Mke aiba namba za siri za mumewe na kujitumia pesa kila mwezi na kujinunulia vocha kila siku. Nimemwambia amwache usiku huu huu

Baada ya kuinasa amekuwa akijirushia 5,000-10,000 mara mbili kila mwezi na muda wa maongezi wa tshs 1,000-2,000 kila siku.

Mume anataka amuache sasa hivi na mimba yake akilalamika kuwa ni mwizi na asiye na shukrani kwani amekuwa akimtunzia ndugu zake na mtoto aliyemkuta kwa miaka mingi tu huku huduma akizitoa.

Lakini pia anadai kuna cases nyingi tu za ye kupoteza hela kila mara bila kuelewa, ingawa alidhani ni yeye mwenyewe tu anazipoteza lkn kwa hali hii anahitimisha kuwa itakuwa ni huyo mke aliyekuwa anamchezea michezo hiyo.

Kwakuwa siku za mwizi ni arobaini amegundua hilo juzi tu baada ya kutumiwa hela ya mtu huku salio likiwa hilo tu, sasa kila akijaribu kutoa anaambiwa salio halitoshi. Alipowapigiwa huduma kwa wateja wakawa wanamwambia mbona umetoa hela mwenyewe. Sasa alipochukua taarifa za miamala ndipo alipokutana na hayo. Mke alikuwa anafuta jumbe zote anazofanya miamala mume asione.

Mimi nimemwambia amwache, tena leo usiku huu huu kwani sio mtu wa kawaida huyo dada.......huwezi kujua ameshamdanganya mangapi na amepanga mangapi dhidi yake! Vipi wadau nimeshauri vibaya?!!!!!
Sasa hiyo ni sababu ya kuacha mke kweli?
 
Ajamuacha 7bu ya ela hizo chche
Anataka kumuacha 7bu ni mwizi
Ndio MWIZI
ishi na mtu mwenye TABIA zozote zitavumilika awe mke ndugu rafiki nk zitavumilika
Lakini Mwizi afai
Mke Mwizi ni mbinafsi
Rafiki Mwizi ni mnafiki

Huwezi kuishi na mke MWIZI na MBINAFSI
Omba upewe

Mm namuunga MKONO ila ampuuzishe aende kwao
Akijirekebishe amrudishe na awaambie ndugu wa huyo mke kuwa mkewe ni MWIZI
Unamnyanyasa mtu kisa elfu 40? Ndo maana tunapambana tupate pesa zetu, manake huwa mnatunyanyasa na vichenchi vyenu.
 
1,000 x 30 = 30,000/=
5,000 x 2 = 10,000/=
Jumla 40,000/= kwa mwezi.

Mshahuri kila mwezi awe anampa mke wake 50,000/= ya matumizi binafsi.

Huwezi muacha mtu kisa cha kingese ivo.
jamaa anaweza kuwa anatumia zaidi ya 50,000 kwenye kunywa BIAAAA
 
Mwanamke sio mwizi mwanaume hawajibiki kwa mkewe shida vocha na vipoketi money tujijengee tabia ya kuwapatia mahitaji madogo wenza wetu kadiri ya uwezo tulio nao

Akizidi hapo inakuwa hulka Binafsi nilitegemea jamaa ako ungesema huwa anampa vocha mkewe huwa anampa buku Tano za akiba umekuja kulalama kuwa ni mwizi tuuuu

Unataka akamuibie baba ake mzazi ameiba kwa mumewe

Kama mume kamind apige hesabu hizo anazokwapua awe anampa mkononi kiasi hicho ili ijulikane ni mwizi au mume hawajibiki
 
Hii sijaelewa kabisa, mfano kwenye account yangu ya benki ukitoa hela either kwenye ATM au SIMbank lazima nipate ujumbe wa kuhakikisha kama hela iliyotolewa nimehusika. Au alikuwa akitumia simu ya mmewe kutoa hela, na huyo jamaa inamaana muda wote yupo nyumbani hiyo simu yake inafanya miamala miwili mpaka mitatu kwa siku kila siku?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Anaweza kufanya usiku ukiwa unakoroma au bafuni unaoga. Meseji zinafutwa tu fasta mkuu.
 
yote hayo angeyaepuka kama asinge oa


KATAA NDOA
EPUKA VIBAKA
SAVE KIBUNDA
 
Back
Top Bottom