Mkurugenzi Mkuu Tanesco Ajiuzulu

Kalazimishwa kukanusha uamuzi wake wa Jana. Habari za ndani zadai kuwa serikali itafikiria maoni yake na kuwa wale jamaa wa Tanga cement washalipa gharama zote za wizi wa umeme.

Aliamua kujiuzulu baada kulazimishwa arudishe umeme kiwanda cha cement tanga. Simba cement walikutwa wanakwiba umeme, kisha walipokuwa invoiced wakakataa kulipa. yasemekana pale kuna 2 kaburuz ambao walishawahi fanya kazi tanesco kipindi cha netgroup. wao ndio walioleta jeuri ya kugoma kulipa.

pia ikumbukwe kuwa idriss ana bifu na kazaura (Board chairperson) baada ya kumtimua ofisini Tanesco na kumnyima pesa za kuendeshea ofisi hiyo. Habari toka ndani TANESCO zinadai kuwa mwenyekiti huyo wa board kipindi cha netgroup alipewa ofisi ya kudumu ktk jengo la TANESCO la mjini na ofisi yake ambayo ilijengwa kwa garama kubwa ilikuwa inapewa Sh 1 milion kila mwezi kama gharama za uendeshaji. Idriss aligoma na akamtaka aondoke, kwani yeye sio mtendaji wa tanesco na hapaswi kuwa na ofisi ya kudumu.
 
..............Pili kuna mkono wa EL kuhusu uchunguzi unaoendelea juu ya Richmond.
Kuna taarifa kuwa wafanyakazi sita wa makao makuu wamepewa barua za kuhamishwa vituo vya kazi, na kama hili ni kweli basi hapa kuna kuficha ushahidi juu ya richmond................,

EWURA au sio?
 
Asante Mkuu. Hakuna mtuanayebisha kuwa umeme ni expensive commodity. Wasi wasi wangu ni priorities zetu. Na(i) na (ii) zimewekwa wazi lakini ya muhimu zaidi(iii)? Hatuna hakika nayo! Mimi ningemuelewa kama angeanza na hiyo kwanza; Ndugu zangu kuanzia sasa wakurugenzi wote watachangia magari. Kama wakurugenzi wanne wanaelekea Dodoma, wote watapanda gari moja ambalo litakuwa linaendeshwa na mmoja wao, Wakuu wote watapanda economy kwenye safari za nje isipokuwa zenye kuchukua zaidi ya masaa 12 wataruhusiwa kupanda business, posho ya board members imeshushwa kuanzia ....hadi......, vikao vya board vitafanyika on-line isipokuwa mara moja kwa mwaka ambapo vitafanyika Makao makuu na havitachukua zaidi ya siku moja, tumefanyia energy auditing majengo yetu ili kuhakikisha tunatumia umeme kikamilifu, wafanyakazi pamoja na wajumbe wa bodi watalipia umeme kwa bei inayotozwa wateja, tunampango kuwaelimisha wafanyakazi wetu ili waongeze productivity yao na wale ambao hawaelimishiki tutawalipa mafao yao na kuwaaga, etc etc. Ndugu zangu, kwa kufanya hivyo tumeweza kuokoa kiasi kadhaa ambacho kitaturuhusu kupandisha bei ya umeme kwa kiasi... badala ya.... tuliyotarajia wali. Makofi! Zaidi ya hapo, tunafanya kila jitihada kuangalia vyanzo mbadala ya mafuta k.m kutumia mafuta ya alizeti na tunawashauri wananchi waanze kupanda hizi kwa wingi, kuendesha jenereta zetu. Mpango huu utachukua miaka kadhaa. Vile vile tunampango kabambe wa kusambaza umeme vijijini lakini hili litategemea RUZUKU kutoka serikalini. Blah, blah, blah. Haya najua kwa wengi hizi ni longo longo na siasa lakini cha msingi ni kubadilisha priorities zetu na kuwaheshimu wananchi wetu kwa kuweka kila kitu wazi. Kwa mimi ambaye sijawahi kufika Boston, hii ni common sense.

1. Kwa nini Wafanyakazi wa TANESCO na elimu yao waishi kwa taabu? Je unadhani utawapa wafanyakazi motisha kufanya kazi kwa bidii kwa kupunguza maslahi? Kwani wao wana kosa gani? Wewe unadhani hawa wafanyakazi TANESCO wanaishi sana maisha ya anasa? Unajua ugumu na riski kazi TANESCO? Kwani Mashirika mengine serikali wanaishije?

2. Hata ukibana matumizi ndani kiasi gani-how much can TANESCO save- wakati operation costs ni billions of shs kwa mwezi? Yet they have incurred and accumulated losses amounting to a staggering 700bn/-.

