Mkoa maskini kuliko yote Tanzania

kwa africa mashariki miji unaokua haraka sana ni mtwara na lindi hii niliipata kwa mzungu mmoja amekaa africa mashariki kwa muda mwingi na kwa wakati huo alikuwaanakimbilia mikoa hiyo kwa uwekezaji
kwa mujibu wa taarifa za waziri mkuu mkoa wa mwisho ni singida ukifuatiwa na dodoma kwetu

Haya bana, wewe subiri tu mpaka mzungu aje akwambie. Jitahidi uchanganye na zako kidogo. Kuna vigezo vichache tu ambavyo vingekusaidia: kipato cha kaya, kipato cha mtu mmoja mmoja, upatikanaji wa huduma muhim katika mkoa, mfano, maji, afya, elimu, bara bara nk!
 
Hivi kigezo cha umaskini ni kutokuwa na bahari au maghorofa? For me singida beat almost a half of all regions In tz
 
Tabora waliambiwa walime tumbaku kwa wingi, wakalima alafu wakakosa pa kuuzia hiyo tumbaku yao, huku tayari washakopa pembejeo za kilimo, yaani hata ukiuza tumbaku yote bado unadaiwa kudadeki..!

Na ardhi yao washaiharibu haimei mazao mengine kudadeki. Alafu mkakati wa kidunia ni TUMBAKU ATARI KWA AFYA YAKO.

Fungua macho hapo.
Kudadeki..!
 
hivi ng'ombe, pamba na mpunga haviangaliwi au ni madini yanayotajirisha ccm tu.










MSUASO vp? neno umaskini lina maana pana sana lakini kwa ujumla tunaangalia ni mkoa upi ambao wananchi wanaishi kwa maisha duni zaidi ya mkoa mwingine. Aidha tunaangalia upatikanaji wa huduma za kijamii pia huduma zingine kama vile za kifedha, masoko ya bidhaa na bila kusahau mzungo wa fedha.

Asee niko njema. Tumia vigezo hivyo hivyo kuijadili shinyanga na utoe mifano halisi. Yaani nyie pamoja na kukamua mafuta ya pamba,samli, kutumia wanyama kwenye kilimo kwa kiasi kikubwa, miji na vituo vya biashara za ndani na nje still unasema shy is poorer. Kama ni huduma za jamii zitolewazo na serikali kama maji,hospitali na shule niambie penye nafuu ukiacha miundombinu ya mkoloni.
 
Kwa upande wangu nafikiri ni mkoa wa Pwani..kwani si umasikini wa chakula tu bali hata huduma za kia
afya na elimu..kama sisi pwani ya mwambao tunaishi kwa kutegemea bahari..
 
Wengine mtashangaa lakini ndivyo ilivyo. Kwa mujibu wa vigezo vya serikali miaka michache ilopita mikoa 5 masikini zaidi ni Kagera, Kigoma, Pwani, Singida, na Dodoma. Dodoma ndio uliotajwa kuwa Mkoa masikini zaidi na vigezo hivyo havikutajwa.
 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina mikoa 32. Ukipanga mikoa kimaendeleo ni lazima utapata wa kwanza na wa mwisho.
Mi nadhani cha msingi ni kujadili kama mipango ya kuikwamua nchi kutoka kwenye umaskini uliokithiri inafanikiwa au la. Ni vizuri tukaelewa kuwa hata kwenye mkoa tajiri kuliko yote, maskini hohehahe wapo lukuki. Kazi ni kwako!!!
 
Msula eve, hahahahaa....!!!!!

Sasa umeona Tabora nzima tunaishi kwa kutegemea Asali na Tumbaku? Mbona mie ninafuga samaki na ninaishi kwa hela nzuri tu. Nina umeme masaa 24, internet, ninakula vizuri tu kuzidi wewe na watoto wangu wanaishi maisha mema. Sasa hayo uliyoandika hapo umeyaokota wapi?

Panga pangua, waweza changanya hela zako na baba yako, na bado hamfikii hata nusu ya hela zangu. Sasa hizi dharau mnaziokota wapi? Wewe kweli Mwana Mtoka Pabaya.


Yale yale..... Umeilisha wewe Tabora miaka yote hiyo? Huku Sikonge ni nadra sana kuletewa chakula na Serikali na mie tangu nizaliwe, sijawahi kula chakula cha msaada cha serikali hata kama ni cha kununua. Baba yangu alikuwa anahakikisha ana chakula cha miaka miwili ijayo mbele kiasi kwamba hata ukitokea ukame, tuliweza kuishi mwaka mmoja bila kulima wala kuvuna na tukawa na ugali hadi wa kuuza.

Kazi ya kulima tumbaku, ukiifanya wewe utalilia mama yako akurudishe huko alikokutoa. Ile ni kazi ya NGOSHA na si ya vitoto vilivyodekezwa na dharau kama wewe. Ile kazi ya Wanaume mtoto.

Hizo asali na takataka nyingine, wanafanya wafanya biashara uchwara wanaovamia maeneo hayo na jitu linakuja kusema Wanyamwezi wavivu. NOYAGA!!!!!

Kwa hiyo wewe ndio Tabora nzima?

Unaweza ukajaza ukurasa lkn bado suala likarudi pale pale kuwa naizungumzia Tabora na si mtu mmoja. Mimi sina dharau nimesema ukweli tu. Wewe umekurupuka mbio, ooh mimi nafuga samaki. Sawa, wewe mmoja ukiwa na gitaa nyumbani kwako ndio tupigie mstari kuwa watu wa Tabora woote ni wanakwaya?

Halafu mimi sina HELA dogo slow down, mimi nina FEDHA. Hela zinakaa mfukoni na mimi sina mfuko nina akaunti
 
Singida,Lindi na Mtwara sidhani kama watakosa kuingia top 5,ikifuatiwa na Dom.Hawa ndiyo mama wa umaskini tz waliko wekeza magamba.

mbona hi ulotaja ni mikoa ya watu flani wa pale mashariki ya kati
 
Hivi kuna mtu aliwahi kutembelea mkoa wa kusini pemba....nenda huko ndo utajua umasikini ni nini.
 
Tuache chuki jamani mkoa wa pwani unatia huruma!shime jamani tuwasaidie wenzetu hawa!!
 
Mkoa wa Kagera unaongoza kwa umaskini. Wahaya wanaishi kwa kula ndizi siku zote hawana hata mifugo kama mikoa mingine.
 
mbona watu wanakuwa defensive na offensive sana? mtu alie anzisha thread anatafuta maoni ya watu kuhusiana na mikoa ambayo ina shida ambazo zinatatulika kwa njia za siasa, meaning that a good political intervention may most likely result in a betterment of the lives of the people in that particular area. so bearing this in mind, let us contribute towards that with a positive outlook.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom