Mkoa maskini kuliko yote Tanzania

Kuna mtu mmoja aliniambia kuna mkoa fulani eti chakula chao kikubwa ni Kumbikumbi! Sijui ni mkoa gani tena ule? ngoja nimpandie hewani anitonye tena halafu nitawaambia.
 
Tabora kiwanja, Waulizeni waha na wachaga watawaambieni. Au hamjafika singida, Dodoma na katavi? Au hamjui maisha wanayoishi wazawa wa Dar.
 
Singida,Lindi na Mtwara sidhani kama watakosa kuingia top 5,ikifuatiwa na Dom.Hawa ndiyo mama wa umaskini tz waliko wekeza magamba.

Singida haiwezi kuwa maskini, huu ni uzushi unaoenezwa kwa wajinga wasio kama nyie. Singida ni Supplier wa Mazao mengi sana kwa mikoa ya TZ. Ndio maana ukizungumzia Kuku, Mafuta ya Alizeti, Vitunguu n.k Singida inahusika. Think Outside the Box
 
kuna mtu mmoja aliniambia kuna mkoa fulani eti chakula chao kikubwa ni kumbikumbi! Sijui ni mkoa gani tena ule? Ngoja nimpandie hewani anitonye tena halafu nitawaambia.

unamaanisha senene!
 
I think Singida na Dodoma ni mapacha wanaofanana katika hali ya umaskini, mikoa hiyo wananchi wana hali duni, wana njaa ya kila mwaka inayosababishwa na mvua kidogo na watu kubadilisha tabia ya ulaji inayowapelekea kuacha kulima nafaka aina ya mtama inayostahimili ukame badala yake wanakimbilia kulima mahindi ambayo hukauka wakati wa kutoa mbelewele. Hivyo, pamoja na ukosefu wa mvua, mabadiliko katika tabia ya ulaji pia huchangia sana kuendelea kuwepo njaa katika maeneo mbali mbali. Natamani serikali ingepitisha sera za kilimo kikanda badala ya uhamasishaji tu. Ipi bora, kulima mahindi isiyoiva, au kulima mtama unaouiva na kukawa na chakula cha kutosha.
 
singida, wanyaturu wanauzia mahindi shambani kabla hayajakomaa...nilishakaa pale, siku nahama nilirusha jiwe, sishuki pale nikipita na basi hata kukojoa tu,..nimepachukia balaa.
 
Singida haiwezi kuwa maskini, huu ni uzushi unaoenezwa kwa wajinga wasio kama nyie. Singida ni Supplier wa Mazao mengi sana kwa mikoa ya TZ. Ndio maana ukizungumzia Kuku, Mafuta ya Alizeti, Vitunguu n.k Singida inahusika. Think Outside the Box

Yaani unataka kuniambia pamoja na wale Kuku wengi wa kienyeji kutokea huko lakini Singida pia ni mkoa masikini??

Na mimi nimestuka kidogo kusikia Singida ndo maskini zaidi. Ingesemwa PWANI ningeamini zaidi. Wakati nasafiri na reli ya kati kituo kikuu cha msosi kilikuwa Saranda (Salanda), hapo kulikuwa na kuku wa kumwaga na nyama choma kwa wingi. Na pia kama alivyosema Mkimbizwambio, SIngida ndo supplier mkuu wa kuku wa kienyeji na mafuta ya alizeti kwa DAR ukiachilia mbali vitunguu n.k
 
Singida, Dodoma, Mtwara, Lindi, Tabora,Pwani. Hapa kuna namba 1 hadi 7 pangilia mwenyewe
 
Kagera, pwani singida ,dodoma panga mwenyewe ipi ianze source mtakwimu mkuu wa serikali
 
Umaskini wa nini unaozungumzia?

Kama wa Rasilimali, sijui. Lkn kama umaskini unaotokana na occupants wa mkoa wenyewe, basi ni Tabora. Mtu mzima na akili zako huwezi kuishi utegemee nyuki wakulishe. Wanyamwezi mpoooooo! Nakaribisha matusi kwa kuwa najua ukweli unauma

Msula eve, hahahahaa....!!!!!

Sasa umeona Tabora nzima tunaishi kwa kutegemea Asali na Tumbaku? Mbona mie ninafuga samaki na ninaishi kwa hela nzuri tu. Nina umeme masaa 24, internet, ninakula vizuri tu kuzidi wewe na watoto wangu wanaishi maisha mema. Sasa hayo uliyoandika hapo umeyaokota wapi?

Panga pangua, waweza changanya hela zako na baba yako, na bado hamfikii hata nusu ya hela zangu. Sasa hizi dharau mnaziokota wapi? Wewe kweli Mwana Mtoka Pabaya.

Na kwa akili yako mwenyewe ya Kinyamwezi umeona hapo umenifumaaaaa!

Tetea hoja kama kuna la maana mnalofanya shambani. Kila mtu na kikopo chake chenye tundu ili nyuki waingie na yeye akawahi stendi na chupa zake za konyagi kuuza asali kwenye mabasi yanayotoka Mwanza.

Igunga kuna kashule kamoja tu ka A-Level na bado watu hawajai, wako bize na magogo wanayatoboa kwa kati kati.
Yale yale..... Umeilisha wewe Tabora miaka yote hiyo? Huku Sikonge ni nadra sana kuletewa chakula na Serikali na mie tangu nizaliwe, sijawahi kula chakula cha msaada cha serikali hata kama ni cha kununua. Baba yangu alikuwa anahakikisha ana chakula cha miaka miwili ijayo mbele kiasi kwamba hata ukitokea ukame, tuliweza kuishi mwaka mmoja bila kulima wala kuvuna na tukawa na ugali hadi wa kuuza.

Kazi ya kulima tumbaku, ukiifanya wewe utalilia mama yako akurudishe huko alikokutoa. Ile ni kazi ya NGOSHA na si ya vitoto vilivyodekezwa na dharau kama wewe. Ile kazi ya Wanaume mtoto.

Hizo asali na takataka nyingine, wanafanya wafanya biashara uchwara wanaovamia maeneo hayo na jitu linakuja kusema Wanyamwezi wavivu. NOYAGA!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Kagera, pwani singida ,dodoma panga mwenyewe ipi ianze source mtakwimu mkuu wa serikali

leav kagera alone KG haikosi top ten ushawahi kusikia wanalilia msaada wa chakula wa serikali kwa zama zako ulizoishi KG usiilinganishe na miko uchwara hii Dodoma ,Mtwara,Singida,pwani au Shinyanga heay Tizama mkono wako kabla hujaandika(post) NB:mimi sio mbukoba
 
Back
Top Bottom