Shirika la TANESCO ligawanywe kutengua Mawaziri Wakurugenzi na bodi sio ufumbuzi

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Wadau nawasabahi. Wakati umefika sasa wa kufanya Maamuzi Magumu ya KUIGAWANYA TANESCO. Tumekuwa tunawabadilisha MAWAZIRI WAKURUGENZI na BODI lakini MATATIZO ya TANESCO yapo pale pale na hiyo inaashiria kuwa Uongozi sio tatizo.Tatizo la TANESCO ni UKUBWA wa Shirika kinachotakiwa ni KULIGAWANYA SHIRIKA ktk Makundi yafuatayo:

1.Tanesco Nguzo na kusambaza Nyaya

2 Tanesco Mabwawa na kutafuta Vyanzo vipya.

3 Tanesco Uza umeme na Funga Mita.

Kila kundi liwe na Mkurugenzi wao ila Mwisho wa siku wanatoa Taarifa kwa Mkurugenzi mkuu wa Tanesco.
Kufanya hivi kutaondoa UKIRITIMBA uliopo ndani ya Shirika Rushwa ucheleweshwaji wa Makusudi wa Kutoa huduma utapungua kwani kila KUNDI litakuwa linajitahidi kutoa HUDUMA Mapema ili kuingiza MAPATO yake tofauti na Sasa Ukitaka Umeme mara uambiwe Nguzo hakuna Mita zimeisha au Nyaya hakuna.
 
Nina maswali 3 ukinijibu, nitakubaliana na wewe, nayo yote yataegemea kwenye mgawanyo uliofanya

Kulingana na mgawanyo wa kwanza, Kwa mfano wanaotaka kuwekewa nguzo Wakawa 1000 na kila nguzo tufanye ni 50000 maana yake itapata mapato ya 50m bila kuondoa gharama, Je ni kweli mapato ya 50m yanatosha kuendesha taasisi?

Mgawanyo wa pili, ni Kwa namna Gani hayo mabwawa yatatengeneza mapato yenye binafsi kama kutakuwa na taasisi ya kuzalisha na kuuza umeme?

Katika mgawanyo huu, je hawa watauza umeme utakaotokana na Nini ikiwa hawazalisha?
 
Leta tafiti la Hilo wazo lako kwanza sio unakurupuka tu na kuleta wazo ambalo si njia ya kutatua tatizo,
Kinachosumbua Tanesco ni mipango na utekelezaji .
 
Hapana. Wawepo wazalishaji na wengine wauzaji na wasambazaji. Kampuni mbili. Huyu muuzaji na msambazaji aweze kununua hata kwa watu binafsi. Mtu yeyote aruhusiwe kufungua kampuni ya uzalishaji.
 
Leta tafiti la Hilo wazo lako kwanza sio unakurupuka tu na kuleta wazo ambalo si njia ya kutatua tatizo,
Kinachosumbua Tanesco ni mipango na utekelezaji .
MIPANGO NDIYO HIYO angalieni namna ya KUTEKELEZA tumieni Akili japo kidogo acheni kuogopa kuanza UPYA hata huyo Waziri wa Nishati pamoja na Unaibu Waziri Mkuu wake TANESCO HAIWEZI
 
Nina maswali 3 ukinijibu, nitakubaliana na wewe, nayo yote yataegemea kwenye mgawanyo uliofanya

Kulingana na mgawanyo wa kwanza, Kwa mfano wanaotaka kuwekewa nguzo Wakawa 1000 na kila nguzo tufanye ni 50000 maana yake itapata mapato ya 50m bila kuondoa gharama, Je ni kweli mapato ya 50m yanatosha kuendesha taasisi?

Mgawanyo wa pili, ni Kwa namna Gani hayo mabwawa yatatengeneza mapato yenye binafsi kama kutakuwa na taasisi ya kuzalisha na kuuza umeme?

Katika mgawanyo huu, je hawa watauza umeme utakaotokana na Nini ikiwa hawazalisha?
Nini MATATIZO MAKUBWA na MAGUMU ya Tanesco ? Tuanzie hapo na NINI ufumbuzi wa MATATIZO hayo kwa Mawazo yako?
 
Umaskini wa nchi hii unachamgiwa kwa kiwango kikubwa na TANESCO, mtu siku nzima huingizi pesa kisa wao huu si upumbavu!
 
Back
Top Bottom