Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 4,167
- 11,490
Katika takwimu zote za miaka yote ya makusanyo ya TRA, mkoa wa kagera ni miongoni mwa mikoa iliyojuu katika kuchangia pato la taifa. Kwa report ya hivi karibuni ya TRA, mkoa wa Kagera katika uchangiaji wa pato la taifa imeshika nafasi ya 9. Sasa linapokuja suala la kugawanya pato la taifa kwa kila mwananchi wa Kagera (per capital, GDP), wanauhujumu mkoa wa kagera na kuufanya mkoa miongoni mwa mikoa fukara. Sijui wanapata faida gani kwa uongo huu wa mchana kweupe?
Kwanza kwa wale waliobahatika kukaa au kutembelea mkoa wa kagera, hali ya maisha ya wananchi wake ni bora zaidi saana kuliko mikoa mingi. Hapa tunaongelea malazi, chakula, elimu, barabara, umeme, kiwango cha wasomi, njia bora za mawasiliano ya ardhi na anga, n.k.
Sasa nawaambia nyie nyote mnaotumwa kuuchafua mkoa wa Kagera mshike adabu zenu!!!
Hata mikoa mingine wee nenda, huwezi kukuta mzawa wa kagera amekaa kihasarahasara! Utamkuta yuko vizuri. Sasa huo umasikini mnaotaka kuaminisha umma wa watanzania, mnafanya hivyo kwa faida gani? Wahaya kwanza ni wasomi na wachapakazi wanaotumia brain (akili zao) kupambana na kutoboa! Huwezi kukuta mhaya mtaani akilialia maisha magumu! Pamoja na kutopata mkono wa shirika kutoka serikalini kwa miaka mingi, lakini wananchi wa kagera wameendelea kupambana na kujikwamua huku wakimtegemea Mungu. Mungu ubariki mkoa wa Kagera na watu wake! Mungu ibariki Tanzania kwa ujumla! Amina