3. Naskia one bold intervention aliyofanya Dr. Rashid alimnyang'anya gari na ofisi alilopewa Mwenyekiti wa Bodi. Huenda ndo imeleta pia mvutano hadi wakatofautiana na hatimaye kujiuzulu!
 
haiwezikani sekta moja iingilie kazi za sekta nyengine. suala la kuwa kiwanda cha cement hakilipi bili zake za umeme, halikupaswa kuzungumzwa kwenye kikao cha bodi.

kiwanda kilifaa kukatiwa umeme bila mjadala.......kupendelea baadhi ya viwanda ndio mwanzo wa kukwamwisha taifa
 
Imeelezwa kwamba hatua ya mwisho iliyomfanya ajiuzulu, ni baada ya kugongana na Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Balozi Fulgence Kazaura, kuhusu uamuzi huo.

Hivi huyu mzee Kazaura, bado yupo tu serikalini? Huyu toka awamu ya kwanza mpaka leo? Yaaani hajapitwa tu na wakati?
 
Intresting!
Dr. Rashid ameonyesha msimamo! I like that! It is a good step -this man is bold- tunahitaji akina Rashid wengi ktk mashirika ya serikali!
Hao wazungu wa Tanga walipe tu umeme!
 
...Dr Rashidi alipopigiwa simu na waandishi wa habari wa The Citizen jana usiku baada ya huo uvumi kuwa kaachia ngazi,this is what he had to say "I'm still going on with my duties as MD of this company" dismissing the story as "groundless rumours"
 
Kwani haswa big deal ni nini kama yeye akijiuzulu? Kama ni kweli then pouwa tu atatafutwa mwingine and we move on....jeeeez!!!
 
1. Kwa nini Wafanyakazi wa TANESCO na elimu yao waishi kwa taabu? Je unadhani utawapa wafanyakazi motisha kufanya kazi kwa bidii kwa kupunguza maslahi? Kwani wao wana kosa gani? Wewe unadhani hawa wafanyakazi TANESCO wanaishi sana maisha ya anasa? Unajua ugumu na riski kazi TANESCO? Kwani Mashirika mengine serikali wanaishije?
Nina wajua sana watu wa Tanesco na ninakubali kuwa si wote wanaoishi maisha ya fahari. Lakini hapa si tunazungumzia kunasua shirika katika matatizo lilonayo? Unaamini kweli kuongeza bei ndiyo kutaongeza mapato bila ya kuangalia njia mbadala? Mimi nimewazungumzia wakurugenzi na bod membaz, si kumtaja fundi mchundo na mainjinia wakawaida. Tatizo naona hapa ni kumgusa msomi katika stahili yake! Hivi hilo shirika likifilisika nini itakuwa hawa wasomi watakimbilia wapi? Of course, hupungunzi mishahara( kama inabidi hivyo) hadi unaondoa motisha wa kufanya kazi. La hasha. Na pengine huna hata haja ya kupunguza mshahara. Mimi ni mchokozaji tu
2. Hata ukubana matumizi ndani kiasi gani-how much can TANESCO save- wakati operation costs ni billions of shs kwa mwezi?
Tutajuaje bila kuanza kubana hayo matumizi? Na hizo operation costs zsi moja ya matumizi?

3. Naskia one bold intervention aliyofanya Dr. Rashid alimnyang'anya gari na ofisi alilopewa Mwenyekiti wa Bodi. Huenda ndo imeleta pia mvutano hadi wakatofautiana na hatimaye kujiuzulu!

Na ndiyo matatizo yetu hayo. Kama alimnyang'anya Mwenyekiti hivyo katika kuondoa matumizi yasiyo muhimu, anastahili hongera. Lakini kama alifanya hivyo ili amkomoe ndiyo tunarudi pale pale!!!
 
...Dr Rashidi alipopigiwa simu na waandishi wa habari wa The Citizen jana usiku baada ya huo uvumi kuwa kaachia ngazi,this is what he had to say "I'm still going on with my duties as MD of this company" dismissing the story as "groundless rumours"

Mimi natoa hoja, Muungwana asaidie kutatua tatizo kati ya Mwenyekiti na DR Idrissa.

Mwenyekiti wa board anatakiwa aondoke!
 
Hivi hiki kitu kinafanya kazi vipi? Naona niache kupost, niende shule kwanza. Sasa naelewa kwa nini wasomi wanadai walipwe kulingana na usomi wao!!!
 
Huyu Balozi Kazaura ameshaanza kuelekea uzeeni! Apunguziwe tu majukumu! Kwa mawazo yangu- Mkuu wa Chuo UD inamtosha kabisa! Kumwongezea kero za TANESCO ni kumchosha bure mzee wa watu!
 
