa? Jamani we must change. Not every smart guy should be a politician, there are many things a person can do apart from politics. In fact if you read histrory carefully, very intel;igent people never make good politicians!

Hapo umesema kweli kabisa! CCM inawaharibu viongozi wengi wazuri kwa kuwataka wagombee ubunge ili wapewe uwaziri mara wanapokuwa na mafanikio makubwa mahali popote pale kama watendaji wakuu. Kwa mfano, Prof Sarungi alifanya vizuri sana pale muhimbili na akawa ni kipenzi cha wafanyakazi na mazingira yake yakaanza kupendeza. Sifa za kazi yake zikafika kwa wanene wakamuomba agombee ubunge naye akafanya hivyo. Mara baada ya kuondoka Muhimbili ikaanza kutetereka.
 
Pia mwenye simu ya mbunge wa CUF (Mnyaa)pamoja na mwakyembe mwenyekiti wa kamati ya richmond basi aweze kuwauliza kwani wapo hapo kwa ajili ya uchunguzi wao wa wiki mbili.
 
FD

Vipi jamaa kageuza kibao nini? Ha ha ha haaa............

Nafikiri hii itakuwa funga mwaka.
 
Kithuku,
Kaazi kweli kweli! Siasa ndo hizo zimeifikisha TANESCO hapo ilipo- ina madeni kibao- bei nafuu na wengine wanaachwa hawalipi ndo hayo!
Cut your coat according to your cloth!
Mwanauchumi Dr. Idris (PhD- Boston) anakuambia haiwezekani- this way we can not run TANESCO. Options:
i)Serikali itoe ruzuku kubwa zaidi na kupunguza matumizi mengine or
ii)Kuongeza bei ya umeme! (Dr. Idris ameongeza bei)- serikali inaweza kupunguza for option i) above
iii) TANESCO imepunguze matumizi yake kuongeza productivity- hii nasikia TANESCO tayari wameanza -sijui tu kwa kiwango gani!

This is simple Economics na siyo Rocket Science! Electricity Energy in Tz is expensive commodity- is is a necessity but someone somewhen must pay for it!

NB Kumbuka pia bei ya mafuta iko juu sana kwa sasa na miji mingi Tz bado TANESCO wanatumia diseli!

Asante Mkuu. Hakuna mtuanayebisha kuwa umeme ni expensive commodity. Wasi wasi wangu ni priorities zetu. Na(i) na (ii) zimewekwa wazi lakini ya muhimu zaidi(iii)? Hatuna hakika nayo! Mimi ningemuelewa kama angeanza na hiyo kwanza; Ndugu zangu kuanzia sasa wakurugenzi wote watachangia magari. Kama wakurugenzi wanne wanaelekea Dodoma, wote watapanda gari moja ambalo litakuwa linaendeshwa na mmoja wao, Wakuu wote watapanda economy kwenye safari za nje isipokuwa zenye kuchukua zaidi ya masaa 12 wataruhusiwa kupanda business, posho ya board members imeshushwa kuanzia ....hadi......, vikao vya board vitafanyika on-line isipokuwa mara moja kwa mwaka ambapo vitafanyika Makao makuu na havitachukua zaidi ya siku moja, tumefanyia energy auditing majengo yetu ili kuhakikisha tunatumia umeme kikamilifu, wafanyakazi pamoja na wajumbe wa bodi watalipia umeme kwa bei inayotozwa wateja, tunampango kuwaelimisha wafanyakazi wetu ili waongeze productivity yao na wale ambao hawaelimishiki tutawalipa mafao yao na kuwaaga, etc etc. Ndugu zangu, kwa kufanya hivyo tumeweza kuokoa kiasi kadhaa ambacho kitaturuhusu kupandisha bei ya umeme kwa kiasi... badala ya.... tuliyotarajia wali. Makofi! Zaidi ya hapo, tunafanya kila jitihada kuangalia vyanzo mbadala ya mafuta k.m kutumia mafuta ya alizeti na tunawashauri wananchi waanze kupanda hizi kwa wingi, kuendesha jenereta zetu. Mpango huu utachukua miaka kadhaa. Vile vile tunampango kabambe wa kusambaza umeme vijijini lakini hili litategemea RUZUKU kutoka serikalini. Blah, blah, blah. Haya najua kwa wengi hizi ni longo longo na siasa lakini cha msingi ni kubadilisha priorities zetu na kuwaheshimu wananchi wetu kwa kuweka kila kitu wazi. Kwa mimi ambaye sijawahi kufika Boston, hii ni common sense.
 
Back
Top Bottom