Hivi hiki kitu kinafanya kazi vipi? Naona niache kupost, niende shule kwanza. Sasa naelewa kwa nini wasomi wanadai walipwe kulingana na usomi wao!!!

Fundi, pole sana. Kitu gani tena hiyo inakutatiza... tunaweza kukusaidia?!

BTW, hoja zako ni nzuri na nimezipenda pamoja na kuwa siziungi mkono kwa asilimia 100 zote. Asante.

SteveD.
 
Huyu Balozi Kazaura ameshaanza kuelekea uzeeni! Apunguziwe tu majukumu! Kwa mawazo yangu- Mkuu wa Chuo UD inamtosha kabisa! Kumwongezea kero za TANESCO ni kumchosha bure mzee wa watu!

Pamoja na kuwa inaweza kuonekana kama kuleta vioja, nilishawahi kuuliza hapa... is euthanasia legal in Tanzania?!

Maana list ya majina yanayoweza kuwekwa humo na kushughulikiwa kiaina hiyo kwa faida ya umma Tanzania ni ndefu...

SteveD.
 
RTD katika taarifa ya Habari ya saa 10 jioni hii ni kuwa serikali imekiri kuwa Dr Rshid amejiuzulu Ukurugenzi wa TANESCO!
 
Na ni RTD hiyohiyo niliisikia jana usiku around saa tano usiku ikitangaza kujiuzulu huko. Well it just happened by chance wakti natafuta stesheni tofauti tofauti
 
Fundi, pole sana. Kitu gani tena hiyo inakutatiza... tunaweza kukusaidia?!

BTW, hoja zako ni nzuri na nimezipenda pamoja na kuwa siziungi mkono kwa asilimia 100 zote. Asante.

SteveD.

Asante Steve! Nitakushangaa kweli ukisema kuwa unaniunga mkono kwa asili mia kila wakati!
Ni haya mambo ya ku'quote'. Kuweza kuainisha ni paragraph gani nataka kuzizungumzia. Naamini ni utu uzima na hizi pupa zangu kuparamia vitu ambavyo havinihusu! Mtu wa ngurumo kwenye utandawazi unatafuta nini???
 
Fundi, shukrani.
Muhimu katika hili ni kutumia kanuni (tag) ya "quote": chochote kile unachotaka kuweka katika kunukuhu unaweka katikati ya [] na [/].

Nisiandikie mate ndugu yangu, swali lako limeshasumbua wengi pia, na maelezo yake yalishatolewa na Mwl. Kichuguu kwenye post hii hapo kitambo kidogo. Ni kama ifuatavyo basi:

Mwl.Kichuguu,
Habari yako ndugu yangu?
Ebwana hivi ukitaka kumnukuu mtu kama ulivyofanya kwenye bandiko lako la 26 unafanyaje? Mimi siko inclined sana kwenye mambo haya so naomba msaada. Yeyote yule anaweza kunisaidia.

Mzee Nyani Ngabu,

Hata mimi siyo mkali katika mambo haya ila ngoja nijitahidi kukuelezea kadri ya uwezo wangu. Ku-quote post moja vipade vipande, inabidi uweke vipande vya quotes zako kwenye mabano ya "quote" kama hivi

[ quote] umeona hili ? [/ quote]

bila kuacha nafasi nyuma ya neno quote; unaweza kurudia mara nyingi kadri upendavyo

[ quote] Limezuka jingine [/ quote]

bla bla bla

[ quote] Na hili tena[/ quote]

Kwenye editing toobar, kuna button ya kukusaidia kufanya hivyo bila kuwa na haja ya kutaipu neno "quote"

------------------

Ukikopi hizo quotes nilizoweka hapo juu na kundoa nafasi nyuma ya neno quote utapata:

bila kuacha nafasi nyuma ya neno quote; unaweza kurudia mara nyingi kadri upendavyo

bla bla bla

SteveD.
 
Hapa kupata solution ni ni kama ulivyopendekeza ila nasikia huyu jamaa alikuwa ameonyesha kuleta mwamko ndani ya TANESCO.

Pili nafikiri mirija iliyowekwa Tanesco ni mzigo mzito kwa mtu yeyote ambaye atakuwa Managing Director. Huwezi kufanya kazi nzito halafu unawalipa wengine.

Kweli mtu kama Luhanga ukimuweka pale Tatizo atawasha moto, sijui kwa nini serikali haitumii kichwa hiki. Au wenye data yuko wapi sasa hivi?

Majuzi ameteuliwa na muungwana kuwa mwenyekiti bodi ya wakurugenzi maktaba ya taifa kwa kipindi cha 3 y
 
Back
Top Bottom